Тёмный

Kigogo wa zamani Tucta afichua makubaliano ya kikokotoo 

Mwananchi Digital
Подписаться 1 млн
Просмотров 628
50% 1

Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Nicolaus Mgaya amesema bado wafanyakazi wana safari ndefu ya kupata nyongeza ya kikokotoo, akitaja sababu ni Serikali kushindwa kuiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na ukwasi wa kutosha.
Mgaya pia amekosoa utendaji wa Tucta akisema imeshindwa kuibana Serikali katika kudai haki za wafanyakazi likiwamo suala la kikokotoo.
Suala la kikokotoo lilianza kufukuta mwaka 2018 baada ya iliyokuwa Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuandaa kanuni mpya zilizolenga kukipunguza kwa watumishi wa umma kutoka asilimia 50 hadi asilimia 33 na kupandisha kutoka asilimia 25 hadi 33 kwa watumishi wa sekta binafsi.
Hatua hiyo ilipigiwa kelele na watumishi wa umma, ndipo hayati Rais John Magufuli alipoivunja SSRA na kuahirisha matumizi ya kanuni hizo, akitaka zianze kujadiliwa mwaka 2023.
Akizungumza jana Aprili 30, 2024 katika mahojiano na Mwananchi Digital jijini Dar es Salaam, Mgaya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Tucta kuanzia mwaka 2009 hadi 2016, amesema suala hilo lilianza baada ya Serikali kuwahamisha watumishi wa umma waliokuwa wakichukua pensheni Hazina na kuwaweka katika Mfuko wa Pensheni kwa Watumishji wa Umma (PSSF).
Kwa undani zaidi wa mahojiano haya fuatilia kupitia chaneli ya RU-vid ya Mwananchi Digital

Опубликовано:

 

14 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее
How the Most Elite Spy Agency Operates
22:42
Просмотров 1,9 млн
САМАЯ ТУПАЯ СМЕРТЬ / ЧЕРНЕЦ
1:04:43
FAHAMU KUHUSU KIKOKOTOO KIPYA SEHEMU YA KWANZA
14:16
How to win a argument
9:28
Просмотров 607 тыс.
MJUKUU WA NYERERE AUTAMANI URAIS.
7:02
Просмотров 86 тыс.
🔴KIKOKOTOO CHA MAFAO KILIO KIMESIKIKA, 14 Juni 2024
13:16