Тёмный

Salama Na ALLYBEE SE6 EP72| KULE NI KULE... PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 67 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika.
Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday 😄). So wakati ananiambia nami tayari nilikua nishamuona, basi mengine yakaendelea kwenye meza yetu adhimu.
Story ya maisha yake Ndugu yetu huyu ni ya mateso mengi sana, ila kwa sasa na hata pengine mwanzo kwa adha zote hizo tunamshukuru Allah kwa hayo yote maana hayo ndo yameleta hasira za yeye kutaka zaidi, kuomba zaidi na kufanyia kazi zaidi yote ambayo anayo leo. Ally anakumbuka jinsi alivyofika Dar es Salaam mara ya kwanza na pia amenihadithia adha ya kutokua na sehemu ya kukaa hasa unapokua umekuja mjini mara ya kwanza. Alinifanya nijiulize maswali mengi sana mimi kama binadamu wa kawaida kabisa, au ambaye Mwenyezi kanibariki kwa mengi zaidi ya wengine, nini nafanya kuwasaidia ambao nawaona barabarani? Au ambao hawana uwezo wa kunifikia lakini wana uhitaji? Kanifundisha kuhusu kutochukulia maisha au nafasi ambazo tunazo kwenye maisha yetu kwamba ni kawaida tu. Ki ukweli kila ambacho tunacho kwenye maisha yetu TUNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU AMBAYE AMETUPA. Ila pia inabidi mara moja moja tujipigie makofi kwa mbali ambapo tumetoka na ambapo tumefika lakini zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu azidi kutuimarisha na kutufungulia milango ya Kheri, ZAIDI.
Niamini mimi nikikuambia kuhusu kutoa, kwamba kutoa ni raha zaidi kuliko kupokea ingawa wengi wetu tunapenda zaidi kupokea, ukitaka kujua hilo jaribu kwa kuanza kumpa hata mtu zawadi ndogo tu, hata pipi ambayo alikua hategemei kama utampa au utakumbuka, sura yake itakueleza mengi hata kama yeye ataamua asikuambie kwasababu zake zozote tu. Ally alisaidiwa na mtu ambaye hata walikua hawafahamiani na kuamua kumpa hifadhi katika sehemu ambayo yeye alikua anakaa. Pengine yeye alipofanya wala hakujua kama Ndugu Ally atakuja kuwa mmoja wa ma DJ HODARI na Hyper Man bora ambae nchi hii imewahi kuona.
Leo ningependa tujifunze kuhusu hilo, kuhusu kuwa kind, kuhusu kuwapa watu nafasi kwenye maisha yetu na kutosubiri malipo kutoka kwao maana pengine yanaweza yasije lakini wewe tayari unakua ushamaliza kazi yako.
Yangu matumaini story ya DJ Ally Bee itakua na impact kwenye maisha yako kama ambavyo imekua kwenye maisha yangu.
Enjoy and stay BLESSED.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

18 июн 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 93   
@salmanyangasa1171
@salmanyangasa1171 Год назад
Dah!! Huyu jamaa anaongea ya maana Sana na anaonekana ni mwenye heshma na utu tofauti na umuoneakano wake katika kazi yake! MUNGU AKUBARIKI SANA bro
@RoolkayDrakedrizy-fg9sc
@RoolkayDrakedrizy-fg9sc Год назад
Hii interview ina kupa moyo kwenye kupambana na kuamini unacho kiamini 👊✊
@rhodajackson2213
@rhodajackson2213 Год назад
Sahihi kabisa , naweza toa ushuhuda Kaka ! Wazazi ni kila kitu, R.I.P Mama
@lastsimbatv1497
@lastsimbatv1497 Год назад
Natamanii ujihoji ww salama tujue lifestyle yakoo
@kisianganijob1068
@kisianganijob1068 Год назад
Very inspiring indeed. As a human being we ain't limited at all.
@g2c477
@g2c477 Год назад
A very big fan of Salama na... From Nairobi. Had waited for this interview, finally I get a chance to watch this East African Star. I watch this show with my Tanzanian wife as well huku Pia nikijifunza Kiswahili sanifu kwenye hii show sanaaaaaa tena mno. Salama you're a legendary interviewer, a big fan!🔥!
@alijafar9098
@alijafar9098 Год назад
Me too...Salama is just awesome! Mob love from 🇰🇪
@esterdoriye8377
@esterdoriye8377 Год назад
Ana lafudhi na swaga za chuga/moshi
@zumbeshauri8114
@zumbeshauri8114 Год назад
Allyb afadhari wewe ni lafiki alikukataa mimi ndugu yangu kabisa ndio alinitolea mbavuni
@aldegondejanuary5228
@aldegondejanuary5228 Год назад
🔥🔥🔥namkubalii huyu kaka history yake huwa inanipaa nguvu
@ukhutfatumah1154
@ukhutfatumah1154 10 месяцев назад
Mama mzaramo baba mpare umenisha sna mwanang
@moseshebrews9089
@moseshebrews9089 Год назад
YahstoneTown is a true classroom
@user-fh8fv9dz2b
@user-fh8fv9dz2b Год назад
Daah!! Ur very humble bro ally
@parfaitkalemela8733
@parfaitkalemela8733 Год назад
Salam when u will invite Harmonize I will appreciate
@bakarilimachinga6193
@bakarilimachinga6193 Год назад
Daah yaan hii interview imenifundisha nijuwe kuwa bongo usione watu wametoboa kuna miziki nyuma watu wanapitia hatarii 😅😂😂😂😂
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Mashallah, umeongea point brother.
@lastsimbatv1497
@lastsimbatv1497 Год назад
Salam umeua san namkubar san huyu jamaa kwer hvi vinatokea ila binfsi siwez kuleta dem ghet nkiwa na mshikajii siweziii kbsaa
@360newssource3
@360newssource3 Год назад
Show love to Salama from +254🇰🇪
@barakachalres9316
@barakachalres9316 Год назад
Ajeee
@mickthomas-lh1fs
@mickthomas-lh1fs Год назад
Athumani tajiri umetisha sana bonge moja la yastone town.
@rahmaawadh1695
@rahmaawadh1695 Год назад
Umeongea point nimeipenda kua kuna fadhira kubwa pindi sana kwa wazazi pindi unawafanyia mema
@tiffanymo9453
@tiffanymo9453 Год назад
Big up to you salama,and Am so proud of you Ally B keep it up bro.😍
@ibrahimurichard377
@ibrahimurichard377 Год назад
Very inspiring Salama tunaomba part 2 isikawie
@user-jc7mi4nf4i
@user-jc7mi4nf4i Год назад
salama Queen interviewer
@MkenyaN
@MkenyaN Год назад
17:25 hapo kweli kabisa. Story of my life
@GivenTobago
@GivenTobago Год назад
Ali B ni mjasiri
@rashidaliy5635
@rashidaliy5635 Год назад
Nasemajeee kula nyama nyamaza ww✌️
@podahsalim2296
@podahsalim2296 Год назад
Nasemajee!! Nasemajeee😂😂
@hudehude7501
@hudehude7501 Год назад
Kichaa ndani ya nyumba
@OMANOman-qc1lm
@OMANOman-qc1lm Год назад
siku zote tharau mbaya ukisha pata shida ndo binadam unarud chini na kujifunza umejifunza kuheshim watu sasa hivi sasa umekua na heshima vizur nitham ndo kila kitu ukiwa maskini au tajir heshima ndo kila kitu
@user-zt7de9hv5k
@user-zt7de9hv5k Год назад
Kaka 😂😂 appendix umetisha unatengenza box za nyaja
@bainolatino3412
@bainolatino3412 Год назад
Pesa nyingi Kelele kidogo
@johnriwa2854
@johnriwa2854 11 месяцев назад
Asumanii, Salama pure talents
@mnyamwezijuma1140
@mnyamwezijuma1140 Год назад
Asumoney. 😅 asumaniiii 😅😂
@shaffycjg536
@shaffycjg536 Год назад
Nimesubir sana atimae asuman
@godfreymiho4927
@godfreymiho4927 Год назад
🔥🔥✨🎵🎶
@Views-mf8ir
@Views-mf8ir Год назад
Wakazie ivo ivo mtu wangu ..
@suleshbinmkoba1194
@suleshbinmkoba1194 Год назад
Big up broo😍
@Yanga_tv
@Yanga_tv Год назад
Msasani home 🏠 welcome again brother
@muzafarsharif9465
@muzafarsharif9465 Год назад
salama I luv u ❤
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
Asuman💃👌🏽
@mbwanadavid4371
@mbwanadavid4371 Год назад
Mimi Ni shabiki mkubwa wa Salama tangu enzi za mkasi mpaka Sasa Salama na... Kama unasoma comments za sisi mashabiki zako mbona hatuoni feedback coz nilieomba tangu kipindi kilipokua pale EATV. Naomba umlete ALI CHOKI mzee wa Farasi pliz🙏🙏🙏
@rashdiyange7758
@rashdiyange7758 Год назад
Mie nacho mpendea uyu jamaa nimsafi mpaka laha bigup baba sumaniiiiiiiii🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣👊👊👊👊👊👊
@ukhutfatumah1154
@ukhutfatumah1154 10 месяцев назад
Auna baya DJ ALLYB PAMBANA BABA UMEASO SNA MUDA WAKO HUUU TUMIA BABA
@Goshithedon95
@Goshithedon95 Год назад
This is the reality show i loved the most apart from lil ommy podcast #big up da salama
@abuuarushadawg7158
@abuuarushadawg7158 9 месяцев назад
He used to be big in Arusha back in th days
@cooler3263
@cooler3263 Год назад
Nakubali sana
@rajabyahya8942
@rajabyahya8942 Год назад
First to comment
@whizzycindy1476
@whizzycindy1476 Год назад
Tunaomba next awe wema sepetu jmn
@mosesmaryz3535
@mosesmaryz3535 Год назад
Second to comment
@vonniemarry2680
@vonniemarry2680 Год назад
The guy is being really
@daggerslick
@daggerslick Год назад
Wakwanza likes zanguu😊😢
@shamsasoud2989
@shamsasoud2989 Год назад
Mnakera mbwa ww
@daggerslick
@daggerslick Год назад
@@shamsasoud2989 😂😂😂😂naww unakera shenzii kbsa
@idmtech9868
@idmtech9868 Год назад
You get it
@justinlucas4268
@justinlucas4268 Год назад
Izo like zitakufikisha wap sas
@user-zt7de9hv5k
@user-zt7de9hv5k Год назад
Nyanya
@lucasezekiel9782
@lucasezekiel9782 Год назад
💛💛💛
@rasjamal9854
@rasjamal9854 Год назад
❤👊👊
@TheUraniumz
@TheUraniumz Год назад
Ally B 🙏
@abbashussein-hz4dr
@abbashussein-hz4dr Год назад
Jamaa tumesoma shule moja mawenzi primary school pale stand ya bus tunatazamana darsa moja alikua anatuita fidodido tuko mapacha hasan na husen mafidodido ndo majina yetu dah mwamba km unanikumbuka big up sana unamkumbuka mwalimu nkya 😂😂😂😂
@user-zg9zq6so4r
@user-zg9zq6so4r Месяц назад
Acha ushamba
@goodlucktemu3149
@goodlucktemu3149 5 месяцев назад
uyu ameiedit ii story nsikilize mimi, Aliyefanikiwa awezi kukupa full story yake.
@ezekielhamis887
@ezekielhamis887 Год назад
Wanangu wa tpc
@najmaahmed3840
@najmaahmed3840 Год назад
Allyy b
@MultiKelvin1994
@MultiKelvin1994 Год назад
14:49😅
@MusaMargwe-ol9iu
@MusaMargwe-ol9iu 11 месяцев назад
Umegundua nn hapo huyo msela ni Mchugastan
@vonniemarry2680
@vonniemarry2680 Год назад
🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
@winfridangoloke1916
@winfridangoloke1916 Год назад
Bwana said kokote uliko nakuaalimu😂😂😂😂😂😂😂
@sofiaissamkandama2742
@sofiaissamkandama2742 Год назад
Kula nyama nyamaza kuna kitu anatuficha kuhusu mafanikio yake
@edwardkasubi5135
@edwardkasubi5135 Год назад
Tuambie wewe
@user-ou4nx5om2o
@user-ou4nx5om2o 11 месяцев назад
We ni ally Kurwa Kama sikosei
@ashurashabani7249
@ashurashabani7249 Год назад
Athumaniiiii😊😅🤗
@asyafatma532
@asyafatma532 Год назад
😂😂😂😂😂😂😂
@Boaz22
@Boaz22 Год назад
Kuji adjusti adjusti ndo nini, watangazaji kuchanganya kiingereza na kiswahili inakera hamjui tuu..mara inspiration yako,mxiewwwww
@joycemfuru4752
@joycemfuru4752 Год назад
Wivu tu na shida zinakusumbua kalale hukoo
@zagadat1129
@zagadat1129 Год назад
Ivi 2010 boda boda zilikuwepo??
@sophishebby6274
@sophishebby6274 Год назад
Yah boda zilianza 2007
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 Год назад
Yap
@rizikiabdalla2501
@rizikiabdalla2501 Год назад
Zilikuwepo my mm mwenye nilikuwa na boda boda wangu nikiumwa ananipeleka hospital nikiwa dodoma ila ndioo nilikuwa zinaaazaaaa
@fahadfahmy
@fahadfahmy Год назад
Inasikitisha Mzee wako ni Imamu na wewe umeangukia kua Dj
@abedomar5183
@abedomar5183 Год назад
Huyu Dj nae mbembwe nyingi Hana lolote anaongea sana
@edwardkasubi5135
@edwardkasubi5135 Год назад
Heeeeeeeeeeee,,,,,roho bhaaana
@neemaberny3598
@neemaberny3598 Год назад
Unateseka ukiwa wp na wivu😂
@thomasmassawe5847
@thomasmassawe5847 Год назад
Acha makasiriko
@maestro1902
@maestro1902 Год назад
We ndo said nin😂😂😂
@bakarilimachinga6193
@bakarilimachinga6193 Год назад
Kuna watu Wana nongwa 😂😂😂
@user-zt7de9hv5k
@user-zt7de9hv5k Год назад
Nyanya
@ecostats51
@ecostats51 Год назад
Nasemaje, kula nyama nyamaza. 😂😂😂👏👏
@user-zt7de9hv5k
@user-zt7de9hv5k Год назад
Nyanya
Далее
Каха и суп
00:39
Просмотров 1,2 млн
Sheria Ngowi Aifungua Shajara Yake Kwa Babie Kabae
55:41
Happy 4th of July 😂
0:12
Просмотров 30 млн