Тёмный

Kuna Saratani za kifamilia kama ya matiti, utumbo mpana, tezi dume na mayai. 

CHUMBA CHA HABARI CLOUDS MEDIA GROUP
Подписаться 631
Просмотров 5
50% 1

"Kuna Saratani za kifamilia kama ya matiti, utumbo mpana, tezi dume na mayai. Ndio maana tunashauri kama kwenye familia yenu kuna mtu ana Saratani mojawapo kati ya hizi ni muhimu ukacheki mapema afya yako"- Dkt. Julius Mwaiselage, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani, Ocean Road
"Jinsi umri unavyokuwa mkubwa na uwezekano wa kupata Saratani unaongezeka kwa sababu ulipata visababishi ukiwa na miaka 30 ukifika miaka 60 Saratani inaanza kutoka kwahiyo umri ni mojawapo ya visababishi"- Dkt. Julius Mwaiselage, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani, Ocean Road.
"Pia jinsia Saratani inawapata sana wanawake kuliko wanaume kutokana na maumbile na vichocheo. Pia kuna ishu ya kifamilia kuna baadhi ya familia zina uwezekano wa kupata Saratani zaidi kuliko wengine kwa sababu Saratani ni ugonjwa unaohusiana na seli na DNA.
"Taasisi yetu inahusika sana na mgonjwa ya Saratani. Tulipitishwa mwaka 1999 kwa sheria ya Bunge na katika hiyo sheria majukumu ambayo tumepangiwa kuyafanya ni zaidi katika huduma za Saratani, kusimamia hospitali ambayo ndio tunayo lakini pia huduma za wagonjwa wa ndani na nje. Tunatoa huduma za elimu kwa wananchi mambo ya utafiti, mafunzo na pia kutoa ushauri kwa wadau mbalimbali kuhusu masuala ya Saratani"- Dkt. Julius Mwaiselage, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani, Ocean Road.

Опубликовано:

 

8 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее
Поплатился за подлые удары!
01:00
KP KWENYE UWEKEZAJI WA TAIFA
39:06
Просмотров 63
KUGEUZWA  | STARTING POINT | 6 Oktoba, 2024
1:23:18
Hukumu ya kesi ya Nyundo na wenzake wanne
38:03