Тёмный

Dizasta Vina - Mbuzi 

Dizasta Vina
Подписаться 52 тыс.
Просмотров 90 тыс.
50% 1

Official Lyric video of the record MBUZI as prepared and performed by Dizasta VIna. Off the studio album, A father figure
Stream/Download
RU-vid - • Dizasta Vina - Mbuzi
Mdundo - mdundo.com/song/2936009
Boomplay - www.boomplay.com/albums/88641986
Audiomack - audiomack.com/dizastavina/son...
Apple music - / mbuzi-single
Other Musical contents
Audiomack - audiomack.com/dizastavina
Boom play - www.boomplay.com/artists/3288611
RU-vid - / dizastavina
Mdundo - mdundo.com/a/2263
Spotify - open.spotify.com/artist/1IC2b...
Apple music - / dizasta-vina
Deezer - www.deezer.com/artist/67967532
Spotify Playlist - open.spotify.com/playlist/37i...
Connect with Dizasta Vina on social medias
Instagram - / dizastavina
Twitter - / dizastavina
Facebook - / dizastavina07
sw.wikipedia.org/wiki/Dizasta...
Business: Pan.authentik@yahoo.com
Website - bio.link/dizastavina
Lyrics
Mbuzi alipata wadudu kwenye kwato
Iliathiri furaha na nguvu alizonazo
Mchungaji alihakikisha mbuzi ananawa
Aliondoa wadudu wote kisha akamweka dawa
Alikampangusa chawa akampa chakula kwa wakati
Akamjengea chumba kwa nafasi
Ajisikie huru, Akashika ratiba na itifaki
Muda ukapita afya mbuzi ikatamalaki
Mtaa ikahamaki ukasukwa uvumi
Kuwa bwana Kheri Anatoa muda kisha sumni
Japo hali yake ya uchumi ilikuwa ni duni
Aliuza matunda mboga chache na kuni
Hakuna siku mbuzi alipiga kelele kwa njaa
Watu walimwonea gere balaa
Alinawiri kwa kilele cha umaridadi
Majambazi walipiga misele kadhaa
Na usiku hauwi mwanana akisikia mbiu
Mbuzi akilalama kwamba anahisi kiu
Mchungaji alikuwa macho, Akatambua kuna
Magonjwa nyemelezi akavumbua chanjo
Mbuzi aling’ara alinona
Manyoya yalitawala kuashilia afya kila kona
Hakuwepo hata mwanga mmoja wa kuroga
Hata Waliojaribu kuchanja walikoma
Najiuliza maana ya upendo nini
Mpaka uwe na kingi ndio ushee?
Au pesa kipindi michango ya sherehe?
Au mzazi anayetamani uendelee?
Ndio maana anakulea ile umlee
Inasadikika kuwa upendo wa kweli ni kujali
Mama mzazi homa ikikushika tu halali
Tabasamu analokupa unaposhika Masarali
Ungekuwa hai ingekuwa kutoa mimba ni halali?
Wazalendo wanahitaji hela na nyadhifa
Wanalipwa kutetea sera za taifa
Wadini wanakumbatia itikadi na imani yao
Mpaka wanamwaga damu wenzao
Au mapenzi kwenye timu inapoingia mtimani
Unaumia inashika mkia na hauhami
Kufichiana dhambi tabia wanayoisifia masela
Au mjeshi anavyofia bendera
Nani anajua siri ya kupenda penda?
(Ni) kujitoa sadaka kwa ajili ya mwenza?
Wapo wanaosema kuwa kupenda ni ushupavu
Wanaumizwa wanachukia wanaandika vitabu
Ukijua mwenza wako ana mtu anampenda
Utampa nafasi aende upige moyo konde?
Mama akifariki na una dawa ya kusahau maumivu
Swali ni utakula vidonge?
Je upendo wa kweli ni mpaka aagize mungu?
Aliyesema ufuge paka alafu umchinje kuku
Amemmtoa mwanaye kama mdhamini msalabani
Awafie watu ambao dini hazifanani
Bado Mawazo yananisumbua nasinzia
Nawaza ingekuwaje tungechagua familia
Je mtoto angempenda baba angekuwa lofa?
Au Baba angemchagua mtoto angejua ni shoga?
Wanandoa tungekuweka kwenye Time Chamber
Muda urudi ungemchagua patner wako tena?
Wangapi wanawish wangepita sehemu hii?
Wangapi wangemchagua Justin Bieber na Jay Z?
Kabla ndoa haijakufunga pini
Jiulize kama mkeo angekuwa na wewe ka' ungekuwa chini?
Licha ya hizi nyimbo zinazofanya watu walie sana
Washikaji walingoja niwe msanii ndio niwe mwana
Pengine inabadili maana ya upendo
Na kuacha swali upendo je ni haja au matendo?
Mchungaji alifuga mbuzi alifuga na ajenda
Alimjali lakini si kwa sababu alimpenda
Kwani ilipofika sikukuu alitoa vitu
Sufuria jungu kuu akanoa visu
Yule mbuzi mzuri aliyenona sana
Ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama
read more about Mbuzi genius.com/Dizasta-vina-mbuzi...

Видеоклипы

Опубликовано:

 

16 апр 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 725   
@dizastavina
@dizastavina 2 месяца назад
Nunua nakala yako ya A FATHER FUGURE Kwa whatsApp, Email au telegram. Tuma 10,000tzs au 650ksh kwa Mpesa +255 762 158 871 au Tigopesa +255 655 696 811 (Jina Edger Vicent Mwaipeta). Kisha tuma jina au sms ya malipo kwa hizo namba.
@hamismbwana8592
@hamismbwana8592 2 месяца назад
Ina nyimbo ngap?
@danielsande4815
@danielsande4815 2 месяца назад
@@hamismbwana8592 20
@thomaslima921
@thomaslima921 2 месяца назад
Poa big brain rapper,ndyo maana DUBO alisema mc mbovu utakata tamaa ukimsikiliza dizasta we ni darasa tosha
@Mungopark187
@Mungopark187 2 месяца назад
Jamn mkuje sasa mnunue albamu yenye magoma makali.. Verse kali, beats kali.. Yani kilakitu kikali.
@terminal_Kituo
@terminal_Kituo 2 месяца назад
Despite being an MC, I bought this Albam na sijajutia ...nafikiri vijana wengi wangefata failsafA za dizasta maana nawaona Akina Karl max Napoleon hill na wengine wengi Sana ktk history...walioongelea kuhusu ukombozi wa kifikra...dizasta katuletea mawazo Yao in a simple form Kwa Lugha adhimu Sana ya Kiswahili akiilenga jamii yetu....AFF ni album yangu pendwa na nasikiliza Kila siku ubongo unapata Chakula...Dizasta is the master Art, and the only orchestrated symphony...
@magotimtani2180
@magotimtani2180 2 месяца назад
Sehemu ya kwanza ya wimbo inaonekana kuashiria uhusiano kati ya mchungaji na mbuzi kama mfano wa uhusiano kati ya watawala na wananchi, au hata kati ya watu katika jamii. Mchungaji anawakilisha nguvu au serikali, wakati mbuzi anaweza kuwakilisha raia au watu wa kawaida. Mchungaji anajitolea kumtunza mbuzi, ikionyesha wajibu wa serikali kwa wananchi wake, lakini kuna maudhui ya utata kuhusu nia ya mchungaji - je, anamtunza mbuzi kwa upendo wa kweli au kwa sababu ya faida zake binafsi? Sehemu inayozungumzia bwana Kheri inaonesha changamoto za kiuchumi na jitihada za kujikimu katika jamii. Ingawa bwana Kheri anajitahidi na hali yake ya uchumi ni duni, anaonyesha uvumilivu na ujasiri katika kukabiliana na changamoto za maisha. Katika sehemu inayohusu upendo, wimbo unachunguza maana ya upendo na kujitolea kwa wengine. Inaleta mifano mbalimbali kuhusu jinsi upendo unavyoweza kueleweka na kutekelezwa katika maisha ya kila siku, iwe ni katika uhusiano wa kimapenzi, uhusiano wa kifamilia, au hata katika uhusiano kati ya watu na imani zao au utamaduni wao. Mwisho wa wimbo unatoa picha ya kusikitisha ambapo mbuzi, licha ya kutunzwa na kustawi chini ya uangalizi wa mchungaji, anakatwa na kuliwa. Hii inaweza kuashiria udanganyifu wa watawala au nguvu kuu katika kutumia na kudhulumu watu wa kawaida kwa manufaa yao binafsi, huku wakionekana kama wachoyo au wasiojali. Na hii verse ya mwisho ndio inasahihisha nia ya utata inayotajwa katika verse ya kwanza. Verse ya kati, ni kama anaonesha tu upendo wa kweli ni nini, ili aje afanye hitimisho vema kwenye verse au eneo la mwisho
@alphanlukombe3774
@alphanlukombe3774 2 месяца назад
Upo sahihi mwamba
@ferdnandshija2334
@ferdnandshija2334 2 месяца назад
swadakta
@brunoh_bx
@brunoh_bx 2 месяца назад
Asantee kwa uchambuzi👏👏👏
@user-cg3cm4qv4q
@user-cg3cm4qv4q 2 месяца назад
Oya, huu mbona kama unamuhusu sana Lunya
@munixpicentertainment
@munixpicentertainment 2 месяца назад
@@user-cg3cm4qv4q😂😂😂😂 ila watu n wasen
@insectondama798
@insectondama798 2 месяца назад
Mchungaji alifuga mbuzi Alifuga na agenda Alimjali, lkn si kwa sababu alimpenda Kwani..... Ilipofika sikukuu ..alitoa vitu Sufuria jungu kuu.. akanoa kisu YULE MBUZI MZURI ALIENONA SANA , NDIE... ALIECHINJWA NA ADHUHURI ALICHOMWA NYAMA
@YunusYahya-gr6ks
@YunusYahya-gr6ks 2 месяца назад
Waliorudiaa hio nyimbo Zaid ya.mara 10 piga like hapa Jamaa anauwasha Hakuna kama hii kichwaa
@lukasbuyamba4135
@lukasbuyamba4135 2 месяца назад
Hem ngojeni kwanza. Mna hakika huyu jamaa ni mwanadamu wa kawaida.. aseeee big up brother Ediga
@gotintito4455
@gotintito4455 2 месяца назад
Rafiki zangu wengi wamekuwa wafuasi wa dizastavina baada ya kuwasikilizisha ngoma kazaa...Jana Tu Kuna mwana mmoja kaisifia sana hii ngoma alafu Leo umekuwa released aisee...tunaomba uandae show moja Yako mwenyew tutaingia kwa gharama yoyote.
@ibni_H2TL6r
@ibni_H2TL6r 2 месяца назад
Coment Yangu Ni Ya 99 Dizasta Vineration 17 April 2024 when you read My Comment In 2099 Generation this Dude Was The Best & Genius
@allychilinga1958
@allychilinga1958 2 месяца назад
Ina pigwa violin inapigwa guitar Tunasikia neno baada ya neno..mpangilio mzuri wa Mashahiri hakuna yo-yo..
@user-vy1lw6wk7y
@user-vy1lw6wk7y 2 месяца назад
Aseee nmeelewa kuwa ukiskiza nyimbo za vina ni sawa na siskilizi nyimbo za wanadamu wenzetu..bado natafuta jina la kiumbe wa kumuita tofaut na binadam wa kawaida ila sijafankiwa kupata asee👊🏼🙌
@CertifiedStoic
@CertifiedStoic 2 месяца назад
Tulionunua Album day one tu ilivyotoka tunakosa cha ku-comment maana tulishachambua wimbo mpaka tukauchambua tena. Big Up Vina 🙌
@ismailmtengwa8370
@ismailmtengwa8370 2 месяца назад
Jamaa kipindi unajiita dizasta vina ulikuwa unajua kuwa jina lako litakuwa linaendana na vina vyako mwanangu unajua sana sioni wakukufananisha nae
@msimika_III
@msimika_III 2 месяца назад
Nadhani ni muda wa kukubali sasa kuwa Dizasta vina ndie msanii mwenye maarifa mengi zaidi na ana namna nzuri zaidi ya kufikisha kuliko msanii yeyote wa hip hop kwa sasa Asilimia 90 ya nyimbo za hip hop bongo humalizi hata verse moja unaona unazichosha tu ngoma za masikio yako, lakini ukimsikiliza muwa wa Dizasta vina unatamani hata uwe na verse kumi Dizasta vina ndie msanii pekee ambaye huwa nakuwa na shauku sana ya kusikia his next project, bro is pure genius, too good for this industry Sijui hii nyumba ya hip hop imebaki na mihimili mingapi mpaka ianguke ila Dizasta vina ni miongoni mwa mihimili inayofanya ili jumba la hip hop lisianguke All the best Dizasta vina natumai utakuwa na Madusko yanayoendana na kipawa chako na juhudi ulizowekeza kwenye sanaa yako
@JREMPIRE-jd1ms
@JREMPIRE-jd1ms 2 месяца назад
mifumo ya taifa letu d..vina umeuwa...🙄🙄 yule mbuzi mzuri aliyenona sana ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama......
@jovinkivelege7604
@jovinkivelege7604 2 месяца назад
SIO POA WE JAMAA UNAJUA
@susumantalanta8505
@susumantalanta8505 2 месяца назад
Siku zinakuja hili Taifa litabadilika, vijana hawata kuwa inspired na machawa bali ngoma kama hizi....thamani yako itakuwa ya juu sana....Big Up Rasta
@robygeniuz
@robygeniuz 2 месяца назад
Nadiliki kusema tangu niwe mshabiki wa HIPHOP uyu mwamba ndio msanii wangu bora tangu niijue hiphop nikiipokea mikononi mwa prof J oyaaaaa 👊
@user-badboyrozay
@user-badboyrozay 2 месяца назад
Vina juu ya vina humu ndani Kuna bonge la disaster kiufupi hamna usalama🔥🔥❤
@SAMAMBIRE
@SAMAMBIRE 2 месяца назад
Mnasifia sana tungo za vina ila mnajifanya kama hamuoni namba za kutuma iyo miamala mazee afu kesho na kesho kutwa vina aka pause music mtasema vina kapotea
@gajalugano6808
@gajalugano6808 2 месяца назад
Fact buddah
@lampadshigonko3006
@lampadshigonko3006 2 месяца назад
Nimeelewa kipande cha mbuzi kinanikumbusha tukio la ngwajima kula muhumini wake.
@soudyruge-fi9xv
@soudyruge-fi9xv 2 месяца назад
Huyu mwamba nilichelewa kumjua ila nilivomjua nikamfanya Best RAPPER wa muda wote haiwezi kupita siku bila kusikiliza ngoma zake kama 5, nikianza na TRIBULATION, ACHIA JALA, WACHEZAJI WA TIMU, NO ONE IS SAFE, (zote) na HATIA (Zote)
@fredrickmsomba4123
@fredrickmsomba4123 2 месяца назад
Likewise
@langemwepesi
@langemwepesi 2 месяца назад
Kama vile nazama namuona mwamba kadondosha sijui niseme nizare la professa😂❤
@godblessluvanda9808
@godblessluvanda9808 2 месяца назад
Kweriii huyuu jamaa NI NYOKOMBILI 🙌🙌🙌🙌🙌🎧🎧🎧🎤🎤
@YunusYahya-gr6ks
@YunusYahya-gr6ks 2 месяца назад
Yanii huyui mwambaa anapigaa mamboo ambayoo hata fid q anakubalii mwambaa anajua kufichaa maana huyu ni kama langaa wa pilii ila mwambaa sijuii wakumgananisha naee dizastaa ni zaidiii yaoooo aiseeee
@rockonsonmlandi2818
@rockonsonmlandi2818 2 месяца назад
Mimi naomba bifu ya vina na Rapcha tena 🤤...
@user-hx7dk9vb4h
@user-hx7dk9vb4h 2 месяца назад
Marafiki zangu wamebadilika na wamekuwa wakielimisha wengine kupitia mistari ya huyu mwamba wengine walipata wapenzi kweli huyu ni Mungu wa Rap 100%
@ayubukaduma1017
@ayubukaduma1017 2 месяца назад
vina tungo imesimama mzee , n wateule wachache sanaaa tunaelewa izi chuma unatuachia keep moving broo tunakufuata
@user-badboyrozay
@user-badboyrozay 2 месяца назад
Vina juu ya vina humu ndani Kuna bonge la disaster kiufupi hamna usalama🔥🔥
@patrickmgaza9927
@patrickmgaza9927 Месяц назад
hapa ndipo tunapopimwa IQ zetu huyu jamaa kama umezoea kuskiliza singeli huwezi muelewa bonge moja la ngoma
@Antary9
@Antary9 2 месяца назад
BLACK MARADONA. SALUTE KWA MADINI BRO.
@dankirunda3368
@dankirunda3368 2 месяца назад
Daaah peni imezingatiwa sana humu 🔥
@JosephRobert-uf5dr
@JosephRobert-uf5dr 2 месяца назад
Dizasta aseee sema media za bongo chai sana hawasikiagi hivi vyuma kutoka kwa mwana kuvichaka...
@terminal_Kituo
@terminal_Kituo 2 месяца назад
Sisi hatutaki media za Bongo....tununue Albam Kwa Dizasta ...Vina
@rigajunior8487
@rigajunior8487 2 месяца назад
Mwanangu...! Sema tu kiki ndo hunaga but katika watu ambao ni blessed na branded upo kaka yan ni wewe na darassa yani ni brand za kitofauti mno na ladha kali❤❤. Mbeyahood.
@shenamtukufu1224
@shenamtukufu1224 2 месяца назад
Asante sana homie hujawai tufelisha wana.
@ahutamorris
@ahutamorris 2 месяца назад
Utaratibu au mpangilio wa kutuma pesa kutoka Kenya hadi Tanzania ni upi kakangu @Dizasta Vina
@mchattachattanoga7795
@mchattachattanoga7795 2 месяца назад
Kweli dizasta akiwaka anaweza kumgeuza fid akawa sajna
@Yegon254
@Yegon254 2 месяца назад
Hii ni aina ya mziki ninaoupenda haswa wakati nimetulia
@Goalscores12
@Goalscores12 2 месяца назад
Dizasta vina ni Extraordinary 😂💥💥
@omarabdulaziz3786
@omarabdulaziz3786 2 месяца назад
Level 5 sorcerer kutoka far future!!
@talebanistudio4513
@talebanistudio4513 2 месяца назад
Oya wanangu wa mziki mzuri kama huu tusiishie ku like na kusifia tununuue ngoma na tisapoti mziki mzuri ili mwana aendelee kutudondoshe ngoma Kali kama hizi Kuna vitu vingi vya kuimba ila wasanii wa bongo banaa mapezi mapenzi wana boa sana dizasta tuna kuaminia wapige msasa wasani wa mapenzi kila siku❤
@emmanueljames9215
@emmanueljames9215 2 месяца назад
👊 vina kisha somo, umesomeka vina uwezo wako hauwezi kupimwa kwa tuzo za pombe
@mukrimkhamis678
@mukrimkhamis678 Месяц назад
Uyu mwamba kma akili yako ya kawaida huwezi kumuelewa kbsa###@dizasta🔥🔥🔥
@stapinuswilliam860
@stapinuswilliam860 2 месяца назад
Japo hali yake ya uchumi ilikuwa duni liuza matunda mboga chache na kuni
@AhmadMuya
@AhmadMuya 2 месяца назад
Jaman na mm Leo naombeni like zenu håtä 10
@tariqkhassim4059
@tariqkhassim4059 2 месяца назад
SOON HUU MZIKI UNAANZA KUA NO 1 ON TRENDING INSHAALAH
@antonyngao131
@antonyngao131 2 месяца назад
Vina! Vina! Vina,nimekuita ngapi? Noma sanaa
@wilbardlameck8025
@wilbardlameck8025 2 месяца назад
Aliyeelewa hii ngoma anieleweshe tafadhari
@khatibkapire877
@khatibkapire877 2 месяца назад
Dizasta nataka nimguse huenda sio binadam
@mulanmike1997
@mulanmike1997 2 месяца назад
wa kwanza kucomment mbuziiiiiiiiiii
@faymarabdoul3590
@faymarabdoul3590 2 месяца назад
First like, just a minute ago. Mbuzi 🐐♑
@dizastavina
@dizastavina 2 месяца назад
Lets goo
@stanleysamwel2679
@stanleysamwel2679 Месяц назад
Daah wew jamaaa ni hatari m. It’s 2025 we here
@sharifukitori239
@sharifukitori239 2 месяца назад
Huu wimbo umeacha athari chanya katika mtazamo wangu kuhusu maana ya upendo..nina maswali kadhaa ambayo nimekosa majibu hadi sasa lakini kukosa majibu huko kunanifanya nitabasamu kila mara ninapojiuliza maswali hayo hayo. GOOSEBUMPS 1:16 1:48 2:00 2:12 Nahitimisha..Ringle ni mmoja wa Goated producers wa hapa bongo. Vinanda ya humu ni vyamoto mno kuvigusa🔥
@dizastavinafanaccount
@dizastavinafanaccount 2 месяца назад
Mwisho hapo wameandika Music by Dizasta kaproduce Dizasta hii. Beats za Ringle zina sign tag ya jina lake
@runtown____3587
@runtown____3587 2 месяца назад
Bro this guy deserves more support nunueni album much love dizasta.
@VictorKotein
@VictorKotein 2 месяца назад
Wewe mwamba unajua sana unafanya ubongo wangu utafakari sana
@hasanibakari6924
@hasanibakari6924 2 месяца назад
Serikali hainitambui na ushairi Wangu shule 😂👏👏👏🙌
@DennisUnju
@DennisUnju 2 месяца назад
Kudadekiiii unajua we Fara
@matugarecords
@matugarecords 2 месяца назад
Dizasta Mtu Mbad, My best Rapper hapa TZ 🔥🔥🔥🔥🔥🔥HAUPINGWI
@lucasjonas2987
@lucasjonas2987 Месяц назад
Kubababakee umu tu unajua sana mwanangu sema ndo ivo hauishi angani
@user-rq3xd2ef4f
@user-rq3xd2ef4f Месяц назад
Mmmh huyu mwamba tumpeleke trend ndo rapa bora now kwa bongo hapa diamond tuwekee huyu wasafi tuishi nae
@hashimswalehe1550
@hashimswalehe1550 2 месяца назад
ukijuwa mwenza wako ana anampenda utampa nafasi aende upige moyo konde🔞🧠🎤🎤
@wizzyjabary7777
@wizzyjabary7777 2 месяца назад
DIZASTA UMETISHAA SANA UJUMBE MZURIII NGOMA KALIII SANA🎉🎉🎉🎉🎉
@MalickMazikublood-gq2fs
@MalickMazikublood-gq2fs 2 месяца назад
Hivi dizasta unavyo andika wimbo kichwa kinakua kinauma au kuna machine unatumiga kutungia nyimbo zako, mm nahis sio kichwa cham2 kinacho andikaga
@allyhabibu1117
@allyhabibu1117 2 месяца назад
Acha wajisifie nimarapa bora ila wewe ndo mwalim wao✊✊✊
@thomaslima921
@thomaslima921 2 месяца назад
🎉🎉🎉🎉
@Jida-tz
@Jida-tz 2 месяца назад
Kama masikio na akili zako vilishazoea kusikia "WEE ZOMBII,,HAUJUIII" hapa hutoelewa kitu😂😂😂
@DullahXella-xb4cz
@DullahXella-xb4cz 2 месяца назад
DVN is G.O.T
@AbdulJuma-yj7py
@AbdulJuma-yj7py 2 месяца назад
Mwisho wa siku mbuzi akaliwa nyama😂
@KijukuuMtemi
@KijukuuMtemi 2 месяца назад
Makonda hii nyimbo isikulize kuna vitu utajifunza ukiisikiliza kwa makini @
@KijukuuMtemi
@KijukuuMtemi 2 месяца назад
Hii nyimbo imfikie makonda
@dmgaya8856
@dmgaya8856 2 месяца назад
@Mbuzi 💥💥💥
@Almarsprince254
@Almarsprince254 2 месяца назад
Nmedakia juu kwa juu,,,❤❤
@NachiLapa-zo9ld
@NachiLapa-zo9ld 2 месяца назад
Magoma ndo kama hayo kutoka kwenye album ya dizasta vina inaitwa a father figure 😅😅 Sasa kuelewa kilichoimbwa kwenye hizo ngoma inategrmea na matokeo yako ya form four ulipata ngapi!😂😂😂
@AmiriMchikirwa
@AmiriMchikirwa 2 месяца назад
😂😂😂😂 FOUR KARIBU NA ZERO
@musafadhili7950
@musafadhili7950 2 месяца назад
Na sisi tulio kimbia hata form 4 hatujafika inakuaje hapa😂😂😂
@cdeegwau551
@cdeegwau551 2 месяца назад
😅😅😁
@mbegumohammed7398
@mbegumohammed7398 2 месяца назад
Yani huyu mwamba kashashindikana kabisaaa🙌🙌
@shaddyqualityfurniture3595
@shaddyqualityfurniture3595 2 месяца назад
Goat 🐐
@cauyadibo9653
@cauyadibo9653 2 месяца назад
Dizasta mungu azidi kukuweka uachie vigongo we ndo msanii wa hip-hop Wang wa milele
@insectondama798
@insectondama798 2 месяца назад
This ma'faka is an alien💥💥
@pcthemaster9096
@pcthemaster9096 2 месяца назад
Ujawai kosea mzee. Nice
@abelmsaki
@abelmsaki 2 месяца назад
Kazi nzuri sana mwana fanya kazi moja na bele 9 am sure it will be a banger
@chidi_don
@chidi_don 2 месяца назад
Unyama ni mwingi sana bro unajua sana 🔥💯✈️
@BonyTz
@BonyTz 2 месяца назад
ivi uyu mwamba ni mtanzania kweli 😅😅
@leonardmhagama5828
@leonardmhagama5828 2 месяца назад
😅😅😅Aseee mwenyewe simuelew huyu mwamba sasa tukubaliane tu kuwa yeye ni toleo la mwisho la chapa yake.
@invocavitmbise5296
@invocavitmbise5296 2 месяца назад
Hahahahaha wee unawaza kama ni Mtanzania badala ya kuwaza kama yupo duniani??😂😂
@allyseba172
@allyseba172 2 месяца назад
​@@invocavitmbise5296mm nime skilza lakin daaah sjaelewa bado
@denzetz3391
@denzetz3391 2 месяца назад
Ni m-argentina husikii MARADONA
@hinikasteve176
@hinikasteve176 2 месяца назад
Ni mtanzania ila.sio binadam mwenye akili ya kawaida
@elizajafaphary6559
@elizajafaphary6559 2 месяца назад
Umetisha mkali wa vina 🔥🔥🔥
@gaddibullahtzg5635
@gaddibullahtzg5635 2 месяца назад
Dizasta vinaaaaa umetisha sana nasubiri uchambuzi but you deserve great Honor in Hip-hop Industry
@josephmasenga7718
@josephmasenga7718 2 месяца назад
Nipo kwenye top 2 and iam not second ile ngoma uliua sana
@dismasmushi9328
@dismasmushi9328 2 месяца назад
Kila siku unaniachia lines kwa kichwa leo nmeshika hii,,, je mtoto angempenda baba angekuwa lofa au baba angemchagua mtoto angejua nishogaa
@vancykhan234
@vancykhan234 2 месяца назад
na wangap wangechangua huu wangap wangemchangua justin bibier na jay z
@show...002
@show...002 Месяц назад
ili umuelewe disasta ni lazima umsikilize mara nyingi na usiwe na mambo mengi wakati wa kumsikiliza maana ana vina vikali mno vyenye mafumbo ..anawapa somo mbuzi wanaotamba kwa mistari miraisi na kujiita wakari wa hiphop
@tariqkhassim4059
@tariqkhassim4059 2 месяца назад
BILA MEDULA HUWEZ KUENJOY MZIKI MTAMU HUU
@AhmedYasseen-eg2kz
@AhmedYasseen-eg2kz 2 месяца назад
Black maradonaa..... Vinaaaa🙌🏾🙌🏾🙌🏾
@shenamtukufu1224
@shenamtukufu1224 2 месяца назад
NONDE SUA KWA KWA MZEE NANI? 😢AU MSWANGA AHAHA
@mozu2450
@mozu2450 2 месяца назад
Lazima uwe msomi na mwenye falsafa ya hiphop ndo uweze kumuelewa DIZASTA🔥
@makero04
@makero04 2 месяца назад
Oya hii ngumu mno
@ibrahimmrutu
@ibrahimmrutu 2 месяца назад
​@@makero04🤣🤣🤣
@essauleesomogo2468
@essauleesomogo2468 2 месяца назад
Je upendo wa kweli aliagiza mungu aliesema tumfuge paka tumchinje kuku?? 😂🙌🙌🙌😊
@IbrahimuRamadhani-vy8wz
@IbrahimuRamadhani-vy8wz 2 месяца назад
ila @dizasta hapa umeniacha bhna
@bahopamontana6381
@bahopamontana6381 2 месяца назад
Kama kweli unampenda Dizasta em tukanunue Iyo nakala ya A FATHER FUGURE mapema saaaaaana... 2:36
@user-gx4of6cc2x
@user-gx4of6cc2x 2 месяца назад
nikiwa mkubwa niwe kama wewe, sijui unamaanisha Nini huu wimbooo😢😢😢😢😢😢😢
@LudeofficialXworldwide
@LudeofficialXworldwide 2 месяца назад
Hii Hot Kabsa🔥
@nicksonchisunga3062
@nicksonchisunga3062 2 месяца назад
GOAT DIZASTA VINA
@ramadhanishabani7095
@ramadhanishabani7095 2 месяца назад
Nakupenda Sana HIP HOP
@kingcopper_tz
@kingcopper_tz 2 месяца назад
🎉🎉 🎉nilivoona tittle nkajua distrack kwa dogo lunya 😂 kumbe ni more than that, bonge la masterpeace
@user-cg3cm4qv4q
@user-cg3cm4qv4q 2 месяца назад
Hii ni diss kwa Lunya, skiliza vyema
@soudyruge-fi9xv
@soudyruge-fi9xv 2 месяца назад
​@@user-cg3cm4qv4q😅😅😅 sio dis dhima ya hii ngoma iko mwishoni
@Simulizitube
@Simulizitube 2 месяца назад
Ukweli ni kwamba hakuna mapenzi ni maslahi yetu tu ila binaadamu tunadanganya mpaka nafsi zetu Maana hata mungu angekuwepo kweli na anavyodai anatupenda Kisha atutese ndio atupe pepo ni ujinga na uvundo tuliokaririshwa
@yasinimalya4001
@yasinimalya4001 2 месяца назад
Love from 🇺🇸, albam kali kama tindikali, Maji ya betri 🔥💯
@IbranMeekmill
@IbranMeekmill Месяц назад
ukimskiliza vina nd unaona tofauti kati ya wasanii na waimbaji
@innowatamaduni9248
@innowatamaduni9248 2 месяца назад
Sawaaaaa mzee
@onionpeeling5822
@onionpeeling5822 Месяц назад
YOOOOOOOOH , WHOS THIS GUY!!!!!!!!???. HES SOMETHING ELSE !, HE GOT BOOKS
@cdeegwau551
@cdeegwau551 2 месяца назад
😅😅😅 🙌 flow tamu, beat imetulia., japokua sijaelewa amemaanisha nin, DVN ni Allien 🙌
@thomaslima921
@thomaslima921 2 месяца назад
😂😂😂
@user-eh5fw5gj4c
@user-eh5fw5gj4c 2 месяца назад
Mbuzi ni mwanamke au demu
@mbegumohammed7398
@mbegumohammed7398 2 месяца назад
Dizasta ni fundi Aisee🙌🙌🙌🙌😂
@nickbway2052
@nickbway2052 2 месяца назад
Mbn kama bado haija isha mkuuu🎉
Далее
Dizasta Vina - Wachezaji wa timu
7:25
Просмотров 71 тыс.
ПОЮ ЛЕТНИЕ ПЕСНИ🌞
3:16:55
Просмотров 1,7 млн
ДВЕ МЕДИЦИНЫ В ОДНОЙ СТРАНЕ
43:03
TOXIC - SOUND YA BUFA EP 02
2:30
Просмотров 79 тыс.
Dizasta Vina - Hatia V
8:16
Просмотров 110 тыс.
Dakika 10 Za Maangamizi-  Dizasta Vina | Planet Bongo I
12:06
Hiki ndicho alichomanisha Dizasta Vina kwenye "MBUZI"
2:01
TOXIC - Meeh
2:33
Просмотров 132 тыс.
Dizasta Vina - Achia jala  Ft Kaa La Moto
8:34
Просмотров 110 тыс.
Artur Arakelyan - Ser Ka
3:02
Просмотров 757 тыс.
Janona
4:09
Просмотров 1,4 млн
Jakone, Kiliana - Асфальт (Mood Video)
2:51
Просмотров 3,3 млн
BABYMONSTER - ‘FOREVER’ M/V
3:54
Просмотров 46 млн
GODZILLA
2:09
Просмотров 883 тыс.