Тёмный

TWENZETU KILELENI 2024 YAZINDULIWA RASMI 

Подписаться
Просмотров 57
% 0

Twakwimu zilizotolewa na Shirka la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA zinaonyesha kwa kipindi cha miaka 110 Barafu katika Mlima Kilimanjaro imeshuka kutoka Kilomita za mraba 20 hadi kufikia kilimota 1.7 huku Mabadiliko ya tabia ya nchi na uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu kama ukataji Miti ovyo ukitajwa kama miongoni mwa visababishi vya kushuka kwa barafu hiyo
Nelson Munema.....
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam kuhusu Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro Mwaka huu kusheherekia Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika kamishna msaidizi kitengo cha Maendeleo ya Biashara TANAPA Jully Bede Lyimo amesema kaulimbiu ya mwaka huu ya Stawisha uoto wa Asili Tanznaia okoa Barafu ya Mlima Kilimanjaro itatoa uelewa kwa Wananchi kuulinda Mlima huo kwani Tafiti zinaonyesha unaathiliwa kwa kasi na Pepo kavu ambazo zinatoka Baharini na maeneo mengine ya nchi na zikifika kwenye Barafu zinapekelea barafu kupungua ukubwa wake
Safari hii ya Kupanda Mlima Kilimnajaro ni ya Nne kufanyika tangu kuanzishwa Rasmi mwaka 2021 huku zaidi ya wageni 500 kutoka ndani na njee ya Nchi wakitarajia kupanda Mlima Huu mrefu kuliko yote Barani Afrika wenye Maporomoko ,Barafu na Kasoko [Creter] kubwa kuliko zote Barani hapa

Опубликовано:

 

8 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии