Rais William Ruto sasa amesema yuko tayari kuwasikiliza vijana ambao wamekuwa wakiandamana kupinga mswada tata wa fedha. Rais akizungumza mjini Nyahururu kaunti ya Laikipia amepongeza kile anasema ni ujasiri wa vijana. Nje ya kanisa la ACK alikokuwa rais, mamia ya vijana waliandamana kutaka rais kuwasikiliza. Emmanuel Too anatuarifu zaidi kuhusu yaliyojiri kwenye hafla hii iliyosheheni maafisa wa usalama
22 июн 2024