well organized..thanks..to director..and all members of choir..heavenly voices..good indication ..amiable facial expressionnof smiles filled w Holy Spirit..from.negros mission sequijor..
Walianza mwendo kwenda, wakakwea Hadi Bashani, palipokuwa na mfalme mmoja jitu aitwaye Ogu. Mungu alishaamuru ni sharti wapitie nchi ya Waamori, waweze kutua Kanani. Zaidi ya miaka mia nne Mungu alisihi "Waamori badilika, mrejee mienendo yangu" ila sasa kikombe Cha ghadhabu kilikuwa kimefurika, wafalme wao Ogu na Sihoni wakasita kuwapisha.. Chorus Nani aliye jasiri? Twende tuwapige makonde. Mungu aliwalinda wanaisiraeli katika vita, Waamori wakaangamia kwa kiburi Cha dhambi. 2. Ni mara ngapi wakristo, tumemzuia Mwokozi afanye mapenzi yake mioyoni mwetu sababu ya dhambi? Tusiwe kama Ogu na Sihoni. Yesu abisha malangoni mwetu, ale nasi kwenye karamu. Twapuuza neema ya Mungu wetu tunapoganda katika ulimwengu. Ole wetu sie waoga! Wajasiri wataziasi dhambi na anasa za Dunia, tena watamshinda mwovu shetani, kwa nguvu zake Mwokozi.