Тёмный

Salama Na PATOO SE6 EP24 | PLAYMAKER...PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 13 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Patoo aka Patrick Nyembera ni Kaka yangu, kabisa tena. Katika watu ambao wamekua wakiniona nakua na yeye pia namuona anakua basi ni sisi wawili ambao mpaka leo kwa Rehema za Mwenyezi Mungu bado tunaendelea kupambania kombe kwaajili yetu na familia zetu za watu walotuzunguka ambao kwa kwa namna moja au nyengine wanatutegemea kiasi flani na wanatuombea sana tuendelee kwenda pazuri ili nao ya kwao yawaendee. Na kwa kweli Mungu anaendelea kutubariki na bila ya shaka anaendelea kumbariki Kaka yangu huyu aendelee kufanya kazi nzuri na kung’ara.
Tukiwazungumzia ma playmaker ambao wameweza kuubariki mchezo wa mpira wa kikapu nchi hii na ukiacha kulisema jina la Patoo 6 basi wewe utakua una yako mengine au itakua hujawahi kumuona Patoo akiwa uwanjani enzi zake hizo. Na kama hukuwahi kumuona basi huna haki ya kumuelezea, pengine ukae chini watu wakukhadithie ni jinsi gani Kaka yangu aliweza ku dominate enzi zake. Mtu yoyote ambaye alishamuona Patoo akicheza basi hatoacha kumwagia sifa zake na wala hatoshangaa anapomuona Patoo anachambua michezo mbali mbali kwenye TV zaidi football kwasababu kwenye michezo yeye ndo alipokulia!
Mke wake pia alishawahi kuwa bingwa wa Table Tennis hapa nyumbani kwa miaka mingi sana. Na ukutanaji wao ulianzia uwanjani bila shaka, naamini walishakua wakienda kwenye michezo inayokutanisha shule za Sekondari hapa nyumbani na pengine kwenye matamasha ya michezo mbali mbali. Ukaribu wao ambao ulianza kwa urafiki ndo ambao unawafanya waendelee kuwa pamoja mpaka leo hii.
Patrick anakumbuka siku ya kwanza aliponiona mimi, hiyo ni story ndefu ya siku nyengine ila inachekesha kwa kweli, na sikutaka kumuuliza kwa kituo juu ya hilo maana najua ataniambia na mengine ambayo yanaweza kuwa na chumvi nyingi ndani yake kwahiyo sitaki 😃. Nakumbuka lakini jinsi alivyonipokea, alivyokua anafundisha na kunifanya nijiskie niko nyumbani. Ukichukulia nilikua ka binti tu kutoka Zanzibar ambako kalikuja Dar kutafuta maisha na ndoto za kutaka kuwa Pro Basketballer pia zilikuwepo, usicheke, nilikua serious mwenzio ahahaha.
Tulisafiri pamoja kama team, tulishinda pamoja na kufungwa pamoja na baada ya hapo tukaanza kufanya kazi pamoja kwenye kituo cha TV cha East Africa Television aka Channel 5. Patoo alikua anafanya kipindi cha michezo na mimi nilikua nafanya Radio na TV. Kwahiyo bado tulikua tunaendelea kuonana kila siku mpaka pale mimi nilipoamua kwenda zangu shule. By the time narudi nikaamua kuwa nafanya mambo yangu mwenyewe na yeye pia baada ya muda alihamia zake Azam TV.
Humu tunaizungumzia hiyo safari yake na mitihani ya hapa na pale, mustakabali wa michezo hapa nchini na jinsi ambavyo familia yake ilikua ikimsapoti kipindi hiko anacheza zaidi kuliko kufanya kazi. Humu pia tunaongelea maisha yake binafsi na pengine nafasi ya yeye kuweza kucheza Ulaya au Marekani kwa kipaji kikubwa alichokua nacho. Nini kilimfanya asiende? Na je, basketball ina upinzani kama iliokuwepo miaka ya nyuma? Nini kimebadilika? Je tuko pazuri? Yeye alifaidika na nini haswa? Na mafunzo gani aliyapata? Atataka mtoto wake afanye kama alivyofanya yeye au atamlinda na kumtaka pengine asijihushishe na mambo ya michezo?
Yangu matumaini utaipenda episode hii na kama pia utapata mawili matatu ya kujifunza basi hiyo itatupa sisi faraja zaidi.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

3 июл 2022

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 10   
@jamaalsaleem2926
@jamaalsaleem2926 2 года назад
wakwanzaaaaa leoooo
@rodrickmataba8999
@rodrickmataba8999 2 года назад
Hujambo is back...
@paulmtae1738
@paulmtae1738 2 года назад
Salama samahani Salama na zuchu haipo kwa playlists yako naomba kama waweza dondosha link tuicheki please.
@nassoroally123
@nassoroally123 2 года назад
We Babu Seya salama ustaadh dah kitambo haswa
@zanzibaryetusportonlinetv7499
@zanzibaryetusportonlinetv7499 2 года назад
Sijawah kufikiria kabisa kwamba dada ulikua basketball player 🤣🤣🤣🤣 Really fun
@nassoroally123
@nassoroally123 2 года назад
Dah za siku haswa tangu infocom technologies
@osmanmtambo6804
@osmanmtambo6804 2 года назад
mbona Jesca apitipitiii yupo Mashallaa
@catenzeki678
@catenzeki678 2 года назад
hahahahaha...ata mm nmemiss
@mussakhamis2377
@mussakhamis2377 2 года назад
Bigup salama uko uzur good interview
@abrahamkirondomara
@abrahamkirondomara Год назад
Patrick Nyembela kwema kaka long time no see you broh!!
Далее
Украшаю чехлы 🎀
00:51
Просмотров 79 тыс.
Salama Na Masoud Kipanya
52:05
Просмотров 8 тыс.
Salama Na Goodluck Ep 31 | WASTAHILI SIFA Part 2
24:51
Приятного аппетита 🤣
0:15
Просмотров 6 млн