Тёмный

WANAFUNZI 400 WAHITIMU CHUO CHA WAGANGA WA JADI, MBUNGE AFUNGUKA “HAKUNA MILA POTOFU NI UONGO” 

Millard Ayo
Подписаться 5 млн
Просмотров 60 тыс.
50% 1

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amesema sasa ni wakati sahihi kwa serikali kuweka somo linalofundisha Mila na Desturi za kitanzania mashuleni ili Watoto wajue na kufahamu mambo yanayohusu jamii yao.
Akisisitiza kuhusu jambo hilo Kishimba amesema kumekuwa na tamaduni za kigeni ambazo Watoto wamekuwa wakikuwa na kuzikuta ambazo zinapelekea kuharibu makuzi ya Watoto hasa wanaokulia mjini na kuwafanya kuamini mambo ambayo sio ya kwao na kupelekea kuwepo kwa wagonjwa wa Afya ya Akili kutokana na msongo wa mawazo
Kishimba amesema hayo katika mahafari ya kwanza Tanzania ya chuo cha waganga wa Jadi cha Modesta kilichopo Kagongwa wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga ambapo wanafunzi Zaidi ya 400 wamehitimu mafunzo ya dawa asili ya Modesta baada ya kusoma kwa mwaka mmoja na watu Zaidi ya 1000 wamehudhuria mahafari hayo “Mjini wanaugua ugonjwa wa msongo wa mawazo mbona kijijini hawaugui huo msongo wa mawazo kwanini tusiende kwao kuwauliza lazima na sisi watu wa Mila tujitetee kwasababu Maisha yetu ni mazuri Zaidi ila tunashambuliwa mno kuwa ni mila Potofu, hapa hakuna mila potofu ni uongo kama ingekuwa ni mila potofu Ng’ombe angelala nje sisi tunalala ndani mbona sisi wa mjini wajuaji na tunamageti na ndani hakuna chakula” mbunge Kishimba

Опубликовано:

 

2 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 344   
Далее
Teeth gadget every dentist should have 😬
00:20
Просмотров 1,6 млн