Тёмный

HISTORIA YA LAWRENCE GEORGE SAGINI -1926-1995 BY ANANNIAS EDGAR AND DENNIS MPAGAZE 

GLOBAL TV KE
Подписаться 58 тыс.
Просмотров 6 тыс.
50% 1

...............................................................................................................
Mfahamu Lawrence George Sagini; Waziri wa Kwanza Kutoka Jamii ya Wakisii Kukataa Mishahara Miwili, Washenzi Wakamshangaa!
______________
Siku hizi ukipata nafasi yenye fursa ya kuiba usiibe utaitwa fala. Ujanja ni kuiba! Wanaita kupiga. Watu wanatafuta uongozi ili kupiga kwa jina la kuwatumikia wananchi. Wakiwa majukwaani wanahubiri kuutumikia umma, wakipata nafasi wanauibia umma.Hiyo ndo itikadi ya viongozi wa sasa. Viongozi wa zamani hawakuwa na itikadi hiyo. Wao walitenda walichohubiri, tena kwa moyo na jasho maana waliongozwa na utu zaidi ya vitu.
Katika ardhi ya Gusii alikuwepo Lawrence George Sagini, waziri wa kwanza kabisa kutoka Gusii, lakini pia ni kiongozi aliyepewa kazi mbili zenye mishahara minono akadondosha mmoja.Alipoulizwa kwa nini unakataa ulaji? Yeye alijibu “I cannot scoop soup from two plates at the same time!” akimanisha hawezi kunywa mabakuli mawili ya supu kwa wakati mmoja. Hapa wenye tabia za wizi hawataamini, watasema ni sound tu.
Yamefanyika mengi mazuri zaidi ya hilo sema hatujui historia ndio maana Samuel Okemwa ameamua kutushika mkono katika hali na fedha kuandika historia za viongozi wa Gusii tangu uhuru, viongozi walioijenga Gusii kwa moyo ikaja kubomolewa kwa nyongo! Viongozi wanaoshindana kuitafuna Gusii hadi John Ariisi akaimba kuwaomba wapunguze wizi. Tutasikiliza kibao hicho baadaye, ngoja kwanza tumfahamu huyu mzalendo aliyekataa mshahara wa serikali.
Sagini ni kifungua mimba cha Mzee Ndemo Kibagendi kutoka katika ukoo wa Mwabogonko Nyakundi, mpiganaji jasiri aliyepambana na mwingereza alipojichanganya kwenda Kisii kujenga ofisi za kikoloni. Mama yake ni Bi Esther Nyanganyi. Alimzaa Sagini Januari 1, 1926. Baba yake alikuwa Mwanasheria mkubwa tu nchini. Alikuwa Rais wa Mahakama ya Kiafrika ya Kisii. Kumbe Sagini alitoka familia ya mboga saba ndo maana hakuwa na tamaa na vijisenti. Unajua wakati mwingine umaskini humfanya mtu awe mwizi ingawa si maskini wote ni wezi. Sema wengi ni wezi, usiwaamini sana.

Опубликовано:

 

26 мар 2021

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 1   
@williamorwaru1136
@williamorwaru1136 Год назад
Asante sana mr okemwa
Далее
Siasa za Kanda ya Africa | Mirathi ya Siasa
29:03
Просмотров 166 тыс.
MAITI YA RAISI IPATIKANE - 2 SIMULIZI YA UPELELEZI.
53:36
George Morara’s 48-hour ultimatum and death
18:39
Просмотров 75 тыс.
Mirathi ya Siasa: Siasa za watu wa Abagusii
25:36
Просмотров 52 тыс.