Тёмный

MNAFANYA KAZI NZURI, WAZIRI NDEJEMBI 

Shirika la Nyumba la Taifa
Подписаться 6 тыс.
Просмотров 70
50% 1

Wizara ya ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), licha ya kuingiza faida nzuri na kuwa na ukwasi wa shilingi trilioni 5.16 kutosahau malengo ya kuanzishwa kwake mwaka 1962 ya kuwajengea Watanzania makazi bora kwa mpango madhubuti.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, ametoa msisitizo kuhusu umuhimu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kutekeleza malengo yake ya msingi kwa kuwajengea Watanzania maskini makazi bora na yenye gharama nafuu.
Akizungumza katika kwenye ziara yake fupi kama ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Wizara ya kujitambulisha Shirika la Nyumba la Taifa, Waziri Ndejembi alisisitiza kuwa Shirika halipaswi kupoteza mwelekeo wake wa awali, uliowekwa na muasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
"Tusisahau kuwajengea Watanzania maskini makazi bora, na tuweke mipango madhubuti kuhakikisha kwamba tunatimiza azma hii. Shirika lazima liendelee na miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi, hususan wale wa kipato cha chini. Vilevile, lazima tuhakikishe kuwa hakuna wizi wala ubadhirifu wa fedha za umma, hasa katika ununuzi wa ardhi, ambapo ni muhimu kuzingatia uhalisia wa ardhi tunayoinunua," alieleza Waziri Ndejembi.
Sekta ya nyumba ina umuhimu mkubwa katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. NHC, kama mtekelezaji mkuu wa sera za makazi, ina jukumu la kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata makazi yanayokidhi vigezo vya ubora, usalama, na unafuu wa gharama.
Waziri Ndejembi aliongeza kuwa katika juhudi hizi, Shirika lazima lijikite katika kuhakikisha makazi yanapatikana kwa urahisi kwa
wananchi wote, hasa wale wa kipato cha chini ambao wanakabiliwa na changamoto ya kumudu gharama za makazi.
"NHC inapaswa kuhakikisha kuwa makazi tunayojenga ni bora na rahisi kufikika. Hii ni muhimu kwa sababu makazi bora yana mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.
Naipongeza NHC kwa kuanzisha mpango wa Samia Housing Scheme, ambao unalenga kujenga nyumba 5,000. Awamu ya kwanza imeanza Dar es Salaam, na nyumba 560 nyingine zinatarajiwa kujengwa Dodoma," alisema Waziri Ndejembi.
Akielezea zaidi kuhusu mpango huo, Waziri Ndejembi alibainisha kuwa si lazima kila nyumba inayojengwa iwe kwa ajili ya kuuza. Badala yake, alihimiza umuhimu wa Shirika kuzingatia pia upangishaji wa nyumba hizo ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kumudu makazi bora kwa gharama nafuu.
"Katika hili, haina maana kila unit tunazojenga zinakuwa za kuuza; hapana, ziwepo pia za kupangisha ili kuwapa nafasi wananchi wengi
zaidi kumudu makazi bora. Pia, naomba muanzishe mpango maalum wa kuwajengea wananchi nyumba ambazo zitakuwa ndani ya uwezo wao kumudu gharama," alihitimisha Waziri Ndejembi.
Kuhusu Wafanyakazi na utendaji kazi, Waziri Ndejembi amesisitiza kuwa atahakikisha kuwa anafanya juu chini ili wafanyakazi wapate hazi zao zilizokuwa zimekwama muda mrefu zikiwamo kupandishwa madaraja, mishahara na vinginevyo, ingawa amesisitiza wafanyakazi kutekeleza wajibu wao wa msingi wa kutenda kazi ili kulisongesha Shirika mbele.

Опубликовано:

 

5 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее
Bro's Using 3 Weapons
00:36
Просмотров 3,5 млн
Песня РАСПУТИН на русском!🔥
00:56
NUNUA NDEGE KWA DOLA 225,000 TANZANIA
8:53
Просмотров 20 тыс.
How to win a argument
9:28
Просмотров 587 тыс.
MAOMBI YA USIKU WA MANANE by Innocent Morris
3:14:49
Просмотров 129 тыс.