Тёмный

Mambo 5 Ya Kufanya Kwenye Mtandao Kuwafikia Wateja Wengi na Kuuza Bidhaa Nyingi 

Dr. Said Said
Подписаться 14 тыс.
Просмотров 14 тыс.
50% 1

Jifunza kunasa wateja kama smaku hapa: goo.gl/SXFSzk
Kama wewe ni mjasiriamali mwenye bidhaa au huduma nzuri lakini unashindwa kuwafikia watu wengi kwenye mtandao basi hakikisha unanipa macho na masikio yako kwani huenda makala hii ikawa moja ya makala muhimu utakayosoma mwaka huu.
Kutokana na uzoefu wangu wa kutumia mtandao kupata wateja, nimegundua kuna mambo 5 ukiyafanya vizuri basi utawafikia watu wengi na kuuza bidhaa nyingi sana.
Mambo yenyewe ni:
1. Zingatia Ubora:
Ukiwa unatoa bidhaa au huduma nzuri kwenye soko yenye kutatua matatizo ya wateja wako, basi utapata majeshi ya watu watakaokusaidia kusambaza ujumbe kuhusu bidhaa yako bila ya wewe kuwalipa chochote.
Wajasiriamali wa Silicon Valley, Marekani wana msemo wao unaosema,
The goal is to develop a product so good that customers will move the products for us before we consider marketing it.
Yaani,
Lengo ni kutengeneza bidhaa nzuri sana kiasi ambacho wateja wetu watatutangazia kwenye soko kabla ya sisi kufikiria kuitangaza wenyewe.
Na moja kati ya sifa muhimu wawekezaji wa makumpuni ya Silicon Valley (akina Facebook) wanaangali ni bidhaa nzuri zinazoweza kutangazwa na watumiaji?
2. Kuwa Tofauti
Ukiwa tofauti unakumbukwa.
Moja ya kosa kubwa linalofanywa na wafanyabiashara wetu ni kuangalia washindani wako wanafanya nini na kuwaiga.
Ukifanya hivyo basi usitegemee biashara yako kudumu miaka mingi.
Kuwa mbunifu na jiweke tofauti kabisa na washindani wako.
Mfano mzuri ni kampuni ya viatu iitwayo Vibram Five fingers, viatu vilivyokaa kama glovu za mikono.
Walipoviingiza viatu vyao sokoni vilianza kuenea kama virusi vya flu na kila aliyekuwa anaviona viatu hivyo alikuwa akivitamani.
Kwa nini? Mbali na bidhaa yao kuwa nzuri, walikuwa tofauti kabisa na viatu vyengine.
Ukiwa tofauti utakumbukwa siku zote.
Hutafananishwa na mamia ya washindani wako wanaofanana.
Na kila ikiwa rahisi kukumbukwa inakuwa ni rahisi vile vile kuwafikia watu wengi.
3. Toa Kabla Hujapokea
Japokuwa umeanzisha biashara yako kutengeneza pesa, jiulize kitu gani unaweza kutoa BURE kabla ya kuuza bidhaa yoyote?
Hii ni muhimu sana kwani wateja wako watarajiwa hawakujui, hawakupendi na wala hawakuamini.
Kwa hivyo ukiwazawadia kitu chochote, utajenga uaminifu kwa urahisi na kwa kasi kubwa sana hususan katika mtandao.
Vitu unavyoweza kutoa ni kama:
Ushauri
Sampuli ya bidhaa
Mafunzo (kama haya ninaokupa mimi)
N.k. (Kuwa mbunifu)
Lengo la utoaji ni kuwaonesha wateja wako watarajiwa kuwa hupo pale kula pesa zao bali unawajali na unataka bidhaa / huduma unayotoa iwasaidie kutatua matatizo yao.
4. Tengeneza Smaku Ya Kunasa Wateja Kwenye Mtandao
Tengeneza mashine kwenye mtandao yenye kuwasiliana na wateja wako watarajiwa, kukujengea uaminifu na kukuuzia bidhaa zako kwa niaba yako.
Watu wengi nikiwaambia hili hawaamini kuwa ni jambo linalowezekana lakini kwa dunia ya sasa amini usiamini ni jambo ambalo mtu yoyote anaweza kufanya hata kama hana elimu ya kompyuta.
Hii ni topic ndefu kidogo ila kama unataka kujifunza zaidi nimetengeneza video yenye kueleza namna ya kufanya hivyo hapa.
5. Tangaza! Tangaza! Tangaza!
Na jambo la tano na la muhimu sana la kufanya kuweza kuwafikia watu na kuuza bidhaa nyingi ni kutangaza.
Matangazo ni kama petroli kwenye gari lako.
Ukiacha kutangaza biashara yako haisogei mbele. Inakwama au inarudi nyuma.
Kwa vile washindani wamekuwa wengi kutangaza si jambo la hiari.
Ila ni muhimu kuzingatia matunda unayopata kutokana na kila tangazo uweze kuboresha na yazidi kukuletea faida.
Lengo ni kuwekeza pesa yenye kukusaidia kuleta mauzo yenye faida kubwa kuliko gharama za matangazo yako na kuendelea kufanya hivyo kila siku ili biashara yako ikuwe.
Ukiwa na mfumo mzuri kwenye biashara yako (ya mtandaoni na nje ya mtandao) kazi yako kubwa itakuwa ni
Kutangaza na
Kuboresha bidhaa na huduma zako
Kama una mchango au swali lolote, comment hapo chini.
Wako,
Dr. Said Said - CEO Online Profits
• Mambo 5 Ya Kufanya Kwe...

Опубликовано:

 

13 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 34   
@onesmolaurent210
@onesmolaurent210 Год назад
Kiongozi nashukuru sana kwa somo lako zuri sana , lakini mimi bilingual kwenye biashara ya suppliant nashindwa kupata wateja sijjajua Jinsi ya kujibrand
@mahmoudmzee-pr3vs
@mahmoudmzee-pr3vs Год назад
Shukran for good guidelines
@avand4237
@avand4237 2 года назад
Nilichelewa sana kuonana na Dr Said said popote ulipo Mungu akubaliki sana.
@josephmwinulla3737
@josephmwinulla3737 2 года назад
Mafundisho ni mazuri sana. So resourceful and educative. Thank you.
@khadijamwinyi5873
@khadijamwinyi5873 2 года назад
Shukrni Sana umeeleweka vizuri umenisaidia pakubwa Dr
@BestNtola
@BestNtola Год назад
Kaka hongeraa asante asante sana🙏🙏
@dr.saidsaid
@dr.saidsaid Год назад
Asante
@khadijamwinyi5873
@khadijamwinyi5873 2 года назад
Dr Mimi nafanya biaahara ya Network market ya Foreverliving product naipenda Sana natumia njia ya kuongea nawatu Ana kwa Ana na mikutano midogomidogo Ila bado cijawa nawateja wengi naomba msaada
@godlovebruno3395
@godlovebruno3395 7 лет назад
Ahsante kwa kutufumbua macho
@zuberyhaule5732
@zuberyhaule5732 5 лет назад
Shukrani
@mahadimatsawily5809
@mahadimatsawily5809 3 года назад
Ahsante
@vailethjohn4067
@vailethjohn4067 4 года назад
Kwajina naitwa vailet mjasiliamari mdogo, nauza mchele lakini napata wakati mgum kupata wateja, mpaka nakata Tama naomba msahada wakuelimishwa, Asante
@dr.saidsaid
@dr.saidsaid 4 года назад
Vaileth John huo mchele ni brand yako au brand ya kampuni nyengine?
@INTERPRENUER42
@INTERPRENUER42 2 года назад
🔥🔥
@annetcliford8801
@annetcliford8801 Год назад
Nimechelewa kujua ila umenifundisha kitu nataka kuazisha biashara ya chakula Ila kwa kupikia nymbni alafu nisambaze nitapata je wateja naomba wsp namba yko iliunileweshe nitapataje wateja online
@silverfinancialservicescol9306
Dr. Habari asante kwa somo nataka kujua nalipiaje tangazo ninapotaka kutumia social network haya ya fb nalipia kupitia vp
@jameseligius9459
@jameseligius9459 7 лет назад
awesome
@zainabushabani3881
@zainabushabani3881 5 лет назад
Samahani naomba namba yako
@mickidadyplanet6476
@mickidadyplanet6476 4 года назад
Sante sana...naomba kujua unaweza kufanya matangazo kwa kutumia smart phone au mpaka computer???
@sylveresentore8726
@sylveresentore8726 3 года назад
Kwangu Mimi nitawezaj kujenga vyashara nikiwa nauza asali
@richkinji2583
@richkinji2583 2 года назад
Hutoi number bro
@MwamvuaSihaba-hf2kw
@MwamvuaSihaba-hf2kw Год назад
Kwaiyo kama unataka kutuma matangazo mtandaoni iyo dollar 5 unaweka mb au vipi hapa sijafahamu
@dr.saidsaid
@dr.saidsaid Год назад
Unawalipa Facebook/Instagram
@taqiyaommy5470
@taqiyaommy5470 4 года назад
Nomba namba yako
@dr.saidsaid
@dr.saidsaid 4 года назад
Taqiya Ommy tupigie hapa 0679 536927
@conniesilayo250
@conniesilayo250 5 лет назад
Kaka unaongea kitu chenye ukweli.
@sarahkyando189
@sarahkyando189 6 лет назад
naomba msaada wanamba whatsap
@mashakaabduly4506
@mashakaabduly4506 6 лет назад
So great
@leocadiahussein6744
@leocadiahussein6744 4 года назад
Naomba uniunge kwa group lako wsp namba 0683052634
@dr.saidsaid
@dr.saidsaid 4 года назад
Wasiliana nasi hapa 0679 536927
Далее
Ufanye nini watu wa kupende zaidi?
9:09
Просмотров 132 тыс.
Njia 4 Kubwa Unazoweza Kutumia Kumshawishi Mteja.
7:01
ОНА БЫЛА ПЕВИЦЕЙ🤪
3:13:12
Просмотров 1,1 млн
Jinsi ya Kuingiza Milioni Yako ya Mwanzo Mtandaoni
25:28
Jinsi ya Kuuza Bidhaa za Bei za Juu Sana Kwa Urahisi
11:33
JINSI YA KUANZISHA MAZUNGUMZO - JOEL NANAUKA
7:30
Просмотров 43 тыс.
Njia Rahisi Zaidi Ya Kupanga Bajeti Yako
6:05
Просмотров 262 тыс.
Kilimo kinalipa, nawashangaa wanaokimbilia kuajiriwa
8:50
KUTENGENEZA BRAND KWA MITANDAO YA KIJAMII
4:25
Просмотров 1,1 тыс.