Тёмный

MAANDAMANO YA EKARISTI TAKATIFU 2019 KANISA KUU LA MTAKATIFU YOSEFU DAR ES SALAAM 

Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM
Подписаться 15 тыс.
Просмотров 12 тыс.
50% 1

Karibuni kutazama Maandamano ya Ekaristi Takatifu kwa mwaka 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo kuu la Dares Salaam. Maandamano hayo yaliambatana na vikundi na jumuiya mbalimbali kama Jumuiya za Kiingereza, Kwaya ya Familia Takatifu, Kwaya ya Mtakatifu Yofesu, Masister, Wanafunzi wa shule ya Saintt Joseph's Cathedral Millenium High School, Watoto waliopokea Sakrament Takatifu ya Ekaristi. n.k
Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya Upendo, ni zawadi na sadaka ya Kristo Yesu anayejitoa mwenyewe kama: Kuhani, Altare na Sadaka ili kuwafunulia watu wa Mungu huruma na upendo wa Mungu usiokuwa na mipaka. Huu ndio upendo unaofumbatwa katika Fumbo la Umwilisho linalopata utimilifu wake kwenye Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu! Ekaristi Takatifu ni chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni!
Ni Fumbo la imani linalopaswa kusadikiwa, kuadhimishwa na kumwilishwa katika huduma ya upendo, udugu na mshikamano; hasa na maskini pamoja na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, kwani Ekaristi Takatifu ni shule ya umoja, upendo na ukarimu unaobubujika kutoka katika Fumbo la Utatu Mtakatifu. Ekaristi Takatifu ni chemchemi ya maisha mapya inayowawezesha waamini kushiriki uhai wa Fumbo la Utatu Mtakatifu, ili kujenga na kudumisha Agano Jipya na la milele linalofungwa kwa njia ya Damu Azizi ya Mwanakondoo wa Mungu.
Ekaristi Takatifu ni chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa; ni kielelezo makini cha umoja wa Kanisa. Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican wanawataka waamini kuhakikisha kwamba, wanashiriki kikamilifu na kwa uelewa mpana maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu katika maisha yao na kamwe wasiwe ni watazamaji wa mafumbo ya Kanisa! Lengo ni waamini kuwa kweli ni mashuhuda wa kile wanacho amini na kuadhimisha!

Опубликовано:

 

10 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 15   
@emmanuelmroso7668
@emmanuelmroso7668 4 года назад
Amina
@rafaelkuroy4231
@rafaelkuroy4231 5 лет назад
asanteni wakatoliki wenzang kwa kumtangaza yesu wa ekaristi watu wote wapate kumjua
@fabianmabano8400
@fabianmabano8400 4 года назад
Hakika ibada ilipendeza.Mwaka huu Mwenyezi Mungu atujalie kufikia siku hiyo na kuisherehekea vyema.Hongereni washiriki wote.Mbarikiwe sana tena sana.
@elizabethwanyonyi609
@elizabethwanyonyi609 5 лет назад
Kwa hakika Yesu alifurahi.
@ngalawekikohingalawekikohi4768
Kristu kwetu ninguvu yetu
@kftstjosephcathedral
@kftstjosephcathedral 5 лет назад
Amina
@stevenfumbi9566
@stevenfumbi9566 5 лет назад
sherehe ilinoga sana
@kftstjosephcathedral
@kftstjosephcathedral 5 лет назад
Tumuabudu na kumtukuza Yesu Kristo wa ekaristi daima
@peterlugomok1372
@peterlugomok1372 5 лет назад
Kanisa kuu
@merinamarandu611
@merinamarandu611 5 лет назад
🙏🙏🙏🙏
@ema_uzazi
@ema_uzazi 5 лет назад
Ubarikiwe wote.🙏🙏🙏
@kftstjosephcathedral
@kftstjosephcathedral 5 лет назад
Amina
@andrewmsunga9425
@andrewmsunga9425 5 лет назад
🙏🙏🙏🙏🙏🙏
@rafaelkuroy4231
@rafaelkuroy4231 5 лет назад
asanteni wakatoliki wenzangu kwa kumtangaza yesu wa ekaristi
@kftstjosephcathedral
@kftstjosephcathedral 5 лет назад
Amina
Далее
NYIMBO ZA KUABUDU EKARISTI TAKATIFU - 2024
22:56
Просмотров 63 тыс.
Kongamano la Ekaristi Takatifu | Padri Titus Amigu
44:34
ROZARI YA HURUMA YA MUNGU
15:37
Просмотров 27 тыс.
Wimbo/KWAKO BWANA ZINATOKA SIFA/by
4:21
Просмотров 1,6 тыс.
Tazama alichotendewa Mama huyu na YESU WA EKARISTI
7:26