Тёмный

JINSI YA KUPIKA BIRIANI YA SAMAKI YA KUCHANGANYA (FISH BIRIANI) 

farwat's kitchen
Подписаться 121 тыс.
Просмотров 7 тыс.
50% 1

Website link👇
farwat.co.ke/2019/03/05/jinsi-...
Vipimo vya mahitaji yote mutavipata kwenye website.bonyeza link hapo juu.
Juana nami
Instagram@farwats_kitchen
Facebook@farwat's kitchen
Email: farwatasaid@gmail.com
❤❤❤
MAHITAJI
👉SAMAKI
🔸Samaki vipande 6
🔸 Kitunguu thomu vijiko vya Kula 2
🔸Fish masala kijiko cha kula 1
🔸Limau/ndimu
🔸 Chumvi Kiasi
👉ROJO
🔸 Tomato 8 zilizosagwa
🔸 pilipili boga
🔸Dania 1
🔸 Kitunguu maji 4 vilivyokatwa katwa
🔸Viazi vikubwa 3 vilivyokatwa vipande vya kiasi
🔸 Maziwa mala nusu kikombe
🔸 Kitunguu thomu kijiko cha kula 1
🔸 tomato ya mkebe/tomato paste
🔸 Pilipili manga iliosagwa kijiko kidogo 1
🔸 Mdalasini iliosagwa
kijiko kidogo 1
🔸Bizari nyembamba(jira) iliosagwa kijiko kidogo 1
🔸 Biriani masala kijiko kidogo 1
👉WALI
🔸 mchele nusu kilo
🔸karafuu
🔸 Chumvi
🔸rangi ya njano
MATAYARISHO
🔸 changanya mahitaji yote ya samaki kisha uwapake samaki vizuri.
🔸Weka rangi ya njano(Orange food colouring) na chumvi kwenye viazi kisha uvikange na uvieke pembeni.
🔸Kaanga vitunguu maji vitatu katika vile vinne mpaka viwe hudhurungi.weka pembeni.
🔸Teleka mafuta motoni uwakaange samaki mpaka waive vizuri kisha waeke pembeni.
🔸Weka mafuta kwenye sufuria uweke motoni tuanze matayarisho ya rojo.
🔸Mafuta yakishika moto, weka kitunguu maji kimoja kilichobaki ukipike mpaka kiwe hudhurungi.
🔸weka kitunguu thomu na spices zote uzipike Kwa sekunde kadhaa.
🔸weka pilipili boga na dania pia uzipike Kwa sekunde kadhaa.
🔸weka tomato, tomato paste,maziwa mala na chumvi kisha ufunike uache itokote Kwa takriban dakika 10_15.
🔸Rojo likiendelea kuiva, weka mchele uliouosha vizuri kwenye sufuria na maji Kiasi kulingana na mchele unaoutumia. Weka Chumvi na karafuu na uache ukauke maji ila usiive Sana.
🔸Rojo likishakuiva na kukauka, weka Viazi ulivyovikaanga, Kitunguu ulichokikanga, samaki na juu kabisa weka wali wako Kwa tahadhari.
🔸weka rangi ya njano.
🔸Funika biriani yako na uiache iive Kwa moto mdogo kabisa kwenye gass Kwa takriban dakika 15_20
🔸kama unatumia jiko la makaa, utafunika Kwa Moto wa juu na chini.
🔸 Biriani ipo tayari.
🔸pakua Kwa kutoa wali ulioko juu ili ubakishe rojo chini.
🔸Andaa mezani Kwa kachumbari, juisi ya maembe na achari ya ndimu/pilipili ya kukaanga.
🔴Kwa mapishi zaidi, utanipata you tube, farwat's kitchen.
Instagram:farwats_kitchen
Facebook: farwat's kitchen
🌹🌹🌹
Instagram@ / farwats_kitchen
Facebook@ / farwats-kitchen-226631...
Email; farwatasaid@gmail.com
❤❤❤

Хобби

Опубликовано:

 

4 мар 2019

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 16   
@fatumamohammed3734
@fatumamohammed3734 Год назад
Masha Allah mapishi mazuri shukran 👌
@farwatskitchen13
@farwatskitchen13 Год назад
Karibu sana ❤
@shammoha5297
@shammoha5297 5 лет назад
MashaAllah. 😋tamuu. Shukran 🤗👍🏽👌🏽
@nadhiruawadh445
@nadhiruawadh445 5 лет назад
Mashallah jazaka Wah haira
@foreveryoung6036
@foreveryoung6036 5 лет назад
Na pilipili Weeeee yashukaaaa Allah akubariki kazi yako
@farwatskitchen13
@farwatskitchen13 5 лет назад
Aaamiiin Shukran Habibty ❤
@switysasha163
@switysasha163 5 лет назад
Mashallah dia
@farwatskitchen13
@farwatskitchen13 5 лет назад
Asante😊😍
@ibrahimzuhaira600
@ibrahimzuhaira600 5 лет назад
Cooking simplified..ahsante
@khalidsaid2993
@khalidsaid2993 5 лет назад
niicceeee
@naimabruno1351
@naimabruno1351 5 лет назад
Wow ♥️
@princesswapwani5495
@princesswapwani5495 5 лет назад
Yummmmmmmy
@princesswapwani5495
@princesswapwani5495 5 лет назад
👍
@OfficialLutfia
@OfficialLutfia 5 лет назад
Video nzuri.. Asante
@saabiryaare9934
@saabiryaare9934 5 лет назад
Karibu kuwa chanal yangu na scribe tadadali
@ramadhanshigara3099
@ramadhanshigara3099 5 лет назад
Vizuri
Далее
BABA YANGU KIPOFU Full episode/15/ #love
50:40
Просмотров 318 тыс.
#TBCMEKONI - JIFUNZE JINSI YA KUPIKA BIRIANI
27:31
Просмотров 290 тыс.
🫓 Xorazim guch 💪  #littos
0:14
Просмотров 10 млн
КУАР КОД✍️
0:11
Просмотров 1,8 млн