Kwani maulidi ni nini? Kwa dhana za watu wengi wanavyodhani maulidi ni kukusanyika na kupiga matari na kula wali tu, hiyo siyo tafsiri sahihi, maulid ni siku ya kuzaliwa kwa Mtume (S) na maana yake halisi kimatendo ni historia ya mazazi Mtume (S), ila kwa bahati mbaya baadhi ya wanaokusanyika ktk vikao vya kufanya sherehe za mazazi hayo yani maulid wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanayoenda kinyume na maulid yenyewe yani wanaenda kinyume na sira au historia ya kuzaliwa kwa Mtume (S), wanapiga matari kama vibao kata au madensi huku mabarobaro wakinengua kama mabinti au kaumu Lutwi hakika huu ni ufasiki wa hali ya juu. Kwa matendo haya ndiyo yanayopelekea wasiojua maana ya maulid wakihukumu jumla jumla kuwa maulid ni haramu jambo ambalo siyo sahihi kwani ukisema ni haramu bila ya kujua unachokiharamisha ni nini katika maulidi hayo maana yake umesema kuzaliwa kwa Mtume (S) ni haramu tafsiri ambayo inayotuweka ktk makosa makubwa yani tunaharamisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S).