Mtunzi: Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Original Song By:
MANENO YA WIMBO
Yatosha sasa mahangaiko haya, yatosha, mapigo ni mengi mno.
Yatosha sasa mateso makali haya, yatosha kabisa, yatosha mno.
1. Ee Mungu tazama chozi langu, sikiliza kilio changu.
Narudi kwako mara nyingine, kulilia huruma yako.
2. Natamani nami nipumzike, Ee Mungu chukua hatua.
Kwa nini unanyamaza kimya, naita mpaka nazimia?
5. Huruma yako Mungu, ni huruma ya milele.
Huruma yako Mungu, nitakufa nikiitumainia.
#wanaromano
#kwaresma
15 сен 2024