@@BeingtheafricanmanHakuna mtanzania asiyelipa kodi. Unaponunua bidhaa yoyote kuna kodi iliyochajiwa tayari ambayo inaingia serikalini. Chunguza unaponunua umeme au unapoingiza vocha kuna msg inayokuja kwenye simu yako inayoonesha makato hayo. Na hayo ndiyo yanayotumika kutupatia huduma mbalimbali zikiwemo kujengewa vituo vya afya, shule, maji, umeme, barabara na kadhalika.