Тёмный

Safari Ya Dina : Asimulia Msoto Aliopitia Kabla Kuwa Mtangazaji | SALAMA NA DINA MARIOUS PART 1 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 39 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Dina Marious ni STAR ambaye amakua akijenga jina lake kwa miaka mingi sana. Kama sote tunavyofahamu hakuna mtu ambaye anaibuka tu siku moja na kupata heshima na kuaminiwa kama hajafanya kazi ambayo itamfanya watu wamuamini na kumpenda. Dina yeye ameteka kabisa soko la Wanawake, kitu chochote kinachohusiana na wanawake na madhila, raha na mambo yao ya kijamii basi ukiangalia kushoto na kulia lazima utamkuta Dina yuko hapo akitoa mchango wake kwenye suala hilo. Iwe kuanzia maandalizi au uwepo wake tu. Hicho ndo ambacho yeye kama Mama na Dada na Binti ameamua kufanya, na anaweza haswa.
Alianzia Radio ya watu ya Clouds FM na baada ya kupata mtoto wake wa kwanza mitihani mingi aliipitia, ile maternity leave ambayo alikaa wakati anamkuza kijana wake ilileta mabadiliko makubwa kwenye maisha yake. Zion (mtoto wake) alipo zaliwa ilimbidi Dina aache kazi kwenye Taasisi ambayo alikua ameizoe mno na kutafuta ustaarabu mwengine bila ya kuwa na mipango hiyo wakati alipochukua likizo yake ya kwenda kujifungua. Mipango ilikua akitoka kwenye likizo yake hiyo ya uzazi basi arudi tu kazini kwake kama kawaida lakini Bosi wake wa wakati huo, Marehemu Ruge Mutahaba alikua na mipango mengine na Dina mipango ambayo kwa mujibu wake anaamini alikua akipigwa chenga tu na hakukua na mpango thabiti ambao ulikua umeekwa kwaajili yake.
Dina anakumbuka nenda rudi alizokua akizipata na kulipwa mshahara bila ya kufanya kazi yoyote, kwa kweli hilo lilikua likimsubua sana na anasema kila akiangalia kushoto na kulia alikua haoni dalili zozote za yeye kuanza kufanya kazi muda wowote wa karibu na kwasababu maswali yake mengi mazito yalikua yakipatiwa majibu mepesi mepesi aliona basi si vibaya kama atatafuta challenge nyengine kwenye maisha yake. Kwanza hiyo plan ambayo alikua amepewa hakua ameifurahia na pili majibu ambayo alikua anapatiwa nayo yalimfanya ajue pale hapakua sehemu sahihi kwake tena.
Kumuuma ilikua ikimuuma sana kama anavyosema mwenyewe, hakukua na sababu yoyote ya kutaka kufanya mabadiliko yale ambayo yalifanyika, ya kutaka kumpeleka yeye kwenye TV wakati tayari alikua ameshatengeneza kundi kubwa la mashabiki kwa wakati huo, na pengine approach iliyotumika pia haikua sahihi na hilo liliacha ladha mbaya kwenye moyo na kinywa chake, na baada ya hapo kwasababu kulikua na ofa nyengine hakufanya ajizi kuziskiliza na uzuri zaidi kwanza hapakua mbali na ofisi yake ya zamani hapo alipokua anatakiwa na pili ambalo ndo KUBWA kabisa, alikua anapewa muda ule ule wa hewani kama ambao alinyang’anywa baada ya kuenda likizo ya uzazi kwenye ajira yake ya zamani. Alikua na kila sababu ya kuchukua hatua nyengine na kujisogeza mbele zaidi, kama ambavyo tunafahamu, mtu huenda aitwapo. Na mengine ndo haya, yamebaki story tu.
Nafasi yake kwenye jumuia za wanawake ni ya kipekee na anaiweza kuikaimu vizuri tu, amekua akifanya shughuli mbali mbali za kutatua baadhi ya adha na pia kuwatunza wale ambao anadhani wanastahili ili kuwafanya wapate nguvu zaidi ya kuendelea kufanya wanayofanya kwa uzuri zaidi. Na amekua mfano mzuri hata kazini kwake maana kipindi chake cha Radio ni moja ya vipindi vinavyo sikilizwa zaidi kwa wakati ule. Hilo halina ubishi.
Kama binadamu wengine na yeye nae ana ushindi mwingi na kushindwa kwingi kwenye maisha yake na kwenye session hii tukiyagusia hayo na zaidi. Kuhusu mapenzi, mtoto, familia yake alitokea, elimu na malezi lakini pia muajiri wake wa zamani na jinsi ya kukabiliana na mambo mbali mbali maishani.
Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza mambo kadhaa kuhusu kazi na jinsi na kujua kutafuta na kupata kutoka sehemu nyengine ukiachana na ile ulokua umeizoea.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

9 окт 2022

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 75   
@hildasawe666
@hildasawe666 Год назад
Jamani Da salama siamini nilichoomba kimefanyika nakupendaje 💖💋uwiiiii hongera sana mpz hakuna kama ww in East Africa Mungu akusimamie..nampenda sana huyu Da Dina 😍💖❤
@babyhamisi1437
@babyhamisi1437 Год назад
Wallai watu walopitia maisha magumu ndio nahisi wana maendeleo sana na niwapiganaji wa maisha vizuri
@CoachHafidh
@CoachHafidh Год назад
#Yahstonetown naomba mumlete stara thomas...naamini ana mingi ya kuuongelea huu mziki wetu na maisha yake kwa ujumla. Regards🙌🏾💛
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 Год назад
daah umewaza mbaali ni kwl yule mdada kitamboo wamletee
@freewillmlay4822
@freewillmlay4822 Год назад
Dada mlete Babalevo Ni “Chawa” but kwenye serious issues he’s so smart 🧠
@abdallahmassah1770
@abdallahmassah1770 Год назад
Madam salama. Nashauri interview ya Salama na Maulid kitenge
@ilovejesus9303
@ilovejesus9303 Год назад
Ooh nliwatch part 1 nkisubiri part 2, kumbe leo dada Salama kabadilisha kidogo
@ballisticsound4796
@ballisticsound4796 Год назад
THIS WAS GOOD AS USUAL....NEXT AJE STARA THOMAS BASI
@edwardmachaku1661
@edwardmachaku1661 Год назад
Hujambo! Hongera.
@kambamazig02024
@kambamazig02024 Год назад
Your enemy does not need a reason to do bad things, ama adui huwa hana sababu ya kutaka kukutendea mabaya.
@tinomasangia5511
@tinomasangia5511 Год назад
Yea hii n part I
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
Hasidi hana sababu 👌🏽👌🏽👌🏽
@barakakusa7606
@barakakusa7606 Год назад
Marlaw tunaomba umlete Salama🙏🙏🙏
@happinessjulius9230
@happinessjulius9230 Год назад
Finally
@tonystratony8131
@tonystratony8131 Год назад
Nice
@achileusmulokozi4963
@achileusmulokozi4963 Год назад
huyu dada jamani,nampenda mnoooooooo
@bish_daddiyao
@bish_daddiyao Год назад
Salama Niletee Juma Nature Au a Upendi kumhojii
@shafee9128
@shafee9128 Год назад
Mtu mwenye kukufanyia hila au ubaya fulani huwa hana sababu za msingi kufanya hilo nalo fanya #salama
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Год назад
Dah kweli mahasidi wanaanzia udogoni😄😄
@agathamatambula538
@agathamatambula538 Год назад
Dinaa🔥🔥
@muscatoman2766
@muscatoman2766 Год назад
Good
@rehemangonji573
@rehemangonji573 Год назад
Yaan ya kwanza ni ya pili na ya pili ni ya kwanza😅😅😅
@Tatizofficial
@Tatizofficial Год назад
Next county wizzy,tuleteee yule boy
@aminasaid7518
@aminasaid7518 Год назад
❤️
@niriacatering172
@niriacatering172 Год назад
Penda Sana salama na Dina Mungu awalinde
@abdulraufmohammedsalum6806
@abdulraufmohammedsalum6806 Год назад
Hasidi ni mtu ambae akiamua kukufanyia Ubaya sio lazm uwe umemkosea Hua anaamua tu kukufanyia Without any reason
@asterialucas4680
@asterialucas4680 Год назад
Nampenda sn Dina Marious
@monicajohn2515
@monicajohn2515 Год назад
Jamani napenda kicheko Cha salama dah
@hosamhilary1877
@hosamhilary1877 Год назад
Heey sorry, mme label hizi parts wrongly. Part 1 imekuwa as Part 2 and vice versa.
@browngennestone5979
@browngennestone5979 Год назад
Next episode fred saganda atishe humu please
@abdulhamis9825
@abdulhamis9825 Год назад
Salama Tutafutie Na Watu Wa Football Sio Watu Walio Kwenye Media Tu
@Tatizofficial
@Tatizofficial Год назад
Huyu da Dina mmi nampenda namkubaliigi,nilikuwa nakushangaaa ukuwahi kumhoji Dina,Dina ni balaa
@fortunatanasuwa6789
@fortunatanasuwa6789 Год назад
Hapo kwenye kuishi na mahasidi kwa akili ndio shida, bora kumtema tu
@babyhamisi1437
@babyhamisi1437 Год назад
Mlete aunty sadaka twamuhitaji
@Tatizofficial
@Tatizofficial Год назад
Iam Dina,fAns
@simonlunyelekwe5520
@simonlunyelekwe5520 Год назад
Salama-Tuletee marlow 🇰🇪🇹🇿
@kakukili6173
@kakukili6173 Год назад
Kweli kabisa marlaw
@clackcharles4253
@clackcharles4253 Год назад
Hii ni part 1 salama
@RamazaniMulongeca
@RamazaniMulongeca Год назад
UMEKOSEA SALAM, hii ndo Part1, but umeadika part2, Na part 2 umesema Part1 Of course wakwanza mimi #1
@ramansitv3292
@ramansitv3292 Год назад
nilidhani hivyo pia lakini soma tittle vizuri mwenye kuwahi hakosi part 2
@RamazaniMulongeca
@RamazaniMulongeca Год назад
@@ramansitv3292 Smart,
@abdulhamis9825
@abdulhamis9825 Год назад
Dina Anazungumza Kiswahilin Kabsa Kwel EFM imekubadili Sana Tofaut Na Dina Yule Wa Clouds
@muna1744
@muna1744 Год назад
Part 1 imeandikwa part 2 na part 2 imeandikwa part 1
@sophiamfikwa7340
@sophiamfikwa7340 Год назад
Live you dada Dina🥰
@approxtv9021
@approxtv9021 Год назад
Tuna miss interview yako na Millard ayo
@tanzaniasafariadventure3635
Wap Salama na Fred Vunjabei
@seyyactor1418
@seyyactor1418 Год назад
Typing error Leo kwenye episode but 🔥🔥
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 Год назад
Soma virzuri kichwa cha habari... Wee ndo umetafsiri kimakosa... #MwemyeKuwahikakosiPart2
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
Awesome c Ya kukosa ii
@hendricksaugustine6967
@hendricksaugustine6967 Год назад
hasidi hana sababu " mtu akitaka kukuletea jam anakuletea tu hatakama haujamkosea
@nicolenabintu2509
@nicolenabintu2509 Год назад
She’s goes 😍
@abdallahcooper3111
@abdallahcooper3111 Год назад
Either write She's gone or She goes, There's no She's goes in English!
@mkamajames2786
@mkamajames2786 Год назад
@@abdallahcooper3111 jamaa kwani lugha iyo yake au wee ndo unajua sana
@khamisidaimambelentakuchom103
@@abdallahcooper3111 qqppp²q
@Tatizofficial
@Tatizofficial Год назад
Salama mwambie Dina yeye kazaliwa Arusha,alafu hapendi kuleta mwanamke wa shoka kaskazinii,
@richardmkude9131
@richardmkude9131 Год назад
Hasidi hana sababu,mtu mwenye ubaya au akitaka kukufanyia ubaya anafanya bila hata ya kuwa na sababu
@ninjaisma7983
@ninjaisma7983 Год назад
Tuletee Nikki mbishi pia tumsikie akijibu maswali yako yakijanja
@daudynaccer4313
@daudynaccer4313 Год назад
kabisa mzee
@CoachHafidh
@CoachHafidh Год назад
Nakuunga mkono
@jumannehassan8131
@jumannehassan8131 Год назад
Stamina na afande sele walete hapo sijawaona kwa kiti
@scholamwasi2782
@scholamwasi2782 Год назад
Ya da dina toka umeanza kujipunguza mbona upungui we kula tu ndo mwili wako uwo
@aishaomarry6996
@aishaomarry6996 Год назад
SALAMA m na Albart Chalamila tunamuomba
@jumannehassan8131
@jumannehassan8131 Год назад
Stamina n afande sele walete bado sijawaona kwa kiti
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 Год назад
"#TITLE" YA KWANZA ILIKUWA "#VERYPHILOSOPHICAL..." Laiti aliyefanya "#editing" angejua alichoondoa kilikuwa na thamani kubwa mmno.
@happyswai8299
@happyswai8299 Год назад
Kuna watu wana bahati
@saidmaulid5609
@saidmaulid5609 Год назад
Salama niaje nakuomba tulete juma nature
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 Год назад
Bonge moja la interview c lakukosaaaa Nature km Nature
@nickjuma3937
@nickjuma3937 Год назад
mbona husemi umesoma shule zipi majina yake!!
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
Hasidi ni mtu anakuharibia hk anajifanya anakuhurumia au anakupeti peti
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 Год назад
Nizaid ya mchawiiii hasidi muharibu wamambo yaaani ktk watu nawachukia ni awa
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
@@mapekhamis3882 yani hasidi na mnafiki wametofautiana kdg tuu
@idamtesigwa6002
@idamtesigwa6002 Год назад
Salama tuletee Max Rioba
@maiyanakupendanadayasanama7033
Nampenda sana dina mazungimzo yake na no mzuri sana
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 Год назад
Yy na Salma Msangi co wakujishaushaua wako real kama ulikula dagaa sema kama ulitembea posta mpk temeke kwa miguu sema tu ni maisha yakawaida binaadam upitia nimependa walivojiachia kwa interview cjui ni kwavile wako ktk iyo section km Salama🙌
Далее
2DROTS vs WYLSACOM! КУБОК ФИФЕРОВ 1 ТУР
07:25
Salama Na Masoud Kipanya
52:05
Просмотров 8 тыс.