Тёмный

Kijana Dereva wa Lori Afariki Kwenye Ajali akiwa Kenya Kikazi | Boss wake Aongea kwa Uchungu Msibani 

Focus Digito TV
Подписаться 33 тыс.
Просмотров 2,2 тыс.
50% 1

Kijana anayejulikana kwa Jina la Augustino Bruno Kindole mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Kijiji cha Wangama Kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa ambaye ni Dereva wa gari (Lori) aina FAW mali ya kampuni ya John Galt Hauliers amefariki Dunia katika ajali iliyotokea Jumapili ya Julai 21, 2024 akiwa kikazi na Lori hilo la mizigo nchini Kenya akitokea nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya John Galt and Phoenix Hauliers ambaye pia ni Mdau wa Maendeleo wilaya ya Kilolo-Iringa, Aidan Mlawa, amefika na kushiriki mazishi ya Kijana Dereva wake anayejulikana kwa jina la Augustino Bruno Kindole (28) aliyefariki katika ajali ya gari (Lori) mali ya kampuni hiyo iliyotokea Jumapili ya Julai 21, 2024 maeneo ya Denge-Kinango (Puma Ward) nchini Kenya akiwa na mzigo kutoka nchini Tanzania.
Mazishi ya kijana huyo (Marehemu Augustino Kindole) yamefanyika Kijijini kwao Wangama kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa ambapo kampuni ya John Galt Hauliers chini ya Uongozi wa Mkurugenzi wake Aidan Mlawa ilijitoa kushughulikia na kusimamia taratibu na gharama zote za kusafirisha Mwili wa marehemu mpaka kuhakikisha umefikishwa mkoani Iringa nyumbani kwa wazazi wa marehemu.
Akizungumza wakati wa mazishi, Aidan Mlawa amesema ameguswa na ameumizwa sana na kifo cha Mfanyakazi wake aliyekuwa akimuamini mpaka kumpa kazi kwenda nchi za nje huku akisema kuwa yeye katika kampuni yake, anazingatia sana utu wa binadamu kuliko thamani za mali ndio maana amejitoa kusimamia taratibu za kusafirisha mwili na mazishi kabla ya kuanza kuhangaikia mali zake.
Mazishi ya Kijana huyo (marehemu Augustino Kindole) yamefanyika Julai 24, 2024 kijijini kwao katika makabuli yaliyopo Kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Marehemu Augustino Bruno Kindole (28) aliyefariki katika ajali ameacha Mke na watoto wawili wadogo.
Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
#FocusDigitoTV
..................
Tufuatilie Zaidi kupitia:
INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team FocusDigitoTV

Опубликовано:

 

10 сен 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 8   
@edigamc6000
@edigamc6000 26 дней назад
Inaumiza sana
@user-xk7vy4gb6g
@user-xk7vy4gb6g Месяц назад
Pole Sana Wazaz kwakuondokewa na kijana 😢😢pole Sana Diwani wetu kindole Mungu awe faraja kwako 😢😢😢. Hakika kifo ni fumbo hakuna aijuae kesho 😢
@PetronilaIngosi-en1gh
@PetronilaIngosi-en1gh Месяц назад
Poleni😢lkn mbona boss anakaa mwigizani wa wrong house 🤔
@EmanuelAllan
@EmanuelAllan Месяц назад
RIP
@apboy8944
@apboy8944 Месяц назад
R.i.p our workmate 🙏🙏
@EndrickSowo-jd7kl
@EndrickSowo-jd7kl Месяц назад
😰😰
@JacklineMzena
@JacklineMzena Месяц назад
Jmn inaumaa tumemzka Jana jamn
@apboy8944
@apboy8944 Месяц назад
R.i.p our workmate 🙏🙏
Далее
KUTANA NA KIJANA WA DARASA LA SABA ALIYEUNDA HELIKOPTA
8:38
▼ЮТУБ ВСЁ, Я НА ЗАВОД 🚧⛔
30:49
Просмотров 532 тыс.
To mahh too🫰🍅 #abirzkitchen #tomato
01:00
Просмотров 1,2 млн
ДОМИК ДЛЯ БЕРЕМЕННОЙ БЕЛКИ#cat
00:45
TAJIRI WA MABUS  SUPER FEO ATOA SIRI YA KUWA BILIONEA
10:36
HII NI KIBOKO YA WAHABI
19:33
Просмотров 7 тыс.
Mtoto aliyefariki na kuzikwa apatikana akiwa hai
52:00