Тёмный

JESHI LA CHINA LAWASILI NCHINI KUADHIMISHA MIAKA 60 YA JWTZ 

Fullshangwe tv
Подписаться 6 тыс.
Просмотров 471
50% 1

Zaidi ya watu 350 wakiwemo Madaktari Bigwa 140 kutoka Jeshi la Ukombozi wa watu wa China wamewasili nchini wakiwa na Meli kubwa ya hospitali yenye vifaa vyote vya matibabu ya kitabibu wakiwa na lengo la kutoa matibabu bure kwa watanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la JWTZ tangu kuanzishwa kwake pamoja na ushirikiano na Jeshi la China.
Akizungumza leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amesema kuwa ujio wa ugeni huo umetokana na ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na China.
Mhe. Chalamila amesema kuwa meli hiyo imekuja na vifaa vyote vya hospitali kwa ajili kutibu magonjwa ya ndani, magonjwa ya wakina mama pamoja na watoto.
“Huduma za kitabibu zinazotarajiwa kutolewa kuanzia Julai 18 - 24, 2024 katika vipimo, tiba za kawaida, upasuaji wa kawaida, magonjwa ya kinamama, mifupa, njia ya mkojo, macho, pua, koo, meno, moyo, utumbo pamoja na ngozi zilizoungua na moto” amesema Mhe. Chalamila.
Mhe. Chalamila amesema kuwa matibabu hayo yatatolewa kwa ushirikiano na wataalamu wa afya wa JWTZ, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Tumbi, Amana, Temeke, Mwananyamala, Jakaya Kikwete pamoja na Jeshi la Ukombozi wa watu wa China.
Ameeleza kuwa huduma za kitabibu zinatarajiwa kuanza kutolewa Julai 18 - 23, 2024 , huku akibainisha kuwa kwa siku moja wanatarajia kutoa huduma kwa watu 600.
“Julai 18, 2024 watakuwa katika hosptali ya Lugalo na Kunduchi, Julia 19, 2024 watakuwa Amana na Bunju, Julia 20, 2024 watakwenda Mwananyamala na Temeke, pia matibabu yataendelea hapa bandarini ndani ya meli hii ambayo ni hospitali” amesema Mhe. Chalamila.
Mkuu wa Huduma za Tiba Jeshini Meja Jenerali Amiri Mwami, amesema kuwa ujio wa meli kubwa kutoka Jeshi la China ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na urafiki uliopo wa Jeshi la Ukombozi watu wa China.
Meja Jenerali Mwami amesema kuwa meli hiyo ni kubwa yenye vifaa vyote vya matibabu katika sekta ya afya ambayo imekusudia kutoa huduma ya matibabu ya afya bure kwa watanzania katika kipindi cha wiki moja.
“Kwa kipindi cha wiki moja madaktari bigwa kutoka China watakaa nchini na watajumuika na madaktari bigwa kutoka hospitali zetu kubwa ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila, Jakaya Kikwete pamoja na Taasisi ya Mifupa kwa ajili ya kufanya kazi pamoja na kubadilishana uzoefu” amesema Meja Jenerali Mwami.
Amefafanua kuwa pia kutakuwa na madaktari wa kawaida kwa ajili ya kutoa matibabu ya msingi ambao watakuwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mbagala Zakhem, Bunju Shule pamoja na Kunduchi, huku akieleza kuwa baada ya saa za kazi madaktari pamoja na wauguzi watashiriki michezo mbalimbali

Опубликовано:

 

13 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 3   
@wisdomhamisi2249
@wisdomhamisi2249 Месяц назад
Fantastic
@alphabartazary9692
@alphabartazary9692 Месяц назад
Wow, that's great
@yusufurhobi9678
@yusufurhobi9678 Месяц назад
Hivi wanajeshi nao wanakuaga na vitambi eti
Далее
Sherehe za kukaribisha mwaka wa nguruwe China
1:19
Просмотров 1,2 тыс.
ну это жиза...  #standoff2
00:13
Просмотров 83 тыс.
when you have plan B 😂 @andreyreactions
00:11
Просмотров 4,4 млн
How to win a argument
9:28
Просмотров 532 тыс.
Karibu Kigoma !! chagua mwenyewe wapi unataka kuishi
7:15
Malalamiko ya Halima Mdee kuhusu uchaguzi
2:07
Просмотров 410 тыс.
ну это жиза...  #standoff2
00:13
Просмотров 83 тыс.