Тёмный

WACHIMBAJI WA DHAHABU CHUNYA WABURUZANA MAHAKAMANI 

MbeyaYetuOnlineTV
Подписаться 234 тыс.
Просмотров 900
50% 1

Mashauri matatu yalizofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa Hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza kuhusiana na mgogoro wa Kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumain Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.
Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya na Wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mwampenza akitetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi akisaidiwa na Wakili Irene Mwakyusa.
Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na Wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Wakili Massawe amempatia Wakili Mwabukusi Hati ya dharula na nakala kuwasilishwa Mahakamani na Wakili Mwabukusi naye kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.
Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi mei 13,2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.
Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayodaiwa katika Mahakama hiyo kupitia Hati ya dharura kuwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.

Опубликовано:

 

13 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 4   
@ZawadiMwampashi-dg9bq
@ZawadiMwampashi-dg9bq 4 месяца назад
Watayamaliza mafagali wawil
@ZawadiMwampashi-dg9bq
@ZawadiMwampashi-dg9bq 4 месяца назад
Mafahali wawil watayamaliza
@AmonCosmas-kt5ot
@AmonCosmas-kt5ot 4 месяца назад
achimbe yoyote ambae shelia inamluusu maana wote niwanyumban😅 bwana mdimi msaada wake kwa chunya unaonekana na luka unaonekana japokua nuna mmoja anamsaada zaid kuliko mwenzake
@emmanueledger8770
@emmanueledger8770 4 месяца назад
KWA kwetu ss luka ndo anamsaada zaid ya mdimi
Далее
TAZAMA BASHE, MPINA WALIVYOKUTANA USO KWA USO
10:18
Просмотров 24 тыс.
Почему не Попал?!
00:15
Просмотров 67 тыс.