Тёмный

Adam Mchomvu: "Ofa Zinakuja, Wanakopi Kile Tunafanya, Tushapigwa Mawe Sana |SALAMA NA ADAM MCHOMVU 2 

YahStoneTown
Подписаться 397 тыс.
Просмотров 73 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Adam Mchomvu ni jina kubwa kati ya majina makubwa ya watangazaji mahiri ambao nchi yetu imeshawahi kuona. Toka kuanzishwa kwa Radio za FM hapa nyumbani ambayo ilikua miaka ya kati kati ya 90 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, hapo pia ndo kilipoanza kuzalishwa kizazi cha watangazaji na ma DJ mahiri ambao pia kwa kiasi kikubwa waliweza kulisukuma soko la vipaji mbali mbali vya muziki na filamu kufikia hapa vilipo leo hii. Kazi nzuri iliyotukuka ambayo pia imejaa jasho machozi na damu ilipitiwa. Mpaka leo hii ukiona watu wana launch album zao au filamu zao ujue kuna kazi nzuri ya kujenga misingi ilifanywa na walioianza kazi hii miaka hiyo ya nyuma.
Kwa uelewa wangu Adam ni Generation ya tatu ya wimbo hilo la watangazaji, ukiachana na kina Charles Hilary, Abubakar Liongo na Marehemu Misanya Bingi au Mike Mhagama, kizazi kilichofuata baada ya hapo ni hiki chetu, cha kiza Dozen na Fetty na Anna Peter na kina Adam Mchomvu. Generation sasa ya Bongo Flava na Bongo movie. Kizazi hiki ndo ambacho umahiri wa Adam ulianza kuonekana, XXL bila ya yeye kwa asilimia 100 utalisikia pengo lake, aina ya matamshi na kusema mambo kwa jinsi yalivyo ndo kumemjengea huo upekee. Ila pia ukaribu wake na wasanii wa Bongo flava pia umesaidia kumpatia story za ndani kabisa pamoja na kujua maendeleo ya kazi zao na struggle zao.
Pengine ukaribu huo ndio ulimfanya na yeye atake kuwa mwana muziki?
Sote tunajua kama mziki una mambo yake mengi sana, pengine wewe unaweza ukadhani unauweza na ni rahisi sana kuufanya lakini nadhani ukimuangalia Adam na kumfuatilia kwa kiasi kikubwa unaweza kujua ugumu wa zoezi zima maana kwa mtu kama Adam ambaye yuko jikoni kabisa ameshindwa kufanya muziki kama kazi yake nyengine au kama ambavyo yeye angetaka iwe muziki ndo maisha yake, si tahisi kama ambavyo unadhania. Kwa miaka ambayo nimekua nilifanya kazi kama mtangazaji wa Radio nimeona watangazaji wengi nao wakitaka kujikita kwenye muziki, ambao wamefanikiwa ni wanawake zaidi kuliko wanaume. Adam ameniambia kwenye maongezi yetu haya kwamba wakati mwengine anaona kama watu wanahisi hayuko seriou pengine, pia ameniambia kuhusu utajiri wa nyimbo alizonazo kwenye hifadhi yake. Hii pia imenionyesha jinsi tunavyokua tunafanya kazi ambayo wewe una hakika nayo ni nzuri sana ila kwa watu upokeaji wake unakua sio kama ambavyo wewe umetegemea.
Mi naamini kuna siku tutamuelewa tu maana kwa kumskiliza tu utaelewa utashi wake na jinsi ambavyo anaangalia vitu na uelewaji wake. Kwa wengi Adam ni HODARI na ambaye ameweza kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa muaminifu pia kwa muajiri wake, kama unakumbuka hapo katikati kulikua na wimbi la wafanyakazi wa Radio kupata ofa kubwa za kuhamia Radio nyengine, na nna uhakika mwingi na yeye ofa hizo alizipata, tena nyingi ila aliamua kuendelea kubaki palepale alipokua. Tunaambiwa loyalty haiuzwi wala huwezi kumfundisha mtu, ni aidha unakua nayo au hauna.
Humu mimi na yeye tulizungumzia mwanzo wake, fahamu zake za vitu na maamuzi yake ya kutaka kufanya kazi ambayo anafanya leo. Jinsi ambavyo wazazi au mzazi wake alilipikea hilo. Pia nilitaka kujua mazingira ambayo amekulia, humu amenielezea utukutu wake na jinsi ambavyo alikua na uwezo wa kumdanganya Mama yake ilimradi aishi kwenye aina ya maisha ambayo alikua ameichagua. Na jinsi pia ambavyo aliweza kujichomoa kutoka kwenye dunia hiyo ambayo ilikua imejaa kupotea kama asingekua makini.
Yangu matumaini kuna kadhaa ya kujifunza na yatakua na faida kwako na kwa uwapedao.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Опубликовано:

 

6 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 142   
@kulwakisoma1019
@kulwakisoma1019 2 года назад
My favourite presenter of all the time
@mrfashion1687
@mrfashion1687 2 года назад
Kali sana hii nilikua naisubiri asante kwa kutuletea SALAMA na MCHOMVU, sasa nasubiri SALAMA na MILLARD AYO, SALAMA na B DOZEN, SALAMA na MWIJAKU, SALAMA na DIVA THE BAWS, SALAMA NA GEAH HABIB, SALAMA na SHAFIH DAUDA na SALAMA na MASOUD KIPANYA ,
@dianerditto
@dianerditto 2 года назад
Mwijaku mtoe kwenye hio list
@allyjuma8120
@allyjuma8120 2 года назад
Adam anajua sana,hyu jamaa nambar 1 tz kw watngzaji wakiume
@dianerditto
@dianerditto 2 года назад
Vibe la Adam jamn me cjawahi lizoea miaka oooote namuona mpya kila cku
@majojo91
@majojo91 2 года назад
Moja ya interview kali nilizokuwa nazisubiri 🙌🙌🔥🔥
@emmanuelmchomvu2676
@emmanuelmchomvu2676 2 года назад
Am happy cz umemkumbuka mtto wako Adamu bila kuanza kula
@derickdepota101
@derickdepota101 2 года назад
Energy ya hii interview ni hatari saaana🙌🏿
@asenathogallo2154
@asenathogallo2154 2 года назад
This guy is a whole vibe 🔥 🔥 🔥
@madownloadionlinetv759
@madownloadionlinetv759 2 года назад
Jamaa nimekutana nae tukabadili namba lakini uwe strictly sana ukiwa nae usiwe mjanja mjanja nakubali ana akili sana Adam mchomvu
@nicolenabintu2509
@nicolenabintu2509 2 года назад
Mchovu Akili sana Kama yangu 🧡😀salama keep going 🔥👑
@mariamusaulo4429
@mariamusaulo4429 2 года назад
Adam yupo vizur, thanx Salama
@emmanuelnzaligo6262
@emmanuelnzaligo6262 2 года назад
Napenda sana interview za huyu jamaa.
@mr.futurefrozie2558
@mr.futurefrozie2558 9 месяцев назад
Adam namwonanmbali, Sana appreciate kwake bruda from home land
@kibwanakhamisi5604
@kibwanakhamisi5604 2 года назад
You doin a good job salama... Mchomvu is always a vibe 🤟🏽
@marwajuma7493
@marwajuma7493 2 года назад
Mirad ayo next
@mbenamdudu7856
@mbenamdudu7856 2 года назад
Salama Leo umetisha sana huyu jamaa ni noma mchomvu walimu mmekutana ktk interview wote wakali mjawai kuharibu wote wawili
@finiaskalist747
@finiaskalist747 2 года назад
Mtangazaji wangu bora wa muda wote
@ChidwadarChidwadar
@ChidwadarChidwadar 6 месяцев назад
Namkubali sana mchomvu nisaidie nataka niwe dj
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 2 года назад
11:33 🔥 17:42 human talking 19:11 😆 funny guy
@smartmussadozen3535
@smartmussadozen3535 2 года назад
Una enjoy interview Adam noma
@nathanaeljimmy5393
@nathanaeljimmy5393 2 года назад
Brandy ya Kitaa... I do appreciate the guy@ Adam mchomvu
@edgardevis8152
@edgardevis8152 2 года назад
I like aunt salama napenda san kipindi chako kina2elimisha sana sis vijana
@nellymatalanga5033
@nellymatalanga5033 2 года назад
Next Dozen, Millard ,Sky.Jonijo...
@irakozeaudrey8643
@irakozeaudrey8643 2 года назад
Adam unanipa Raha sana
@Jefa_Adili
@Jefa_Adili 2 года назад
#AsoHiliAnaLile njmeipenda hii nilikua najua only in -ve way, Adam kaniongezea +ve pia, so imekua Hakuna mwema aso na ubaya, nahakuna mbaya aso na jema, kila mwenye nguvu anaudhaifu wake, na kila dhaifu ana ambalo ananguvu nalo, usiabudu wala kudharau mtu.
@hoseayesaya4751
@hoseayesaya4751 2 года назад
Namkubali bro mchomvu
@jacksonbahemu8172
@jacksonbahemu8172 2 года назад
AD PLUS BEST PRESENTER EAST AND CENTRAL AFRICA
@sarahkitindi3420
@sarahkitindi3420 2 года назад
Asante sana sister salama
@barakakusa7606
@barakakusa7606 2 года назад
Adam ni mwana Sana na yupo humble Sana na yupogo to hapo
@AfricanGiant-te9et
@AfricanGiant-te9et Год назад
Nakukubali sana mzeee
@tanzaniamycountry9308
@tanzaniamycountry9308 2 года назад
Oyaaaa nathaminika ama😀😀😀😀 Nmekumbuka maneno ya mbasha ghafla. Shkamoo Broo Adam😊
@adamore854
@adamore854 2 года назад
Ndoto yangu pia imetimia🙏
@karimhemed9261
@karimhemed9261 2 года назад
Is my Boy Alright Out there? 🙌🏾 Dadies Duties….
@benedictmacoy4798
@benedictmacoy4798 2 года назад
Best of the best presenter Tz,AD +
@robinsonjames9711
@robinsonjames9711 2 года назад
The Classic presenter AD + nakubali😘
@rizikiones5687
@rizikiones5687 2 года назад
Adam anaakili nyingi sana
@secondyoana-uv4wn
@secondyoana-uv4wn Год назад
Flo mbovu,Yani huna saut yakufanya nikusikilize ukifloo by Geoffrey Mbele
@kennedjohn5785
@kennedjohn5785 2 года назад
Namkubaali mbayaaa
@joeljoshua1940
@joeljoshua1940 2 года назад
Great 👍 show. The vibe is great..!
@wilsonchishomi1083
@wilsonchishomi1083 2 года назад
RIP JPM.. you’ll always be remembered 😢
@immaabukuku7180
@immaabukuku7180 2 года назад
Adam si ndio aliyempiga mwenzie mtama si ilikuwa kwenye majukwaa ya wanasiasa
@AlfredCarol_tz
@AlfredCarol_tz Год назад
Mchomvu is always on fire 🔥🔥🔥
@rahabumasebo8084
@rahabumasebo8084 2 года назад
Nimecheka Sana Nampenda Sana huyu kaka.
@johariramadhan5236
@johariramadhan5236 2 года назад
Super star wa nabii
@renatusmpete3527
@renatusmpete3527 2 года назад
Appreciate dada mkubwa
@mbenamdudu7856
@mbenamdudu7856 2 года назад
Salama nakuelewa na Adam pia mtu mbadi
@ngambikomsu64
@ngambikomsu64 2 года назад
Nice interview
@adolfmathew9698
@adolfmathew9698 2 года назад
Eyoo mchomvu #chuga represent
@casablancastudioarusha775
@casablancastudioarusha775 2 года назад
Hot story Big up Sallama na Adam
@marksulle6120
@marksulle6120 2 года назад
Adam ur so charming
@baliatuhamis9696
@baliatuhamis9696 2 года назад
Bongo fleva bado inakuhitaji sana AD..mpk mda huu bado hawakuelew...
@majatv1088
@majatv1088 2 года назад
He is real may god keep him up…
@damiankimaro9665
@damiankimaro9665 2 года назад
One of the best
@mohammedmwarizo3700
@mohammedmwarizo3700 2 года назад
Noma sana hii naisubir na salama na fatma hassan (dj fetty)
@gibsonbitende
@gibsonbitende Год назад
Adam we noma sana umetema checheza moto interview ya maanakinoma noma
@justnjustn6168
@justnjustn6168 Год назад
Jamaa awali chakula
@BBrown_vevo
@BBrown_vevo 2 года назад
Kali Sanaa hiiii
@raimajimoto1122
@raimajimoto1122 2 года назад
Adam aka Jack chan...zee la mitama
@martinechangwa2046
@martinechangwa2046 2 года назад
Jamaa anajua
@gibsonkabusola6923
@gibsonkabusola6923 2 года назад
Yaani mi napendaga mchomvu anavosema komba mwiko Fm😂😂😂
@Mnangoja_Tailoring
@Mnangoja_Tailoring 7 месяцев назад
Makn san brother smart
@michaelkipara8205
@michaelkipara8205 2 года назад
tunahitaji pia interview ya salama na zuchu
@FrankDeus-y8o
@FrankDeus-y8o 2 месяца назад
Mama kasema is the project
@chiticollemans
@chiticollemans 2 года назад
He is very funny 😂
@khamseysagrado7547
@khamseysagrado7547 Год назад
Sidhani kama ninaflow mbaya kushinda sugu😄😃😃😃😃@ad+
@shukurumswagala5256
@shukurumswagala5256 2 года назад
KIUKWEL MCHOMVU NAMKUBALI MBAYA
@dilipdab3714
@dilipdab3714 6 месяцев назад
Good salaam
@rwehumbizajonathan8689
@rwehumbizajonathan8689 5 месяцев назад
Bonge la Interview, Vibe la kutosha. 💪🙌
@princenyerere4048
@princenyerere4048 2 года назад
Great interview, keep up the good work. please correct the video description *wimbi Sio wimbo
@ubaoni57
@ubaoni57 2 года назад
Salama Na B dozen
@mussamoshi3205
@mussamoshi3205 2 года назад
Namkubali sana mwamba .adam big up
@allynizam7138
@allynizam7138 Год назад
Namfaham sana kwajina THE INK
@enrico955
@enrico955 2 года назад
Yoo such a nice interview .....
@nyamarasapeter4302
@nyamarasapeter4302 2 года назад
Nice and fun interview
@carenmsafiri8498
@carenmsafiri8498 Год назад
aiseee the best interview everr
@hudsonhenry1849
@hudsonhenry1849 2 года назад
Mtafute na unju sasa
@salimtiba4614
@salimtiba4614 2 года назад
Namkubari sana uyu mwamba Mkrisilam mwenzangu natmani siku nikutane nae tupige story za kutoosha
@laflame3450
@laflame3450 2 года назад
Next Luffa🔥
@jamesnatai7430
@jamesnatai7430 2 года назад
Nampataje mchonvu nje ya mjengoni?????
@ibrahimkibira9943
@ibrahimkibira9943 2 года назад
Nice interview as always 👌 👍 👏 🙌 😊
@danielagustino3130
@danielagustino3130 2 года назад
Bm kama bm.....#mchomvu..!!
@brianrichard9022
@brianrichard9022 2 года назад
that man yuko na slang nzur
@fadhilhussein8845
@fadhilhussein8845 2 года назад
Huo ni uongo huo niuongo bhana mchomvu ashawahi kuwa MC katka chama mapinduzi ndio siku aliyompiga mtama mbashs
@aliganzel6512
@aliganzel6512 2 года назад
Alikuwa pale as Mic controller wa event na sio part ya campaign haina tofauti kati ya alichofanya Adam na alichofanya Haji Manara
@waziriseif5384
@waziriseif5384 Год назад
Interview nzur san...
@susannesusie3217
@susannesusie3217 2 года назад
😂😂😂😂😂😂 Utuletee milard Ayo
@sumay8817
@sumay8817 2 года назад
Chiii nice interview
@denislazaro818
@denislazaro818 Год назад
AD PLUS
@johariramadhan5236
@johariramadhan5236 2 года назад
Yaan adamu leo anamuhoji yeye salama
@1000Brain
@1000Brain 2 года назад
Umetuongopea hapo kwenye media yenu kujihusisha na siasa. Clouds ni ccm tupu
@LumolaSteven
@LumolaSteven 2 года назад
Salama unajua sana
@lusekelomgellela8748
@lusekelomgellela8748 2 года назад
Really hustler is HERE... Thanx salama
@adrianboniventure5509
@adrianboniventure5509 2 года назад
Good one
@sabanajr6455
@sabanajr6455 2 года назад
🔥🔥🔥🔥
@smashowupdates2377
@smashowupdates2377 2 года назад
Bro unajua sanaa
@hassanikipusa8328
@hassanikipusa8328 2 года назад
Nondo za kutosha (Content)
@johnpetro1069
@johnpetro1069 2 года назад
Salama nakuamini sana 🥰🥰❤
@omarmahewa928
@omarmahewa928 Год назад
Yote kwa yote Salama mi sijapenda hivyo viti kwakweli!
@itNeza
@itNeza 2 года назад
SALAMA Tunamtaka Mbasha. 😂
@agathamatambula538
@agathamatambula538 2 года назад
😆😆😆😆
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Adam Umetisha 😂😂😂
@fraitmgala5966
@fraitmgala5966 2 года назад
Adam mchomvu (Tall wa Ajabu)
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 года назад
Ila huyu Mchomvu...😂🙌😂
Далее