Тёмный

Salama Na MASOUD KIPANYA SE6 EP60 | HERI KUFA MACHO… PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 40 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Habibi Masoud Kipanya ni Ally Masoud Nyomwa ambaye ni LEGEND. Kwa mujibu wake alizaliwa huku kakunja ngumi na dhana yake ni kwamba alizaliwa ili awe bondia! Kwa anacho kifanya na ambacho amekua akikifanya tena kwa ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi bila ya shaka ni UBONDIA. Hakuna ambaye atabisha juu ya hilo. Amekua akipigania mambo tele na kuyasemea mengi pamoja na kuchekesha na kuelimisha kupitia kalamu yake. Kwa mujibu wake yeye ni mbobevu katika taaluma ya kupuuza na kuchukulia mambo poa kwa kipindi sasa. Lakini pia anaamini yeye ni MTATA. Tukienda mbele na kurudi nyuma, hapo kwenye UTATA hakuna ambaye anaweza kumbishia, hasa kwa wale ambao kalamu yake imewanyoosha kwa kiasi kikubwa.
Mimi na yeye tulikutana kwa mara ya kwanza takriban miaka kumi na tisa iliyopita, wakati huo mimi mbichi hasa na yeye akiwa kashajielewa na chemchem yake ya kipato tayari ilikua inatoa neema. Mimi nilikua ndo kwanza naanza kazi ya kujishikiza pale Times FM kipindi hiko bado ilikua kule Kamata. Masoud alikua analichorea gazeti la Majira ambalo lilikua liko kwenye mwamvuli mmoja na Radio ambayo nami nilikua nimejishikiza baada tu ya kumaliza skuli. Urafiki wetu ulikuja naturally tu maana sote tunapenda kucheka. Kupitia Zuhura Yunus na Binti mwengine wa kuitwa Rahma ndo mimi naye tulifahamiana. Wakati huo yeye alikua na gari kwahiyo lifti za hapa na pale zilikua hazikauki. Pia tulikua tunaitumia gari yake kama sehemu ya ku chill na kuskiliza muziki kwenye parking za Times FM.
Huwezi kukaa kwenye tasnia moja kwa muda mrefu kama wewe si hodari na mwenye kujielewa. Moja ya vitu ambavyo naviusudu kutoka kwake ni uelewa wake wa mambo tele wa tele, IQ yake ni ya juu sana na jinsi ambavyo ana reason ndo huwa anamaliza kabisa, kama binadamu wakati mwengine ni bora kukubaliana kuto kukubaliana na kwakwe yeye wakati mwengine jinsi anavyo wachora baadhi ya matukio na watu huwa haviishii kuzuri lakini hiyo haikuwahi kuwa sababu ya yeye kuacha kufanya ambacho anakifanya na ambacho amekua akikifanya kwa muda sasa. Uelewa wake kwenye mambo ambayo yanaendelea, uwezo wake wa kuona mbali na kuweka sanaa yake hiyo kwenye karatasi kisha kutuachia sisi tung’amue maana yake kwa kweli ni kipaji cha kipekee ya sana. Mmoja anatakiwa akae tu mbali na ku admire akifanyacho na hiko ndo ambacho mimi nimeamua kufanya.
Nilikua nataka anielezee maana halisi ya baadhi ya michoro yake ambayo iliacha gumzo kwa muda mrefu lakini kwa sababu ambazo niliziheshimu alisema asingependa iwe hivyo, uhuru wa kuwaacha watu watafsiri wao ndo raha ya kazi yake ingawa yeye anajua hasa kwanini alichora na maana yake hasa ni nini! Kwa heshima ya sanaa ilibidi nikubali matokeo. Toka umeanza kumjua na kufuatilia kazi yake, mara ngapi ushawahi kuskia Masoud yuko matatani? Yaani kakamatwa au hajulikani alipo? Kwangu mara kadhaa lakini haikuwahi kuwa kizuizi cha yeye kuacha kufanya afanyacho, kuogopa je? Nadhani kama binadamu kuwa na uoga ni jambo la kawaida, ila unafanyaje baada ya hapo ndo tofauti yetu.
Episode hii inajumuisha karibu yote ambayo niliwahi kutaka kumuuliza, mengine nilipata majibu nlotaka na mengine yalitolewa mbavuni, kwa ki vyovyote vile nili enjoy sana mimi na wenzangu na kutoka kwetu tunatumai nawe uta enjoy kama ambayo nasi tuli enjoy na kujifunza kutoka kwa MWAMBA huyu.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

27 мар 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 102   
@peterlujuo1640
@peterlujuo1640 Год назад
Ukiitoa show ya ruge kwenye mkasi, hii ndo show bora ya salama, mahojiano yenye contents. Nime enjoy na kujifunza big up y'all
@philomenamushi5606
@philomenamushi5606 Год назад
Hakika nimejifunza vitu vingi na ninazidi kujifunza 🤲🙏salama 🤲🙏masoudy🤲🙏asantee kwa darasa
@veridianacharles4511
@veridianacharles4511 Год назад
Masoudy ni kama muda wake ulikuwa mdogo ilifaa aendelee kutuambia mambo mengi zaidiiii ....... nimejifunza I wish maisha plus irudi tena
@johnmwandu2116
@johnmwandu2116 Год назад
Hilo swali la "Tanzania yako unaiona wapi" majibu yake aiseeee, ni akili ya kiwango Cha juu Sana🙏🙏🙏🙌
@msunjigfx8644
@msunjigfx8644 Год назад
This is the one of the Greatest Man in the World, pengine hatukumwaga damu back in a days kipindi cha uhuru, ama pengine amani tuliyonayo inatufanya tunarelax na kujisahau but INAWEZEKANA
@cheka480
@cheka480 Год назад
indeed
@JohnMadaba-gb1je
@JohnMadaba-gb1je Год назад
Salama kama unahitaji kujua uwekezaji was hisa na Hati fungani niambie. Ntakusaidia elimu for free. I am your fan
@lutufyojason2598
@lutufyojason2598 Год назад
Kaka John .naomba uniongeza na mimi
@gracepaulo704
@gracepaulo704 Год назад
Namm nahtaj weka no bro
@joshuamacha8751
@joshuamacha8751 Год назад
Mimi nataka kujua pia
@aloycemwambwiga2318
@aloycemwambwiga2318 Год назад
Salama J! Kipindi chako kinaelimisha, kinajenga ujasiri, kinakuza kiimani. Nawe Mungu akuweke kama ulivyomwambia Masoud
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Mungu akupe umri mrefu na Afya NJEMA Masoud Wetu 🙏
@mrfashion1687
@mrfashion1687 Год назад
Kali sana hii na nilikua naisubiri hongera kwa kutuletea huyu mtu, sasa bado SALAMA NA MILLARD AYO
@frankphiri2666
@frankphiri2666 Год назад
This guy is one of a kind my best quote "mnanunua hela mnapata wapi" kama nyie ni consumers na si producers
@STEPHENJUSTINE-ty4nh
@STEPHENJUSTINE-ty4nh Год назад
Mtu muhimu sana kwenye taifa letu na maisha ya WaTanzania ...💯🔥
@alifocusmsham7623
@alifocusmsham7623 Год назад
Yani intrerview imeisha wakati ndokwanza inataka kuanza
@Curioustraveller254
@Curioustraveller254 Год назад
Watu wasikujue saana...Familiarity breeds contempt Masoud nailed that
@mwandamboevans-wj8kp
@mwandamboevans-wj8kp Год назад
Shukran sana Kwa hichi Sister Salama,mbalikiwe sana na muishi sana
@mwengmfaume5301
@mwengmfaume5301 Год назад
Nilikuwa nampenda malkom tangu akiwa mdogo japo nilikuja kumuona akiwa amekuwa kuwa,nakumbuka nilikuwa ndo kabinti niliuwa sipitwi na kipindi cha wàtoto chuchuchu , kaka masood na malkom,marehem Amina chifupa na rahmani,,yaani nino, na kaka bonda yey hakuwa na mototo walikuwa wakimcheka kimatani,,aisee
@jerrymwakapemba5644
@jerrymwakapemba5644 Год назад
Nakupenda sana Masoud, huwa sichoki kukusiliza. MUNGU azidi kukutunza, una vitu vingi sana kwa ajili ya kuisadia jamii yetu (nchi yetu). Salama, nakupenda pia, kipindi chako kina mambo mengi sana ya muhimu kwetu. Big up you all!
@Bob-kz2ql
@Bob-kz2ql Год назад
Strong heart Boss Kipanya, hiyo mentality wachache sana wanazo hasa wababa so tumejifunza mamb mengi sana hapo hasa sisi wanaume…be blessed Salama zaidi tupe watu makini sio wale channel za udaku na kutafuta umbea😂😂
@hellenmroso6786
@hellenmroso6786 Год назад
Hiii show imekuwa fupi sana. "Tafuta taarifa upate maarifa"
@glorykileo8601
@glorykileo8601 Год назад
Vp ile show ya maisha plus bonge moja la show itufunza mambo mengi sana kama vijana tunaihitaji tafafhali
@kamuchidyblez2136
@kamuchidyblez2136 Год назад
God bless you masoud wewe ni genius sana aise naamn watu walio karibu na wewe kuna vitu vingi sana wanavipata kutoka kwako ,pia nikupongeze sana salamaa uko smart kwenye kazi yako #greatinterview
@rm9756
@rm9756 Год назад
Plz Salama tuna muitaji tena japo 2hrs tu maana Ana vingi vya kutufunza From Kansas in USA 🤜🏿🤛🏿
@veridianacharles4511
@veridianacharles4511 Год назад
Niliona kama kuna mengi tunahitaji kujifunza toka kwake
@alifocusmsham7623
@alifocusmsham7623 Год назад
Huwa sikuzote simalizi kiu yangu ya kumsikiliza Masoud, nimeangalia interview zake nyingi sana lakini bado nataka zaidi na zidi.
@businesstanzania
@businesstanzania Год назад
Masoud Amezaliwa Zama Ambazo Sio Zake, Atusamehe Bure, Tukitaka Kumuelewa Tumpe Nchi.
@salamisindimwo303
@salamisindimwo303 Год назад
Kipindi kizuri...shukran kwa Mtangazaji,shukran kwa mgeni Ustadh Msoud...tumenufaika na kufaidika piya kupitiya mazungumzo yenu...
@mfaumejuma2375
@mfaumejuma2375 Год назад
What an Interview.....Absolutely Sensational!
@giftwieland6322
@giftwieland6322 Год назад
There is very thin line between love and hate🔥
@abdulhakimmwango9370
@abdulhakimmwango9370 Год назад
Kuna content mmezikata na zilikuwa zinaumuhimu mno sanjari na Hilo bado show ni Kali mashaallah
@emerensianamaganza8322
@emerensianamaganza8322 Год назад
Hawa ndo watu wa kuwekwa serikalini walete elimu na mabadiliko katika jamii, siyo tuu watu watuuu
@lukullikiwamba6494
@lukullikiwamba6494 Год назад
Masud kipanya ni Kati ya watu wenye fikra nyingi sana katika nchi ya Tanzania na bara lake sema sisi watu weusi tumeloga na aliyetuloga kafa, watu Kama yeye uwa tunawachukulia kawaida sana …… mungu ampe maisha marefu kaka yetu kwani bado ana mambo mengi sana kutujuza toka kwenye kichwa chake, Salama sina mengi ya kusema juu yako , you one of the best interview ever live in our generation, was good talk I love it
@priscajonas7805
@priscajonas7805 Год назад
Daaaaah nimejifunza kitu kikubwa Sana thank brother 🙏
@enockcharles6750
@enockcharles6750 Год назад
salama si haki hii ya mwaka jana iruduwe bwana
@josegisbert4351
@josegisbert4351 Год назад
Naomba umuhoji Masoud kila siku...
@joycembuya8480
@joycembuya8480 Год назад
🤣
@UgandanAllstarTales
@UgandanAllstarTales Год назад
SHIRT LAKE KALI SANA
@faridaissa909
@faridaissa909 Год назад
This is the best asante sana salama 🙏
@gtunewaves2867
@gtunewaves2867 2 месяца назад
masoud anaongea vizuri na kwa ufasaha sana
@allenmanzi9869
@allenmanzi9869 9 месяцев назад
Safi sana Masoud. Hapo kwenye Business Plan. Ni Ukweli Mchungu. very true.
@egbertpesha4082
@egbertpesha4082 Год назад
Great interview. Thought-provoking. Masoud has a big mind.
@petermadokola7625
@petermadokola7625 Год назад
Masoud I'm 55years, I studied mechanical engineering, based to motor vehicle, for over 30year, you inspires me big time, man you have great mind weather we want it or not but the truth stand still, Is there any chance we can meet, I would say we are some way alike, I'm a practically man ,you won't regret lay the table with me,
@dianerditto
@dianerditto Год назад
Hili ni darasa huru nimechukua point za kutosha sana leo, ahsante.
@mwajabumalekela5563
@mwajabumalekela5563 Год назад
Duuuuhhh!! Nimejifunza kitu kikubwa saaana, hongera sana cis Salama na big up kaka Masoud, Mungu aendelee kukuweka na kile kilichopo ndani kiendelee kumea
@maridadi_2g
@maridadi_2g Год назад
Men 🎉 Big up to Masoud I like your critical thoughts. Asante salama
@aminanamoyo83
@aminanamoyo83 Год назад
❤ masoud, thanks Salama but please mrudishe tena tafadhali 🙏🇹🇿🇨🇭
@georgemuigai7427
@georgemuigai7427 Год назад
Hakika nimejifunza kitu kwa brother masoud,Mimi nataka kitabu nitakipata wapi?
@abdulhamis9825
@abdulhamis9825 Год назад
Rais Anateua Watu Kushika Nyadhifa MbaliMbali Katika Serikal Na Maeneo Ya Nchi Lkn Iman Yngu Mpka Leo Bado Hajajua Ww Utashka Nafas Gani Ww Ni GENIUS
@brownngullo4051
@brownngullo4051 Год назад
Masoud akili nyingi sana.. very inspired
@heriethalexander5145
@heriethalexander5145 Год назад
This is hands down the best interview I have listened to tangu hii show ianze
@ayubustanley9069
@ayubustanley9069 Год назад
NAWAKUBALI SANA.NBRO.masoud Kipanya nakukubali sana
@barengayabomiriam
@barengayabomiriam Год назад
Yaani baba Malcolm iko kama Mimi simtu wamarafiki.naninapenda saaaana kuka pekeangu kwa sababu Mimi nafkiria saaaaaaaana
@glorykileo8601
@glorykileo8601 Год назад
Nimependa hapo kwa rafiki
@fredgrapher9838
@fredgrapher9838 Год назад
Masoud, my faviurite presenter…since Chuchuchu ya Clouds fm, power breakfast…you are genius
@rehemarwanda6039
@rehemarwanda6039 Год назад
I love Masoud Kipanya huyu jamaa ana akili nyingi sana
@bakarishaha7331
@bakarishaha7331 Год назад
hua namuelewa sana huyu jamaa. (kipanya) ni moja ya hazina , well done , please tuletee kaimu shehe wa mkoa DSM.
@emanuelsolomoni7003
@emanuelsolomoni7003 Год назад
Let me challenge Masoud, Dubai leo ina mafuta na utalii hela wanapata huko as Nation, Urussi ina Gas na Mafuta inapata fedha hapo, sisi tuna Gas, Madini, Utalii how we optimise these resources ziwe na tija kwa Taifa huoni kuna sehemu hatuko sawa, our Gvt needs to be Rich enough tukifika hapo itakuwa simple wao kufacilitate hizo manufacturing ma exports na kuleta Technology mpya, Serikali kama hela ya budget yake ni mpaka itafutane hatufiki, hiyo china, Marekani, Urussi, hata urabuni serikali zao zina hela nyingi sana kwakuwa ni wakali na wamesimamia ukweli kwenye resources zao!!
@abdallahmakombo3866
@abdallahmakombo3866 11 месяцев назад
Shida kuu Kwa nchi zetu ni , Elimu na ufahamu, Tumekosa elimu na ufahamu Kwa viongozi,mtu mmoja mmoja na jamii zetu, Hizo nchi uzitajazo Zina technology, knowledge, Ufahamu huo huwapa , Mawazo, ambayo huwatafuta watu sahihi Kisha hao watu huwapa mtaji / capital ambayo huleta kutatua changamoto za kidunia Kisha hupata zawadi( fedha nyingi/ THAMANI zaidi. Kwa hiyo Kuna haja kubwa ya kuwekeza kwenye wazo ( maarifa)Kisha technology ( mifumo ya uzalishaji Mali kisasa ,na ndipo tufike mbali ,HUKU TUKIJUA UJASUSI WA KIUCHUMI KIMATAIFA . Bado sana
@raheemkareem8055
@raheemkareem8055 Год назад
Super genius🔥
@GAVANA-ut2ek
@GAVANA-ut2ek Год назад
Masoud amebarikiwa IQ kubwa..! Best Interview 🙏
@martinmhando8351
@martinmhando8351 Год назад
Genius Masoud.
@mungonyamilambo1157
@mungonyamilambo1157 Год назад
Bonge la interview 👏👏👏
@petermadokola7625
@petermadokola7625 Год назад
I have worked for 30 years I did different kind of innovation, at the meantime I'm thinking of working with sustainable agriculture based to irritation, your a philosopher,
@johnmwandu2116
@johnmwandu2116 Год назад
12:10,🤣🤣🤣🤣🙌🙌🙌, magari siyo matikiti au siyooo😂😂
@AmonAmon-bn6vn
@AmonAmon-bn6vn Год назад
Akili hzi za masoud Hawa ndio ilitakiwa wawepo bungeni,bahati mbaya wapo Africa.
@mucci_AI
@mucci_AI Год назад
Duuh bonge la interview
@Mfundo272
@Mfundo272 11 месяцев назад
Ningefurahi sana Kama nitapata namba ya Kipanya, from Germany
@naziakijangwa983
@naziakijangwa983 Год назад
Makini broo❤❤
@maximillianmasangya4784
@maximillianmasangya4784 Год назад
Nimejifunza shukran sana kwenu
@mhangwacastory8765
@mhangwacastory8765 Год назад
Ruge Mutahaba, Masoud kipanya ,Massanja,Zembela, Roma mkatoli ,Nauka nafikiri Hawa jamaa Tanzania inabidi iwatumie sana!
@charlesmasesa89
@charlesmasesa89 Год назад
Masud nakukubali na kunakitu chakujifunza toka kwako
@raimajimoto1122
@raimajimoto1122 Год назад
Nakukubali kaka
@ishakafaki3501
@ishakafaki3501 Год назад
Salma na ston town show naomba mniruhusu nitukane ili kiongozii wetu ajee hapa kumsikiliza huyu Kaka 😢😭😭😭
@yohanacosmasmachalila9016
@yohanacosmasmachalila9016 Год назад
Big up brother Masoud na dada yetu Salama
@Emiliana97
@Emiliana97 Год назад
Big brains maahn🙏
@dullywa9973
@dullywa9973 Год назад
only content in this mahojiano 🎉
@lowkeybongo
@lowkeybongo Год назад
Masoud mtu special
@katikatisafaris
@katikatisafaris Год назад
Big brother is not a show to impact an African community, nothing in there. May Allah make it easy for Kipanya to continue with MaishaPlus
@richardmweusi6261
@richardmweusi6261 Год назад
Asaalaam Alleykum naomba utuletee na ezden jumanne!
@nevilekileo8262
@nevilekileo8262 Год назад
Nasubiria salama na Roma mkatoliki, salama na Kala Jeremiah
@Muuaah
@Muuaah Год назад
Voice over artist
@pauldmajo6827
@pauldmajo6827 Год назад
On Podcast is 2 good hours, this is summarized.
@mmn7480
@mmn7480 Год назад
Mi napenda tu slama tabasam lake
@MwanaidChomba-wx7ty
@MwanaidChomba-wx7ty Год назад
Maisha plus ingerudi Tena
@jacksonndabhisiye4848
@jacksonndabhisiye4848 Год назад
kitabu chake kinaitwaje na kinapatikana wapi
@Sportscastletz
@Sportscastletz Год назад
Natamani sana kama utakuwa unaleta watu wahivi wengi kuliko ambao hawana uwezo mkubwa wa kuzungumza vitu sensitive kama hawa mkifanya hivi wallah mtafika mbali hata vipindi vyenu kuwa namba 1 tanzania kuliko channel nyingi za hovyo cause hapa kuna vitu vingi vya kujifunza
@fundiseremalamohammedmdoe3711
Masoud kipanya atafutwe tena, bado hajakata kiu yetu kama watazamaji
@dnewztz
@dnewztz Год назад
12:13 utemgenezaji wa magari sio kilimo cha matikiti😉😉
@abdallahmakombo3866
@abdallahmakombo3866 11 месяцев назад
Hakika, SISI WA TANZANIA NI WACHUUZI KABISA. BIDHAA ILIOTENGENEZWA NA MWINGINE HALAFU UNANUNUA ILI KUUZA KWA FAIDA
@mcrramon4649
@mcrramon4649 Год назад
Moja kati ya watu ambao wanafanya nijivunie kua Mtanzania
@ramadhanijuma9655
@ramadhanijuma9655 Год назад
Wakwanza
@araphatywanyamale6475
@araphatywanyamale6475 Год назад
Why wasimpee aat uongoziii uyu jamaaaa ... mee naaminii iii Dhahabu kwa watanzaniaa aseee
@jobbyandrew4313
@jobbyandrew4313 Год назад
wa pili
@dengahmediatz1230
@dengahmediatz1230 Год назад
Jmn mahojiano mbn mafupi
@mwanaidimohamed9200
@mwanaidimohamed9200 Год назад
Watatu
@reinatave780
@reinatave780 Год назад
I wish Maisha plus Ingerud tena ngoja tuendelee kuomba dua
@erickmorro8852
@erickmorro8852 Год назад
Startup is hassling 🛺💪🏿, asante sana KP
@erickmorro8852
@erickmorro8852 Год назад
eMo Bodaboda Tanzania
@manstiko5890
@manstiko5890 Год назад
Usimruhusu mtu akakujua kuna siku atakutumia vibaya sana kukujua kwako
Далее
🤔
00:28
Просмотров 276 тыс.
Всегда проверяйте зеркала
0:19
Кот Оказался В ЗАПАДНЕ🙀☠️
0:38