Cheza sasa kupitia shorturl.at/jqzU6 na ushinde
Baadhi ya wafanyabiashara wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, wamesitisha huduma za maduka yao kwa kile wanacholalamikia ushuru wa huduma (service levy) unaokusanywa pasipo utaratibu maalumu.
Wakizungumza na Mwananchi leo Ijumaa wafanyabiashara hao wamesema mbali na kukusanywa kiholela, pia wanadai wanatozwa kiwango kikubwa nje na utaratibu wa leseni zao.
Mkazi na mfanyabiashara katika soko la Misungwi, Ibrahim Manyasi amesema wanashindwa kuelewa utaratibu wa ukusanyaji wa ushuru huo, hali inayosababisha wengi wao kukamatwa pindi wanaposhindwa kulipa kutokana na gharama yake kuwa kubwa zaidi ya leseni yake.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Misungwi, Deogratius David amesema wafanyabiashara hao wamekubaliana kuendeleza mgomo huo mpaka Jumatatu Machi 25, 2024, pindi wakikutana na uongozi wa wilaya na kutatua changamoto hiyo.
Awali akizungumza na wafanyabiashara hao Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Abdi Makange amewaomba wafanyabiashara hao kufungua maduka yao, huku akiahidi Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kukutana nao jumatatu Machi 25, 2024 kwa ajili ya kusikia kilio chao na kulipatia ufumbuzi.
14 окт 2024