Kwa mara ya kwanza namuona Jenerali Ulimwengu asiyeusema ukweli wote juu ya mtu uliyemfahamu vema, tena kwa kukusudia kabisa! Nadhani ulikusudia kumsifu kwa vipawa ambavyo alividhihirisha ktk nafasi alizozishika, jambo ambalo ni sawa kwako kulifanya na ni haki yake kufanyiwa. Lakini umekwepa kabisa kuzizungumzia hoja za msingi za nakisi kubwa ya maadili zilizojengwa dhidi yake ambazo ndizo zilizosababisha asipate fursa ya kuwa Rais. Hata kama kwa sababu zako zozote hukukubaliana na tuhuma nzito za ulaji rushwa dhidi yake, ulipaswa kuzieleza tuhuma hizo walau kwa kiasi kile ulichokijua, yaani "ktk sura mbili, tatu" kama ulivyosema mwenyewe mwanzoni mwa mazungumzo yako. Inafahamika, kama alivyosema jaji Warioba, mwl Nyerere ndiye aliyekuwa wa kwanza kumkataa Lowassa ktk vikao vyao vya uteuzi mwaka 1995. Nashangaa kwamba hata aliyoyabaini mwl Nyerere juu ya ulaji wa Lowassa umeyapa kisogo, ingawa wewe ktk makala zako nyingi umemtaja mwl kama mtu asiye na upendeleo. Kudai kwamba ''waziri mkuu ni tarishi tu'', na wakati huo huo ukimsifu juu ya ujenzi wa UDOM, shule za kata, hatua ktk mkataba wa DAWASA, n.k ni CONTRADICTORY. Kwa nini umpe sifa wakati hiyo ni "nishati ya tarishi/garasa?" Kwa nini basi tulimsifu sana PM Sokoine kama alikuwa 'garasa' tu?? Hivi ni lini Lowassa alikuwa mnyonge kiasi cha kukubali kashfa asizohusika nazo? Kila alipoulizwa juu ya alikopata ukwasi wake, alijibu "MIMI NACHUKIA UMASIKINI"...hivi hilo ni jibu kweli? Tunaujua ugumu wa kuyasema mabaya yake mtu aliyekutendea wema uliouhitaji, na Lowassa alisifika kwa ukarimu kwa wengi-nimemsikia Chenge, prof Tibaijuka na wengine. Huenda Jenerali nawe uko hapo, lakini tutakubaliana kwamba uongozi wa juu ktk nchi lazima utanguliwe na uadilifu wa kutosha ndipo nishati na uwezo wa uendeshaji vifuate. Vinginevyo, moral authority ya kuzuia maovu haitokuwepo na hatufiki popote!
General ungekuwa wewe Rais ungependa Mawaziri wako wajiamulie mambo makubwa ya nchi bila wewe kuyaafiki? Mfumo wetu ni wa Executive President. Bila badiliko kwa hilo, Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri wengine bado watabaki kuwa wasaadizi wa Rais na si vinginevyo.
Jenerali umezungumza vizuri kumuhusu Edward. Lakini ninachojiuliza wewe na wengine wenye platform za kuzungumza mlikuwa wapi wakati Edward anadhalilishwa na kukashifiwa? Mlikuwa wapi wakati Edward akitukanwa na kina Slaa na CHADEMA yao lakini alivyotukanwa na watu CCM alipohamia upinzani!!!!? Au na ninyi mnaendeleza falsafa ya kusifia watu wanapokufa!!!?