amen 🙏 pastor umetufunza leo nko dubai naomba kupita driving test huku dubai Wednesday, mungu wa pastor mwai na Jesus winner nakuamini sana hiyo test ni huyu mungu atafanya si kwa nguvu yangu dubai nko tuned
Shikol listening today's service nikiwa lebanon,Leo neno ni motomoto Asanteh sana Bishop endelea kabisa kuambia watu the Truth Gospel wabadilike ili wajifungulie baraka zao.
AMINA. Wakristo Mungu Atatubariki sisi watu wa JWM na marafiki zetu. Atawabariki wote wadogo kwa wakubwa na hata watoto, kizazi kitabarikiwa. Atujalia tuongezeke. Mungu Wetu ni wa kuongezeka si wa kutoa toa.Tutaongezeka wapende wasipende. Tutabarikiwa na Mwenyezi Mungu Aliyeziumba Mbingu na dunia. Mbingu ni ya Jehova na dunia ni yetu. Na kama Jehova Ametupatia dunia chochote kiko hapa "we have authority to receive it." Mungu Anapenda wanaompenda na wanaomtafuta kwa bidii humpata. Utajiri na heshima ni Zake. Fedha na dhahabu zote ni mali Yake. Tukiwa waadilifu Mungu Atatembea katika njia zetu. Mungu huwatajirisha wanaompenda na hujaza tele hazina zao, tukipenda Mungu Atatutajirisha.
AMINA. Wakristo tukiwa waadilifu na wenye haki Mungu Atafanya tukue kama mtende. Hata kama watu wamesema kuna kiangazi Mungu Atafanya baraka zetu zimee na Atatufanya tukue kama miti ya Lebanoni. Hakuna kukauka. Majira ikikubali, majira inayopendeza ikikuja kwetu hata maisha yetu haitakauka tena. Baraka itakuja "in season and out of season." Hiyo miti inakua kwa Nyumba ya Mungu itakua kwetu. Madhabahu ikibarikiwa nasi tunabarikiwa, Madhabahu ikiinuliwa nasi tunainuliwa. Tunaomcha Mwenyezi Mungu na tumtumainiye, Yeye Ndiye msaada wetu na Ngao yetu. Tutakumbukwa na tutabarikiwa. Tulionekana tumesahaulika, majira yetu yalikuwa mabaya na yalionekana hayapendezi lakini sasa tunakumbukwa.
AMINA. Kila mtu hapa "either" wewe ni tajiri ama maskini Mungu Amekupangia mazuri. Usiwahi dharau mtu kwa sababu ya shida. Kuna watu hudharau maskini na wale hawana kitu sana. Na haujui ni Mipango ya Mungu. Huyo Mungu Amekuinua Anaweza Kukurudisha kwa hiyo madharau. Hata kama hatutoshani, Mungu Ana sababu kwa nini hatutoshani. Tuache kiburi na majivuno na tukae na watu kama watu. Kuna fikra hapa Mungu Anataka Kubariki lakini hizo fikra ziko na maneno ya kidunia. Ni sisi tumezuia tubarikiwe, tugeuze mawazo na tubadilike. Tusiwahi jidharau, sisi ni mbegu ya maana na Mungu Ako na haja nasi. Kile Mungu Amepanga tukuwe tutakuwa na vile Anataka tukae hakuna mtu atazuia. Hiyo mbegu Mungu Ataiinua. Mbegu ya Jehova haitakufa na hawataisha. Tutachomoka!