Тёмный
No video :(

Dizasta Vina - Hatia VI 

Dizasta Vina
Подписаться 54 тыс.
Просмотров 55 тыс.
50% 1

Official lyric video of Dizasta Vina perfoming Hatia VI, Marking a 3rd release Off the album A father figure
Stream/download Hatia VI
Mdundo - mdundo.com/son...
Boomplay - www.boomplay.c...
Apple Music - / hatia-vi-single
Audiomack - audiomack.com/...
Spotify - open.spotify.c...
Dizasta Vina on socials
Instagram - / dizastavina
Twitter - / dizastavina
Facebook - / dizastavina07
Lyrics
Salamu baba mi mwanao
Naandika waraka kwa maana hutaki vikao
Nahitaji majibu nikihisi ni haki yangu
Najisikia vibaya kusikia unaishi na sina ngao
Nimeshika kalamu haya maandiko
Yametoka mahala timamu palipo wito
Sijatumwa na wenzangu hii ni akili yangu mwenyewe
Waraka huu ni salamu zangu za mwisho
Nina akili najua mambo yanapokuwa mrama
Natambua uhalisia nazitambua njama
Pengine nitachokisema kitazua laana
Nitaibeba lawama kwa kujifanya najua sana
Ndugu zangu wanachosema sisawiri
Mpaka wanahisi nimeanza kuchezwa na akili
Hata wakitaka kunitenga sibadili
Ulinitenga jana siogopi kutengwa mara mbili baba
Majirani wanatamba kukuongelea
Wakisema sina baba na kazi ya kukusemea
Na ukweli ni kwamba ni utata sana kukutetea
Maana shida ilinibana na baba haukutokea je
Utachukia nikiegemea penye power
Au utanipa hatia mikono michafu niende nawa
Nipo mbele yako kamwe siigizi uwepo kama wewe
Basi jibu kero zangu twende sawa
Juzi nilikuhonga maua, Jana nikakuhonga na tena
Subira gani isiyo na heri shaabash
Nimechoka kuchomwa na jua
Jionyeshe leo nimechoka barua
Nimechoka barua
Barua zako zinahubiri ushindi
Kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki
Na cha ajabu maadui ni wa kurithi
Chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithi
Njoo ulee wagonjwa ndo' uongee kuhusu upendo
Tuvae bendera moja ndio uongee kuhusu uzalendo
Msamehe aliyekufanya uondoke ndo' uendeelee
Kuhubiri kutubu kuhifadhi na kusamehe
Jenga daraja baba mahusiano yanavunjika
Hamna faraja huoni wanao wamekaza ndita
Jenga imani tena kwa wote waliogadhibika
Jenga kama ambavyo uliijenga hii nyumba kwa siku sita
Haukuja tulipopita kwenye
Miaka 400 ya utumwa njaa maradhi vita giza nene
Nipe sababu moja vipi nikujali vipi nikupende
Sababu moja tu kukusikiliza wewe
Nyumba uliyotupa ina twiga ina ndovu
Majirani warembo wenye figa na vitovu
Vinavutia, kuna dhahabu kadhalika
Zinatutajirisha ila zinafanya tuwe waovu
Huu uchafu atatetea wakili gani
Siri ipi na asili zetu hazilingani
Japo akili mali sio siri asili ghali
Tunamwagana damu kugombea rasilimali
Tunaisha kwa wivu wetu
Tunasita kwa uvivu wetu
Tunazikwa na mbinu zetu
Tunapikwa na kinu chetu
Tunasita kushika insha
Tunapitwa na wapita njia
Umoja unavunjika huku
Tumeshikwa na simu zetu
Sina tofauti nna watoto kama wewe
Napata changamoto kama wewe
Kama soja kwa ajili yao napambana naposhindwa
Tunateseka pamoja Kwani sina roho ndogo kama wewe
Asante kwa ulezi dhanifu
Asante kwa kuniandikia sheria za kishenzi
Kwenye pegi nadhifu asante kwa kuniacha stendi
Nikisubiri mapenzi ya ahadi nakesha nikienzi wasifu
Asante kwakuwa mbali nami
Kiasi nina shaka kuwa haujui nina hali gani
Umeacha barua ndefu ambayo sijui kama yako
Au ya kufoji na bado inahitaji mkalimani
Ona Napanga mipango ya kijinga
Ona naghafirika nafanya uliyopinga
Ona napinda napika chuki wenzangu
Wenye nyumba ndinga maana mimi ngano tu inanishinda
Huko mbali umejitenga nashanga
Haujui kinachosemwa na jamaa
Haujui usafi ni ndoto, ndoto iliyotengwa na ridhaa
Haujui ni ngumu sana kuwa mwema ukiwa na njaa
Haujui kuhusu adha za dunia
Haujui kero maana maudhi yalipokupata ukakimbia
Haujui kuhusu kifo na magonjwa haujui kuhusu
Insha na maandiko haziwezi tibu hivi vidonda
Ndugu zangu umewajenga kwa vpaji
Wapo kadhaa umewapa pesa za mitaji
Wengine warembo wenye vyeo wenye hadhi
Sisi tusio na hali tulalamike kunyimwa haki
Imechafuka taswira inaenda slow focus
Pengine its all bogus
Pengine I'm mad
And I'm talking to my own conscious
Labda haupo ni hadithi tu
Na kama ulifikia kifo ufalme umefika mwisho
Haurudi tena so nawaza
Lini utakuwa mwisho wa uhanithi huu
Uzazi sio simple but I still care
Nina watoto shida zipo and I'm still here
Matatizo yanapokaba kwenye shingo sikimbii
Napambana mpaka mwisho like a real man
Sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo
SikujuI sura maana hauna picha Google
Nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma
bakshishi niwe ninajua kuwa zinafika huko
Wenye majoho rangi nyeupe na dhahabu
Wana barua zako za tafsiri za kiarabu
Wanasema wanakujua kuliko ninavyokujua
Nikiwatilia shaka wananiita mwanaharamu
Je ni kweli uliwapa uwakilishi
Ni ngumu kuwasadiki hasa ukiwadadisi
Kama wanaongea uhalisi au wanachonga sera
Sometimes hawafundishi wananiomba hela
Thibitisha hizi hifadhi si uwongo
Uliowaacha wana nishani za,,,,
read full lyrics - genius.com/Diz...

Опубликовано:

 

5 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 622   
@dizastavinafanaccount
@dizastavinafanaccount 8 месяцев назад
the talent immense
@alphoncesamwel6973
@alphoncesamwel6973 8 месяцев назад
"Matatizo yavavokaba shingo skimbii ....Napambana mpaka mwisho like realMen" ka imekutia hamasa basi like hapa twende sawa na Dizasta Vina as real Men.
@emmanuelpius6387
@emmanuelpius6387 8 месяцев назад
Nimesikiliza mara kadhaa nimejifunza mambo mawili, mara ya kwanza nilijua baba anayeongelewa ni baba mzazi ambaye alitelekeza familia yake akiwemo mtoto wake huyu ambaye ameamua kumuweka wazi kuwa hamtaki tena, Baadae nimegundua aliyezungumziwa ni Mungu baba ambaye ameumba dunia na akawatelekeza watoto wake wanashambuliwa na matatizo kama umasikini na njaa vinavyopelekeq chuki na maovu, anasema UNAJUA NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA. Mungu ameacha wosia ambao haujulikani ni wa Mungu kweli au ni wa kufoji ? hapo anamanisha BIBLIA
@Njokaa
@Njokaa 8 месяцев назад
Rudia tena kusikiliza broo hajamaanisha Mungu
@mingajohn6518
@mingajohn6518 8 месяцев назад
​@@Njokaawe ndo umepotea kabisa rud ukasikilize vzuri,,huyo mwamba kaongea sahihi
@dizastavina
@dizastavina 8 месяцев назад
Lipia copy yako ya album ya #AFF sasa. Album itatumwa kwa EMAIL, WHATSAPP au TELEGRAM. Tuma 10,000tzs /700ksh kwenda MPESA 0762 158 871 au TIGO PESA 0655 696 811 (jina EDGER MWAIPETA) kisha tuma sms ya muamala wako kwa namba uliyolipia. Usisahau kutuma Email au namba yako ya WhatsApp kwa ajili ya kupokea album. Let's go #DZSTVN
@Wayatz
@Wayatz 8 месяцев назад
Kutoka Panorama🎉🎉
@KelvinEmersonSteven
@KelvinEmersonSteven 8 месяцев назад
Pamoja sana
@Goalscorer12
@Goalscorer12 8 месяцев назад
Yeeesiir ❤
@nickyvanich6214
@nickyvanich6214 8 месяцев назад
Deal done, gv us music bro
@geombaji
@geombaji 8 месяцев назад
Wazi
@freakboy1804
@freakboy1804 8 месяцев назад
2 Tim 2:13 SUV Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. Mungu aturehemu sisi viumbe wake tusio stahili hata kulitaja jina lake. Utukufu wako Uishi Milele na Milele Amina
@dizastavinafanaccount
@dizastavinafanaccount 2 месяца назад
Meen shut up
@davabackup7767
@davabackup7767 8 месяцев назад
Kumamake hadi nimeogopa ila sio kwa ubaya bali kwa fact ulizoongea asee ziko on point daah yani kifupi am speechless mwamba sina la kukulaumu pia sina la kumlaumu mungu Dizasta wewe ni zaid ya fire ama moto wa jahannamu 🔥🔥🔥
@moudyboe
@moudyboe 8 месяцев назад
be careful what you saying next broo 😅😅😅
@lucasgodfrey6976
@lucasgodfrey6976 8 месяцев назад
Fikra zilizoandikwa hapa hazipaswi kuhukumiwa kama utashi wako haujauacha iwe huru. Kwanza ruhusu utashi wako upokee hizi frikra huru alaf usione hvyo vitu unavyoviona vya thaman kila mmoja anaona hivyo. Hii ni kubwa sana inahitaji mtu mwenye moyo huru na akili huru
@TanflixLLC
@TanflixLLC 4 месяца назад
Haswaa
@DeLaP2908
@DeLaP2908 8 месяцев назад
Uumbaji ni mara moja tu. Muumbaji huwa hageuki nyuma. Akishaumba mara moja anaweka vimelea vya usahihi katika mahesabu yake na kuacha utashi na chembe ya usahihi katika viumbe na miimili ya uumbaji na kila kiumbe kujiendesha chenyewe. Muumbaji ndio uumbaji wenyewe, Muumbaji sio mtu, sio baba, sio mama, wala sio mtoto. Muumbaji ni nishati huru, nguvu kubwa uliyopo katika kila kitu. Muumbaji hahusiki na dini wala siasa, hahusiki na mifumo yoyote dhalimu ya kibinadamu. Muumbaji anaona na haoni, Muumbaji yupo na hayupo. Muumbaji ni kila tunachokiona na tusichokiona. uumbaji ni fumbo. Muumbaji hahukumiwi wala hahukumu. So Hakuna hukumu bali kujihukumu wenyewe. Ila kuna hatia. HATIA IS REAL. and the writer is confronting his own consciousness, na mwandishi pia hana hatia. OVER!!
@AhmedNadhiru-qe5pl
@AhmedNadhiru-qe5pl 8 месяцев назад
Hii hatia no ngap
@terminal_tz
@terminal_tz 8 месяцев назад
Mim nmekuelewa thanks...
@LambeDon_
@LambeDon_ 8 месяцев назад
​@@AhmedNadhiru-qe5pl 6
@d.i.cthedon5709
@d.i.cthedon5709 8 месяцев назад
👏👏👏👏
@mingajohn6518
@mingajohn6518 8 месяцев назад
Noma jamaa kaandika haswa
@Njokaa
@Njokaa 8 месяцев назад
Kabla sijaskiza nacomment kwanza coz najua Vina anajua sana
@user-ih6hk5nh7v
@user-ih6hk5nh7v 8 месяцев назад
Dizasta vina ni next level bongo nzima hakuna huyu jamaa n hatar ni umeme mkubwa
@ussiussi3413
@ussiussi3413 8 месяцев назад
Good artistic work. Ni ishu ya kugusa existence (uwepo) and inexistence (kutokuwepo) kwa Mungu yaani, imani ya kuamini yupo na yanayofanyika yote ni kwamba kwanini hatuoni reaction yake physically, halafu imani ya kuamini hayupo na yanayofanyika yote ujinga tu wa hii dunia. Ukiwa una akili nzuri utaelewa hapo kwenye uwepo wake amegusa imani hasa ya Kiislamu(wenye majoho meupe na tafsiri za kiarabu) na hapo anapozungumzia inexistence (kutokuwepo kwa Mungu) anazungumzia imani ya wale "Wasioamini Mungu"(ATHEISTS), hapa kawagusa sana Jamaa zetu ambao wengi ndio Matajiri wa dunia(Mabilionea na watu maarufu) walipoegemea na ndipo wimbo ulipobeba maudhui yake makubwa na hoja nyingi alizozizungumza humu ni za hawa ATHEISTS. Skiza vzuri wimbo then, ukielewa ninachokwwmbia like hapa.
@Macaveli_tz
@Macaveli_tz 8 месяцев назад
Sikiliza tena huu wimbo kwa umakini,,, upo nje ya theme Kuna code bado hujazipata vzr ili kuelewa DZST anaongea na nani hasa kwenye huu wimbo
@ussiussi3413
@ussiussi3413 8 месяцев назад
@@Macaveli_tz Bado hujataka kuelewa Bro, ngoja nikupe mwanga kidogo labda utafungua bongo yako, ni hivi; "HATIA" ni hali ya kushuku au kubaini uwepo wa makosa/ dhambi yaliyotendeka au kutokuwepo, yeye Msanii ame-act kama ni mtoto anayejaribu kuteta au kulalama uwepo wa Baba yake au kutokuwepo kwake wakati yeye (Msanii) yupo physically kwa maana anaonekana na mhitaji wa mambo lakini mahitaji hayo huyapata kwa shida bila uwepo wa kuonekana kwa Baba yake kwa lengo la msaada wa wazi so, ww unadhani ni Baba gani anayezungumzwa!!!??? Hilo moja, lakini pia unapaswa kutambua kuwa, yeye hana uhakika na mafundisho juu ya maisha yake na imani yatokanayo na watoto wenzake(Mitume, Maaskofu, Mapadri, Makasisi, Walimu, Masheikh, watu wa kawaida kwa ujumla waliopita zamanj na wa sasa) hapo alimgusa Yesu kama ni mtoto kwa maana alikimbia baada ya dhiki kwa maana hajarudi hadi sasa na hajui kama amekwenda mazina bila kurudi tena ulimwenguni, tatu ni kwamba yeye Msanii anajaribu kutaja Imani 3 ambazo ni Uislamu kwa maana pale alipotaja waliojivisha majoho meupe na wenye kumtafsiri Mungu kwa lugha ya kiarabu, imani ya pili ya kikrosto pale aliposema Wakivutana kwenye majadiliano na wakati mwengine humuomba hela(sadaka na zaka makanisani) kwa maana kuna usanii, lakini pia imani ya 3 ni hiyo aliyoibeba yeye zaidi kwenye wimbo na kuwekeza mawazo yake mbayo ni imani isiyoamini Mungu (ATHEISM). Bro nadhani kichwa chako bado kina akili changa, pull up your socks utaelewa ukiwa muda umeshakupita kitambo.
@ommygraphics4355
@ommygraphics4355 8 месяцев назад
Fact
@rusellcleopas1282
@rusellcleopas1282 8 месяцев назад
Umeenda mle mle ninamofikilia mfano hii verse "sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo , sikujui sura maana hauna picha google, nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma bakishishi niwe najua kuwa zinafika huko" kwa nilivyoelewa anaongelea swala la kutoa sadaki
@dizastavinafanaccount
@dizastavinafanaccount 8 месяцев назад
majoho meupe ma dhahani Catholic..Tafsiri za kiarabu ni Quran
@fredrickwarioba713
@fredrickwarioba713 8 месяцев назад
Enyi watoto wa 2070, nawakumbusha kwamba huu wimbo umetoka leo 05/01/2024. Na huyu ndiye msanii wetu pendwa wa hip hop. Toleo la mwisho la viumbe wa aina yake
@emmanuellwinga5686
@emmanuellwinga5686 8 месяцев назад
😂😂😂😂😂umeiweka kitaalamu kaka utakumbukwa
@aminmohammed4249
@aminmohammed4249 8 месяцев назад
Dizasta FANS ..we are in safe HANDS🙌🙌🔥…the kid delivers what we’ve been waitin for
@dariusmsagha
@dariusmsagha 8 месяцев назад
The writing is incredible and very relevant to the socio-economic setting of African communities. Great love from Kenya.
@sunsetstudioz
@sunsetstudioz 8 месяцев назад
🔥Hamuongelei baba uliemuacha nyumbani.... Mwana ana kikao na BABA WA MBINGUNI... UTUNZIIIIIII NI NEXT LEVEL. 🔥
@msakatonge.
@msakatonge. 8 месяцев назад
Napiga magoti chini na kushukuru uwepo wa @dizasta ,sanaa na ujuzi alonao ni safi ni kama nanasi kwa maana ni tamu sana, HESHIMA KWAKO BROTHER kwa maana unatupa tunavyovihitaji na sio tunavyovitaka , Nakiri Kwa kusema Elimu yako ni kubwa zaidi ya masterz levels. I love u so much bro, Napenda sanaa yako ,napenda uwasilishaji wako , napenda ideas zako❤❤❤
@LambeDon_
@LambeDon_ 8 месяцев назад
Kama humpendi dizasta vina nenda Muhimbili kapimwe mkojo + akili nitalipia Gharama za matibabu🎉
@mbarakanassibu5234
@mbarakanassibu5234 8 месяцев назад
The black Maradona,hakika hiki ni kiumbe kipo katika dimension ya pekee, Mungu akuweke tuendelee kupata madini kwani kwa sasa tumetumia robo ya akili yako hata nusu hatujafika hii ndo maana ya MSANII NA MWANAFALSAFA. Be blessed Dizasta
@user-fw9jz6jk3w
@user-fw9jz6jk3w 8 месяцев назад
I ngoma naisubiri sana mana kila ngoma ya vina lazima iwe kali
@juliustinala4372
@juliustinala4372 7 месяцев назад
Tunapaswa kutambua kua msanii ni kioo cha jamii dizasta alichokifanya humu ni kizuri kabisa maana kunawatu wanawaza hivi....yeye kazungumzia mawazo ya mtu au watu waliokata tamaa na wamejaribu kumkaribia Mungu lkn wanahis bado hawajapata majibu Tunapaswa kujua msanii ni mtu huru na ni muwakilishi wa watu,wanayowaza na wanayoyapitia so the guy is presenting peoples feelings Imani inachangamoto nyingi sana Mm ni mkatoliki na naipenda imani yangu...wakati fulani nilipokua katika huduma moja namuubiria mtu aliniuliza je utajuaje kama Mungu amekusamehe na humuoni!? So dizasta ametisha sana humu..MUNGU akubariki edger kwa watu wa imani ya kweli hii ni challenge wala sio kufuru🔥🔥
@directorerikey3291
@directorerikey3291 8 месяцев назад
Wakwanza kukoment daah the long wait is over
@mohamedshabani619
@mohamedshabani619 8 месяцев назад
I wish dear father angejibu hii diss track kwake ili Dizasta aendelee kusema maana anaonekana bado ana meng ya kumuuliza Baba hasa juu ya Bakshishi anazotuma
@Mtumishi2000
@Mtumishi2000 8 месяцев назад
Mungu kashamjibu kabla ya yy kuzaliwa... kamjibu kwa kumpa pumzi aliyotumia kuandika na kuingiza vocal kwenye hii Beat. Binafsi kanichanganya, wengi hawaelewi aliyeongelewa humo "Baba"
@morganmwaikusa8194
@morganmwaikusa8194 8 месяцев назад
Dizasta vina a living genius. Kumbukumbu zinaonyesha watu kama hawa hawakufikia idadi ya 100 miongoni mwao ni Dizasta vina, leonardo da vinci, michalangelo, socrates na wachache wengine kadhaa… kama sisi ni wanae BABA kwann hajengi daraja tumfikie, alipopata changamoto ya dhambi zetu hima alitoeka asirudi kwann kajificha na anajua mm ni kiumbe dhaifu yeye ndiye alinizaa… hakika nimemtafuta sana lkn kajificha hatak nimuone hivyo nimechoka nae ni dhamu yake kunitafuta maana anajua pakunikuta dear. Wachungaji na masheikh wananiomba pesa ya kuwa wanamtumia lkn sina hakika kama hizo bakshishi zinafika huko.. vina GENIUS 😂😂😂
@sunsetstudioz
@sunsetstudioz 8 месяцев назад
Mwaka haujaisha ila hii tayari ishakuwa my TOP SONG
@emmanuellwinga5686
@emmanuellwinga5686 8 месяцев назад
Aiseh huyu mwamba noma
@raqamzomaica2836
@raqamzomaica2836 8 месяцев назад
Mufti mLamba haraM🔞
@dizastavinafanaccount
@dizastavinafanaccount 8 месяцев назад
Dizasta ni msanii, ni kioo. Taswira yake ni reflection ya alichokiona au kusikia kwa watu. Hana hatia kuwakilisha mawazo ya watu.
@reaganmakallo6824
@reaganmakallo6824 7 месяцев назад
Hii ngomaaa nimeisikiliza zaidi ya mara 24 ndio nimeielewaà..tena nimetafuta eneo ambalo hakuna sauti nitakayosikia zaidi ya sauti ya hii nyimbooo.. Ukiwa na imani ndogo hii nyimbo inakupoteza Na ukijifanya unaiman sana utashindwa kujibu hoja hata moja... ....he think more and more "Utanihukumu vp na una hubiri masamaha""
@erastomichael9840
@erastomichael9840 8 месяцев назад
Nikiteta hadithi utahisi NGUGI 🔥🔥🔥
@EjidyJosephu
@EjidyJosephu 8 месяцев назад
Toleo la mwisho la viumbe wa aina yake na hawatokuwepo tena big up to Dizasta vina (KING VINA)
@rick_bey
@rick_bey 8 месяцев назад
Kaka umemgeukia na mshua kabisaa
@AzadiSaidi
@AzadiSaidi Месяц назад
Co malaika we n Mungu w rap!yesu wa hi generation,🎉,
@mosesdavid-vm5hk
@mosesdavid-vm5hk 8 месяцев назад
Kwanza nimechukua maji ya uhai makubwa kabla sijamsikiliza T'TCHA DIZ kisha napitia comments za wanna kisha kila mmmoja unapiga like kwangu kisha tunamsikiliza GENIUS himself✔️
@raphaelchuche6281
@raphaelchuche6281 8 месяцев назад
mmmmmh kumuelewa vina inabidi uwe umekula umeshiba na huna stress 🔥
@Njokaa
@Njokaa 8 месяцев назад
Yaani mm mpaka kichwa kimeanza kuuma bado sielewi , kwani ka zungumzia nini broo!
@gagalinodenatrick1652
@gagalinodenatrick1652 7 месяцев назад
​@@Njokaamjomba nenda kamsikilize zuchu na mond wameachia ngoma mpya kwa huyu maradona utameza sana panado
@arnaldo7319
@arnaldo7319 8 месяцев назад
Uyo baba anakuja kama Mungu alafu anakata,yani kiufupi sielewi
@tcm.republic
@tcm.republic 8 месяцев назад
Siku zote huwa nategea kupata muziki mpya kutoka kwa dizasta vina 🔥💯
@emmanuelkiserere3523
@emmanuelkiserere3523 8 месяцев назад
Vinaah mwanamuziki genious anaeishi.... Tz kwa sas hv
@user-hv6qw2zw2y
@user-hv6qw2zw2y 8 месяцев назад
Uyu mwamba akitoaga ngoma sina muda wa ku loading chapo na download then naunganisha Bluetooth nasikia HIP HOP ASILI 😅😅. Ndomaana ni DIZASTA VINA
@carlospaul1032
@carlospaul1032 8 месяцев назад
Huyu dizasta ni rafiki yangu sana japo hajui Hilo Nakubali sana this story-teller
@PatrickIssafungameza
@PatrickIssafungameza 22 дня назад
Sooo interigent man in africa... Generous
@dawhacker2216
@dawhacker2216 8 месяцев назад
Commenter wengi mnaniangusha Kwenye huu wimbo beba linalo kuhusu km alikuhusu mute tu utakuwa ujaelewa😊 MARADONA MWEUSI👊🇹🇿
@titusjairo6482
@titusjairo6482 Месяц назад
Watu wengi wamekuwa wakimuomba mungu wakifanikiwa huwa wanamshukuru ila wasipofanikiwa huwa hawamlaumu mungu kwann? Nahisi bwana vina kaamua kuelezea jibu langui😊
@Njokaa
@Njokaa 8 месяцев назад
Mm nilikosea badala ya kusikiliza wimbo kwanza nikatizama comments na comments ya kwanza kuiona ilisema jamaa anaongea na Mungu na ndo maana nilienda kuiskiza ngoma nilipata taabu sana kuielewa mpaka kichwa kikaanza kuniuma an
@azezizokukufarm825
@azezizokukufarm825 8 месяцев назад
Wenye akili kama za DIZASTA, mara nyingi hujenga hoja kwenye kila jambo na ni ngumu kuamini kuhusu MUNGU
@DismasPhidason-vu6bt
@DismasPhidason-vu6bt 8 месяцев назад
Kweli Unapika Mawe Yanaiva Maverse... Salamu Baba Mi Mwanao Naandika Waraka Kwa Maana Hutaki Vikao Nahitaji Majibu Nikihisi Ni Haki Yangu Najihisi Vibaya Nikusikia Unahishi Na Sina Nguo... VINA 💪
@selemanmzee5804
@selemanmzee5804 8 месяцев назад
Here we go
@tracejeezy8917
@tracejeezy8917 8 месяцев назад
Vina anaongea na Mungu .
@moudyboe
@moudyboe 8 месяцев назад
huna baya bkack maradona sijui huwa unawaza nini upatunga tungo tata much respect
@user-mb7jh4vh6d
@user-mb7jh4vh6d 8 месяцев назад
Kama umegundua Baba anayezungumziwa hapa ni MUNGU ngonga like ❤
@Macaveli_tz
@Macaveli_tz 8 месяцев назад
Sikiliza tena huu wimbo kwa umakini,,, upo nje ya theme Kuna code bado hujazipata vzr ili kuelewa DZST anaongea na nani hasa kwenye huu wimbo
@carlpeterthegreat5007
@carlpeterthegreat5007 8 месяцев назад
We. Ni nyoko Ngoma Kali
@EarningsEdge101
@EarningsEdge101 8 месяцев назад
Utakuwa muongo ukisema umeielewa hii ngoma kwa kuisikiliza mara moja tu. Its need 🔂🔂🔂
@tracejeezy8917
@tracejeezy8917 8 месяцев назад
Yaani mara ya kwanza tu bila hata kurudia, nimejua anaongea na Mungu, maybe anatafsiri yake lakini kwangu hiyo ndio theme ya ngoma nilong'amua.
@ramadhanichitendile9332
@ramadhanichitendile9332 8 месяцев назад
We jamaa una sayari yako 👊
@dinnoboy5803
@dinnoboy5803 8 месяцев назад
Hatia namba 6 ni wimbo ambao nimeuelewa vizuri na mkasa ote unamuhusu mungu lakini pia unaweza usimuelewe vizuri kama utatumia vitabu vya kidini kumuelewa sababu dini hujazaliwanayo ni (program) ambayo baada ya kuzaliwa ndio ukaanza kuwekewa taratibu ili ubongo wako uzowee. Lakini pia dini zinaweza zikawa hazijakosea kufundisha ila uelewa wa watu wenyewe ndio tatizo linapoanzia mfano: nikisema "mungu yupo" simaanishi ni (object) au ni kiumbe bali ninguvu ambayo ipo kila sehemu, kwakila mtu na kila kiumbe lakini wapumbavu ndio wanamuumba mungu nakusema yupo sehemu anaangalia wanadamu tunavyo teseka😢
@mtwichetz4514
@mtwichetz4514 8 месяцев назад
Bro..wwe ni black Maradona pia
@shadowmatingo5072
@shadowmatingo5072 8 месяцев назад
Viongoz wa dini njoonu mumtetee MUNGU we u huku
@zillerbas7048
@zillerbas7048 9 дней назад
Barua kwa baba mkimbizi
@user-sw4rh6wo1g
@user-sw4rh6wo1g 8 месяцев назад
Hakuna rapper kama Dizasta apa Bongo case closed 🔥👨‍⚖️🙌
@tabora_boy
@tabora_boy 8 месяцев назад
Akili kubwa Sana 🔥🔥🔥
@mzeewakazi2439
@mzeewakazi2439 8 месяцев назад
Tiba ya ubongo skuzote💪
@user-ru2oz8zj2y
@user-ru2oz8zj2y 8 месяцев назад
NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA👏👏👏👏🔥🔥🔥🔥🔥🔥🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙋
@hr_VIP
@hr_VIP 8 месяцев назад
Let's go🔥🔥
@nawinahke710
@nawinahke710 8 месяцев назад
Wa pili
@BrunohBrunoh
@BrunohBrunoh 8 месяцев назад
Your The speaking book 📖 🙏 thank you for the free class fam 🙏🙏
@g_eazmusic1329
@g_eazmusic1329 8 месяцев назад
Aujui ningumu sana kuwa mwema ukiwa na njaa 😂😂😂
@zolomwashinga9074
@zolomwashinga9074 8 месяцев назад
Uyu ni baba mungu kama sikosei ila umemqambia ukweli yeye anajua pa kukutia
@bogertze3129
@bogertze3129 8 месяцев назад
the hottest raper @dizasta Vina "nashangaa wenzangu wanakesha wakiimba utukufu Wa dhambi zako"
@FedrickDanielJob
@FedrickDanielJob 8 месяцев назад
Here we go kaka ❤❤❤❤
@AlexLihogosa-om3zh
@AlexLihogosa-om3zh 8 месяцев назад
Kumbe sijachelewa
@user-ju8ud8tx1d
@user-ju8ud8tx1d 8 месяцев назад
Nime like kabla sijaskiza maana najua hatia ni noma kila siku
@simbaforex
@simbaforex 8 месяцев назад
Nani ameelewa baba anaye zungumziwa 🔥🔥 Dizasta vina tunzi zimetukuka...✊🏾✊🏾
@user-ih6hk5nh7v
@user-ih6hk5nh7v 8 месяцев назад
kaka mm sijaelewa
@michaellutonjagospelsinger6611
@michaellutonjagospelsinger6611 8 месяцев назад
Jamaa anateta na sir God
@Njokaa
@Njokaa 8 месяцев назад
Hii ngoma ni ya kusikiliza hata porin pasipo na kelele la sivyo huwezi ambulia kitu hajamaanisha Mungu
@jonasibraysoni1859
@jonasibraysoni1859 8 месяцев назад
Uyu jamaa mjanja sana kama akili yako kichwa majia apo ajamzungumzia baba ake kazungumzia mungu😂😂😂😂
@karama-kitungano
@karama-kitungano Месяц назад
Niwenye doumesema sio yeye au mimi
@daudmaikomwakapoma213
@daudmaikomwakapoma213 8 месяцев назад
Ujumbe kutoka kwetu unaotuwakilisha tunasema kazi umeifanya vyema tumeisikia na tunakushushia baraka tele kutoka Unyakyusani Afrika Tanzania Mbeya. Tunakusihi endelea kuwaeleza ukweli kuwa hizo hisia walizoambiwa ni za kiroho zimefunika furaha yao ya mila na utamaduni wao na kuhubiriwa kukimbia mila zao Kaulimbiu AJHOBILE MAGUFULI
@brunoh_bx
@brunoh_bx 8 месяцев назад
Mwamba huyu hapaaaa🔥🔥👏👏
@mdcalive
@mdcalive 8 месяцев назад
Miaka 6 iliyopita kwenye kanisa nikasema this man is hopsin wa bongo and he prove again
@japharysety6890
@japharysety6890 8 месяцев назад
Dini nayo ni matrix mbaya sanaa
@KassimAlly-en3qj
@KassimAlly-en3qj 3 месяца назад
Mh vina umesoma shule Gani
@paccowilly5672
@paccowilly5672 8 месяцев назад
Siri ipi na Siri zetu hazilingani / G.O.A.T shukrani sana 🙌🔥🔥🔥
@richardmloha1762
@richardmloha1762 8 месяцев назад
Hikii kichwaaa🔥🔥🔥🔥
@geffects1141
@geffects1141 8 месяцев назад
Hakuna Rapper kama Disaster Vina DUNIA nzima 💪💪💪💪💪💪
@taseni_vevo
@taseni_vevo 8 месяцев назад
Una wazimu
@Mox-lh6yt
@Mox-lh6yt 8 месяцев назад
Kaka unajua mpaka unatia huruma 😊
@boygavana4674
@boygavana4674 8 месяцев назад
Kwanza beat kali na limekutana na fundi wakuchora
@marokeyLFM
@marokeyLFM 8 месяцев назад
Nimechelewa ku coment wahuni wamewai hii 😂 kama una mkubali Dizasta weka moto 🔥
@vascobruno3936
@vascobruno3936 8 месяцев назад
Kaka ulimaliza KANISA Hatia V1 umegusa muhusika Salute sana
@AlbetoGwoma
@AlbetoGwoma Месяц назад
Mungu ni nguvu ya asili
@ivansixbert3602
@ivansixbert3602 3 месяца назад
We love you our bro 🇹🇿🇹🇿🙌🙌
@McBabuAyub-dr1po
@McBabuAyub-dr1po 8 месяцев назад
Umeiweka hip hop lever za juuu sana
@Valiant0790
@Valiant0790 8 месяцев назад
Vina ndo jina🙌
@willinjowritter206
@willinjowritter206 8 месяцев назад
Dude was born in wrong era.. much love and blessings from Kenya.
@hafidhhemed1514
@hafidhhemed1514 Месяц назад
Whenever I listen to this masterpiece I get goosebumps.. kila neno kwenye hii kitu cuts deep.. one of my fav rapper duniani
@Steven3.
@Steven3. 8 месяцев назад
Ngoma Kali blood uko vizuriii
@alextanzania
@alextanzania 8 месяцев назад
Ringle beats aksante kwa mdundo.
@phinaphina3201
@phinaphina3201 4 месяца назад
Sons a genius
@taufiqkweka669
@taufiqkweka669 8 месяцев назад
Uwanja ni wako mwenyewe
@Deejay_plannet255
@Deejay_plannet255 8 месяцев назад
Hiki kisa ni cha kweli na kuna watu wameishi maiaha ambayo mnyama DIZASTA VINA kayoongelea kabisa. Daima utabaki kuwa mwana hip hop bora na storyteller wa muda wote🎉🎉❤❤
@schigangermayala7706
@schigangermayala7706 7 месяцев назад
❤❤❤
@user-um5yd8ly9z
@user-um5yd8ly9z 8 месяцев назад
Respected all ever my favourite 🎉🎉🎉
@johannesjoseph7496
@johannesjoseph7496 8 месяцев назад
Ushauri wenye upendo kabisa..naamini vina ni muelewa na hii ni challenge kwetu tunaompenda ila yuko imani tofauti na sisi...tutafte namna ya kujibu hoja zake za msingi...yeye anadai Mungu amejificha, anakwepa majukumu nk.. Shida ni kwamba elimu kuhusu Mungu aliyonayo inafikia hapo... Shida nyingine anaamini sana ktk yeye mwenyewe(selfbelief) ambavyo ni vzr kujiamini kuliko kiumbe kingne chochote isipokua Muumbaji, ..natamani nipate mda nae tuelekezane unabii, kama ni mwana wa Mungu ataelewa, kama ni mwana wa Lucifer ataendelea na msimamo na inabaki kuombeana tu mwisho mwema.....kwa kifupi uyo anaetamani kuonana nae siku si nyingi kila jicho litamuona, na maswali hayo kama hataruhusu au kutafta majibu yake kwetu tunaojua atajibiwa na yeye mwenyewe..Baba hajajificha wala hajakimbia wala hajatuacha wapweke..Baba ni roho(anaishi ndani ya mioyo ya watoto wake_we feel his presence through holly spirit)).Anachodai D kua yuko mpweke ni sawa maana atheist hawaamini uwepo wake hivyo hayuko nao na amewaacha wafuate akili zao za upotovu...yaani wanafanya karma/jin(mf aladin lamp)-nguvu ya asili kua ndo mungu kumbe hiyo nguvu ya asili nayo imewekwa na Muumbaji(Mungu)....uzuri tupo ndani ya saa moja wa shetani na mawakala zake kutawala kisha Masihi arudi na kuondoa matrix iliyopo na kusimika falme mpya ambamo ndani yake Baba tutamuona kama alivyo katika utukufu wake...Tumepewa ishara za mwisho kabisa kabla ya masihi na Baba kushuka na mji wa yerusalemu hapa duniani....moja ni yule mwana wa kuasi kujidhihirisha na kujiinua ndani ya hekalu la Mungu na pili ni ni watu wote kutiishwa chini ya utawala wa mwana huyo wa kuasi...uzuri sasa ata wenye nuru kiasi wameanza muona na mifumo inazidi imarika adi mataifa ya uku kwetu ambako teknolojia ndo kikwazo kikubwa cha kuyatimiza haya..Nimekuombea rafiki yang D, hunijui ila mi ni mmoja wa fun wako wakubwa mno...imagine kwenye simu yangu sina nyimbo za secular zozote ila zako tu...napenda namna unavyotazama mambo kwa namna tofauti na huo ndo ubunifu unaonivuta kila ukitoa ngoma lazima niitafute, Umekua ukimsema sana Mungu nae ni mwingi wa rehema anakujua vzr kuliko sisi tunavyokujua ndo maana maana bado anakuvumilia kama anavyotuvumilia sote...nakuombea uo utaji uliofunga sub conscious yako utoke ndo conscious mind yako itaweza ngamua ukweli kuhusu Baba...kama kweli unataka majibu toka kwa Baba-sikiliza majibu toka kwa ndugu zako-kua na moyo wa kisomi uliotayari kujifunza maarifa mapya na kukubali ulipopungua ila wajuzi wakujazilizie....
@reaganmakallo6824
@reaganmakallo6824 7 месяцев назад
Ameuliza ni vipi utanihukumu na unahubiri msamahaa??
@mhogomchungu7882
@mhogomchungu7882 7 месяцев назад
Mungu ni conscioussness yenyw it is here and now. Be at the present and sense your being (essence)
@johannesjoseph7496
@johannesjoseph7496 6 месяцев назад
​@@reaganmakallo6824ametoa mda mrefu wa waovu kutubu na kusamehewa makosa yao kabisa--alivumilia maovu yetu ata baada ya kuteswa aliwaombea msamaha, bado anawaita watu watubu ili anapoenda kuishiliza dhambi wasipotee pamoja na waasi..Mungu hafurahii kuangamiza alichoumba
@johannesjoseph7496
@johannesjoseph7496 6 месяцев назад
​@@mhogomchungu7882consciousness(utashi) ni sehemu ya ubongo inayotusaidia kuamua kutenda jema au baya...Mungu katupa hii ili tumpende kwa utashi pasipo kumonitiwa kama robot....ni kwel Mungu ni omnipresent ila haimaaniishi yeye ni sehemu ya uumbaji-yey ndiye aliyeumba na yupo kila sehemu kupitia nguvu ya roho mtakatifu-ulimwengu wote unathibitika kwa nguvu yake
@titusjairo6482
@titusjairo6482 Месяц назад
Ulipo andika neno lucifer nimejua kitu kuhusu wewe 😂😂 am so sorry
@mzee012
@mzee012 8 месяцев назад
Kichwa cha uyu jamaa ni hatari aiseee,anawaza mbali sana uyu jamaa ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
@simoncmatanda5135
@simoncmatanda5135 8 месяцев назад
Fundi kama fundi hatia namba 5,, n shidaaaa,, hii ni hatia seriz
@jephramso
@jephramso 8 месяцев назад
DZSTVN… Father Figure dropping Hatia VI 🙌🏼🙌🏼🔥🔥🔥
@valencepaul4604
@valencepaul4604 8 месяцев назад
Hii Ndo kitu tunahitaji Imani inakuwa kwa kuhoji Vina kashatupa karata tunasubiri majibu ya wenye kanzu nyeupe na alama za misalaba au mwezi na nyota😤
@khalifasultan2677
@khalifasultan2677 8 месяцев назад
NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA🔥🔥✊🏾
@richcotizz4077
@richcotizz4077 8 месяцев назад
Bana hii ni uzito
@monixkarim-st4qm
@monixkarim-st4qm 8 месяцев назад
Sikupingi genius , naenjoy coz kila nikisikiza ngoma zako huwa na madetate uwezo ulio nao wa uwandishi
@ngotamohamedi1793
@ngotamohamedi1793 8 месяцев назад
Akili kubwa
Далее
Dizasta Vina - Hatia V
8:16
Просмотров 116 тыс.
Dizasta Vina - Wachezaji wa timu
7:25
Просмотров 80 тыс.
Dakika 10 Za Maangamizi-  Dizasta Vina | Planet Bongo I
12:06
KINYA MISTARI - SINA FT DIZASTA VINA & BOSHOO NINJA
3:08
Tribulation
11:27
Просмотров 26 тыс.
Dizasta Vina - Hatia IV
7:37
Просмотров 160 тыс.
Dizasta Vina - Achia jala  Ft Kaa La Moto
8:34
Просмотров 118 тыс.
Dizasta Vina - Shahidi
6:38
Просмотров 187 тыс.