Тёмный

Safari Ya Adam Mchomvu, Kusoma Uganda Mpaka Kufanya Kazi Clouds | SALAMA NA ADAM MCHOMVU PART 1 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 132 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Adam Mchomvu ni jina kubwa kati ya majina makubwa ya watangazaji mahiri ambao nchi yetu imeshawahi kuona. Toka kuanzishwa kwa Radio za FM hapa nyumbani ambayo ilikua miaka ya kati kati ya 90 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, hapo pia ndo kilipoanza kuzalishwa kizazi cha watangazaji na ma DJ mahiri ambao pia kwa kiasi kikubwa waliweza kulisukuma soko la vipaji mbali mbali vya muziki na filamu kufikia hapa vilipo leo hii. Kazi nzuri iliyotukuka ambayo pia imejaa jasho machozi na damu ilipitiwa. Mpaka leo hii ukiona watu wana launch album zao au filamu zao ujue kuna kazi nzuri ya kujenga misingi ilifanywa na walioianza kazi hii miaka hiyo ya nyuma.
Kwa uelewa wangu Adam ni Generation ya tatu ya wimbo hilo la watangazaji, ukiachana na kina Charles Hilary, Abubakar Liongo na Marehemu Misanya Bingi au Mike Mhagama, kizazi kilichofuata baada ya hapo ni hiki chetu, cha kiza Dozen na Fetty na Anna Peter na kina Adam Mchomvu. Generation sasa ya Bongo Flava na Bongo movie. Kizazi hiki ndo ambacho umahiri wa Adam ulianza kuonekana, XXL bila ya yeye kwa asilimia 100 utalisikia pengo lake, aina ya matamshi na kusema mambo kwa jinsi yalivyo ndo kumemjengea huo upekee. Ila pia ukaribu wake na wasanii wa Bongo flava pia umesaidia kumpatia story za ndani kabisa pamoja na kujua maendeleo ya kazi zao na struggle zao.
Pengine ukaribu huo ndio ulimfanya na yeye atake kuwa mwana muziki?
Sote tunajua kama mziki una mambo yake mengi sana, pengine wewe unaweza ukadhani unauweza na ni rahisi sana kuufanya lakini nadhani ukimuangalia Adam na kumfuatilia kwa kiasi kikubwa unaweza kujua ugumu wa zoezi zima maana kwa mtu kama Adam ambaye yuko jikoni kabisa ameshindwa kufanya muziki kama kazi yake nyengine au kama ambavyo yeye angetaka iwe muziki ndo maisha yake, si tahisi kama ambavyo unadhania. Kwa miaka ambayo nimekua nilifanya kazi kama mtangazaji wa Radio nimeona watangazaji wengi nao wakitaka kujikita kwenye muziki, ambao wamefanikiwa ni wanawake zaidi kuliko wanaume. Adam ameniambia kwenye maongezi yetu haya kwamba wakati mwengine anaona kama watu wanahisi hayuko seriou pengine, pia ameniambia kuhusu utajiri wa nyimbo alizonazo kwenye hifadhi yake. Hii pia imenionyesha jinsi tunavyokua tunafanya kazi ambayo wewe una hakika nayo ni nzuri sana ila kwa watu upokeaji wake unakua sio kama ambavyo wewe umetegemea.
Mi naamini kuna siku tutamuelewa tu maana kwa kumskiliza tu utaelewa utashi wake na jinsi ambavyo anaangalia vitu na uelewaji wake. Kwa wengi Adam ni HODARI na ambaye ameweza kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa muaminifu pia kwa muajiri wake, kama unakumbuka hapo katikati kulikua na wimbi la wafanyakazi wa Radio kupata ofa kubwa za kuhamia Radio nyengine, na nna uhakika mwingi na yeye ofa hizo alizipata, tena nyingi ila aliamua kuendelea kubaki palepale alipokua. Tunaambiwa loyalty haiuzwi wala huwezi kumfundisha mtu, ni aidha unakua nayo au hauna.
Humu mimi na yeye tulizungumzia mwanzo wake, fahamu zake za vitu na maamuzi yake ya kutaka kufanya kazi ambayo anafanya leo. Jinsi ambavyo wazazi au mzazi wake alilipikea hilo. Pia nilitaka kujua mazingira ambayo amekulia, humu amenielezea utukutu wake na jinsi ambavyo alikua na uwezo wa kumdanganya Mama yake ilimradi aishi kwenye aina ya maisha ambayo alikua ameichagua. Na jinsi pia ambavyo aliweza kujichomoa kutoka kwenye dunia hiyo ambayo ilikua imejaa kupotea kama asingekua makini.
Yangu matumaini kuna kadhaa ya kujifunza na yatakua na faida kwako na kwa uwapedao.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

25 сен 2022

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 210   
@mahinga
@mahinga Год назад
Tunataka Millard ayo munipe like kama tunakubaliana
@innocentsimika1937
@innocentsimika1937 Год назад
Adam is most recognised media personality in Tz.. Mshikaji anajielewa sana, Akili yake inafanya kazi effectively.. Ona hapo alivyowatoa matongotongo wafiadini na wale wanaojifanya wakihudhuria sana huko kwenye majumba ya ibada ndio kuiona pepo.
@emmanuelnzaligo6262
@emmanuelnzaligo6262 Год назад
Napenda sana interview za Adam Tisha sana.
@edgardevis8152
@edgardevis8152 Год назад
Napenda sana Hiki kinamafunzo mengi yamaish nk Naomba 2wekeeni na yamchungaji Rich
@KhamisHaroub-uj5ci
@KhamisHaroub-uj5ci Месяц назад
Hakuna Krislam hommy # Allah akuongoze ln Shaa Allah uelekee kwenye Haki nothing but sharing good vibes
@Heismasai
@Heismasai Год назад
hii Krislam kama nipo nayo jamani!! naamini huyu Mungu wetu ni mmoja wa wote Mimi Mkristo na Waislam Pia...God bless us
@msafirikilongo7429
@msafirikilongo7429 Год назад
Salama ungekuwa mwalim Basi ingekuwa unafundisha watoto na wangekuelewa sana.......humble
@makantaafrika
@makantaafrika Год назад
Mchomvu anabonga sana! Kumsikiliza hachoshi kabisa ✊🏿🙌🏿
@Kobe_254
@Kobe_254 Год назад
Vicks Kingo was our best advert when growing up in Kenya..🇰🇪🇰🇪🇰🇪 big up!! Your story inspires na sikujua eti wewe Toto la Arusha, kumbe ndio maana kijiti cha majani ni kama ibada, big up Adam Mchovu🤝👏🏿👏🏿👏🏿
@joiana4663
@joiana4663 4 месяца назад
Adam Mchomvu the krislam, imekaa vizuri
@baswarimohamedi2766
@baswarimohamedi2766 Год назад
Adamu nakubal sana... presenter
@chesterbrand6723
@chesterbrand6723 Год назад
His my brother from another religion the first Man kwa dunia Arifu. ....
@salumuseif3324
@salumuseif3324 Год назад
Mtangazaji anayependwa na vijana mchomvu
@uzungupoint
@uzungupoint Год назад
Namkubali sana AD+ daaaah basi tu 🔥🔥🔥🔥🔥🔥
@shabanijuma2085
@shabanijuma2085 Год назад
Pole siku ukija kujua ushachelewa Mzee.Mungu akupe hidaya.Isha allah
@gerry_macopper3808
@gerry_macopper3808 Год назад
Noma sana
@epiphaniaallute2726
@epiphaniaallute2726 Год назад
🤣🤣🤣🤣🤣big up @adammchomvu nimecheka sana Asante Dada Salama umenipa kicheko.
@michaelmpagwa2553
@michaelmpagwa2553 Год назад
Mwanangu mwenyewe AD+ namkubali sana
@nurumwangoka5924
@nurumwangoka5924 Год назад
Kubwa sana hiiiii hongera sana mchomvu
@hildayona852
@hildayona852 Год назад
Dada salamà nakukubali mno kwanza tangu no kuone nampenda sana kitu unacho kisema kweli uko vinzuri naomba mungu sikumoja tuonane tuongee
@godfreybeatusmahavile2250
@godfreybeatusmahavile2250 Год назад
Interview kal sana 🔥🔥🔥🔥🔥🔥📌
@maigajohn5828
@maigajohn5828 Год назад
Salut kwako salama jabir
@mmn7480
@mmn7480 Год назад
Napenda salama anavocheka
@judithsalvatory2892
@judithsalvatory2892 Год назад
Woooow nimewapenda
@alexkalonga5323
@alexkalonga5323 Год назад
Uyu mshkaji Mchomvu ni muhuni anaongea kihuni mpka anaharibu interview usela mwingi sana Brother mpka unaharibu
@allywaziry6419
@allywaziry6419 Год назад
Bangi mbaya sana....
@josephngowoambroce418
@josephngowoambroce418 Год назад
Namjua Issack Momenaaa
@adolphmwangoje2887
@adolphmwangoje2887 Год назад
Adam bna comed nyingi sana
@RazakiMmalinda-rl3ej
@RazakiMmalinda-rl3ej Год назад
Adam mchomvu namkubali xn
@Igauf3
@Igauf3 Год назад
Adam is a great storyteller ! 😂
@fadhilimkungura7453
@fadhilimkungura7453 Год назад
............
@BONGO_FILAMU
@BONGO_FILAMU Год назад
Huwez Amin nilipanga kusikiliza dakika tatu Ila Mwamba anastory hadi nimemaliza
@mbwanamtessa8607
@mbwanamtessa8607 Год назад
Interview imempata mwenyewe Sasa hapo. Yani hapo mnainterviweana
@gazzahboy9271
@gazzahboy9271 Год назад
Legend 🚬🚬🚬❤❤❤
@sakinagumadi225
@sakinagumadi225 Год назад
Yes mchomvu mzee wa johnii johnii yes papaa
@robinsonjames9711
@robinsonjames9711 Год назад
The Classic presenter AD+
@joppagraphix2868
@joppagraphix2868 Год назад
Salama na gwajima waiting for it
@franksteven
@franksteven Год назад
I had to pause and comment. What a match of energy this is 🙌🏿🙌🏿 So much entertainment and education all in one bundle 🎉
@johariramadhan5236
@johariramadhan5236 Год назад
Namkubali adamu sana
@mohammedrashid2906
@mohammedrashid2906 Год назад
Ipo. Sawa
@edwardmachaku1661
@edwardmachaku1661 Год назад
Appreciated
@waziriseif5384
@waziriseif5384 Год назад
Best interview.... nzur san... haichoshi kbs
@saunyimaaru3133
@saunyimaaru3133 Год назад
Kaza safi
@selemanbuluba6146
@selemanbuluba6146 Год назад
Kislam tukutane hapa
@rosegideon336
@rosegideon336 Год назад
Salama wish u all the best.
@kingmaina1151
@kingmaina1151 Год назад
Aaaaah hii kali sana nataman muda ungeongezwa 😂😂😂😂😂
@emmamatemu8225
@emmamatemu8225 Год назад
Oyaa leo sawaa mtu sahihi
@akidajulius8397
@akidajulius8397 Год назад
Da kweli maisha yanaenda Kasi, Salama Amekuwa mmama Sasa jaman da
@zuwenazuwena7764
@zuwenazuwena7764 Год назад
Yan hata siamini kweli hamna mkate mgumu kwa chai
@claudiabakisa8052
@claudiabakisa8052 Год назад
Alafu kanenepa
@thomasboniphace7254
@thomasboniphace7254 Год назад
AD+ umetisha sana
@samsonwilliams2505
@samsonwilliams2505 Год назад
🔥🔥🔥🔥 bonge la interview
@all-victorious2156
@all-victorious2156 Год назад
Salama anakuwaga msengemsenge sana wao na T.I.D Big up Mchomvu !
@abdulyamiri3546
@abdulyamiri3546 Год назад
broo umetisha
@babag7138
@babag7138 Год назад
Baba john hatari sanaa💥💥💥
@casablancastudioarusha775
@casablancastudioarusha775 Год назад
Acha nitie neno hapa #Bonge la show 🔥
@simaosamrosa6689
@simaosamrosa6689 Год назад
Interview ni mbaya kwa kwel I can't lie . Anahisi kama ana present bado
@editorfrank7471
@editorfrank7471 Год назад
binafs sijaenjoy
@gloryleon4187
@gloryleon4187 Год назад
Kiruuu, salama muhoji kistaarabu, achelewi huyo ku🤸
@maryshirima1234
@maryshirima1234 Год назад
😂🙌😂
@ufugajiwetu7782
@ufugajiwetu7782 Год назад
Bonge la story tamu
@ufugajiwetu7782
@ufugajiwetu7782 Год назад
My favorite interview
@stevewanga957
@stevewanga957 Год назад
Huaga namuelewa sana Salama ...much love from 🇶🇦🇶🇦
@moekan_3612
@moekan_3612 Год назад
Doha au Bahrain
@khamisramadhan5133
@khamisramadhan5133 Год назад
Makaveli--umefika apa
@stevewanga957
@stevewanga957 Год назад
@@khamisramadhan5133 hapa sikosi
@UgandanAllstarTales
@UgandanAllstarTales Год назад
MY DAWG ADAM
@aristidrichardmrema536
@aristidrichardmrema536 Год назад
Adam adam mwanetu sana
@andrewndotela7407
@andrewndotela7407 Год назад
sasa leo umecheza mtu wangu... naacha kazi nicheck hii interview
@Kobe_254
@Kobe_254 Год назад
Mimi naicheki na niko job shift vinomanoma hadi na replay 😅😅
@andrewndotela7407
@andrewndotela7407 Год назад
@@Kobe_254 Hahahah
@kafumash9816
@kafumash9816 Год назад
Me ukufwatilia sana kutoka Nairobi Kenya
@husnaharuna5480
@husnaharuna5480 Год назад
Huyu jamaa namkubali kinoma
@abrahammollel7141
@abrahammollel7141 Год назад
dingi wa hm katisha, salama mwambie Adamu anifundishe namna ya kufunga mastyle hiyo kitu hapo shingoni nazikubali kinoma bas arif
@youngblack6917
@youngblack6917 Год назад
I'm the first one today... I love you salama all the way from Zambia
@winifridambilinyi8043
@winifridambilinyi8043 Год назад
Ila adam🙌🏽😂
@mynambwambo2072
@mynambwambo2072 Год назад
Yani huchoki kumsikiliza ...This interview is 💥💥💥💥
@pascarmwatosya6815
@pascarmwatosya6815 Год назад
Daa nimecheka Sana Sana Mambo lokapu Tena toli wa ajabu
@imanichando2534
@imanichando2534 Год назад
Nimependa sana hii show madam salama
@bobsalim4285
@bobsalim4285 Год назад
Kama huamini Mungu sema tu huna dini. Usiseme una dini zote mbuli na hujui la kujibu. Kama waamini Mungu,iliweka swala ziwe swhemu husika. Kuna swala na kuomba mahitaji yako. Mahitaji waweza omba popote. @salama for all interviews ume do,huyu ameharibu.
@antybabybintrashid2333
@antybabybintrashid2333 Год назад
Salama chavu vipo dada
@claudiabakisa8052
@claudiabakisa8052 Год назад
Kanenepa kweli
@adolfmathew9698
@adolfmathew9698 Год назад
Wape mashavu Wana @adam mchomvu. #chuga #republic
@jacklineswallo3643
@jacklineswallo3643 Год назад
🔥🔥🔥🔥
@abdallahmabondo8566
@abdallahmabondo8566 Год назад
Adam The First Man On The Earth
@hitmanhunter9557
@hitmanhunter9557 Год назад
Viti vimechoka sister mkibadilisha itakua pouwa
@utamutv_
@utamutv_ Год назад
Adamu namkubalisana anajua mpaka anaboa
@johmafareal6730
@johmafareal6730 Год назад
Adamu ni mtu mwenye heshima saaana kwenye game ya bongoflava .........jamaaa uzuri anafanya kitu anachokipenda
@ramazanzibar8264
@ramazanzibar8264 Год назад
Bangi mamae sio poa
@ramadhaniselemani9416
@ramadhaniselemani9416 Год назад
🤣🤣🤣
@andrewmgaya310
@andrewmgaya310 Год назад
Chrislam 🤣🤣 I like that na ni sana bcoz it comes from brother from another mother 🙌🏾
@jorickmaanga3131
@jorickmaanga3131 Год назад
AD+ 🙌
@salumjumah5648
@salumjumah5648 Год назад
Baba joniiiii
@Boaz22
@Boaz22 Год назад
Bangi mbaya nyie,mnamsikia vizuri Adam lakini😂😂😂
@chesterbrand6723
@chesterbrand6723 Год назад
Mjomba hapa NI Paradise ..paradiso...sawa arifu...
@barakakusa7606
@barakakusa7606 Год назад
Siyo bangi ni mjani🤣🤣
@josephstephen1079
@josephstephen1079 Год назад
Adam mabange
@NickTrickaddictedboy18
@NickTrickaddictedboy18 Год назад
Sauti haijatokea vizuri. Nahisi kuna kitu hakikukaa sawa kwenye editing za sauti. All in all hongereni kwa kipindi. Nick Trick hapa niko Maputo Mozambique
@maryshirima1234
@maryshirima1234 Год назад
Acha wivu jombaaaa
@goodlucksway1456
@goodlucksway1456 Год назад
🤣🤣🤣🤣🤣aisee nimecheka sana
@williamkavindi8520
@williamkavindi8520 Год назад
Uwe unabadilisha hilo tisheti Salama!!!
@michaelkipara8205
@michaelkipara8205 Год назад
jamani salama na zuchu tunaisubiri,I love zuchu much
@bakariburuhani7956
@bakariburuhani7956 Год назад
Zuchu alishafanya nae kipindi mbona
@marietakomenkesha8803
@marietakomenkesha8803 Год назад
@@bakariburuhani7956 bado hawajaupload you tube ndo anachomaanisha
@maryshirima1234
@maryshirima1234 Год назад
Alivyoanza tu kujibu swali la kwanza mie hoi...😂🙌😂
@rogersodero3897
@rogersodero3897 Год назад
Salama tunasubiria Esha buheti
@itNeza
@itNeza Год назад
🤣 Eti mpaka sasa Analia tuu 😂
@robbywilson224
@robbywilson224 Год назад
kinachonishangaza bongo watu]hawa wapi'Heshima Wanayostahili Hawa watangazaji wa3 -Fety Mchomvu Na B12…wameipigania sana bongo flavor watu kuielewa km ni kazi sio Uhuni…Ndiomana kila mtangazaji wa kipindi km Chao ataiga swaga zao…
@boniimsokwa8627
@boniimsokwa8627 Год назад
tall wa ajabu way back since 89.5 Mbeya fM
@Antonycharles2697
@Antonycharles2697 Год назад
Ki ukwel kabisa kutoka moyoni hata mimi napenda sana kazi ya presenter ila mm ni fundi umeme
@asueddy1465
@asueddy1465 Год назад
Endelea kutengeneza Balubu
@halemmmbarak16
@halemmmbarak16 Год назад
Waume wa kiislamu tueni makini tunapo panda mbegu. Inasikitisha kuleta duniani mijitoto isokua na iman ya mungu.
@ismailmshana2828
@ismailmshana2828 Год назад
Adam Ni mtt wa kihuni
@lawrencemwakyonde8655
@lawrencemwakyonde8655 Год назад
Kipindi safi sana
@jandaboytzz2755
@jandaboytzz2755 Год назад
Adamu Mtu Peac Sana🖐️
@BBrown_vevo
@BBrown_vevo Год назад
Mchomvuuu
@r14kgroup68
@r14kgroup68 Год назад
Hili jembe nalakubali kinom
@pitbullfamily4499
@pitbullfamily4499 Год назад
😁👌🏾
@HemedKibao-tt7gc
@HemedKibao-tt7gc Год назад
Kutikuamini tu siku ya mwisho hio inakutoa kwenye uislam kwahiyo wewe tayari ni mkristo usichanganye watu
@dickluckyvictor6571
@dickluckyvictor6571 Год назад
BM mwenyewe
Далее
Who has won ?? 😀 #shortvideo #lizzyisaeva
00:24
Mkasi | S13E10 with Ruge Extended Version
40:28
Просмотров 531 тыс.
мы в телеге - hahalivars
0:52
Просмотров 4,3 млн