Тёмный
No video :(

Salama Na MFAUME MFAUME SE6 EP74| TOE - TO - TOE PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 396 тыс.
Просмотров 14 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea shurba kutoka kwake.
Mfaume ni kama wengi wetu ambao tumetokea katika familia za kawaida tu ambayo malengo ya wazazi wetu kwetu ni kuhakikisha unasoma ili uweze kupata kazi nzuri na uje uwasaidie wao na Ndugu zako utakapokua mkubwa, vile vile mambo ya michezo ni kawaida maana kama mtoto unapokua unakua shuleni na mtaani ni lazima kunakua na kucheza, chochote ambacho kiko mbele lakini zaidi huwa ni mpira wa miguu kwa Kaka zetu ingawa sasa dunia imebadilika kiasi, siku hizi hata watoto wa kike kucheza soka ni jambo la kawaida tu na kwa hilo napenda sana.
So kwa Mfaume ni kama kwetu wengine tu, alianza kwa kucheza mpira lakini baadae interest yake ikatoka kutoka kwenye mpira na kuhamia kwenye ngumi, kwa wazazi wake huo ulikua mitihani hasa. Kwa mzazi kukuona mtoto wake akichezea vitasa mara kwa mara haliwezi kuwa jambo la kupokelewa kwa mikono miwili ndani ya nyumba, mtoto anarudi nyumbani kutoka kujifua nae anakua kafuliwa kwelikweli au akijua kwamba una pambano na mwamba flani aliye shindikana ndo hofu inapanda mpaka juu ya dari na inaeleweka kwanini inakua hivyo na kama mpaka sasa hujaelewa au hujaipatia picha basi mwenzetu huna moyo lol.
Alinipa story moja kwenye maogezi yetu haya kuhusu Mama yake, ananiambia kuna wakati alikua na mechi na bondia ambaye alikua anaongea sana, anajisifia na kumtishia sana maisha yake, kwamba atamchakaza vibaya sana tena mbele ya Mama yake, na aliyasema hayo akijua fika Mfaume huwa anaenda na Bi Mkubwa wake kwenye fight zake zote za ndani, ananiambia Mama yake aliogopa sana, alimsihi sana lakini kwa jitihada zake na maguvu ya Allah aliweza kumaliza mchezo wake huo vizuri tu.
Mabondia ni watu ambao wana roho za kipekee sana, unaweza ukamkuta mtu akiwa uliongoni anatoa dozi nzito kwa mpinzani wake ukadhani ni mtu mwenye roho mbaya sana, lakini ukimkuta nje ya ulingo na kwa watu wake utajua ni mtu wa aina nyengine kabisa. Kwa bahati nzuri nna marafiki ambao wanacheza mchezo huu wa boxing ikiwa pamoja na Mfaume mwenyewe, huwa ni watu wakarimu sana na wana mapenzi ya kweli lakini akiwa uliongoni anakua mtu mwengine kabisa, nadhani hiyo ndo tofauti ya masumbwi na michezo mengine.
Yangu matumaini uta enjoy session yetu hii ya mwisho ya msimu huu na mwana huyo humble kutoka kitaa, na pia kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusogeza sehemu.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Опубликовано:

 

5 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 24   
@apti-vp2lu
@apti-vp2lu Год назад
Na nukuu "Siwezi kusema niliumia baada ya kumuumiza matumla hadi ikapelekea yeye kulazwa sababu nitakua namkufuru mungu" maneno ya busara sana nakubali bro.
@abdallahkambangwa7215
@abdallahkambangwa7215 2 месяца назад
jamaa anajua sana kuongea safi sana
@stevenmdabi8637
@stevenmdabi8637 Год назад
salama mungu akulinde kwa ajili yangu
@salmanyangasa1171
@salmanyangasa1171 Год назад
Kwa nidhamu wallah hio uko nayo kweli kabisa Mfaume....MUNGU aendelee kukuinua bro
@emmanuelmbesa2530
@emmanuelmbesa2530 Год назад
Mandoga ajee nae kwenye salamaNa😂😂
@sadcommpalestina4530
@sadcommpalestina4530 Год назад
team nakoz 🔥🔥🔥🔥 mfaume mwamba namkubal sana
@Brama_A37
@Brama_A37 Год назад
Duuh! Kumbe mi ni mzee, Mfaume Mfaume ni mdogo kwangu
@Ram_1893
@Ram_1893 Год назад
Bondia ana mapambano zaidi ya 20 ya Professional kisha anasema ngumi zenye points ni za kichwani pekee 😢😢😢
@rogertuga007
@rogertuga007 Год назад
😂😂😂😂😂Ndio mabondia wetu hao wakubwa na wanaangaliwa kama mfano.
@rogertuga007
@rogertuga007 Год назад
Hata historia ya Mike haijui kama mwamba alikua anaruka mapambano hadi 15 kwa mwaka wakati anaanza Pro. 😂😂😂
@Ram_1893
@Ram_1893 Год назад
@@rogertuga007 Badala ya Kutolea mfano wa mabondia wa miaka hii ya karibuni anataja mfano wa bondia wa zamani ambaye hafahamu hata historia yake 😆😆😆
@AliBumaye-xn4jc
@AliBumaye-xn4jc Год назад
Bonge ya interview salama💪💪
@Fun-ef3ro
@Fun-ef3ro Год назад
ingekua poa sana kama next interview ukafanya na BABA T, kuna madini mengi sana anayo
@ngasamotv358
@ngasamotv358 Год назад
Bravo big brother
@mussasuleiman6136
@mussasuleiman6136 Год назад
salama fanya interview na Fei toto
@didakalaule7840
@didakalaule7840 Год назад
❤❤❤❤
@hamidyngata9014
@hamidyngata9014 8 месяцев назад
29 miaka du...
@GivenTobago
@GivenTobago Год назад
Smart boxer of all time
@mkanulamajid500
@mkanulamajid500 7 месяцев назад
Bondia wa mananasi
@mukirerichard5265
@mukirerichard5265 Год назад
We support you my big bro
@njegeledaniel3446
@njegeledaniel3446 Год назад
Tunaomba episodes zijazo utukutanishe na @mwais mtu mbad
@user-rk1mo7yl8q
@user-rk1mo7yl8q Год назад
NDo Nan hajafikia stage yakuja hapa
@mbwanamohamed9878
@mbwanamohamed9878 Год назад
Salama mlete mjomba mpoto mezani tafadhali
@kayeyemapesa7533
@kayeyemapesa7533 Год назад
Champ..👍
Далее
У ГОРДЕЯ ПОЖАР в ОФИСЕ!
01:01
Просмотров 4,5 млн
INTERVIEW SHOW  BABA LEVO  at COCONUT fm ..ZMOTION
7:05