Kinara wa Azimio Raila Odinga amewataka wakenya kujitokeza kwa wingi jumanne kumpigia kura kuwa rais wa tano wa Kenya. Raila akiahidi kushughulikia kwa haraka matatizo yanayowazonga wakenya endapo atachaguliwa kuwa rais. Akizungumza kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni zake, Raila amesema safari yake ya kupigania mabadiliko nchini imekuwa ndefu na ana nia ya kukamilisha safari hiyo katika afisi ya rais.
5 авг 2022