Тёмный

RC SENDIGA AKASIRIKA, SIKIA ALIVYOMKARIPIA MENEJA TARURA IRINGA 

Wasafi Media
Подписаться 4,8 млн
Просмотров 75 тыс.
50% 1

RC SENDIGA AKASIRIKA, SIKIA ALIVYOMKARIPIA MENEJA TARURA IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga ametoa siku 7 kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoani humo kuhakikisha inaisimamia kampuni ya ujenzi inayojenga barabara ya Zizilang’ombe-Ngerewala Mjini Iringa, kufanya marekebisho kwenye sehemu ya barabara ambayo mifereji yake imebomoka kabla hata ya barabara hiyo kukabidhiwa.
Kauli hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu msamalia mwema ambaye ni mwananchi mkaazi wa Manispaa ya Iringa kurekodi kwa simu yake ya mkononi sehemu iliyobomoka ya barabara hiyo na kurusha katika mtandao wa Instagram.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa anafika katika eneo hilo na kujionea hali halisi kwenye barabara hiyo baada ya sehemu kubwa ya barabra hiyo ya urefu wa KM 1 inayojengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 600 kubomoka hali ambayo inamlazimu kutoa karipio.
WATCH WASAFI TV📺
AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113
LISTEN WASAFI FM 📻
88.9 DAR/ZNZ/PWANI 📻 | 104.1 DODOMA 📻 | 94.5 ARUSHA 📻 | 97.3 MBEYA 📻 | 94.9 MWANZA 📻 | SHINYANGA 106.3 📻 | KIGOMA 101.7 📻
Follow Us On:
INSTAGRAM: / wasafitv || / wasafifm
TWITTER: / wasafitv || / wasafifm
FACEBOOK: / wasafitv
𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2021 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅.
#wasafi #wasafitv #wasafifm

Опубликовано:

 

14 окт 2024

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 151   
@far_hard1301
@far_hard1301 2 года назад
Safi sana tunataka viongozi wenye uchungu kama hawa
@aminaomary5567
@aminaomary5567 2 года назад
Rc uko vizuri sana hapo kinachoendelea ni wizi tu.Una gema/korongo hilo pesa ya wananchi inaliwa tu jamani.👍👍👍
@Zainab-sq1tc
@Zainab-sq1tc 2 года назад
Saf sana kaz nzuri
@margarethpolepole7438
@margarethpolepole7438 2 года назад
Chapa kazi sendiga mungu akupe nguvu zote
@meekpaul7388
@meekpaul7388 2 года назад
Safi mama nimekupenda bure kaza buti usirudi nyuma
@kahemachowdry7346
@kahemachowdry7346 2 года назад
Hongera Mkuu wa Mkoa Iringa,Kuwakwmwa Tarura ni Ahida
@radhiasalum7156
@radhiasalum7156 2 года назад
Huhuhuhuhu kuleni urefu wa kamba zenu😀😀😀🤸‍♂️maneno ya rais wetu
@oscarkasalile5058
@oscarkasalile5058 2 года назад
Mheshimiwa mkuu wa mkoa upo vizuri sana Hongera sana
@denicephillimon9219
@denicephillimon9219 2 года назад
Hupaswi kumfokea mwanaume hivo, maana mwanaume ni kichwa cha familiar, so vp ww mkeo akukaripie hvo hta kama umekosea
@hadijajohn7434
@hadijajohn7434 2 года назад
Safiiii sana sendigaa mkunjekunje mkandarasi arudi china . Mafisadi haooooooo. Barabara mbovuu wapigaa . Dirii haoooo . Sendiga..kawastukia😆😆😆😆😆😆😎😎😎😎😎😎 U
@ramadhanihafidh7732
@ramadhanihafidh7732 2 года назад
Safi sana mama MWENYEZI MUNGU akufungulie rehma zake wewe ni kiongozi
@kasendelukadi2047
@kasendelukadi2047 2 года назад
Sisi congo tunapenda viongozi kama awa wenye wanajali
@jamesnjenga813
@jamesnjenga813 2 года назад
Aah rami imeekwa kidogo sana
@abdumpunda4026
@abdumpunda4026 2 года назад
Hongera mkuu wa mkoa piga kazi na ussiogepe
@kavoomshana7289
@kavoomshana7289 2 года назад
😀😀😀,haya bana safi kiongoz ntakunja kunja mtu nimueke kwenye pochi....
@malecellacaezaryj2414
@malecellacaezaryj2414 2 года назад
🤔🤔
@saxannjo6173
@saxannjo6173 2 года назад
UFISADI, WIZI, NA UPIGAJI WA VIONGOZI UMEENEA SANA BAADA JPM KUTUACHA. WENYE MAMLAKA MUANZE KUJITAFAKARI KAMA MNAFAA KUTUPELEKA TUNAKOSTAHILI.... INATIA HASIRA KWAKWELI
@bonosaugustine6545
@bonosaugustine6545 2 года назад
Huoni wanachkua hatua au unataka kusema upigaji huko haukuepo??
@TamuzaKale
@TamuzaKale 2 года назад
@@bonosaugustine6545 Ulikuwepo. Sema mahaba mkuu!
@allykeita704
@allykeita704 2 года назад
Huyu Dada aongezewe cheo Ni Zaid ya mkuu wa wilaya🙏🏾🙏🏾🙏🏾🇷🇺🇷🇺🇷🇺🇷🇺👏👏👏
@rashdiyange7758
@rashdiyange7758 Год назад
uyu dada nyoko saaa mamaeee safi sana lafu kidogo ana puliza bola jamani wakuuu wamikoa muwe nna pulixa kidogo il mambo yaende
@shabansalee4924
@shabansalee4924 2 года назад
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭daha naumia sana sema sisemi ntatukanwa Mana kila mtanzania anajifanya muerewa
@ismailmashimba3470
@ismailmashimba3470 2 года назад
Hio nimeipenda yani utamkunja hadi aingie kwenye pochi duu
@lazarochatanda755
@lazarochatanda755 2 года назад
Safi sana kwadalili hiyo ukigombea tena uraisi utajizolea kula nyingi apa iringa
@safariyawokovu4413
@safariyawokovu4413 2 года назад
Hongera kiongozi
@charlesmakuri792
@charlesmakuri792 2 года назад
Ndiooo mmemtibua safi ukiendahapo kinyoronyoro
@thomassedo5012
@thomassedo5012 2 года назад
Na me naenda kuishi iringa kwanza DC mrembo natamani ningepewa iyo barabara niijenge mimi😂😂
@lilyjones3584
@lilyjones3584 2 года назад
Huyu RC vipi! Hajaelewa kwamba kina Mama wanasema kwa kalamu! Kelele za mlango hizo......! Asipokuwa makini ataondolewa kwenye hiyo nafasi ili apewe anaeongea kwa upole.
@halimamasai2234
@halimamasai2234 2 года назад
🤣🤣🤣🤣👍👍👍
@juliussuleiman3999
@juliussuleiman3999 2 года назад
Sendiga bigup sans
@rezembuses5739
@rezembuses5739 2 года назад
Viongozi Msitishwe Msiogope Ni bora tufe sote kuliko kurejesha vizazi vyetu utumwani.
@karibunyumbani3824
@karibunyumbani3824 2 года назад
Mwizi wee barabara Haina miaka 2 mitaro imebomoka kweli rc hapo umemuweza
@bwagizoselemani8434
@bwagizoselemani8434 2 года назад
Daah waswahili bana asa ndio amejengaje hivi jaman
@hussmuya5246
@hussmuya5246 2 года назад
Dada jikaze kweli hoa sio wakuongea nao polepole
@privamushi2512
@privamushi2512 2 года назад
Hengara sana mkuu wa mkoa piga kazi
@saadmbaraqa5272
@saadmbaraqa5272 2 года назад
Tamaa zimezidi wanakula mpaka wanajisau na fani zao
@abdallabundala404
@abdallabundala404 2 года назад
Tanzania jmn Tanzania,,, Tanzania yngu jmn Tanzania 🇹🇿, 🇹🇿 nakupenda Tanzania 🇹🇿 kwa sifa zako nzur na rangi zko nzuri. Tanzania 🇹🇿yng nasimama na ww na nitakulinda na maaduwi.
@constanciashangali7523
@constanciashangali7523 2 года назад
Duuuh! ..hawa wakandarasi ...hivi Rais akiamua kuchukua wa nje ya nchi tuu.. mtalalamika kweli🤔
@akidajulius8397
@akidajulius8397 2 года назад
Sasa MH ,huyo utaemkunjakunja na kumtia katika pochi ukaondoka nae😂😂😂,Yani unafurahisha sna, kwa mkwara huo,hata shemeji mtarajiwa ajiandae utamkunja akikuzingua humo ndani kazi itakuwepo,
@muhakizungu1118
@muhakizungu1118 2 года назад
Piga kaz dada ila kuwa nao makini xna awo wakanda rasi
@stanslausbereghe3819
@stanslausbereghe3819 2 года назад
Hao wachunguzwe uraia wao. RC cyo wewe tu, Tanzania nzima
@kwilasacharles1747
@kwilasacharles1747 2 года назад
Kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake au kamba yake imekatika akaenda kula kwa wenzie🤣🤣🤣
@mangulimanguli3974
@mangulimanguli3974 2 года назад
Barabara ya km 1 inajengwa kwa miezi 6 hata haya hawana Alafu mbovu Waafrika ivi tumelaaniwa, inanama Barabara ya km 10 mngejenga kwa miaka 6, Inna lilah wa inna ilahii rajiun
@MariamKileo-mu8rv
@MariamKileo-mu8rv 2 месяца назад
Ila huyu mkuu wa mkoa wa iringa ,,singida na Arusha nawapenda sana yaani mnafatilia had raha ila kuna huyo wa kwetu acheni ninyamaze maana duh ni masikitiko
@josephlorri431
@josephlorri431 2 года назад
Huyo ndo kiongozi..huyu mama alipambana na Magu 2020 kuwania urais..nimeona uthubutu wake..akikoromea wanaume
@AbdillahSalimu
@AbdillahSalimu Месяц назад
Mama alishasema kila mtu ajipimie urefu wa kamba yake
@telaamtauta2227
@telaamtauta2227 2 года назад
Mkuu hao niweziiiii kabisaa sukuma ndanii hao wasikuharibie kazini mapesawamegawana tu hao wakomeshe
@margarethpolepole7438
@margarethpolepole7438 2 года назад
Mwizi huyo mkandarasi wachunguzwe sana huku madereva wa tarula wana magari ya kutembelea na vitambi juu wizi tarula ni mwingi sana na barabara zao ni mbovu
@DM_15
@DM_15 2 года назад
Wamama tafadhali chonde chonde msikurupuke nahizokaulizakuwatia watukwenye pochi hebu ongoing kwakauli zakiuongozi siohizo ikumbukwe mkandarasi hufanyakazi kulingana nahelayako ulionayo
@dinnambogoye9582
@dinnambogoye9582 10 месяцев назад
Kweli
@kefajoseph158
@kefajoseph158 2 года назад
Subilini magu afufuke zitajengwa vizuri
@ezesaxo8764
@ezesaxo8764 2 года назад
Wapigaji wamerudi kwa Kasi kubwa sana
@زيتونتنزانيا
@زيتونتنزانيا 2 года назад
😜😂🤣🤣🤣🤣😅😅😅Mkunja mama kwani bei gani🤣
@vuzotv22
@vuzotv22 2 года назад
Hakuna barabara hapo
@fidelslick2086
@fidelslick2086 2 года назад
Ujio wa Wakuitwa Mama Samia mijizi yamerudi kila kona..Shame
@surusuru1994
@surusuru1994 2 года назад
💪💪🤣🤣🤣Kuja na kuletea poch
@shinipapaya846
@shinipapaya846 2 года назад
Kuna bonge la ngoma nimerekodi linaitwa kuleni kutokana na ulefu wa kamba zenu lakini cha kushangaza wengi wao wamenijia juu eti wanajuta kukubali kutiwa zile kamba fupi tena za Mkonge yarabi tobaaaaa eti wanataka za Minyororo iwe mirefu Dar2Moro 🏃🏃🏃‍♀️🏃‍♀️
@Budyp-c7r
@Budyp-c7r 2 года назад
Haaa haaa haaa haaa queen walikua awakujui boss wangu wa Mika 10 iliyo pita nakumbuka mbali sana kama nakuona
@jennytugara9470
@jennytugara9470 2 года назад
Alafu anatetea upuuzi yaani Mungu tusaidie TZ itajengwa na sisi wenyewe kwa upuuzi huu Mkuu wa Mkoa nakukubali
@zefamange7281
@zefamange7281 2 года назад
NIBORA HH UYU ANGEKUA NDIO RAISI
@mohamedsheikh6618
@mohamedsheikh6618 2 года назад
Mhh ni hali isiokuwa na ladha, tukubali tu haya ndo kiwango chetu cha maisha mimi na wewe tupambanie. Mkate wetu wenye utawala wakusanye kodi wafurahie maisha lakini mabadiliko au maendeleo mhh ni ndoto kwa uhalisia wake, labda tu tukubali haki za msingi kupewa tuseme ndo maendeleo
@hassanathumani1554
@hassanathumani1554 2 года назад
Mmmh iyo mbona km comedy anafurahia camera inamuangaza hovyo tupu.
@malecellacaezaryj2414
@malecellacaezaryj2414 2 года назад
Meneja hatakiwi kudhalilishwa hivyo, ana taaluma yake kitaalam..Daaa nchi hii
@magaritanzania6540
@magaritanzania6540 2 года назад
🔥🔥🔥
@pirminmatumizi5464
@pirminmatumizi5464 2 года назад
Wanachofanya ni kuiba kupitia Manunuzi. Mfano, kazi inahitaji mifuko ya saruji 1000; wananunua 200; Au, kazi ni ya mifuko 200 wanaandika ni ya mifuko 200! Hicho cha ziada kina ingia mifukoni mwao. Ni Mfumo wenye mtandao wa kiuhalifu kuanzia ngazi ya Wizara. Kwa jumla, Nchi ilipofika, panatisha!
@knight6757
@knight6757 2 года назад
Kasomea wapi huyo mkandarasi ?
@barakanestory3521
@barakanestory3521 2 года назад
Kupande Nini fukuza huyo.Mama safi fanya kama magu
@barakanestory3521
@barakanestory3521 2 года назад
Yani mnawapandishia watu nauli huku Hela zinapotea hivi mnashida gani,Magu tunakukumbuka sana
@saididodi3988
@saididodi3988 2 года назад
Wabongo wengi hawawi makini kwenye kaz wanajiamini mno ndo tatizo
@djmeza411a58
@djmeza411a58 2 года назад
Mimi hata mjieleze kabisa unge waweka kwenye pochi ukaondoka nao uzembe Sana mnasubili ajari ndio mtasema nini blabla atutaki kusikia 🤕😡
@fidyboytz7199
@fidyboytz7199 2 года назад
Ka mama aka ban
@waywepet6871
@waywepet6871 2 года назад
Hii ilikuwa na engineer kweli?
@aloycesteven5998
@aloycesteven5998 2 года назад
Ungemtia kwenye pochi tu Mh
@fathimamct232
@fathimamct232 2 года назад
Hii ni sababu ya mvuwa sio kosa la mkandarasi muhimu warekebishe tu na SI kuwa wamefanya kusudi
@nasseralmaqbali6317
@nasseralmaqbali6317 2 года назад
Tanzania kazi ipo, kizazi Cha wizi na ufisadi mpaka kaburini 🙄🙄
@telaamtauta2227
@telaamtauta2227 2 года назад
Kabsaa
@halimamasai2234
@halimamasai2234 2 года назад
Na kweli 😭😭😭
@jumamkunga9809
@jumamkunga9809 2 года назад
Safi, mfano mzuri wa kiongozi katika Tanzania.....usiishie hapo hakikisha barabara inajengwa kama ilivyopaswa iwe na wezi wote wachukuliwe hatua....dhamira yako inaonekana kuwa njema....wewe kweli ni Malkia...kaza mwendo.
@salustiashayo3486
@salustiashayo3486 2 года назад
Asitudanganye aje dar angalie alojenga barabara ya njia ya ngombe mbagala
@selecohabeeb6658
@selecohabeeb6658 2 года назад
Mfano Mzuri wa kiongozi haliisiiii na mzuri!
@J4UPro
@J4UPro 2 года назад
Kwa sasa huyu mama watamuengua we subiri tu. Type za Aina hii zilikuwa enzi za Magufuli.
@biddii1972
@biddii1972 2 года назад
Jaman tunataman kupata mtu kama huyu uku kwetu bumbuli
@shinipapaya846
@shinipapaya846 2 года назад
Mtakoma huko kwenu ni jambazi sugu
@amanikudeli5297
@amanikudeli5297 2 года назад
r i p Jpm
@mudy533
@mudy533 2 года назад
MENEJA HIYO UMEJITAKIA MWENYEWE KUNA KITU KINAITWA SITE INSPECTION NYIE MNAKAA TU OFISINI HADI VIONGOZI WANAO NA INGEKUWA UNATMBELEA BRBR ZAKO UNGEKUTWA SITE UNAREKEBISHWA AU KUTOKUONWA KABISA
@aginessmgaza9899
@aginessmgaza9899 2 года назад
Duh
@barakanestory3521
@barakanestory3521 2 года назад
Kila Mahali wizi du?
@kingwatabata4230
@kingwatabata4230 2 года назад
JIPIMIENI JAMANI MBONA AMUELEWIIII😠
@ramadhanhemedi1554
@ramadhanhemedi1554 2 года назад
Mh tunaomba kakague na njia ya mtera dodoma
@tedlema8105
@tedlema8105 2 года назад
Yamekua hayo kukuona mtu na kumweka kwenye pochi!!!!
@bekaashbai1781
@bekaashbai1781 2 года назад
Naeitetea kila siku serekali ila iyo road mku ondoka na kichwa
@yesayamwambu4431
@yesayamwambu4431 2 года назад
Kauli ya Sendiga Queen RC Iringa ni sahihi kwa watu wapumbavu kama hao wezi huwezi kuongea nao kwalugha ya kijinga hawatakuelewa hongera Rc upo vizuri
@venancerichard920
@venancerichard920 2 года назад
Kaupiga mwingi
@mariasafari1004
@mariasafari1004 2 года назад
Wanawake komesha yenu 😂😂😂
@charlesbarongo2778
@charlesbarongo2778 2 года назад
Hiyo pochi ni kubwa kiasi gani kuweza kumfungia mtu!
@bahatisaimon6019
@bahatisaimon6019 2 года назад
Bora wewe uko uku Musoma mijini Bado sana Mkuu wa huku mda mwingi Yuko Tarime Nyamongo tu
@ezekieljacob5795
@ezekieljacob5795 2 года назад
Huko nyamongo anafanya nini ???? Nyumba ndogo au.
@tedlema8105
@tedlema8105 2 года назад
Imefika mahali ambapo hata utu wa mtu hauheshimiwi tena jamani? Mama nenda polepole yana mwisho hayo madaraka
@lovecutetz9668
@lovecutetz9668 2 года назад
Saafii kemea fisadi
@ramadhanrajabu6772
@ramadhanrajabu6772 2 года назад
Sasa mku wa mkoa anajua zaidi ya mkandarasi katika kujenga kwli?? Kwann asimskkilize na mkandarasi anaeleza kitu gan huenda cha kitaalam
@mackrobert7290
@mackrobert7290 2 года назад
Wewee Kama dishi lako limeyumba, hata kwa macho huoni barabara ilivo haina kiwango hapo ataeleza kitalamu vipi wakati kitu kinaonekana, acha USHAMBA wa NJOMBE
@redref6342
@redref6342 2 года назад
Wakunje kabisa hao wawe kama chapati haiwezekani wanacheza na fedha za umma
@shaqdizo7678
@shaqdizo7678 2 года назад
hiyo Barabara imejaaa udongo tuu, mmepaka tuu rangi Lami gani hiyo? naona kifusi kingi Lami hipo 1 inch?? daahh hii Barabara ya million 600?? wezi wengi sana hapo mmejaza kifusi tuu hata mvua hazijapiga kushaharibika?
@fakihdarusi4385
@fakihdarusi4385 2 года назад
WATIE KWEMYE POCHI MAMA HAO
@enickosanga4921
@enickosanga4921 2 года назад
Chini ya kiwango huo ni wizi mkubwa wabongo sio wazalendo
@sakinaamani1486
@sakinaamani1486 2 года назад
Mwana mma anajiamini kjweli
@akibabruno8168
@akibabruno8168 2 года назад
Wewe wakunje kunje at a sabaya alikuwepo wala hutakuja umzidi makondo na mwanir
@muthegreat3667
@muthegreat3667 2 года назад
Sisi wenyewe huku kwetu kilungule barabara ina mwaka watatu huu haijakamilika na kunavumbi balaa ata maji hawamwaji .
@ramadhanimtetu7246
@ramadhanimtetu7246 2 года назад
LOOO Mkaazi Mwenzangu Wa Kilungule Mimi Naishi hapa kwa Madeni Mkuu nilizungumza Na Mh Mbunge Chaulembo Kuhusu kwa nini Umiminaji wa Lami Umekwama Alinijuza kuwa Mkandalasi amekosa Njia Mbadala ya Kupitisha Magari yaani ni Ujanja ujanja tuuu Unaoendelea palee tatizo Wasimamizi wetu Ni Watu Wenye Maslahi binafsi na Wakandalasi wa Kichina Yaani Hii barabara yetu ya Kilungule kwenda Buza Ni Upigaji tuuuuuu !!!
@philiplenardsylvester6063
@philiplenardsylvester6063 2 года назад
Nabado mje mkague lami za katoro na busere sere ni majanga
@kabwelasutiviraka4765
@kabwelasutiviraka4765 2 года назад
Hamna watu wezi , waongo na mafisadi kama Watanzania yaani wala hawaaminiki Watanzania ni watu wa ovyo ovyo
@deograciakashaigili5973
@deograciakashaigili5973 2 года назад
Umeona wewe! Majizi, Mafisadi, Majungu, undumilakuwili umewajaa baadhi yetu. Tuache hayo jamani.
@salustiashayo3486
@salustiashayo3486 2 года назад
Hahahaa wakunje wote mama
@scoutpwanimchangani6711
@scoutpwanimchangani6711 2 года назад
Lazima warekebishe kwa gharama zao
@Dantaata
@Dantaata 2 года назад
bora hata wewe ungekaa ikulu
Далее
When Royal Guards Fight Back!
8:08
Просмотров 6 млн
Mzee Anena MAZITO kwa RC HAPI kwa Kubomolewa NYUMBA
53:22