Faida Online TV Desemba 21 2022 tumefika katika Hoteli ya kifahari ya RUANGWA PRIDE HOTEL inayomilikiwa na mkulima wa zao la Korosho, Hoteli iliyojengwa katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na kuzungumza na Mmiliki wa Hoteli hiyo Ndugu Mparuka Hashim Mtopela ambae ndiye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo.
Bwana Mparuka amesema Hoteli hiyo ni yake na Familia yake, na hakuna kiongozi yeyote aliyeweka nguvu zake.
Hoteli hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Desemba 30 2022 na Mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
12 сен 2024