Тёмный

Salama Na ROSE MUHANDO SE6 EP53 | NIPE UVUMILIVU PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 397 тыс.
Просмотров 48 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Katika binadamu ambao walinipa wakati mgumu na kusubiri kwingi kabla ya kuja kukaa kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu basi mmoja wao ni Rose huyu wa Muhando. Upatikanaji wake ni kama ukitaka kumuona SIMBA mbugani, lazima uamke asubuhi na mapema au uwe na bahati ya mtende kama ambayo sisi tumepata. Ingawa tulisubiri kwa masiku tele na miezi tele katikati ya mwaka huu tuliweza kumpata na kukaa nae chini ili tuweze kuzungumza nae.
Rose ni wa moto sana, kalenda yake imejaa safari tele za nje na ndani ya nchi, anazunguka mara kwa mara kwaajili ya kutoa elimu na burudani kwa watu wengi ambao nao pia wamekua wakimgojea kwa hamu na kwa masiku tele. Kipaji chake cha kipekee ndicho ambacho kimemfanya awe maalum miungoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa Injili na uzuri wake mwengine ni kwamba amekua akitoa huduma hiyo kwa miaka mingi bila ya ‘kuchuja’.
Sasa nini hasa siri ya mafanikio hayo?! Ukiachana na panda shuka tele ambazo Rose amepitia toka akiwa na umri wa miaka 6, kukata tamaa ni jambo ambalo halipo kabisa katika mambo ambayo huwa anayawaza. Pengine kujiuliza kwanini na anatokaje kwenye hilo zito alilo nalo linaweza likawa ndo swali, ila kusema kwamba hatoweza au haiwezekani hilo jambo kwenye kitabu chake au kichwani chake huwa halipo kabisa.
Ukiskiliza kwa makini maneno ambayo yanatoka katika mdomo wake utagundua Rose ni mmoja kati ya wanawake jasiri sana ambao wamewahi kutokea katika kiwanda hiki cha Sanaa hapa Tanzania. Ukimuangalia macho yake, mikono yake ambayo imejaa makovu na nna uhakika pia kuna sehemu nyengine kwenye mwili wake pia zimejaa makovu lakini hatukuweza kuona unaweza ukapata tu idea ya makubwa na mazito ambayo amepitia na ambayo yameacha makovu makubwa tu si mwilini mwake tu bali hata kwenye moyo wake. Ananihadithia kwenye episode hii jinsi ambavyo watu walikua wanamuadhibu ki mwili na ki akili ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuchomwa moto, kukatwa na kunyang’anywa mali zote ambazo amewahi kutengeneza tokea wakati anaanza muziki ila hayo yote hayajawahi kumkatisha tamaa wala kumrudisha nyuma.
Rose anaamini na aliamini kwamba ana uwezo wa kuvipata vyote ambavyo watu walimdhulumu kwenye kipindi flani kwenye maisha yake, aliamini hakuna ambaye anaweza kumnyang’anya kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amempatia na kwa kupitia hiko kipaji na akiwa hai na mzima basi vyote ambavyo aliwahi kuwa navyo na vikapotea basi alikua na uwezo wa kuvirudisha na ni kweli, kuvirudisha ameweza na vimekuja maradufu yake.
Simulizi zake za safari yake toka siku ya kwanza alipokua mdogo nyumbani kwa Baba na Mama yake huko kwao Morogoro wakati anaumwa ni moja ya vitu vya kufikirisha sana ambavyo nimewahi kuvisikia toka tumeanza kukalia kiti chakavu, na yangu matumaini maongezi haya kwa kiasi kikubwa yatakupa ile vibe ambayo huwa naizungumzia kwenye intro ya kipindi chetu hiki.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Опубликовано:

 

14 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 144   
@ibrajrvlogs527
@ibrajrvlogs527 Год назад
I like the fact that, Salama amesikiliza kila kitu na wakati wa kufunga amefunga kwa sauti ya taratibu kabisa kutokana na uzito wa story Rose aliyoitoa. You both are the best, Pole sana sister Rose
@Thevineyard9889
@Thevineyard9889 Год назад
Aisee, this is purely gospel of Jesus Christ Asante Rose Muhando. Umenifundisha sana na umenitia moyo sana ktk Imani. Hallelujah
@ancytarimo1103
@ancytarimo1103 Год назад
Salama , she is talented. Ana uwezo mkubwa sana . Anamsikiliza bila kumwingilia. Keep it Salama
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Saaana
@pendokissatu937
@pendokissatu937 Год назад
Sanaaaaa Yani she is the Best achana na Hawa watangazaji Wengine ujamaliza kuongea ashakudakia
@alphamgale3020
@alphamgale3020 Год назад
Santé mitume yakuta mm arfa umepa matumaini nimepitia magumu mm nimubeba maono napigwa Vita na wapendwa wenzangu
@thomasmartinez786
@thomasmartinez786 Год назад
Akili ikilishwa kazi itafanya kazi NIMEJIFUNZA KITU🙏🙏🦁
@georgembise7234
@georgembise7234 Год назад
Salama una utulivu wa akili huna mapepe,Sikuwai ku comment toka maguful afariki lkn leo nampa like yangu salama jabir good journalist yupo makin sana ata ktk kuhoji upo juu kama milard ayo!!na unampa nafasi mtu kujieleza na huna mapepe salama una utulivu wa akili.hongera sana sana sana.
@saumuhamisi1603
@saumuhamisi1603 Год назад
I really love her courage. She’s a inspiration to many people 🥰
@michelinehabarugira5549
@michelinehabarugira5549 Год назад
This testimony is a big encouragement to me today. Don’t look behind, move forward 🙏🏾❤️
@104FIKA
@104FIKA Год назад
Nazani kwangu hii ndio best interview kwangu na Rose anaongea vizuri sana ana akili kubwa sana
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Saaana🔥🔥🔥
@zephaniamteule7218
@zephaniamteule7218 Год назад
Ni kweli kabisa.
@gosbertgideon6843
@gosbertgideon6843 Год назад
Rose muhando unazo alama za kumuonesha YESUKRISTO skuhyo kwaajili yake ole wetu sisi
@hafsalucky1088
@hafsalucky1088 4 месяца назад
Dada Rose Umenifundisha kuwa strong na kutokata Tamaa, Asante 🙏
@lovenessaron2669
@lovenessaron2669 Год назад
Nakupenda sn kipenz changu Rose mhando Mungu azidi kufungua Milango yk ya Baraka milele yote na Afya njema Ameen 🙏😍
@genevivermambo4000
@genevivermambo4000 Месяц назад
Asante kwa ushuhuda mzur dada rose umeniinua sana
@peterkichochi7510
@peterkichochi7510 Год назад
Mtu yeyote Mwenye Roho Mtakatifu kuanguka huwa ni vigumu sana, ila Kuna kunakujikwaa na kuteleza lakini lazima usimame..Muombeni MUNGU Roho Mtakatifu.
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 Год назад
Kuna kitu gani Kiko Nyuma ya Pazia ..? VIPI Dada Rose usimtaje jina huyo Mtu aliyekutesa watu Turuke naye..? All in all Pole sana Rose Muhando..Wewe ni Mteule wa Mungu..#WEWE NI MSINDI
@reinatave780
@reinatave780 Год назад
Leo nmejua kujifunza kupitia Dada Rose...mungu azid kutusimamia....👏
@daudpius130
@daudpius130 Год назад
Pole sana rose kumbe hizi dini sio nzuri
@nasramtuluma3949
@nasramtuluma3949 Год назад
Nimeinjoy sana...nawapenda wote
@sophiacharles1196
@sophiacharles1196 Год назад
Barikiwa Rose. Hakuna usiku usiokuwa na asubuhi.
@wakisawakisa5455
@wakisawakisa5455 Год назад
pole sana mama yangu, unayoyasimulia kwa mwingine angeweza kutokwa na machozi tena yawezakana asingemaliza kusimulia...ila umeonesha ukomavu, sijui ni kitu gani kingine kinaweza kuja kukupa stress kwenye maisha maana uliyoyapitia ni magumu mno, pole sana...story yako naifananisha kidogo na ile ya SAIDA KAROLI, wanawake mnapitia magumu sana Mungu awasaidie
@thomasmwendi6600
@thomasmwendi6600 Год назад
Hongera sana. Ni fundisho kubwa sana. Keep it up Rose.
@axmedcumar6196
@axmedcumar6196 Год назад
Blessings Asante Kwa ushuhuda Mungu akakusimamie Rose 🌹
@Baba-JJ
@Baba-JJ Год назад
Kwa kweli Salama you are the best kwenye haya mambo. Kuna kipande kimeruka hapo mwanzoni alipoanza kusimulia kilichomtokea mikononi. Nafikiri yalimhuzunisha sana Salama, unaweza kuona kupitia muonekano wake. Salama kauliza hardly maswali manne au matano tu.
@stevennyondo2215
@stevennyondo2215 Год назад
Ushuhuda huu umenijenga , barikiwa
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Mnoo
@rithakuyala9951
@rithakuyala9951 Год назад
😭😭Pole sana dada Rose pia hongera kwa ushujaa wako Mungu azidi kukubariki I LOVE YOU
@fatmaabdallah7709
@fatmaabdallah7709 Год назад
Rose muhando nakupenda sana wewe ndo ulinifanya nisikilize nyimbo za kwaya na wa pili ni gosbert
@susancharles1660
@susancharles1660 Год назад
Pole sana!Hadithi yako imenihuzunisha sana.
@hillarimtambo482
@hillarimtambo482 Год назад
Rose unaniispya sana nimejifunza kitu ubarikiwe 👏👏
@ndojes711
@ndojes711 Год назад
Dk ya 19:38 KAONGEA fact 🙌🙌🙌 AKILI IKIFOCUS KWENY MAPENZIII INAENDA KWENYE MAPENZI, IKIFOCUS KWENYE KAZI INAFOCUS KWENYE KAZI. I GOT POINT
@doreen9516
@doreen9516 Год назад
Mungu akubariki na akuinue Rose! Amen!🙏🏾
@mathiaslyamunda2526
@mathiaslyamunda2526 Год назад
Kwakweli Rose wewe uliitwa na Mungu mwenyewe hata watu wafanyeje hawawezi kukuangusha. Ubarikiwe kwa Ushuhuda huu mkubwa.
@wisemelodytz589
@wisemelodytz589 Год назад
Huwa naaapenda watu ambao wakiumizwa wanarudi kuelezea ili na wengine wapone na sio wanaokaa kimya
@ndayizeyefredina-ni8uf
@ndayizeyefredina-ni8uf Год назад
Mungu akulinde maman wewenimshindi👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍
@priscajonas7805
@priscajonas7805 Год назад
Hakika Rosse ni shujaa nimebarikiwa mno 🙏
@dorothyliveha8607
@dorothyliveha8607 Год назад
Nashukuru Rose muhando ameonge vizuri ameniongeza kuwa na imani kubwa,na watu wawache kuongea uongo ati rose alikua luminat,
@gaudencemihungo4348
@gaudencemihungo4348 Год назад
Salama hongera sana. Leo umekuwa mpole sana. May good Lord bless you.
@gracej9648
@gracej9648 Год назад
Toka nilipokuona mara ya kwanza Rose, sijaacha kukupenda hadi sasa
@TabithaCherop
@TabithaCherop 2 месяца назад
Nimepata funzo through you rose muhando
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Salama mashaallah leo umependeza sn you look beautiful 😍😍🔥🔥🔥
@jacksonjamesndyabawe495
@jacksonjamesndyabawe495 Год назад
Rose.. We love you so much and the holly might God loves you too... Wish you all the best for your career
@chichigrilltz7707
@chichigrilltz7707 Год назад
Kupitia story hii hakika Mungu amegusa maisha yangu Leo hii. 1/4/2023 Mungu atukuzwe.
@asiamuss3279
@asiamuss3279 Год назад
Kuna watu ana nishangaa kwanini nipo single mda marefu na nawezaje hivi hee kumbe akili yangu haipo kwenye mapenzi da rose asantee 😢😢😢😢😢
@josephmghase5613
@josephmghase5613 Год назад
Rose Maisha ni hadidhi, umetufunza mengi uliyopitia na kukata tamaa ni mwiko, ushuhuda wako umenipa ukurasa mpya katika maisha yangu. Mungu aliye juu ya vyote azidi kukupa amani na furaha. Thanks Salama J, your the best interviewer currently in Tz. God bless you all n the team.
@hellenathadeo685
@hellenathadeo685 Год назад
Dada Rose maisha yako na changamoto zako vimenigusa saaana nimefarijika umenipa fundisho kubwa katika maisha yangu.
@barakakusa7606
@barakakusa7606 Год назад
Rose ni amebarikiwa Kweli🙏
@josephine2191
@josephine2191 Год назад
Sounds like When Michael Jackson signed up with Sony and saw hell in paradise
@blackseedsoilckriss1332
@blackseedsoilckriss1332 Год назад
Nathan Meneja wa kwanza wa Rose
@andymasika5284
@andymasika5284 Год назад
Rose anastahili udaktari wa heshima
@sarahgaula2220
@sarahgaula2220 Год назад
😳😃
@habibajumanondo6527
@habibajumanondo6527 Год назад
Nmetamani kipindi kisiishe salama siku nyingine mwite anatuponya majeraha
@ndayizeyefredina-ni8uf
@ndayizeyefredina-ni8uf Год назад
Nami mi napenda sananyimbozako kamazote.🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮👈👈👈
@halima2286
@halima2286 Год назад
Salama yani ukisikiliza stori ya ros unaweza kulia mungu amtie moyi
@denniskagema2745
@denniskagema2745 Год назад
Kwa kweli unaeza pitia Leo Kwa utukufu w kesho na mungu atabaki kuwa mungu
@mathiaslyamunda2526
@mathiaslyamunda2526 Год назад
Salama Mungu akubariki Sana.
@siphaeljoseph2156
@siphaeljoseph2156 Год назад
HII INTERVIEW DADA SALAMA NA DADA ROSE HAIKUW RAISI IMENIPA NGUVU KUBWA MBARIKIWE SAANA YAHKINGSTONE
@de.charlz
@de.charlz Год назад
Rose Muhando🔥💪🏾
@vickydan2869
@vickydan2869 Год назад
History yako mama ya mateso hunipa huzuni mno hujisikia vibaya mno lakn mungu anajivunia ww
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
😭😭😭😭
@bish_daddiyao
@bish_daddiyao Год назад
Ngangana Hilo Ndo Neno Kwa Siku wetu RoseMuhando:(
@jeanpierrekwizera6400
@jeanpierrekwizera6400 Год назад
I love you Salama and Rose 🇨🇦🇨🇦
@doreenkimbe971
@doreenkimbe971 Год назад
Hakuna kukata tamaa. Kushinda ni lazimaaaa
@yurisongoro2895
@yurisongoro2895 Год назад
Dunia👋🏻🙌🏻😭😭😭 sad story ikiwa mbaya ni mwanadam mwenzie Allah nipe mwisho mwema😭😭😭
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Binadamu wabaya sana
@shadrackmwakilasa7059
@shadrackmwakilasa7059 Год назад
Amen 🙏🙏🙏 mungu akusimamie
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Allah nipe mwisho mwema.
@benjaminshayo32
@benjaminshayo32 2 месяца назад
4:20-4:25😂😂😂😂😂😂
@mgurefanuel5581
@mgurefanuel5581 Год назад
MUNGU AKUTANGULIE SANA ROSE MUHANDO
@gracealbin1555
@gracealbin1555 Год назад
Ni kweli Dada Rose akili inacholishwa ndicho inachokifanya
@AfiSoul103
@AfiSoul103 Год назад
Anaongea Kwa uchungu.. jamanii..🙂
@shangwefisima3993
@shangwefisima3993 Год назад
Salama kaishiwa maswali
@mustaphareginald3264
@mustaphareginald3264 Год назад
Hongera sana
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Love you Rose Mhando God bless you
@Jackson_Kisanga
@Jackson_Kisanga Год назад
BIG UP SALAMA
@aminaomary5567
@aminaomary5567 Год назад
😁😁😁wakaenda walikoenda baba wa watoto.
@marthamshana6942
@marthamshana6942 Год назад
😅😅😅😅
@bernadetamodest6170
@bernadetamodest6170 Год назад
😁😁😁😆😆🤣🤣
@anikaanikaa7617
@anikaanikaa7617 Год назад
Leo salama maswali hayafiki atabkumi😌
@josephlorri431
@josephlorri431 Год назад
Amemruhusu atiririke..ameamua kumtibu Rose 🌹.
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Hakutaka kumuingilia amemuacha awe free 😍❤️❤️
@annaannitaglobal1391
@annaannitaglobal1391 Год назад
I luv rose alwayssss...kabisaaa
@douglaskomba2304
@douglaskomba2304 Год назад
Dunia ina mambo pole sana Rose
@G.S985
@G.S985 Год назад
Maana ya mwanadamu iyo, ukifanikiwa anakua adui yako, pole Dada ila yupo Mungu alie juu ya yote
@gosbertgideon6843
@gosbertgideon6843 Год назад
Wooowww Rose muhando Shujaa wa waimbaji injili afrika
@ministeramanirobin2454
@ministeramanirobin2454 Год назад
Hakika Rose Amebarikiwa
@deneagrofarms5884
@deneagrofarms5884 Год назад
Tuongeze kusubcribe kwa mtumishi huyu SHUJAA WA KRISTU. Tumsapoti kwa kusubcribe
@Bintluckas3918
@Bintluckas3918 Год назад
Pole sana😭😭😭
@MainessJoseph
@MainessJoseph 4 месяца назад
Jmni uje ufundishe kwaya fpct nyagulugulu mwanza mahina
@rebekamwimi1394
@rebekamwimi1394 Год назад
Salama Una utulivu sana
@dicksonwakristo5385
@dicksonwakristo5385 Год назад
Mama rose I love you
@risperkerubo5184
@risperkerubo5184 Год назад
Kupidia mama rose nitashinda haya amina imani yako imenisimamisa amen
@justinendizeye714
@justinendizeye714 Год назад
Mama rose Salut 💪💪
@AfiSoul103
@AfiSoul103 Год назад
Tuilisheni akili zetu kwenye yenye manufaa🤸
@francesmpangwa8801
@francesmpangwa8801 Год назад
Love you Mom 😍😍
@anikaanikaa7617
@anikaanikaa7617 Год назад
Love u Rose❤️
@michaellagwen8198
@michaellagwen8198 Год назад
Wa kwanza leo
@essanfesto3049
@essanfesto3049 Год назад
Mh mpe pole rozi
@miguelmiguel543
@miguelmiguel543 Месяц назад
Swali moja kipindi kinaisha 😅
@MxVisualsTz
@MxVisualsTz Год назад
Adult conversation
@fatmaabdallah7709
@fatmaabdallah7709 Год назад
Huyo mchungaji alikuwa ana jeuri gani ya kukutesa bila kuogopa?!
@GodwinJumbe
@GodwinJumbe Год назад
Huyo sio mchungaji... ni mtu aliye msponsor , japo ni wa kanisani. Na ni mtu maarufu anajulikana sana.
@jenyyusuph4973
@jenyyusuph4973 Год назад
Dhuu hadi nimelia
@charlessadoc2203
@charlessadoc2203 Год назад
That’s the most issues the successful people have they forget to build a security while they know there are lions out Side waiting for you
@petermarash3705
@petermarash3705 Год назад
Nyimbo zote Kwa mpigo
@gladnesskivamba4720
@gladnesskivamba4720 Год назад
☀️
@santinamalale3245
@santinamalale3245 Год назад
ASANTE
@ckkevinkigen4968
@ckkevinkigen4968 Год назад
USHUHUDA UNAOISHI
@victormwakipesile6990
@victormwakipesile6990 Год назад
Love u Rose
@bedabenson6576
@bedabenson6576 Год назад
Lete Mgunda
@vivianalbert2626
@vivianalbert2626 10 месяцев назад
duh
Далее
Тренеруем память physics drop 103 - 104
00:51
ТИПИЧНОЕ ПОВЕДЕНИЕ МАМЫ
00:21
Просмотров 1,1 млн
Rose Muhando - Mteule uwe macho
7:33
Просмотров 8 млн