Mhe.Rais ni kweli amekuwa akiteu pamoja na kubadilisha Mawaziri mara Kwa mara,hata pia Vioñgozi wengine. Mimi nashindwa kuielewa kwanini uteuzi umekuwa wa mara Kwa mara. Hii inaashiria kuwa Washauri wake wamekuwa wakimletea majina ya watu wasio na sifa zinazoendana na Wizara husika! Yawezekana kabisa Washauri hao humpelekea majina ya jamaa zao,jirani zao,kabila zao,Kanda zao;hata kama hawana vigezo sahihi. Pia rushwa yawezekana inatumika ktk kupata majina ya wateule-watarajiwa. Hivyo,Wateule hao baada ya kupewa Wizara au Nafasi husika,wanaonekana kushindwa kumudu madaraka Yao mapya! Hivyo kupelekea Mhe.Rais atengue uteuzi huo,na kuteua wengine Tena. Hata hivyo,wale waliotenguliwa Kwa kukosa vigezo stahiki ,Mhe.Rais huwahamisha kwenda sehemu/Wizara nyingine tu;"Badala ya Kuwafukuza kabisa! Hivyo ,wateule-tenguliwa hao tayari wanakuwa wamepanda ngazi kiulaini tu. Ni vyema kabisa Mhe.Rais achunguze sana majina ya wateule-watarajiwa kabla ya kuwateua! Vinginevyo,washauri wake wataendelea kutumia mwanya huo kama daraja la kupitia kupata nafasi za juu ktk ngazi ya Taifa. Isitoshe,ni gharama kubwa kufanya uteuzi wa mara Kwa mara Kwa sababu Vioñgozi wengi mbalimbali huwa wanahudhuria ktk hafla hiyo. Hivyo Taifa linalazimika kutumia fedha nyingi ktk shughuli hiyo,badala ya fedha hizo kuelekezwa ktk huduma mbalimbali za jamii,km matundu ya vyoo shuleni,vyumba vya madarasa,nyumba za Waalimu,madawa hospitalini nk. Ni Bora kabisa nafasi zinapo tokea basi zitangazwe ili wenye sifa sahihi waweze kuomba,badala ya kufanyika teuzi ambazo hazina tija,badala yake zinapelekea Mhe.Rais kulazimika kuteua Tena Ni Mimi Ally Daudi Ngoyeji wa Itilima,Kishapu Shinyanga.
Haya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yamekuwa yanafanywa kila mara.Jambo hili linatusaidia kwa kiasi gani? Matatizo yetu makubwa tunayoyaona yamebadilika? Matatizo ya ajira za vijana,ardhi za wamasai,muungano,utawala bora, usalama wa raia,n.k yamepatiwa ufumbuzi?
Nilitegemea kusikia habari, lakini hii sio habari,ni historia iliyopita zamani, na kupambwa kwa maneno mengi, na mbwembwe nyingi. Kwa mtindo huu, enyi waandishi wa habari, mnatupeleka wapi?