Тёмный

Salama Na BILLNASS SE6 EP57 | MJUKUU PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 397 тыс.
Просмотров 45 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Katika pita pita zangu siku si nyingi nilimsikia mtu akimzungumzia mgeni watu wa wiki hii kwamba ni ‘Jay Z’ wa Bongo na si kwasababu kamuoa mmoja wa wasanii hodari wa kike na ambao wako juu ki muziki, ila pia akili yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa imemfanya yeye aone hivyo. Kwa ufahamu wangu niliambiwa na kushuhudia suala la maneno na mawazo ‘kuumba’. Pale mtu au watu wanapo kuona na ukichanganya na juhudi zako na nia na madhumuni ya wewe kutaka kufika pale basi mengine kutimia huwa ni suala la wakati tu.
Hivyo pia ndivyo ambavyo mimi namuona Ndugu William Nicholaus Lyimo almaaruf Bill Nass. Mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho ni miaka kama sita au saba iliyopita wakati nafanya kipindi cha Ngaz kwa Ngaz special edition. Ambacho mimi na Josh Murunga tulikua tunafanya ilikua kuwapa nafasi wasanii hodari kuwa ma host wa countdown hiyo ya ngoma zao kali 20 kwa wakati huo na kuzitolea maelezo yake. Kwa Bill Nass ilikua kama kumtafuta Kuku tu, yaani RAHISI sana. Alikua natural wataalam wanasema, kuanzia matamshi (haya wengi huwashusha hadhi kwa kiasi flani) mpaka swagg ambayo mtangazaji anatakiwa awe nayo kwake ilikua ipo. Kuvaa kwake, kuheshimu wakati na kuskiliza maelekezo na kisha kuyafanyia kazi ilikua 100, na mimi kwenye hili nilikua mtazamaji tu, kazi kubwa aliifanya Ndugu Josh akiwa kama Director. Yangu matumaini Bill Nass siku moja atataka kufanya kitu kama kile maana kitamfaa mno na itakua moja ya income zake nyingi ambazo anazo.
Kwake yeye kuamua kumuoa mmoja ya wasanii hodari wa kike ambaye ana mashabiki wengi na pengine wengi wao ni wanaume nadhani lilikua si amuzi mdogo kwao wote wawili. Wawili hawa mahusiano yao yalikua hadharani kwa sote kuyaona na kuwa na maoni nayo. Kuanzia ku leak kwa video yao ya faragha mpaka mahusiano ya mkewe na Marehemu Ruge, kila kitu kilikua nje nje. Je haya yaliathiri au kuyajenga mahusiano yao kwa kiasi gani?
Vipi kuhusu suala la Marehemu Godzilla ambaye kulikua na shutma kwamba alikua anauiga style yake na baadhi ya Radio zilikua zinampa nafasi yeye ili kumficha Zilla? Na je suala la kifo chake ambalo lilimleta yeye karibu na mtoto wa Zilla? Hii ilikua inamsumbua vipi wakati watu wanasema hivyo? Na je alikua anaona jinsi ambavyo ilikua inamsumbua Zilla?
Ukiachana na muziki Nenga pia ni mfanyabiashara mzuri tu ambaye amekua akitumia jina lake ipasavyo ili kuweza kujitengenezea kipato cha pembeni ambacho ni cha uhakika zaidi kuliko mziki ambao anafanya. Nna uhakika na yeye anajua kwamba ana uhakika wa kuuza electronics zaidi kwa mara nyingi kuliko uhakika wa kuwa na hit song nyingi kwa mwaka. Na hiyo haimaanishi kama yeye si msanii HODARI ila zaidi kwenye suala la wimbo kuwa mzuri lakini watu wasiupokee kama matarajio yanavyokua.
Humu pia tulichambua kiasi kuhusu jina lake ambalo amelirithi. Majukumu, biashara, mapenzi, urafiki, usia na familia.
Ningependa u enjoy kama ambavyo sisi tu enjoy wakati tunaongea.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Опубликовано:

 

14 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 100   
@Mimy_keys
@Mimy_keys Год назад
Billnass anajibugi maswali 🤗👌 Alhamdulillah Nimejifunza kuhusu Kumfundisha Mtoto Subra 🙌🙌🙏
@danielkayanda3566
@danielkayanda3566 Год назад
Billnass anajua sana kujieleza. The dude is far beyond watu wengi kwenye interview
@maishakisunzu391
@maishakisunzu391 Год назад
One of the greatest interview, ukiona hadi Salama anakuwa mtulivu ujue kalizika na majibu ya Billnenga!! Big up!
@johnphilipo6760
@johnphilipo6760 Год назад
Hii interview imesababisha nimeangalia kwa utulivu jamaa anajua kujibu maswali had raha jamaa yupo vzr
@ahuriladaniel9849
@ahuriladaniel9849 Год назад
Anajibu kwa utulivu sanaaaaa yaan daaah inavutia
@Lys292
@Lys292 Год назад
Kbsaaaaa 😂🙌🏼🙌🏼 unatuliza akili kama upo darasani
@dayanajones5102
@dayanajones5102 Год назад
Nampenda huyu kaka jamani yuko very smart kwenye kujibu maswali
@hoseambogela9152
@hoseambogela9152 Год назад
Msomi msomi tu,, sikiliza kwa makini elewa swali tafakari halafu jibu. Nenga ni mnoma kumbe safi sana.
@lillianbarongo2807
@lillianbarongo2807 Год назад
Interview nzuri mno ...anayeuliza na anaye ulizwa wana akili na very professional 👏👏👏
@queenofireland898
@queenofireland898 Год назад
🔥
@danielkomba5202
@danielkomba5202 Год назад
Watched this from UK, you guys nailed it, Salama uko very smart na maswali yako namna ya kuyapangilia na kuuliza and Billnass is just superb and a very humble guy for sure, much love from UK to you lads!. 💪🏽❤️
@note_as_being_me2337
@note_as_being_me2337 Год назад
Akili Mingi Sana William Lymo, Hongera Nandy
@iddyally7127
@iddyally7127 Год назад
Salama nipo congo namini ipo siku nitakutana naweye njo ndoto yangu nakupenda
@mfamauomary7969
@mfamauomary7969 Год назад
Dah iko poa sana tena nimejickia faraja sana kumckia mchizi wang wa kitambo @ Billnass❤
@sawaabyahya584
@sawaabyahya584 Год назад
Salama hongera... Kwa kupasua kichwa kututafutia kitu muhimu kutuongeza akili
@mwajabujumanne9025
@mwajabujumanne9025 Год назад
Billnas so genius 😍
@raphaelamour385
@raphaelamour385 Год назад
Billnenga mafioso,smart sana we jamaa,muhuni unaejitambua
@pamanyango8917
@pamanyango8917 Год назад
Billnandy kwa majibu tu👌👌 uko vizuri sanaaa, napenda sana kusikiliza unavyo jibu maswali Mimi ni shabiki yako wewe na mkeo shabiki wenu kindaki ndaki kutoka 🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪
@uzaimaoman9524
@uzaimaoman9524 Год назад
💯
@donatusnicolaus6403
@donatusnicolaus6403 11 месяцев назад
What a beautiful 🪴 interview, haijawahi kuwa masihara interview inayofanywa na salama, your my roll-model $alama, love from Manyara Tanzania
@samsonmtalege4858
@samsonmtalege4858 Год назад
Jamaa anajua sana kuongea point 🙌🙌🔥
@lovenessaron2669
@lovenessaron2669 Год назад
Shem Billinass Tunakupenda sn barikiwa,Ongeza bitii kwa upambanaji wako 😊😍🔥🔥🔥
@stellaraiton6429
@stellaraiton6429 Год назад
Big up Billnass u'r so genius una busara sana ....Salama I do appreciate your work coz sisi vijana tunajifunza mengi sanaa kupitia kipindi hiki ..all in all tunazidi kupambana kusoma na kupata experience na realities za maisha🥰❤️🙏
@deodatuskessy9237
@deodatuskessy9237 Год назад
Interview nmeipenda haichoshi pia inafunza
@justinendizeye714
@justinendizeye714 Год назад
Kijana smart sana hana uswahili kbsa 👍
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Mwamba ni noma sana
@adyaalawy8764
@adyaalawy8764 Год назад
Nandy kapata mme, MPOLE
@lizahadongo1801
@lizahadongo1801 Год назад
Bilnas karibu Kenya napenda vile unakuaga umetulia na hiyo song ya puuh
@khamisbadru9342
@khamisbadru9342 Год назад
Nilitamani kusikia urafiki wake yeye na Idris..maana hawa jamaa bhana wanataniana mno
@apti-vp2lu
@apti-vp2lu Год назад
Billnass huyu mwamba ana hekima ya maneno sana yaan mchakato wa mziki nimeuelewa na ukifuata maneno alio shaur unatoboa kweupe
@Abbasbakarsth
@Abbasbakarsth Год назад
Pia naomba iingizwe kwenye list bora kwa kwa huu ingawa bado mwaka ndo kwanza unaanza ila naomba iwepo
@heriethgodfreyhegoxa5551
@heriethgodfreyhegoxa5551 2 дня назад
Billnas leo amenifundisha kitu kikubwa sana😢😢😢🎉🎉🎉
@sassboy9360
@sassboy9360 Год назад
Somo kubwa humu bill ni smart
@salvinangadaya747
@salvinangadaya747 Год назад
Nimeangalia sijatamani iishe kusema ukweli❤ Billnas A man and a half, Salama very nice interview❤❤
@alimwenda-gi9sr
@alimwenda-gi9sr Год назад
Naomba umkaribishe mbunge wa kahama mjini nae atupe madini ana vitu vingi sn tujifunze kutoka kwake
@nurahnabil1253
@nurahnabil1253 Год назад
Very Smart Guy 👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾
@evaristjenipha-ve2eb
@evaristjenipha-ve2eb Год назад
Finally interview safi na tulivu hongera sana bilnas uko vizuri
@donatusnicolaus6403
@donatusnicolaus6403 11 месяцев назад
Love 💕 you guys best interview ever made love from Manyara 🇹🇿🇹🇿
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Cjawah kumfatilia huyu mwamba Kwa dakika zaidii ya 3 ila Leo nimejua ni mwamba na nusu ❤😅
@salomegomano1788
@salomegomano1788 Год назад
Sema billnas anajua kujb maswali as raha
@lilianmrope1598
@lilianmrope1598 Год назад
Billnass mtulivu anajielewa hakurupuki Ana hekima na busara Sana
@feronandsulubu6711
@feronandsulubu6711 Год назад
Naiskiliza adi nipate swali kuhusu Dylan
@wellbrand3415
@wellbrand3415 Год назад
Wow... Nimeipenda sana hii...
@agnessgeorge108
@agnessgeorge108 Год назад
Nilikua naisubili hi kwa hamu😊
@dullahyunusu3072
@dullahyunusu3072 Год назад
Sijawahi jutia kuangalia interview za billnass, mwana fa, Roma na darasa zinakuwaga na tuvitu tuvitu twingi twa kujifunza na kuongeza maarifa
@saumueunice1716
@saumueunice1716 Год назад
Interview was 👌👌👌❤❤❤🙌🙌🙌🙌
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 Год назад
18:44 🔥 20:08 " kudharau zile brand kubwa zilizoangukaa nikuwavunja moyo wachanga wanao inuka local ila kikazi inastahili kuheshimika" joh makini
@mussamuro752
@mussamuro752 Год назад
The best interview ever, Bilnass anajua sana kuongea
@laurentrueta9625
@laurentrueta9625 Год назад
HUYU JAMAA ANA AKILI SANA
@hajiali8820
@hajiali8820 Год назад
Yani nenga anajibu vizuri
@denislucas8952
@denislucas8952 Год назад
Such a Great Interview. Salama this is the best Thing ever done. Keep Going you are changing lives of many. 👊🏽
@monicajohn2515
@monicajohn2515 Год назад
Sikuwahi kujua billnass ana akili Sana asee
@Dawah99
@Dawah99 Год назад
Salama is special and unique, this channel deserves millions of views. Kudos to you guys. Love from UK.
@bainolatino3412
@bainolatino3412 Год назад
Mambo vp kaka napendaga sana nikiskia watu kutoka ughaibuni nafarijika Sana broh Habari yako
@Dawah99
@Dawah99 Год назад
@@bainolatino3412 poa poa kaka, tupo na baridi yetu vp na ww na familia yako?
@bainolatino3412
@bainolatino3412 Год назад
@@Dawah99 nashukuru mwenyez mungu niko Safi na Familia yangu lkn Kwa Sasa naishi znz na Familia yangu niko nayo mbali,, vp jinsi ya Hali ya maisha na baridi kama hiyo shughuli zinafanywa??
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Год назад
@billnas very very humble smart person 👏👏👏
@salumuseif3324
@salumuseif3324 Год назад
Jamaa ana maneno mazuri ndo mana dada yetu ajachomoka
@cresiannacastory-vp8cm
@cresiannacastory-vp8cm Год назад
The interview was😘😘😘
@emmashayo5159
@emmashayo5159 Год назад
Nenga you are incredible 👏🏾👏🏾💪🏾
@Abbasbakarsth
@Abbasbakarsth Год назад
Sikuwahi kuhisi wala kujua kama jamaa anajua kuongea kwa kutafakar kias hichi... hii naiweka kwenye list yangu ya interview
@dullahyunusu3072
@dullahyunusu3072 Год назад
Mwamba anajua angalia interview zake za nyuma hutokaa umiss interview zake
@prettypretty9745
@prettypretty9745 Год назад
Interview ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥
@mwajumamohamed6426
@mwajumamohamed6426 Год назад
Billnas ana akili sana Nandy kapata mume
@queenofireland898
@queenofireland898 Год назад
kabisa kapata anabusara sana uongeaji wake tu ukimuona his good guy
@jocyjocy3050
@jocyjocy3050 Год назад
Bill Nass Big brain🔥🔥💯
@ernestpaulo7843
@ernestpaulo7843 Год назад
Bilnas❤️
@fatmasaid425
@fatmasaid425 Год назад
Salama tuletee mwijaku
@mosesjnr8436
@mosesjnr8436 Год назад
Very positive
@duxinhojunior9441
@duxinhojunior9441 Год назад
Ndo maan nkawa najiulizaa huyu n nan anaeimba km godzilla?? Kumbe n Nenga😅
@wanzakleruu
@wanzakleruu Год назад
Nenga’s so genious
@lukizatv
@lukizatv Год назад
Wasanii wajifunze kutoka kwako jinsi ya kujibu maswali . watumie hii kama case study . Wengi huwa hawajibu walichoulizwa
@marthawitonde-jb7ng
@marthawitonde-jb7ng Год назад
Nenga ana akili sana anajibu kwa logic
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Mwamba ni noma saba
@lillymotika3980
@lillymotika3980 Год назад
He is a gentleman
@brazatall_tz3902
@brazatall_tz3902 Год назад
Daah ungemuuliza life style yake na Idris sultan amvumilia vp coz matan yako yanavuka mipaka sana
@halimakinyori5502
@halimakinyori5502 Год назад
Bil kama bill
@jackmteuka
@jackmteuka 4 месяца назад
🔥
@phiniasphilemon6514
@phiniasphilemon6514 Год назад
Billnass ana akili sana! Hands down
@zawadimallya-fw3ro
@zawadimallya-fw3ro Год назад
Waoooh
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
🌹
@williamssadala377
@williamssadala377 Год назад
Nenga 🔥
@donatusnicolaus6403
@donatusnicolaus6403 11 месяцев назад
🇹🇿
@marylutego8554
@marylutego8554 Год назад
😍😍😍
@paulomatoke
@paulomatoke Год назад
Huo wimbo hapo mwishoni baada ya mahojiano ni wa nani na unaitwaje
@azaeltumain7528
@azaeltumain7528 Год назад
marco chali - yeeah
@paulomatoke
@paulomatoke Год назад
@@azaeltumain7528 asante sana bro
@fatumamohammed9964
@fatumamohammed9964 Год назад
Billnand
@ReginaFungapili
@ReginaFungapili 6 месяцев назад
Kwan billnas jaman kataja maana ya jina la binti yake?
@paulmwanyika7622
@paulmwanyika7622 4 месяца назад
Ndiyo. Alisema kwenye part 1 ya mahojiano.... Maana yake ni Baraka toka kwa Mungu.
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Mwamba ni noma sana
@stellah3844
@stellah3844 Год назад
Interview iko 🔥🔥🔥🔥
@terrykiselachaupole
@terrykiselachaupole Год назад
Sawa mama mtembezi 👻👻👻👻
@agnessgeorge108
@agnessgeorge108 Год назад
Nilikua naisubili hi kwa hamu😊
@Noriega_of_tanzania
@Noriega_of_tanzania Год назад
Akili mia
@monicajohn2515
@monicajohn2515 Год назад
Sikuwahi kujua billnass ana akili Sana asee
@dennismagehema9283
@dennismagehema9283 Год назад
Sikuwahi kufikiri kama jamaa anauwezo wa kiakili kiasi cha juu. Hongera Nandy kwa kuwa na Wiliam
@edithasamson2389
@edithasamson2389 Год назад
🙏🙏🙏🙏
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Mwamba ni noma sana
@OfficialSwabry
@OfficialSwabry 6 месяцев назад
Mwamba ni noma sana
Далее
小丑调戏黑天使的后果#short #angel #clown
00:16
Слушали бы такое на повторе?
01:00
НЮША РОЖАЕТ?
00:17
Просмотров 948 тыс.
Flipping Robot vs Heavier And Heavier Objects
00:34
Просмотров 39 млн
Salama Na Madee Ep 18 | MPAKA MSHALE Part 1
40:33
Просмотров 68 тыс.
小丑调戏黑天使的后果#short #angel #clown
00:16