All our voices to our Lord God the creator of the universe.We will not stop,THE GLORY AND GREATNESS IS WITH HIM forever and ever,Amen.Channel Administered by Huru Digital Instagram: / hurudigital
Kakukirimia, uwe ulivyo, Atakutumia impendezavyo Akikuinua, inuka, hivyo, Ninakuombea heri vilivyo; Hakunipa hayo, nikuhitaji, Kwa niliyo nayo, upate maji, Na mwisho wa hayo, tuvikwe taji, Tuingie nayo, wa mbingu mji. { Nimeiona nyota yako mashariki (nyota yako) Ninajivuna inavyong'ara rafiki (helelelele) Naandamana kuja unakotamalaki Kumsujudia Bwana aliyekupa milki (ho ndugu) } *2 Sirudi kwa njia, yake herode, Anakuvizia, kila upande, Wivu unamjia, kakunja, konde, La kukuzuia juu usipande; Ni kama Kaini, mwua Abeli, Au Raubeni, wa Israeli, Waliotamani, kuzika, hali, Ya wadogo duni, wake Jalali! Ninakuombea, usife moyo, Maana dunia, si rafikiyo, Wewe fuatia, za Kristu, nyayo, Aliyekufia, kwa mizigoyo; Wa ulimwenguni, watakufumba, Wazuri machoni, moyo mwembamba, Hawatatamani, uitwe, mwamba, Ni wivu moyoni, unawasomba!
Ukweli mbele za Mungu mnaimba vizuri sana sana sana, napenda nyimbo zenu karibia zote hunibariki sana.shetani anona wivu sana,Roho Mtakatifu asiwapungukie azidi kuwalinda daima
Nimeona nyota yako mashariki nimejivuna inatamatala rafiki asante sana kwa maneno ayo yenye kujenga katika maisha yetu Mungu awabariki na kuwajalia nguvu za roho mtakatifu ili mpate kumtumikia siku zote zamaisha yenu amina
siwezi tosheka kusikiliza nyimbo zenu...zanibariki sana..heko!!I wish I had a chance to join Mt.Kizito Makuburi choir...I would be quite glad..barikiweni...taji lawangojea mbinguni..