Dah! Nashukuru Dana Mzee zjJenerali kumleta huyu. mwanamke. Nimependa Dana sana sana Hoja ya ushndani na kutopenda kuhurumiwa! Hapa Kuna mjadala mzito sana Aitwe Tena. Natoka Kagera.Nafuatilia sana Naona Mzee umefurahi sana
Nimesikiliza kwa umakini maelezo ya huyu dada, hapana nimeona kuna mambo yanaleta mkanganyiko, mbali na dini amabzo zinasemwa zinamkandamiza mwanamke lakini tunazo tamaduni za kiafrica ambazo zilikuwepo uwepo wa dini tulihisi umekuja kuondoa hizo changamoto, nadha tunalazimika kupitia tena mafundisho ya dini ishu ni kwamba hatusomi baada ya kufundishwa hivyo ulimwengu unatupeleka tuishi bila imani, kwa mujibu wa huyu dada anashaka na imani yake na mafundisho yake hayajamuingia vyema, mimi binafsi sikatai wanawake wanapitia changamoto lakini kwa namna kubwa dini imelidha utu na thamani ya mwanamke changamoto ni elimu ya dini husika, sababu hata walioleta dini waliitumia kutunyonya. kuna haja dada akapitia tena dini kwa udani kwa kusoma mwenyewe sio kusikiliza, mwanamke anaweza kuishi kama malkia kama atajitambua lakini sio kuhakikisha anamshusha mwanaume that age will never come.
Kwa heshima ya Jenerali, nikachagua kusikiliza kwa makini maana hata mimi nimekua na ukakasi kuhusu feminism. Kwa kweli Dada amefafanua vizuri sana na nimeelewa. Tofauti kidogo ni kwangu binafsi dini izo izo alizoeleza kama chanzo cha mifumo ya kumkandamiza m/ke, mimi ndizo ziliniamsha kuiona nafasi ya mwanamke sio ya chini kama jamii inavyochukulia. Napendekeza dada upitie kitabu cha dini kiitwacho Adventist Home, ili uweze kueleweka zaidi na waumini.