Ulitujali sana Mzee wetu,na ulitupenda sana,Mungu akujalie afya njema na nyota yako ing'are kwa vijana wako hadija na khamisi,maana hukutumia cheo chako kwa watoto kuzarau askari,walikuwa na nidhamu ma uncle na tumewamiss sana(ku)
Mungu aendelee kukupa maisha marefu MH - MWADHIMU MKUU JWT ABDRAHAMANI. Umewaridhisha/IMPART watu na hasa vijana tunu uliyoipata katika maisha yako ya kulitumikia Taifa 🇹🇿. . Moyo wako ulioutoa hata mimi binafsi umenijenga na kunipa matumaini ya kutimiza ndoto zangu.. Nia yako njema toka mwanzo imetikisa. Amaizing GREAT HEART. SUPERB
Bonge la makala, aisee!!! Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi ana historia nzuri sana. Nimejifunza mengi kutoka kwake. Mola amjaalie umri wenye wingi wa afya njema katika maisha yake.
Asante sana Kwa haya mahojiano mazuri sana. Nimetamani kuendelea kumsikiliza. Nasikitika kidogo mtangazaji hajamuuliza mzee kuhusu operation ya Anjuan visiwa Vya Comoros ambayo Kama sikosei ni operation yake ya mwisho kuelekea kustaafu. Lakini pia nilitamani mzee aulizwe kuhusu tuhuma za matumizi ya fedha na ukwasi aliotuhumiwa kuwa nao miaka ya mwisho ya utumishi wake Kama mnadhimu. Mzee anaakili nyingi, afya timamu na anaonekana kuwa na hekima nyingi Mungu ambariki na atubariki Kama taifa kuwa na wazee Kama hawa
Haya ndo mambo jamii inahitaji simlizi za Mashujaa wetu. Siyo mnatuletea habari za kina mayele na majini hizo hazupi afya ktk Taifa. Simlizi za namna hii yaani zinakupakutamani kuwa mwanajeshi.
Afande Inanikumbusha Machungu Sana Na Kazi Kubwa Huko Seychelles Tukipigana Sana Na Askari Wa Kukodi Maeneo Ya Port Lawi ,Bousezuu Nawashukuru Wote Tulio Bali Hai Na Wewe Afande Wetu