Тёмный

Sizonje - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro (Official Video) 

MrishoMpoto
Подписаться 75 тыс.
Просмотров 1 млн
50% 1

Nyimbo Mpya ya Mwaka 2016, Sizonje.
[Kibwagizo - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Bridge - Banana Zorro]
Tulikaa barazani, tukasikia kelele
Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani
Sizonje, karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu
[Verse 1 - Mrisho Mpoto]
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu,
Tulipoficha mundu za kupondea wezi,
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne,
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango,
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili,
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea,
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni,
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Verse 2 - Mrisho Mpoto]
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje
Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?
Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini
Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi
“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”
Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje
Kuna watoto, wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia, ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni
Uone maajabu mengine ya nyumba hii
Sizonje, ukiona tembo anaringa
Ujue mvua zinakaribia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Опубликовано:

 

14 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 410   
@upendorealestateagentintan190
@upendorealestateagentintan190 9 месяцев назад
Mjomba Tanzania imekumiss sana. Tunaamini bado unatupenda yapo mengi tunahitaji utusemee hasa ktk wakati huu.
@kombakomba7922
@kombakomba7922 3 года назад
Nyumba ni nchi,kwa nje inatafsirika na kuonekana ni maskini ila ndani ina utajiri mkubwaa,ila inaibiwa na manyemera wanaopita njia za panya kuiba rasilimali zetu, pia undugunization kwenye ajira ni tatizo,afya za kina mama na watoto,uchumi,rushwa na uwajibikaji ila sizonje ushafika umekomesha hayo yote. Hongera sana sana Mrisho na hongera kwa Sizonje.
@Richplumbing11
@Richplumbing11 2 года назад
Leo ndio nimeielewa atari sana uyu jamaa
@tengezashemisea1787
@tengezashemisea1787 2 года назад
Hongera mrisho, ila bado mwendo hujaumaliza endelea kuwa kumbusha wenye dhamana , hakika bado tunakuhitaji.
@alvinmuthui
@alvinmuthui 2 года назад
Elenzea zaidi tafadhali
@المهلهلالحراصي
@المهلهلالحراصي 2 года назад
duuuuuuh kumbe ndo nimejua leo hii maana ya wimbo huu
@bonfacemark9048
@bonfacemark9048 Год назад
Asante kwa tafsiri yako ndugu from 🇰🇪 🙏
@stephanokigosi656
@stephanokigosi656 2 года назад
huu wimbo ulikuwa special to MAGUFULI..Rest in paradise our icon 🕯🕯😭😭
@mariammalendeja370
@mariammalendeja370 Год назад
nyimbo hii ulimuimbia maghufuli nae akaskia sauti yako akawaadhibu wadhalimu hadi wakaanza kupitia mlangoni r.i.p maghufuli tutakukumbuka milele
@solangeramadhani4038
@solangeramadhani4038 Год назад
Duuuh miaka nenda miaka rudi leo ssa ndonimeelewa maan ya huu winbo
@jimmyfredmwanswaswa4562
@jimmyfredmwanswaswa4562 2 года назад
Tutolee nyimbo nyingine nzuri kama hii Mrisho! Asante kwa kutufundisha Kiswahili na utunzi! Mashairi Yako natamani watoto wetu wayasome shuleni!
@jodasonudavis1131
@jodasonudavis1131 7 лет назад
MLANGO UPO WANAPITA MADIRISHANI.... ..kwamba Kuna utaratibu wa kufikia jambo fulani Ila watu hutumia njia za mkato(rushwa) kupata jambo hilo.....SHIMO HALITUPWI TAKA WALA HAWAENDI CHOO... maana yake Kuna mfumo wa watu kustaafu Lakini Kuna watu hawaachii nyazifa na pia kuna kazi fulani hivi zimekuwa za koo fulani wanarithishana kutoka kwa baba then mtoto hatimae mjukuu mfano(benki kuu) na hivyo kusababisha vilio vya vijana wengi wasomi kuzunguka na bahasha kwa kutafuta ajira na ajira hamna.......This is the best literature song I ever meet. Good work for this guy
@martinnsuhuje4391
@martinnsuhuje4391 7 лет назад
Asante kwa kufafanua kidogo nadhan umesoma kiswahili vzr
@jodasonudavis1131
@jodasonudavis1131 7 лет назад
Sikuachwa nyuma sana katika fasihi
@davidomemu471
@davidomemu471 7 лет назад
Nakubaliana nawe Jodasonu kabisa, the best oral lit, of modern time, big up MPOTO.
@khadijambuta4360
@khadijambuta4360 7 лет назад
Jodasonu Davis yani huko benk kuu ndio ucseme watu wapitishana tu msemo wao hpa kaz tu
@doreenmalesi6039
@doreenmalesi6039 6 лет назад
Asante kwa kunifafanulia
@allyhussein516
@allyhussein516 5 лет назад
Bila akili ya ziada kwa mrisho mpoto hutoki na kitu njooni tuungane jaman gonga like hapa kama umeikubali hii
@josephseleman7780
@josephseleman7780 4 года назад
Kama unamkubari mrisho mpoto gonga like hapa
@VictorMligo-t9c
@VictorMligo-t9c 7 месяцев назад
Ila mpoto I nyimbo nimekuja kuelewa leo trh 5-3-2024😂😂😂
@Gbril45
@Gbril45 7 месяцев назад
Inamaanishi nini kwani? Mimi bado naangaika
@phillies846
@phillies846 8 лет назад
Mrisho mwalimu wako wa kiswahili alikuwa anapata shida saana kwa kukosolewa na wewe 🙏🏽 amen
@merryn4891
@merryn4891 6 лет назад
😀😀😀😀
@ssur5797
@ssur5797 5 лет назад
Nampnda mpka bac huyu kaka mola ampe umri mrefu wenye kheri ishllh
@catenzeki678
@catenzeki678 5 лет назад
@S Sur AMINA
@JosephatJuma-dj5tq
@JosephatJuma-dj5tq 4 месяца назад
Mjomba hapa Kenya unapendwa kakangu
@johnambrose7223
@johnambrose7223 8 месяцев назад
Siku hizi mrisho mpoto haimbi tena
@ivanmutwol2549
@ivanmutwol2549 10 дней назад
A true Patriot, maisha marefu
@saidbarawa9096
@saidbarawa9096 Месяц назад
Mrisho shujaa shujaa shujaa,saluti kwako,mimi ni mkenya anaefurahia kazi yako nzuri mungu akubariki
@kenneth.m.siwale9699
@kenneth.m.siwale9699 5 лет назад
Pamoja na hayo mjomba Mpoto,leo hii nikiwa natokea kwenye kilele cha sherehe ya kilele cha miaka mia moja ya vita kuu ya Dunia ya kwanza! Mjomba Mpoto nimelazimika kutumia au kuiba jumbe zako hizi kwa mapenzi na ujumbe sahihi kwa wakati mwafaka hasa hapa kwetu Zambia!
@muddysimba887
@muddysimba887 4 года назад
Yuliopo hapa 2020 tupia like
@kenneth.m.siwale9699
@kenneth.m.siwale9699 5 лет назад
Mjomba Mpoto utaniwia radhi kwakweki mjomba uliwahi kuniliza enzi za awamu ya nne ya Mzee wetu Dr. wa Ukweli wa Msoga, niliwahi kulia na kucheza sana pala LUGOBA!ulikuwa wimbo Adela,na Sasa hivi SIZONJE huu si tu ni wimbo ni FASIHI KALI!!!!. Wewe kweli ni aina ya akina Shaban Robart
@msafirisalehe563
@msafirisalehe563 8 лет назад
Kama umesoma sana vitabu vya Hayati Shabani Robert,hakika hutokuwa na kazi kubwa ya kumuelewa Mpoto.
@barackolgeno1076
@barackolgeno1076 8 лет назад
this guy is marvellous... your Tanzanian fan from Australia
@samwelmkondo10
@samwelmkondo10 6 лет назад
We are together
@nyabisemaro2095
@nyabisemaro2095 6 лет назад
Mrisho Unajitahidi sanaaaa kusema kweli nazipenda nyimbo zakooo hasa Sizonje,kitendawili,nikipata nauli,Waiteee nk
@rosenamilia4140
@rosenamilia4140 2 года назад
Sizonje ni jina la HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI,alilopewa na Ndugu yetu msanii Mrisho Mpoto.Nyumba ktk wimbo huu ni IKULU YA RAIS MAGOGONI Dar es Salaam.
@SostenesMasawa-ls1eo
@SostenesMasawa-ls1eo Месяц назад
2024 eeeeeh 🔥 "MASTERPIECE"
@abbouramsey154
@abbouramsey154 8 лет назад
Apo Godfather au nenene? bonge la kichupa straight to Urban top Ten
@eusebiusjmikongoti6625
@eusebiusjmikongoti6625 7 лет назад
Nakukukubali sana mtaalamu Mjomba, kazi zako huwa zina nipa shida kuzielewa lakini huwa nakuelewa taratibu. Ninahisi hakuna kazi niliyowahi kukuelewa kwa 100% maana kila nikirudia kusikia wimbo fulani huwa naongeza kitu fulani kutoka humo! Wewe ni Shaaban Robert wa pili kwakweli, yapasa nawe uandike kitabu cha KUSADIKIKA kama mzee Shaaban, sijui utakiita SIZONJE....., au NYUMBA YETU!
@mwangacharles8474
@mwangacharles8474 8 лет назад
Kaka hongera sana kaka, nimeielewa sana nyimbo hiii, hasa choo kipo lakini hakitumikiiii. Unatisha kaka.
@mohdkhalifa8828
@mohdkhalifa8828 Месяц назад
Hekima kaka safi sana
@lightnessmruma9740
@lightnessmruma9740 8 лет назад
nmeelewa kidogo,anamkaribisha maguful ikulu(nchi yetu)....asiye mtaka kaja hahaha I like this ....japo mafumbo n mnge
@mhonamisaomar7011
@mhonamisaomar7011 8 лет назад
ukiisikiliza mankini itailewa 2..hongera. mjomba coz umenifanya ninitulie xanaa kukusikiliza Na kufafanua..wakuache jomba..nakusikiliza. mwana Kenya nikiwa saudia nimetua mankini..
@thedoctor8301
@thedoctor8301 8 лет назад
SIKU ZOTE MWENYE HEKIMA HANUKI MDOMO NA MWENYE AKILI HASEMI NDANI YA MAJI.... HESHIMA KWAKO MR MPOTO NATAMANI NIJIFUNZE ZAIDI TOKA KWAKO.
@IrineKimaro
@IrineKimaro 4 месяца назад
Mjomba tumemiss mashairi yako, come back legend
@FredySokolo
@FredySokolo 5 месяцев назад
Kiongozzzz unajua sana ,sasa sijajua umesoma kiswahili sana au mimi ndio btplms
@fatmafetty4117
@fatmafetty4117 5 лет назад
Sizonje naipenda mnoo sichoki kuiangalia wallah love u bro mrisho ❤️❤️❤️❤️❤️ kazi nzur sanaaaa👌👌👌👌👌👌
@fatmafetty4117
@fatmafetty4117 5 лет назад
@@rashidikufinyu444 pouwa
@DoubleDlyrics-v7k
@DoubleDlyrics-v7k Год назад
Dah!!na mkubali sana mrisho miaka 7 imepita nasikia wimbo huu ila leo ndo mmeelewa sahihi ya wimbo huu
@ernestshaha1932
@ernestshaha1932 5 лет назад
Huu wimbo nimeusikiza Mara 7 sai Mjomba juu wimbo unamafundisho saana
@abukiczan6600
@abukiczan6600 8 лет назад
Mwenye akili ndogo hawezi elewa nyimbo zako but wewe ni zaidi ya msaniu hapa afrika na natamani siku nikukumbatie kwa furaha. U are the best mjomba
@winstonkwoba1994
@winstonkwoba1994 4 года назад
madhumuni nimeyapata
@rumbikamachumu3292
@rumbikamachumu3292 8 лет назад
one of the best video and nice message to Tanzanian. kazi nzuri Mjomba endelea kuelimisha ,kufundisha na kukosoa jamii
@silassambia876
@silassambia876 4 года назад
My all time Tanzanian Artist..love from🇰🇪
@anitaphilip2070
@anitaphilip2070 8 лет назад
upenda Wangu nimependa kilakitu wanao sema sinzuri wajaribu nawao tuona zao zitakuaje
@salumkanju1732
@salumkanju1732 7 лет назад
daah kwa sisi tuliosoma arts aisee mzee mpoto unatisha baba angu.....nakutamani san katik matumizi ya lugha na hasa lugha ya picha kikubwa zaidi ni hiyo nyumba yaudongo lakin ndani noouma!! bila shaka watanzania waliotazama video hii wamejifunza kitu, binafsi sanaa yako sio tu kiburudisho kwangu maana najifunza mengi san na ni miongoni mwa mhimili wa utamaduni wa nchi yetu! unaimba kwa kusoma upepo unavyovuma ila ulituomba nauli ili uwende kwa mjomba na je sizonje ni naniiiiiii?
@gospelman3720
@gospelman3720 2 года назад
Mmmmmmmh huu wimbo aliimbiwa JPM
@boazmosses8204
@boazmosses8204 7 лет назад
kwamba kwa nje inaonekana kkukuu lakn ndani imejaa vitu vya thamani😂😂😂😂tz hyo
@Franko-zd6hc
@Franko-zd6hc 3 года назад
Huu ni usanii wa hali ya juu.Utumiaji wa kejeli ilikupeana ujumbe flani.
@MishenOnMission
@MishenOnMission 2 года назад
Mbona mrisho haimbi tena..
@eliatalented7592
@eliatalented7592 5 лет назад
Who else is still here in 2019
@zulferabour607
@zulferabour607 4 года назад
Wakati leo nasom kiswahil ....mwalim wanv kantolea mfano wa mwanafasihi anaetumja lugh y fasihi kufikish ujumb ktm jamii....ndipo akntajia huu wimbo ....hap nmeelewa kwann mrisho umeamua kutmia lugha hii....hongera sana
@kailembobrigita2657
@kailembobrigita2657 8 лет назад
mchanganyiko sana sielewi
@ezrambilinyi6788
@ezrambilinyi6788 3 года назад
Mhhh ngoja niseme ukweli tuuu. Ni miaka 3 now nasikiliza nyimbo za huyu jamaaa cjawai elewa anae elewa anielekezeee
@Catherinemichael1995
@Catherinemichael1995 2 года назад
Amemaanisha kuwa nchi inaonekana masikin wakati ndani yake inautajir tena amemaanisha sheria ipo lkn watu wanatumia njia ya mkato ameelezea mambo mengi
@leonardcharles3169
@leonardcharles3169 8 лет назад
video ni nzuri, tuendelee kumpigia kura tuzo ya kola! wonderful video,
@sirialemmy37
@sirialemmy37 8 лет назад
Yes Leonard!
@PapaTheKingKenya
@PapaTheKingKenya Год назад
Unloving memory to magufuli
@davidomemu471
@davidomemu471 7 лет назад
Mjomba, kwa kweli nyumba za Africa mashariki zina mambo na maajabu, zaidi hapa Kenya.
@mwitaadah3649
@mwitaadah3649 3 года назад
Mjomba umetulia Sana. Tupe mashairi baba🔥
@nicksonrichard9411
@nicksonrichard9411 8 лет назад
nyimbo nzuri ya kiafrica zaidi
@sirialemmy37
@sirialemmy37 8 лет назад
hehehe ya kiafrika zaidi, hehehe, l wish if this man's philosophy is well understood
@estherurio6155
@estherurio6155 2 года назад
Mmmh!!! nyimbo ngumu hii😭😭😭
@mariajohn2752
@mariajohn2752 8 лет назад
duuuu empty kabisa but nice song mashair magumu sana inabid usikilize kwa makini sana
@Vincent-sj2oj
@Vincent-sj2oj Год назад
Naupenda huu wimbo
@aminagoliama8668
@aminagoliama8668 8 лет назад
Weng ni vijan na wanabahasha za kaki mikonon daaaaah nimeelewa sana nakupend sasa mpot ii ndo nyumb yetu TZ ingia uyaone Kile ni choo wanaoish hawajawai kukitumia mean hospital zipo ila wanaenda nje hahahahahahaha 😍💞💕😘💜👏👏👏
@augustinomkongwa5444
@augustinomkongwa5444 4 года назад
Usiyemtaka kaja, sizonje huyu huenda akawa ni JPM aka Jembe aka Chuma cha Pua, siyo lazima niwe sahihi kumtambua Sizonje kwenye ghani hii ya Mrisho
@kedmondkepha7707
@kedmondkepha7707 6 лет назад
Daaaaaaah mjomba ulisomea wapi kiswahili chako maana hayo mashairi yako hakuna anaeyaweza duuu big up sana mziki wako ni wa kibantu zaid
@Tutankhamun-s3n
@Tutankhamun-s3n Год назад
Nyimbo ngumu sana kuielewa inahitaji utulivu wa kutosha
@nelsonkimutai5526
@nelsonkimutai5526 5 лет назад
I love the patriotism in this guys music,
@abdulhalim5950
@abdulhalim5950 8 лет назад
nyimbo kamuimbia MAGUFULI kama anamgahamisha kua nchi ya Tanzania ina maajabu mfano vijana wamesoma ila hakuna ajira. aliposema. " watu huja na bahasha za kaki na kuhoji kama hamtupi taka shimoni. Pia kamfahamisha kua wahalifu waliokuwemo nchini hawaadhibiwi. mfano akiposema- " watu wa nyumba hii hawaendi chooni wala jalalani kutupa taka shimoni
@husseinhassainlugeje6042
@husseinhassainlugeje6042 6 лет назад
Asante
@eliyadigasson6679
@eliyadigasson6679 4 года назад
Vr good
@piusthomas5713
@piusthomas5713 2 года назад
PongeZi pia kwa director aise ameitendea haki hii ngoma
@shankyse2576
@shankyse2576 7 лет назад
Mimi shabiki wako mkuu..... Nairobi/ Kenya
@Nairobipicturesstudios
@Nairobipicturesstudios 3 года назад
Alaaah! Mrisho wanidekua kwa mishororo na ushairi wako kila tungo lanijenga ajabu. mie nasoma sana fan wako mpya hapa toka Kenya.
@mabudaissere2295
@mabudaissere2295 7 месяцев назад
Ana kiazi cha moto mdomoni ataimbaje sasa
@planbmauwezo4853
@planbmauwezo4853 Год назад
DAH W MZEE MWENYZ MUNGU AKUPE UMRI MREFU SAN
@ibrahimzuberi1029
@ibrahimzuberi1029 8 лет назад
yan nimeskiliza zaid ya 10 tym sijaeleza zaid ya bahasha za kaki2...daaah shkaaaaamooooo burazaaaaa
@nyabisemaro2095
@nyabisemaro2095 6 лет назад
Wana fasihi tupo tunakuewaga sanaaaa Asante MWL wanguu wa kiswahili MWL MACHUMU, MWL Alexander na PRISCA Bila nyie mm nisingejuaaa ujumbe wa mpoto Mbarikiwe sanaaa
@rich.kizza10
@rich.kizza10 2 года назад
hii ngoma bhana ni balaa
@masirian06
@masirian06 2 года назад
nazipenda kazi zenu safi sana wanaTanzania... mwatufunza maadili mema ya upendo sis kama wakenya lakini wote tu waafrika na hivyo nafurahia kazi zetu,, hongera sana
@kihanda2554
@kihanda2554 8 лет назад
Long live Mrisho mpoto. Nimekuelewa vzr mnooo. Mfumbie mtoto mkubwa ang'amue
@hadijapazia8255
@hadijapazia8255 4 года назад
Naikubali xn hii ngoma🔥🔥🔥🔥👌🏻👌🏻👌🏻👌🏻
@sirajiabdallah6824
@sirajiabdallah6824 10 месяцев назад
Wale WA 2023 tuktane
@ezekielbituro7969
@ezekielbituro7969 8 лет назад
nimeilewa asee...mashairi yanaeleweka kiasi! HII NDO TANZANIA
@saknamtaki8168
@saknamtaki8168 7 лет назад
Nyimbo nzuli kweli uko posh kak kimziki nakupa respect
@amosnguvumali7869
@amosnguvumali7869 8 лет назад
hahaha kwel mtoto hawez kuungua kwa kiaz kilichopo kwenye kiganja cha mama yake ahsante sana
@emmanuelmsambya5293
@emmanuelmsambya5293 5 месяцев назад
Hii nyimbo iliimbwa na watu wenye IQ kubwa
@wilhardjohn8287
@wilhardjohn8287 8 лет назад
huyu hanscana ni director anayejielew pengine kuliko wote kwa sasa young but a real inspiration in music industry
@juniorlangen2648
@juniorlangen2648 2 года назад
Wewe ni mwalimu , kazi zote zako hujawahi kosea
@mwalimmaroaibrah8051
@mwalimmaroaibrah8051 7 лет назад
Dah! Kwakweli mashairi yamesimama sana. Hongera Mrisho kwa mashairi haya
@paulomroki1979
@paulomroki1979 3 года назад
2021 am still listening!! Mungu akubariki sana
@bwakilamychanel5951
@bwakilamychanel5951 5 лет назад
sizonje hii ndiyo nyumba yetu ingia uyaone hapa anaizungumzia tz yetu jinsi watu wanavyopenda rushwa na kurisishana madaraka na wakat kila mtu ana haki
@iamjimba9775
@iamjimba9775 8 лет назад
duuh! maishairiii nondo sana
@sirialemmy37
@sirialemmy37 8 лет назад
hehehe yes yes mr
@hermanngaiza9327
@hermanngaiza9327 8 лет назад
Kiukweli wimbo umetulia una ujumbe wa maana sana.ukionesha kwamba tuwe na nguvu na kupambana ahsante brother Mpoto
@shamsally6277
@shamsally6277 3 года назад
Genious sijawahi pata ona
@xxlnairobitv9503
@xxlnairobitv9503 8 лет назад
Can't get enough of this song. Good Job. From Nairobi Kenya.
@tiaschris7070
@tiaschris7070 7 лет назад
aisehhh hii nyimbo ni hatari, xijui km ntakuja kuisikia nyimbo km hii tena
@alfredally1955
@alfredally1955 3 года назад
Tanzania inaonekana masikini ndani nitajiri hyo ndio jambo nimeona
@moviccreativestudio
@moviccreativestudio 7 месяцев назад
Mimi na mpoto ndio tunaelewana hapa wengine kapa
@johannesshornest4916
@johannesshornest4916 8 лет назад
we unayesema amealibu au angemuonesha sizonje auna uelewa kumbuka wimbo uu ni fumbo akikuonyesha sizonje utaelewa yeye mpoto anatupa mtiani tumjue sizonje ni nani kua mwelewa sio unakulupuka kuongea tu au unadhani mpoto ni sawa na wale wa mpenzi nakupenda
@bitaetenge3989
@bitaetenge3989 8 лет назад
Johanness Hornest Mbona hote mnabaki jujuhu majela yamejengwa lakini wafisadi wakubwa ambao wangefaha watupwe na kuozea huko kama kinyesi kinavyo hozea chohoni awatupwi huko. Wasomi wanaho maliza awapewi kazi wanashinda waki zunguka mahogisini lakini awapati milango. Sizonje niserekali na nyumba ni inchi. Sio Tanzania tu Africa yote.
@barick
@barick 7 лет назад
Huyo mzee anavyo Lia na mimi nimelia mmh!sizonje
@isackyakobo7829
@isackyakobo7829 4 года назад
Asante sizonje, Kwa sasa wenye nyumba tunalala vyumban piah, Magufuli Oyeeee! Bahasha za kaki tu ndo bado ila karbu tena 2020, ulitatue na hlo! Kwa sasa hawapt madrishan tena,
@richardjuma7708
@richardjuma7708 4 года назад
Hatari sana
@jovituskamugisha
@jovituskamugisha 8 лет назад
Maudhui, mashairi, rekodi,... Nimeipenda. Ahsante sana Baba Mrisho Mpoto.
@christopherkipeke7547
@christopherkipeke7547 8 лет назад
Mlisho kwangu hata usipoimba, kitendo cha kukuona nahisi nguli na gwiji la sanaa anajambo analitoa
@NabakiZanzibar
@NabakiZanzibar 8 лет назад
Natamani sana kuona hii video on MTV, Trace, ect. coz idea na shots zimetulia sana. Nashukuru sana kwa mashaili (Poetry) #MrishoMpoto kazi nzuri sana. Mungu akubariki, iposiku wataelewa tu.! @ThomGypsy #ThomGypsy
@tibrucemushi1735
@tibrucemushi1735 7 лет назад
picha mbili kubwa.... KATIBA.😂😂😂😂😂😇
@ibrahimjuma8577
@ibrahimjuma8577 8 лет назад
hongera Mjomba mi huwa nakuelewa sanaa nice song babaa
@enockjohn332
@enockjohn332 8 лет назад
mtoto hawezi kubembelezwa kwa wimbo mbaya,na mtoto aungui na kiazi kilchopo kwenye kiganja cha mama yake,nimekusoma mjomba
@JoashJoseph-yt7en
@JoashJoseph-yt7en 6 месяцев назад
Sijaelewa ki😢😢2chcht
Далее
Mrisho Mpoto - Waite ( Official Video HQ)
5:24
Просмотров 792 тыс.
SAMAHANI WANANGU | MRISHO MPOTO FT MAUNDA ZORRO
7:07
Sharo milionea Ft Dully Sykes ( official Music video)
4:51
Banana Zoro - Zoba
7:43
Просмотров 1,3 млн
Neema
6:56
Просмотров 218 тыс.
MPOTO: 'Ukweli Mtupu Kuhusu Fumbo la 'Sizonje'
10:06
Просмотров 68 тыс.
Isha Mashauzi - Sio Levo Yako (Official Music Video)
4:11