Тёмный

Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 149 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV.
Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo.
Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa.
Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu.
Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII.
Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

28 май 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 234   
@ganjatunikilemile719
@ganjatunikilemile719 7 месяцев назад
Naitizama hii interview mara ya 10 na bado na mpango wa kuitizama tena na tena
@mchangeboy5928
@mchangeboy5928 Год назад
NAELEWA KWA NINI ANAANGALIA JUU WAKATI ANAPOMZUNGUMZIA MAMA AKE. NI NJIA PEKEE YA KUZUIA CHOZI LOVE YOU MAMA...🌺💕
@moneythemes
@moneythemes Год назад
Sure sure man, mwanaume akifanya hivyo huwa ndani yake anazuia sana hisia.
@abisaimuhanji3687
@abisaimuhanji3687 Год назад
salamaa anahoji vyema sana
@mchangeboy5928
@mchangeboy5928 Год назад
Yaah maana uchungu na hisia kali ndan yake
@cdeleo9336
@cdeleo9336 Год назад
Mr blue anajielewa sana na yupo very humble. Kwake tabata ni karibu na nyumbani kwa wazazi wangu
@dicksonlukiko820
@dicksonlukiko820 Год назад
Salama ikiwezekana tuletee Kalapina ikiwezekana
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Год назад
anajitahidi sana kutolia wakati anamuongelea mama ake""Mungu amrehemu
@vickydan2869
@vickydan2869 Год назад
Amen maskin analia kiume
@rahelrodin5486
@rahelrodin5486 Год назад
Mr blue nimtoto wa rafiki Yangu tulimlea mimi na mama yake Halima na mimi naitwa Rahel naishi Sweden kwa sasa
@mussahancy6591
@mussahancy6591 4 месяца назад
Hongera kwa malezi mama
@godymasuvata3990
@godymasuvata3990 4 месяца назад
hongre
@user-fz1ph3cn4s
@user-fz1ph3cn4s 4 месяца назад
Hongerah sana wewe na familia yako kwa utu wenu.
@dostovan5142
@dostovan5142 Год назад
I appreciate Mr Blue not coz of his music but coz he is very honest to himself
@esterdoriye8377
@esterdoriye8377 Год назад
Hapo kwa mama from jela mpaka kuishi mtaani akakupa 500 nahisi kulia kabsa
@pillyjuma3095
@pillyjuma3095 Год назад
The way he say... "Yeah Dada yangu".. one of my favorite artist 🥰
@hidayabakari4
@hidayabakari4 11 месяцев назад
Asante
@CoachHafidh
@CoachHafidh Год назад
Noo wayyy....🔥🔥🔥🔥🙌🏾 Daah, Naomba niseme ukweli tu leo...Ni hivi leo tu nimemuwaza sana Mr. Blu kwann hapati Mualiko hapa na #Salama?? Daah kama Milunzi yaani Swali langu limepata majibu leoleo❤️🙏🏾 Big up #JahStoneTown💛💛
@javanwatson6675
@javanwatson6675 Год назад
12:00 to 12:12 kumenitoa machozi. Ahsante Mungu kwa kuturudisha kwenye mstari kila mara tunapotoka 🙏
@sophiakassim6784
@sophiakassim6784 Год назад
Naomba ni like kabla hata sijaisikiliza maana I'm sure 100% it's gonna be a marvelous interview ever
@bellarmeeuma1653
@bellarmeeuma1653 Год назад
Next Salama na Majani(P.Funk)
@SallyMinja
@SallyMinja Год назад
Mr Blue anajali sana familia yake,huku kwetu Kinyerezi Mbuyuni kuna duka la viatu basi anakujaga na watoto wake kuwanunulia viatu,ukimkuta sasa anasalimia kila mtu mwenyewe siku hizi kweli hana dharau,havimbi tena😂 peace mwenyewe na fans wake tunaompenda,hapo wife wake yuko kwenye gari, anasubiri wamalize, love his humble self.
@andrewmmbaga1665
@andrewmmbaga1665 Год назад
🤣
@pelagyaldehyde323
@pelagyaldehyde323 Год назад
Sally the greatest soul
@BarakaAllen
@BarakaAllen Месяц назад
Wee sema kweli
@Heismasai
@Heismasai Год назад
Napenda heshima anayo onesha Kwa Salama!! Mwanaume anapoita dadangu na ujazaliwa nae inamaana anakueshimu sana
@ibrahmpinga380
@ibrahmpinga380 Год назад
SURE
@johariabdalla3319
@johariabdalla3319 Год назад
Bonge la interview,Byser katulia kwenye maongezi,moja ya interview kali na yenye ubora wa hali ya juu
@AsSd-fi1bg
@AsSd-fi1bg Год назад
Hapa kwenye marafiki broo nimekuelewa yan wanapotosha kama mm sinywi sina sikendo za ajab uli wapo marafiki wanipambania niingie huko nawakimbia balaaaa Yan daah na lock nafuta no mtu anakwambia kuolewa nn diri kujiuza marabila pombe ww sio mjanja mm ni mwendo wakuwakimbia tu nikiwa a mama alinipambania sana had kuwa hapa nilipo na mungu kaniona Asante Mungu 💯💕🙏leo nije nimfanye mzaz wangu alie kisa mm hapana 😭💪
@cheka480
@cheka480 Год назад
Naliaa😢kuna neno ameongea ndicho nnachopitia na watoto wangu namuomba Allah subhanah wataala aje kuwa wenye huruma na upendo kwangu waje kunilea. Am happy mr blue kasema kweli we must be humble. Alhamdulilah
@innocentmushi1550
@innocentmushi1550 Год назад
🙏
@yusuphswai6851
@yusuphswai6851 Год назад
Pole Mungu atakufanyia wepesi
@Jumamabela
@Jumamabela 6 месяцев назад
Pole.mungu.atakufanyia.wepesi
@khadijakimana8809
@khadijakimana8809 5 месяцев назад
Allah akufanyie wepesi🤲
@msafirikilongo7429
@msafirikilongo7429 Год назад
Kwenye interview yoyote Ile ambayo salama hutocheka itakuwa mbaya👍
@noeljacob9644
@noeljacob9644 Год назад
Salama fanya mpango utuletee ITD au CHID BENZ. tuwasikie
@mussahancy6591
@mussahancy6591 Год назад
Salama tafuta msudani mmoja pale muhimbili,hojiana nae tusikie,gonga like kama unaunga mkono
@salhatmfinanga9467
@salhatmfinanga9467 5 месяцев назад
Very humble May Allah bless him Even more and his family. One of the best interviews ❤
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 Год назад
Moja ya interview Bora sana! Mchanganyiko wa hisia za kweli, ukweli wa mambo na umakini katika kuuliza na kujibu maswali! It's one of the best!
@mohamedslh5478
@mohamedslh5478 Год назад
Blue nilikutana nae kwenye show pool bar kenya jamaa nilimuita jina lake halisi akashtuka sana ikabidi anite nyuma ya steji tutulie tutie story mtu safi sana
@ismaelmatano3571
@ismaelmatano3571 Год назад
Pool bar kitambo mwana sikuizi ipo lakni walibadilisha Jina na wanaleta live band wa Congo
@mohamedslh5478
@mohamedslh5478 Год назад
@ismaelmatano3571 yap bro wameibadilisha jina yakitambo izo ilikua ndio semu yetu ya kujirusha analipa mtu 1 tunaingia mtu 2 bure tunagandishana zile stump zao
@abiboseleman1649
@abiboseleman1649 Год назад
legends wangu kwenye ubishoo nakupenda.madem😅😅😅
@MohammedMohammed-uo5sk
@MohammedMohammed-uo5sk Год назад
MR BLUE HE IS AMAN
@MuniraShughuli-kc7vj
@MuniraShughuli-kc7vj Год назад
Mola awapee maskizano daima kkangu na mkeo in, sha Allah 🤲
@G.S985
@G.S985 Год назад
Interview nzuri na tamu kuisikia,Mr blue tumecheza nyimbo zako mpaka basi,nimefurahi Salama kutuletea uyu kaka
@dostovan5142
@dostovan5142 Год назад
Apewe maua yake na miti, na bidha zingine za kilimo
@crershawmafia1009
@crershawmafia1009 Год назад
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
@asantehyera6746
@asantehyera6746 Год назад
I wish to see Salama na JB (Jacob Stephen) HII NI KIU YANGU KUTOKA YAHSTONE TOWN
@FranklinMtei
@FranklinMtei Год назад
Tunaisubiriiii
@nicolenabintu2509
@nicolenabintu2509 Год назад
Mr bleu ame kuwa responsable 🙏🏾😍
@hassanshame5385
@hassanshame5385 Год назад
Blue..❤
@rubberbandman1213
@rubberbandman1213 Год назад
Brue that day alikuwa balaa,hakuna msanii aliyekuwa anavimba kama yeye,akikaa anapinda mgongo😀😀 kwa mikogo
@chunanachu2529
@chunanachu2529 Год назад
Humble man mashallah
@boniface3710
@boniface3710 Год назад
Back in the days more love from Kenya.....big up bro
@mgallason...5686
@mgallason...5686 Год назад
Unajua sana kujishusha, umejaa heshima Keep T up
@MuhammedAy-tj4yh
@MuhammedAy-tj4yh Год назад
Tunamtaka chid Benz nahisi itakua best interview
@kekiplus1andonly
@kekiplus1andonly Год назад
Heri sana😂
@misanyamisanya7499
@misanyamisanya7499 Год назад
Lmbaoo Blue interview yako inanifurahisha sana unapozungumzia BHANGI.. 😀😀😀 Kwa mwaka huu salama na Blue naipitisha. Alafu dada salama tuletee MPOKI ikikupendazaaa
@wahidatwalib4822
@wahidatwalib4822 Год назад
😅😅😅😅😅nilikua na watu wanguuuuu hahahhaa wa kuwavimbia 🎉🎉🎉🎉😂 🇰🇪🇰🇪🇰🇪
@Curioustraveller254
@Curioustraveller254 Год назад
Asante Salama kwa kumleta Byser
@saidsirya6716
@saidsirya6716 Год назад
Oyoo Byser kajikaza kidogo alie... 😢Mzee imenigusa
@fongaamike2768
@fongaamike2768 Год назад
Kweli asee.. aja tokwa machozi ila una weza kuona moyoni ana lia
@saidsirya6716
@saidsirya6716 Год назад
@@fongaamike2768 huyu kweli amepitia mengi
@JanethiRohoma
@JanethiRohoma Год назад
Nimemkubali blue kuongea ukweli kuhusu bangi,mana alikua ananikodi kama tax drive kutoka tbt mpaka ilala kuvuta bangi tu.miaka ya 2005 - kuendelea.
@richardkalanga7216
@richardkalanga7216 Год назад
Story ya mama ake imenigusa mno hata kaka Blue almost atoe chozi akati anamuelezea mama ake may her great soul rest in Paradise.
@AsSd-fi1bg
@AsSd-fi1bg Год назад
Unaakiri sana broo nakupenda sana broo nimejifunzakitu hapo💕🙏nimecheka ety mibangi🤭😂😂😂😂
@floranusgwau7122
@floranusgwau7122 Год назад
Jamaa jinsi anavyoongea utafikiri ana PhD 🙌, Babylon byser
@DavidMbwilo-qk1bz
@DavidMbwilo-qk1bz Год назад
Kuongea na PhD wap na wap😂😂😂 jaman
@azamazam3279
@azamazam3279 Год назад
Yani anavutia sana
@user-wq5fx4iu4c
@user-wq5fx4iu4c Год назад
Lovely soul millionaire ❤❤❤
@Modoo_255
@Modoo_255 Год назад
msikilize mr blue then nenda kasikilize ngoma yake ya tabasam ndo utamuelewa vzur
@maigajohn5828
@maigajohn5828 Год назад
Hongera sana blue katika Maisha dharau ni kujisikia ni mbaya sana katika Maisha hongera sana kurudi kwenye mstari Maisha Dunia ndo Elimu ya pili ukitoa Elimu ya darasani
@safiahassan6121
@safiahassan6121 Год назад
Sauti kama ya mzee yusufu
@mr.yahzadochuno7914
@mr.yahzadochuno7914 Год назад
I’m love love blue
@user-lr4im4vt7y
@user-lr4im4vt7y Год назад
Mlete Millard Ayo
@pepynomfugale9311
@pepynomfugale9311 Год назад
Mwamba huyu
@ClipsRUs204
@ClipsRUs204 Год назад
Mwamba kakazia "Mabangi"........
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Legendary Bayser, nakukubali sana ❤
@estermselle188
@estermselle188 Год назад
Umengaa😂😢🎉❤
@benjaminsemwenda3152
@benjaminsemwenda3152 Год назад
Star Wangu Wa Muda Wote Babylon Byser Mr Blue, Namkubali Sana Mchizi Ana Kipaji Na Hajui Kulinga Na Hana Dharau Kweli Maisha Ya Kula Ugali Na Kachumbari Yalijitahidi Kumbadilisha, Much Respect Kwake Mzee Wa Kazi
@nelsonmwaipaja3727
@nelsonmwaipaja3727 Год назад
Najifunza vitu vingi kutoka kwa brother Bizzy 💓💓💓💓
@obafemibuhari3098
@obafemibuhari3098 Год назад
Bizzy kwenye game🔥🔥
@tariqabdulkarim5892
@tariqabdulkarim5892 Год назад
salama vp tozzy
@pastoraile7195
@pastoraile7195 Год назад
Bru bonge lajembee
@mussahancy6591
@mussahancy6591 3 месяца назад
Leo nimeangalia tena mara ya 37
@drkiti
@drkiti Год назад
Thanks Salama for bringing Mr Blue, such an inspiration🫡
@HumoudSalim-ct1tz
@HumoudSalim-ct1tz 5 месяцев назад
Salama haujambo unamkumb uka bikati na sabriwake mimi humoud nduguyake sefu mmanga na shoga yako farida mimirafikiyake almlaruhum abdul njegere m/ almukepepon amen na bro musa jabir inrahim kuki abudu ndo nimekuwanao ujana wetuwote sisi ndowenye kiponda bila kumsahau dada yetu halima na boss khamisi wake
@affleckmusic3709
@affleckmusic3709 Год назад
thanks for bringing mr Blue..let next be majani p funky
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Год назад
Hapo itakua❤❤❤
@frankkajoba8372
@frankkajoba8372 Год назад
Hata mm ningependa kumuona Pfunk
@user-qo6wb4le9i
@user-qo6wb4le9i Год назад
P funk mwamba sa a
@davidibrahim9138
@davidibrahim9138 Год назад
Blue interview zake huwa zinafunzo sna alafu yupo real sna
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 Год назад
5:18 😂 6:28 mama 💕 6:34 📌 njaa 9:18 mama 💕💕 13:15 📌 18:24 📌📌📌
@marcodavid7448
@marcodavid7448 Год назад
Last week niliingia RU-vid Kuuliza salama na mr blue ila sikuona kitu nikajiuliza why? Nikakumbuka kuna scandal ya salama kutoka na byser way back a.k.a nyani zee 😂
@jacquesmulalirya1704
@jacquesmulalirya1704 Год назад
Mutu wangu ngoma hautuletei ,,hatukusikiii huku congo tena
@lionelgahungu3442
@lionelgahungu3442 Год назад
Next time mulete mukongwee, Chid Benz,Chumaa
@FranklinMtei
@FranklinMtei Год назад
Blue ni mdogo wangu sana. Nipo kwenye hii fani kabla hajazaliwa. Itoshe kusema he is the GOAT! Toka dakika ya kwanza nausikia wimbo wa BLUE nikajua a star was born! Hajawahi kuniangusha. Yeye na Jay Mo. Hawajawahi kufeli! H
@stevewanga957
@stevewanga957 Год назад
Nyani zee namkubali since day za Tabasamu ...much love from🇶🇦🇶🇦
@didamugya6039
@didamugya6039 Год назад
LIL Sam A' aka Mr Blue kawainspire wasanii wengi sana upande wa kuchana kwa pozi, kuimba kwa pozi, swaga, mavazi, n.k. he is a Legend
@sweetcorner-jx6qb
@sweetcorner-jx6qb Год назад
Nilivoona tu interview ya Byser NIKACLICK, nasubiri interview ya BELLE 9
@neemaedward852
@neemaedward852 2 месяца назад
Blue mtu mkweli sana sanaa
@macknonkibona2401
@macknonkibona2401 Год назад
Huyu mwamba yupo real sana + mh. FA
@maigajohn5828
@maigajohn5828 Год назад
Mr blue alianza muziki mdogo sana Hadi kawa mzee baba
@RBSMABATI
@RBSMABATI 9 месяцев назад
Cool
@rapamafia3365
@rapamafia3365 Год назад
Kibenzi cha watuu bless sana mr blue byser ❤
@yahcanonbenisrael650
@yahcanonbenisrael650 Год назад
TABASAM Mr Blue..mad love from Kenya 🇰🇪
@mchinjanyau9055
@mchinjanyau9055 Год назад
Nachopenda Mrblue Anasema Ukweli Na Mtu Peace Sana Hata Nilpo Kutana Nae Day Wani Na Producer Sulesh Sikutegemea Alivyo Nichangamkia Kama Mi Mtu MKUBWA Vile Tukaenjey Na AkachaMshangoo Kwatu Kama Najuana Nae Before Ana Roho SAFI SI Mtu Wamajivuno Blue MUNGU Amzidishie MAISHA Mareeeeeeeefu Na Furaha Teeeeeele
@kazkaz1943
@kazkaz1943 Год назад
Maua yako byser🎉
@saurijafary3581
@saurijafary3581 Год назад
😂😂😂 eti Daah leo nimeyakanyaga
@mahmoudaziz4717
@mahmoudaziz4717 Год назад
Namkubali sana blue babilon chilembaa😂.
@ernestpaulo7843
@ernestpaulo7843 Год назад
Sapenda sana intarview za salama ,una jua sana dada
@kilamiko8299
@kilamiko8299 Год назад
baisa uko sawa
@Elia-ty4pl
@Elia-ty4pl 3 месяца назад
Nimeipenda sana jamani mungu awajalie ❤❤❤❤
@mukirerichard5265
@mukirerichard5265 Год назад
I'm excited to see again Mr blue
@husseinmaganga6947
@husseinmaganga6947 Год назад
Life teach us a lot big up sana byser one of the best interview
@Paplick9
@Paplick9 Год назад
Legend 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
@yousramutwale2463
@yousramutwale2463 Год назад
Nice interview asante sana salama
@vincentmkanda9785
@vincentmkanda9785 Год назад
Big up saana Mzee wa Upala U a humbleman
@jamilaathumani5481
@jamilaathumani5481 Год назад
Apo alipomzungumzia mama yake ameniliza mana ameongea Kwa filings
@thomasbuheri5466
@thomasbuheri5466 Год назад
Wanawake wa Kiafrika wana uwezo wa pekee sana.
@HashimuHashboy-bo2wl
@HashimuHashboy-bo2wl 3 месяца назад
Mr blue utaliza watu sad story na umeonyesha umekuwa very fasta ,but umekuwa baba kaza
@hobbieh
@hobbieh Год назад
Grew up in his era. Blu and TID, Ferroz and Prof Jay were the bongo flaza guys. They made my days here in Kenya.. good interview.Kindly find Ferroz and interview him.
@yoo_its_yaqub8722
@yoo_its_yaqub8722 Год назад
Fleva not flaza bro
@hobbieh
@hobbieh Год назад
@@yoo_its_yaqub8722 typo bro
@yoo_its_yaqub8722
@yoo_its_yaqub8722 Год назад
Ooooh sorry bro
@hidayabakari4
@hidayabakari4 11 месяцев назад
Blooo Kweli unaujua mziki hongela sana
@user-ui4jk6ej8z
@user-ui4jk6ej8z Год назад
Yani leo ume akikisha turikua tume mutamani saanaaa mr blue much love from Bdi
@thebeststudio8076
@thebeststudio8076 Год назад
Next Salama na Bishop Eliasaph Mattayo Suleiman
@OMYUUN
@OMYUUN Год назад
LEGEND🕳️
@davidwalalason7630
@davidwalalason7630 Год назад
So emotional 😢
@SPK450
@SPK450 Год назад
This gonna be the best interview this year.....
@shamsally6277
@shamsally6277 Год назад
I love you salama you present the best content
@abrashizorashid117
@abrashizorashid117 Год назад
Nice interview
@jaykabyser229
@jaykabyser229 Год назад
Byzy kwenye gamu
@tnftz1461
@tnftz1461 Год назад
beezy🙌
Далее
Lasagna Soup @Lionfield
00:35
Просмотров 10 млн
Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1
33:07
Просмотров 309 тыс.
Salama Na JOTI Ep 47 | SIMPLY SPECIAL PART 1
35:15
Просмотров 462 тыс.
Mkasi - SO5E09 With Mr Blue
29:33
Просмотров 147 тыс.
Salama Na VANNY BOY Ep 54 | NDAGHA PART 1
39:49
Просмотров 464 тыс.
Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1
41:27
Просмотров 468 тыс.
помолодела получается 🤣
0:12
Просмотров 1,5 млн
тгк: katylazarevaa
0:16
Просмотров 1,2 млн