Тёмный

Mafunzo ya Ufundi Magari yanayotolewa katika Vyuo vya VETA . 

VETA Tanzania
Подписаться 7 тыс.
Просмотров 20 тыс.
50% 1

Matumizi ya magari kama vyombo vya usafiri yameenea ulimwenguni kote. Pamoja na uwepo wa njia zingine za usafiri, magari hutumika sana kwa usafiri wa watu binafsi; usafiri wa umma,yaani abiria na hata kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ni dhahiri kuwa matumizi ya magari ambayo yanazidi kuongezeka kila siku yanaleta mchango mkubwa sana katika maendeleo na kurahisisha maisha ya watu wengi. Magari haya pia yamezalisha ajira kwa watu wengi na hasa vijana ambao hutegemea kazi ya udereva katika kuendesha maisha yao na ya familia zao.
Kukua na kupanuka kwa matumizi ya magari kunazaa hitaji kubwa la mafundi wa magari hayo, kwani kama ilivyo kwa vyombo vingine vya usafiri, magari hayo hupata hitilafu na kuhitaji matengenezo au marekebisho.
Uhitaji wa matengenezo ya magari umeibua fursa ya ajira kwa vijana wengi nchini. Mathalani, katika sekta isiyo rasmi, vijana wengi wamejiajiri kufanya shughuli za ufundi magari katika maeneo mbalimbali, hasa mijini na vituo mbalimbali kwenye barabara kuu. Vivyo hivyo, taasisi na makampuni mbalimbali, hasa yanayoshughulika na usafiri na usafirishaji yameajiri vijana wengi kwa ajili ya matengenezo ya magari.
Hata hivyo, kumekuwa na changamoto kubwa ya uwepo wa mafundi magari wasiokuwa na ujuzi wa kufanya matengenezo ya magari kwa uthabiti, hali inayosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri. Vijana wasiokuwa na ujuzi mara nyingi hufanya uharibifu zaidi kwenye magari wanayopewa kwa ajili ya kufanya matengenezo na kusababisha hasara kwa wateja wao.
Kwa kutambua changamoto hiyo, VETA imeendelea kutoa mafunzo bora ya ufundi magari ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi stahiki wa kuendesha shughuli za utengenezaji magari. Kwa kutambua mahitaji makubwa ya ujuzi wa ufundi wa magari, Asilimia kubwa ya vyuo vya VETA hutoa kozi hiyo.

Опубликовано:

 

7 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 28   
@KhalidKhan-ud9cz
@KhalidKhan-ud9cz 4 месяца назад
Mzuri Sana kweli 💖
@DianaWilawila
@DianaWilawila 6 месяцев назад
Chuo mix sana veta pwano
@winifridangowi6153
@winifridangowi6153 2 года назад
Good education to me
@abineligerady2124
@abineligerady2124 2 года назад
hiv unaweza kujifunza ufund wa magar kwa muda wa miez mitatu kwa mtu ambae hajaweza kufany hiyo kazi kabisa.
@davisnkoba2683
@davisnkoba2683 Год назад
Big up
@samsonsauga8004
@samsonsauga8004 4 года назад
Chuo kicho kipo xehem gan
@user-fi9fg2lq9k
@user-fi9fg2lq9k Год назад
Jamani Nina mtoto wangu nataka aje asomee ufundi magari SAS fomu napataje au naombeni namba zenu za Whatsapp kwa maendeleo yetu na watoto pia
@hamasagame9197
@hamasagame9197 3 года назад
Na kwahuku Pemba, zanzibar muje muweke brunch yenu... Mana huku Hakuna chuo cha veta
@denismajura1448
@denismajura1448 Год назад
Samahani naitji nafasi. Yakazi ya fundi mko sehemu gani
@thomasnashon4746
@thomasnashon4746 3 года назад
Naweza pata mawasiliano ya chuo icho nataka unishauri juu ya ufundi magari
@giftmyombe101
@giftmyombe101 3 года назад
Natakujifunza gar
@israahofficial8179
@israahofficial8179 10 месяцев назад
Nahitaji kujiunga
@kaiskisoma8946
@kaiskisoma8946 4 года назад
Mm naomba maelekezo zaidi kuhusu short kozi
@salimalriyami7779
@salimalriyami7779 2 года назад
Je hmna online corse ?
@salminmchimi7743
@salminmchimi7743 3 года назад
Injector pump je inafundishwa
@aminamaulidi1788
@aminamaulidi1788 3 года назад
Naitaji mwanang aje asome ufundi wa umeme
@stewardmeshack4463
@stewardmeshack4463 3 года назад
Tegea kauli yako kwahiyo kazi ya ufundi Ni ya watu wasiokuwa na kazi mtaani acha ufala
@lizzybahati9833
@lizzybahati9833 3 года назад
😃😃😃
@alfredmanana1306
@alfredmanana1306 Год назад
kwani mpaka ujue kusoma
@FlavianNdanzi-nf5qk
@FlavianNdanzi-nf5qk Год назад
Nafasi za masomo
@lizzybahati9833
@lizzybahati9833 3 года назад
Chuo chenu kipo mkoa gani
@gidofond5119
@gidofond5119 2 года назад
VYUO VYA VYETA VIPO ALMOST KILA MKOA ILA KWA DAR ES SALAAM, CHUO KIPO CHANG'OMBE NA KIMOJA KIPO KINGINE PALE KIPAWA ICT.
@user-fi9fg2lq9k
@user-fi9fg2lq9k Год назад
​@@gidofond5119Nina mtoto wangu yupo Dodoma atapata nafasi yakujua kusoma huko
@floridalupala1228
@floridalupala1228 4 года назад
Samahan ,je course ya umeme ipo?
@johnsport294
@johnsport294 3 года назад
Ipo
@user-ry1zd2ol2n
@user-ry1zd2ol2n 10 месяцев назад
Nataka kujifunza Ila naombeni namba yenu ya WhatsApp
@user-ry1zd2ol2n
@user-ry1zd2ol2n 10 месяцев назад
Naombeni namba yenu ya WhatsApp
Далее
#USAFIRIWAKO: Umeme wa Magari.
29:25
Просмотров 6 тыс.
MBOWE AELEZA MAZITO KIFO CHA MOHAMEDI ALLY KIBAO
11:55
CHUO CHA VETA IRINGA CHAWANUSURU MADEREVA KUPOTEZA KAZI
20:31