Тёмный

Mwipopo Aichangia Vinono Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini | Ateta nao Kuelekea Uchaguzi 2024/25 

Focus Digito TV
Подписаться 33 тыс.
Просмотров 61
50% 1

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Iringa na Mkurugenzi wa Shule za Real Hope zilizopo katika Mafinga mjini, Dickson Mwipopo amechangia kiasi cha Shilingi Millioni Tatu (3,000,000/=) kusaidia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Iringa Vijijini ambapo amekabidhi Milioni mbili hapo hapo huku akiahidi kumalizia milioni moja iliyobaki hapo baadae.
Mwipopo ametoa mchango huo alipokuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM Iringa Vijijini kilichofanyika katika Ukumbi wa Siasa na Kilimo uliopo kata ya Gangilonga Manispaa ya Iringa mkoani Iringa kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mario Kihongo.
Vilevile, Mwipopo ameahidi kutoa Msaada wa Vifaa vya TEHAMA ikiwemo Kompyuta (Desktop), Printer na Photocopy Mashine kubwa kwa lengo la kurahisisha Shughuli na utendaji kazi katika ofisi za Jumuiya hiyo ambapo pia ameahidi kutoa simu janja (Smartphone) mbili ili kusaidia katika usajili wa wanachama wapya kujiunga na Jumuiya hiyo.
Sambamba na hilo, Mwipopo amewahasa viongozi wa Jumuiya hiyo kuhakikisha michango na misaada inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo inatumika vyema kulingana na mahitaji na kwa wakati huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuhakikisha wanavilinda na kuvitumia ipasavyo Vifaa atakavyotoa ili viweze kuwafaa kwa matumizi ya muda mrefu.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Iringa Vijijini, Mario Kihongo amemshukuru Dickson Mwipopo kwa moyo wake wa upendo na utoaji huku akiahidi kutumia vyema michango Iliyotolewa na kuhakikisha kila kitakachokuwa kikifanyika kinakuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa hali ya juu.
Aidha, Kihongo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuishika mkono Jumuiya hiyo huku akisema kuwa Jumuiya hiyo ni kama imesahaulika na wadau haipiwe nguvu na kipaumbele kama zilivyo Jumuiya nyingine ndani ya Chama cha Mapinduzi hasa Jumuiya ya Vijana(UVCCM) na Jumuiya ya Wanawake (UWT).
Dickson Mwipopo akizungumza na Viongozi pamoja na Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Iringa Mjini kwa lengo la kuwahimiza wajumbe hao kuwahamasisha wananchi wengine kushiriki vyema uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kujindikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao.
Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
#FocusDigitoTV
..................
Tufuatilie Zaidi kupitia:
INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team FocusDigitoTV

Опубликовано:

 

10 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии    
Далее
BeastMasters Hawk just had enough #ti13
00:30
Просмотров 259 тыс.
гендер пати🩷🩵
00:21
Просмотров 113 тыс.
Ruaha Catholic University 2017 ( HD Video)
9:45
Просмотров 34 тыс.
BeastMasters Hawk just had enough #ti13
00:30
Просмотров 259 тыс.