Bandari ya Mtwara imevunja rekodi kwa kutia nanga Meli kubwa yenye urefu wa Mita 240 iliyobeba Makasha yasiyo na kitu 459 kwa ajili ya maandalizi ya Msimu wa zao la Korosho kwa mwaka 2024/2025 ambapo Bandari hiyo ndiyo itakayotumika katika kusafirisha Korosho kwa msimu huu kama alivyoagiza Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenan Sawala ametoa wito kwa wanunuzi kuja Mtwara kununua zao hilo huku akisema wao kama Serikali wamejipanga vyema kuhakikisha usafirishaji wa zao hilo unaenda vizuri.
SUBSCRIBE RU-vid CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU.
4 окт 2024