Тёмный

AFANDE SELE - ULIMI ULITELEZA | NAOMBA RADHI | NIMESHA MUOMBA MWENYEZI MUNGU | AMESHANISAMEHE 

Muslimu Tv
Подписаться 7 тыс.
Просмотров 36
50% 1

Afande Sele leo ametaarifu wa Tanzania Kuwa Ameomba radhi kwa aliyokosea juu ya kumtukana Mwenyezi Mungu (S.W) na Pia Ameeleza kuwa Ameshaomba Radhi kwa Mwenyezi Mungu na Ameshamsamehe.
Kuomba msamha maana yake ni kuomba radhi kwa Mola akusamehe kwa yale makosa au madhambi ambayo uliyafanya, na ni sawa ikiwa kuomba kwa moyo na ulimi au kuomba moyoni tu. Kwani Mola anajua nia ya mja Wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil Aali-`Imraan aya ya 135, “
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ…
Maana yake, “Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao…”
#Afandeselekumtukanamwenyezimungu #afandeseleaombaradhi #afandeseleaombamsamaha #afandeselenurdinkishki #afandeselesheikhkipozeo
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamrisha waja Wake waliofanya madhambi wamuombe msamaha Yeye tu, kasema katika Suratil Muzzammil aya ya 20, “
… وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
Maana yake, “…Na ombeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.”
Na katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari, Mtume S.A.W. kasema, “
"وَاللَّهِ إِنِّي لأسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً."
Maana yake, “Naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi naomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na natubu Kwake zaidi ya mara sabini kwa siku.”
Vile vile Luqmaan alimwambia mwanawe: Ewe mwanangu! Zoesha ulimi wako kwa kusema “ALLAAHUMMA GHFIRLII. Hakika Mwenyezi Mungu S.W.T. anazo nyakati hamrudishi muombaji.
Pia Hassan L-Basry R.A.A. kasema: Zidisheni kuomba msamaha katika nyumba zenu, na kwenye njia zenu, na kwenye masoko yenu na katika vikao vyenu. Kwa hakika nyinyi hamjui wakati gani huteremka maghufira (msamaha).”

Опубликовано:

 

16 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее
@HolyBaam ультанул в конце 🧨
00:34
Просмотров 375 тыс.
KISA CHA BIBI MWENYE KUJIBU MASWALI KWA QUR AN
52:57
Просмотров 2,8 тыс.