Тёмный

WAZIRI SILAA AMTAJA MTUHUMIWA NO. 3 WA UTAPELI WA ARDHI DSM-''TABIA YAKE NI KUPORA MAENEO YA WAZI... 

Global TV  Online
Подписаться 5 млн
Просмотров 16 тыс.
50% 1

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama kujisalimisha kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam akiwa na baadhi ya watu waliouziwa eneo la viwanja namba 1 kitalu 22 lililopo Kibada Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam ili kurejesha kwa wananchi eneo hilo liweze kujengwa shule ya sekondari.
Silaa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara katika eneo hilo Manispaa ya Kigamboni baada ya mgogoro huo kuwa wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo na baadhi ya watu walionunua eneo la shule akuwemo Allex Msama.
Aidha, Waziri Silaa amemtaja Alex Msama kuwa ni tapeli namba 3 wa viwanja jijini Dar es salaam na tayari ameishaagiza baadhi ya maeneo anayoyamiliki kinyemela kunyang'anywa ikiwemo eneo la wazi na eneo la fukwe lililopo Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa watuhumiwa wa utapeli wa viwanja ambao tayari wameishatiwa nguvuni ni Johnson Mahururu na Paul Mushi ambao wote tayari wameishafikishwa Mahakamani, ikiwa ni katika orodha ya matapeli 7 aliyowataja Waziri silaa kama matapeli sugu wa Ardhi.
Operesheni hii imekuja tangu kufanyika kwa Kliniki ya Ardhi ya Jijini Dar es salaam iliyoanza mapema mwezi Novemba 2023 na kuhitimishwa mnamo tarehe 3 Machi 2024 kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua jiji la Dar es salaam kwa muda mrefu.
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)
⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_y...
⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globa...
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusiv...
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/gl...
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx

Опубликовано:

 

4 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 37   
@55goodmen
@55goodmen 6 месяцев назад
AFRICA TUNAHITAJI HAWA VIONGOZI kama Slaa, we desperately need these leaders because we should away far up big time!!! Mh Slaa unafaaa kabisa. Piga jembe baba. Salute!!
@petroyohana1126
@petroyohana1126 6 месяцев назад
Elimu na kujielewa inakusaidia sana mheshimiwa waziri Slaa, umenyooka sana
@ChadeLukanyanga
@ChadeLukanyanga 6 месяцев назад
Asante kiongozi kiongozi watetee wanyonge baba slaa
@MarcoPeter-y5n
@MarcoPeter-y5n 6 месяцев назад
MUNGU Baba Wa Mbinguni Akubariki Sana Mheshimiwa na Timu yako
@MiriamAziz-z5t
@MiriamAziz-z5t 6 месяцев назад
ALEX MSAMA NI TAPELI MKUBWA SANA DAR....ANATUMIA KIVULI CHA DINI NA ANASHIRIKIANA SANA NA BAADHI YA MAAFISA ARDHI....AMEDHULUMU SANA HATA WAJANE, MAYATIMA NA WANYONGE WENGI NYUMBA NA ARDHI ZAO. HUYO MSAMA ALIWAHI KUPIGWA MARUFUKU NA WAZIRI WA ZAMANI WA ARDHI MH. LUKUVI.
@MiriamAziz-z5t
@MiriamAziz-z5t 6 месяцев назад
VIVA MH. WAZIRI SILAA....MWENYEZI MUNGU MTUKUFU AKUBARIKI.
@AbdulmalikFredrick
@AbdulmalikFredrick 6 месяцев назад
Asante kiongozi wangu nakupenda sana wazili wangu na laisi wangu Samia suluhuhasani Alha akufanyiewepesi inshallah
@petroyohana1126
@petroyohana1126 6 месяцев назад
Well said mheshimiwa waziri
@GervasiSafiel
@GervasiSafiel 6 месяцев назад
Global tivi njoo vikawe wananchi wanalia viwanja wametapeliwa njo na waziri ushuhudie waziri wetu
@davidbenson661
@davidbenson661 6 месяцев назад
Mungu akutunze sana muheshimiwa
@FredMwamgogwa-td6ni
@FredMwamgogwa-td6ni 6 месяцев назад
Huyu waziri anapiga kazi sana
@bagaileshabani3179
@bagaileshabani3179 6 месяцев назад
Mawaziri wote wangekua kama huyu bwana tanzania ingekua mbali sema mengine yote majingamajinga
@mahamudali1453
@mahamudali1453 6 месяцев назад
Mheshimwa slaa hawa matapeli wa arthi wakishirikyana na wasajili na mawakili waserekali wanawo towa nyaraka bandiya si uwapeleke mahakamani wafungwe?
@jasonwatz7457
@jasonwatz7457 6 месяцев назад
Wanamtandao mkubwa sana
@reginamkonya7614
@reginamkonya7614 6 месяцев назад
Hizo ni laana za watu unaowadhulumu na bado mungu atakuonyesha hicho unachojidaia karibu kinafika mwisho lips watu haki zao huyo rose muhando mwenyewe anakulaani.
@adamkapolo8817
@adamkapolo8817 6 месяцев назад
Kwa mara ya kwanza nimeanza kuwa na imani na wizara hii kazi zinaonekana,imulikeni mapinga bagamoyo dhulma ni kubwa sana
@emmanueligohe7276
@emmanueligohe7276 6 месяцев назад
Waziri njoo Bunju Beach wapo watumishi wako wanapima viwanja juu viwanja vingine.
@kamkubwa
@kamkubwa 6 месяцев назад
Mwamba anajifanya mtu wa dini kumbe mpigaji ila haya yanatokea mbona ardhi hawashughulikiwa wanaohusika kudhulumu nae? Watu wamekufa kwa pressure sababu ya kutapeliwa mali zao
@shabanponera2895
@shabanponera2895 6 месяцев назад
Daaah
@Hajer-be2kh
@Hajer-be2kh 5 месяцев назад
Huyu baba huwa kabila gani 😊
@petroyohana1126
@petroyohana1126 6 месяцев назад
Wizara imepata dawa
@reginamkonya7614
@reginamkonya7614 6 месяцев назад
So viwanja tu hata wafanyakazi wake hawalipi mishahara yao no tapeli hajalo anadai anajulikana na viongozi hata mama anammmudu anadhambi Sana halipi mishahara mheahimiwa angaoia na wafanyakazi wake was food point wanalia hawalipi Kama ni uongo fatilia mshenzi Sana huyu baba
@personalitiesan9806
@personalitiesan9806 6 месяцев назад
Kumbe hata msama duuuh
@georgekimasaofficial1629
@georgekimasaofficial1629 6 месяцев назад
Kitambo sana ndiyo mambo yake 😂😂😂
@TwahaMpakani-pn4ov
@TwahaMpakani-pn4ov 6 месяцев назад
Wew tunataka uwe rais baada ya mama
@allyfutto8763
@allyfutto8763 6 месяцев назад
mkwapuzi wa maeneo anamjuwa na kulindana ni kanuni inayo ihangamiza serikali na inaendelea kufumbiwa macho itawatokea puwani
@abdalaomari8430
@abdalaomari8430 6 месяцев назад
Safi Mweshimiwa waziri ombi langu Naomba uje uweke sawa mgogoro wa muda mrefu wa mpaka wa msitu wa kazimsumbwi na Chanika maana hii ni kero ya muda mrefu sana na mpaka sasa haujapata ufumbuzi wowote tunakutegemea sana ktk kipindi cha uongozi tutajua mbivu na mbichi
@GodfreyOsward
@GodfreyOsward 6 месяцев назад
Asipokuwepo slaa?
@GervasiSafiel
@GervasiSafiel 6 месяцев назад
Tunakuomba waziri wetu asilimia 90 wananchi wako wanalia wametapeliwa nanyumba washajenga na wanaishi nafamilia zao ndani njo waziri wetu uwatete wanyonge wako hatuna pakwenda
@JaziraMustafa-g9p
@JaziraMustafa-g9p 6 месяцев назад
FIDDA HUSSEIN NI MWIZI WA ARDHI ZA WANYONGE DAR
@emmanuelmlowe-ew7gx
@emmanuelmlowe-ew7gx 6 месяцев назад
Hao ni wewe nawababe sana,wapo wengi sana tz
@rwanzukafidel5019
@rwanzukafidel5019 6 месяцев назад
Hua inanoga sana anapotokea kiongozi mwenye msimamo,mwelevu,asiyetamaa,anajikubali na mtoto wa mjini anaejua chocho zote dash!!!! Itoshe kusema huyu copy ya JPM enzi hizo wizara ya ujenzi
@emmabrownmissana6996
@emmabrownmissana6996 6 месяцев назад
Unatafuta sifa Sana cheo Ni dhamana eti leo unadhalilisha watu kwa kuwaita matapeli ss umegeuka mahakama!
@farijala1
@farijala1 6 месяцев назад
Watu kama nyie mliozoweaWizi Hamkosekanagi. Na unathibtisha UBinaadamu wako wa hovyo. maana Hana Jemaatakalofanya mtu Umsifie, Jiangalie utakuwa Mchawiinaonekana una roho Mbaya
@Hongkongman2
@Hongkongman2 6 месяцев назад
Hujawahi tapeliwa atdhi ? Au na ww ni katika hao matapeli ? Yeye tapeli anapodhalilisha mayatima na wajane kwa kuwatapeli ardhi yao hua haikupi shida Inakupa shida pale tapeli anapotakiwa arudishe ardhi za watu tu sio ?
@AminiMsellem-gk3yy
@AminiMsellem-gk3yy 5 месяцев назад
Huna lolote inaonekana wanaotapeli ni jamaa zako waziri yuko Sawa na anafanya kazi
@geofreymgeni2668
@geofreymgeni2668 6 месяцев назад
Angekuwa maguguli hapo jama angelia paska jela huyo
Далее
WAZIRI SILAA AAGIZA ALEX MSAMA AKAMATWE
3:35
Просмотров 7 тыс.