Тёмный

Salama Na JERRY SILAA SE6 EP22 |KUKIWA JUA, KUKIWA MVUA PART 2| SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 396 тыс.
Просмотров 7 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
KUKIWA JUA, KUKIWA MVUA
Jerry Silaa ni Mheshimiwa na cheo au vyeo ambavyo ni dhamana mwenzetu ameanza siku nyingi,toka akiwa na umri mdogo kabisa na kama tujuavyo amekua muadilifu na ndo maana vimekua vikija tu toka alipokua na umri mdogo.
Kutoka kwenye familia ya Baba ambaye alikua Pilot wa helicopter nadhani Jerry alikua akijiona haswa akiwa mtu fulani, mtu muhimu katika maisha yake na ya watu walomzunguka, alike akiona ule mwanya ambao hayo yote kuyafanya yalikua yanawezekana.
Mazungumzo yetu yalianzia pale pale ambapo tuliishia mara ya mwisho tulipozungumza kwenye kipindi changu cha MKASI zaidi ya miaka saba au nane iliyopita na nguvu na nia na mipango ya kwenda mbele zaidi bado iko pale pale pengine kilichobadilika ni muonekano tu, bado mtanashati pia sana, shati lake jeupe ni jeupe kweli kweli, kama la mwanafunzi wa darasa la kwanza. Pengine mvi za hapa na pale nazo zimemfanya awe na muonekano wa kimaalum.
Sasa Jerry ni mmoja wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akiwa analiwakilisha jimbo la Ukonga kwa uchaguzi ambao ulifanyika mwaka 2015 na kwenye jimbo ambalo Chama Tawala ililichukua kutoka kwa wapinzani, tunaweza kusema kwamba jimbo hilo lilikua ni moja kati ya majimbo ambayo Chadema walikua wanajivunia, sasa kwake yeye je alijua kama anaweza kushinda hiyo nafasi? Ukiachilia na kwamba yeye pia ni mzaliwa wa jimboni hapo, nini hasa kilimpa UJASIRI huo? Nani alimshawishi kama kulikua na ushawishi wowote? Kwenye sehemu ambayo wapinzani wamejikita, Jerry aliona nini hawakifanyi sawa, wapi walikua hawajatimia mpaka yeye akajiweka?
Mimi naamini haiku kazi ndogo hata kama yeye alishawahi kura Kiongozi tena mkubwa tu ukiachana na ule uongozi ambao alikua anapata wakati yuko sekondari na chuo, Jerry alishawahai kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na hicho pengine kile ndo cheo cha juu kabisa ambacho mwenzetu ameshawahi kukishika kabla ya kubwa Mbunge.
Jerry ameo na aliyemuoa na mtu ambaye wamekua pamoja toka wakiwa sekondari, amemuona rafiki yake ambaye wamekua wakifahamiana kwa muda mrefu, hiyo kwa mujibu wangu ni moja ya vitu vizuri mmoja anaweza kupata, pengine tuseme ni Bahati kama utaweza kuoana na mtu ambaye anakufahamu vizuri, anayekujua kabla ya watu wengine kukujua ambaye huna haja ya kujifanya mtu mwengine ukiwa mbele yake na ambaye anaweza kukuambia ukweli kuliko watu wengine ambao labda wanaogopa kukukwaza au kupoteza kitu flani pale wanapofikiria kukuambia ukweli.
Kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010 Jerry alimpoteza Baba yake mzazi kwenye ajali ya helicopter ambayo pia ilikua imembeba aliyekua Mbunge wa jimbo la Ludewa Marehemu Deo Filikunjombe, Baba yake Jerry ndiye aliyekua akiendesha helicopter hiyo. Yeye pekee ndo anajua kwa undani nini hasa anamiss kutoka kwa Marehemu Mzee wake ambaye kwa mujibu wa Jerry ni watu waliokua karibu sana na anaikumbuka siku ile vizuri tu. Hapa mimi nilitaka kujua jinsi ambayo aliipata habari hii na kwa kumbukumbu zake alinirudisha nyuma kabisa kwa siku moja kabla ya Mzee wake kuanza safari ya kuelekea Ludewa. Jerry pia anakumbuka tu jinsi aliyoamka na kukuta simu nyingi alizopishana nazo wakati amejipumzisha jioni ile. Hii ni moja ya simulizi ambazo zilinitia majonzi sana, na ni maswali ambayo ilibidi yaulizwe kama unavyofahamu.
Jerry anaikumbuka siku ambayo aliamua kugombea Ubunge na kuna simulizi pia humu za Marehemu Rais John Pombe Magufuli na jinsi ambayo alikua anawahi kwenye sehemu ambazo alikua anaenda kufanya kampeni na jinsi pia ambavyo ukichelewa tu kidogo unakuta alishapita, siku zote alikua mbele ya muda na kuna watu wengi tu ambao walipishana sana na misafara yake.
Humu pia tuliongelea maswala ya elimu na utafutaji wa kazi, heshima za kwenye meza na jinsi ambavyo watu wengi huchukulia personal mambo ambayo wana ambiwa kwa faida zao ila kwababu ni mazoea wengine huona kama wanavunjiwa heshima.
Yangu matumaini utaipenda hii session na bila ya shaka utapata kumfahamu vizuri ndugu yetu huyu ambae mwaka jana tu alizua gumzo baada ya kwenda Bungeni kukutana na Kamati ya Maadili akiwa anaburuza begi lilolajaa vitabu na huku vyengine akiwa amevishikilia mkononi. Hili pia tulilizungumzia na alianza kwa kunikumbusha taaluma yake 😀
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Опубликовано:

 

10 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 8   
@evaristmrope
@evaristmrope 2 года назад
My favourite content nilimiss sana huku youtube big up Salama na team nzima ya production
@hemedrashid6525
@hemedrashid6525 2 года назад
Tunamuomba Hussein bashe madam salama
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 года назад
Kwa kweli huyu aletwe.
@kingbet6906
@kingbet6906 Год назад
sogeza mike kwa jerry
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 года назад
Good jobs salama, kazi nzuri sana
@OnlyRuky
@OnlyRuky 2 года назад
Today sauti kidogo mgeni ipo chini
@ibrahimahead6133
@ibrahimahead6133 2 года назад
wakwanzaaaaaa
@bonifacenicholaus5167
@bonifacenicholaus5167 2 года назад
Kipindi kizuri
Далее
Jagadish In Nerechowe | Old Episode | Manorama News
22:27