Тёмный

Nilikutana Na Mzee Mengi Gym, Sikuwa Najua Yeye Ni Nani" | SALAMA NA MADAM RITA PART 2 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 64 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
SOMETHING SPECIAL
Ms Rita Sundi Paulsen Hans ni mtu muhimu kwangu na kwa mamia kama pengine si maelfu ya wenzangu hapa nyumbani Tanzania. Yeye ni Mama kwanza, Dada kwa wengine, Aunt poa sana kwa kina Malik na Jamal, Bosi ya Mboka kwa Salama na wenzie lakini kubwa kabisa ni MJASIRIAMALI, jambo ambalo amekua akilisimamia lile analo liamini kwa miaka zaidi ya 30 sasa. Rita au Madam Rita alianza kufanya kazi toka alipokua na miaka yake ya mwanzo kabisa ya 20.
Mtoto kutoka kwenye familia ya kitajiri maana Marehemu Mzee Paulsen hakua mnyonge. Baba Mjerumani na Mama Mwenye asili ya kisukuma, kirudi na mchanganyiko wa makabila mengine kadhaa ambayo atatuambia humu ndani. Amekulia kwenye mitihani mingi mara baada ya Baba yake kufariki wakati yeye ana miaka 12 tu. Kutoka kwenye mazoea ya maisha ya kishua mpaka kupata mimba akiwa na umri mdogo na hilo kumlazimisha yeye kuondoka nyumbani akiwa na umri mdogo ndo mi naamini lililomfanya awe CHUMA mpaka leo. Naamini vile wanavyosema kila mtu na njia zake. Kila kitu kinachotokea kwenye maisha yetu kina sababu yake. Yeye kufariki kwa Baba yake ndo kulipelekea kupita KOTE alipopita. Shida na mitihani wakati mwengine huja kwa baraka tele, BARAKA ambazo mpaka leo hii ambayo mimi naandika waraka huu kwa majivuno mengi juu yake. Kweli kila kitu hutokea kwa sababu ili kitu kengine kizuri zaidi kiweze kukufuata ulipo.
Mimi na yeye tulifahamiana kwaajili ya kazi, nadhani wengi wanaijua hiyo khadhithi, ila kama hufahamu mimi na yeye makutano yetu ya kwanza yalikua ya kunipa kazi ya ku host Kili Music Awards ila hiyo kazi ilikuja baada ya pinduapindua nyingi alizo zifanya pale EATV baada ya siku moja mimi kuisema vibaya moja ya video ambazo kampuni yake ya Benchmark ilizitengeneza. Ilikua mtihani haswa baada ya kuskia naitwa tena ofisini kwake? Haya jengine lipi tena? Kumbe round hii ilikua kwa Neema sana, ila Bahati mbaya hiyo kazi wala sikuipata maana na watu wa Kili nao walinikataa kwasababu huko nyuma pia niliwasemea tuzo zao ambazo ki ukweli zilikua za kiwango CHA CHINI MNO considering hela ambazo wanazo wao kama KAMPUNI, kwa kweli lile halikua linapaswa kunyamaziwa.
Basi, peleka mbele mwaka mmoja au miwili baada ya hiyo incident akaniita tena kwaajili ya kazi ya Bongo Star Search sasa, na hii nyengine skia, nilipoitwa sikujua kama yeye ananitaka mimi kama Judge, mawazo yangu yalidhani anataka MTANGAZAJI wa shindano hilo, kumbe yeye alikua na BETTER idea, kama wazungu wanavyosema, the rest is history.
Rita ameniona mimi nakua mbele ya macho yake, nami pia nimeona transformation ya maisha yake kama Mama na Dada. Mengi amepitia ya hadharani na kwas siri, ninayo yajua na nisiyo yajua, ila ambalo nina uhakika nalo ni JINSI AMBAVYO MIMI NAJIVUNIA YEYE, kwa mishale yote ALOIKWEPA na kuendelea KUSIMAMA IMARA, Rita Paulsen Hans ni SHUJAA NA NUSU.
Mengi ameyaongea humu, ambayo ningependa uyaskie MWENYEWE bila ya mimi kudokoa lolote, hakuna chumvi wala sukari ilozidishwa humu ili ‘picha ipendeze’, badala yake ni simulizi nyundo ambazo kama kawaida zitakufanya ujifunze mambo mengi na pia kuangalia baadhi ya vitu kwa jicho jengine.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

20 мар 2022

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 158   
@zedekiasamara1783
@zedekiasamara1783 2 года назад
Maan, Salama is just too good. The ability to switch the questions based on a shift of emotions is top notch. Salama is the best interviewer in Tz, and it's not even close.
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 года назад
MADAM 💕😘 Ila interview imekuwa fupi jamani, Salama tunamtaka tena Madam, hatujatosheka 😍
@jessicamagoke6800
@jessicamagoke6800 2 года назад
NAWAPENDA SANA NYIE WANAWAKE MUNGU AWABARIKI SANA 🙏🙏🙏💞💞💞
@issrahayattv1356
@issrahayattv1356 2 года назад
Hi 👋 spread love this side
@abelmirwatu544
@abelmirwatu544 2 года назад
Nimempenda sanaa Madam Ritha...ni mkweli na anaroho ya kizungu sanaa.
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 года назад
Such an inspiration... I love you so much madam Rita.
@sylviaoum2943
@sylviaoum2943 2 года назад
That switch😍😍😍🙌🙌🙌.... Love u madam Rita &Salama.
@masturaabdul1007
@masturaabdul1007 2 года назад
Watu wazuri usoni ila nimejifunza wanamaumivu Makali Sana moyoni.
@susancharles1660
@susancharles1660 Год назад
Sana sikutegemea amepitia yote haya.
@juliananasari2526
@juliananasari2526 4 месяца назад
Yah
@ashminaabdulla8946
@ashminaabdulla8946 3 месяца назад
Ndiyo Dunia
@nigananurunjema
@nigananurunjema 3 месяца назад
Maumivu ya watu hayakó machoni.
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
SAAAANAAAA
@elizabethmollely3940
@elizabethmollely3940 2 года назад
Highest achievement ni watoto and I love that she is strong lol
@hamidafundi-pw1gw
@hamidafundi-pw1gw 3 месяца назад
Kazi nzuri sana Salama Na....Ni bonge la interview. Pamoja na ufundi wa namna ya maswali. Inavutia kusikiliza. Pongezi kwenu nyote.
@sistersade9039
@sistersade9039 2 года назад
I cried all along with madam Rita. Very sad childhood, but as u say madam, it eventually made who u r today. Mola kweli kajua vipi kukufuta machozi. As for u Salama u r simply an amazing interviewer.
@happymahega2000
@happymahega2000 9 месяцев назад
Madame Rita she is a very grateful woman,this interview is so emotional
@kelvinbanoth3013
@kelvinbanoth3013 2 года назад
What an interview, am so much moved by it!
@SharifaMohammed-el3ug
@SharifaMohammed-el3ug 2 месяца назад
Basi kwa kwa umelia. It is good to burn your eyes. Lakini ni kwambie kitu, umewaponya wengi Leo. Mungu awabariki
@happyhousekeeper
@happyhousekeeper Год назад
😥😥 I can feel madam's pain 😞😞, it's well madam. RIP Mengi uwiii
@LilacAlm
@LilacAlm 2 года назад
Salama you're a super talented interviewer,you know exactly when to step and to release the gas peddle😁 and That Madame Rita is a natural born figher. May God bless you all for wonderful work that you do. Keep up the good work👊🎤
@sylviaoum2943
@sylviaoum2943 2 года назад
😍😍😍👏👏
@susannesusie3217
@susannesusie3217 2 года назад
Salama najua unajua your the best but nakukumbusha your the best of the best 👍
@gwajeemmanuel4137
@gwajeemmanuel4137 Год назад
Nimeangalia vipindi vingi sana vya "salama na" am very excited with Madam Rita Story i even wish to see her someday and share more on her story she is extraordinary super woman fikisha salam zangu kwake
@nicolenabintu2509
@nicolenabintu2509 2 года назад
Habo kwa Walter chilambo njo nime penda, ila uyu dada ninavio mzimia Mungu mwenyewe ana juwa, Madame you're such a inspiration to me ♥️👏🏾
@Mariahhymatia
@Mariahhymatia 3 месяца назад
A very touching story mirroring almost exactly what I went through, except I am of a different gender! Bless her for revealing her life struggles.
@roseamos9930
@roseamos9930 2 года назад
Kweli kujikwaaa sio kuanguka I never had this before .penda huyo Dada sana
@user-vm5yf8cs2r
@user-vm5yf8cs2r 3 месяца назад
So good Madam Rita Wewe. MZURI Sana Tumejifunza mengi
@nigananurunjema
@nigananurunjema 3 месяца назад
Real Walter Chilambo is a talented person. That's how Ngoni people we are.
@saimonmwambilike2191
@saimonmwambilike2191 2 года назад
Am so greatful and bigg fan of SALAMA NA.... not only for being entertained but I learn alot about life. I never thought if behind madame Rita there were a lady who struggle in an exceptional way... you cure my pain by desolving my past and starting fresh as the new King.
@winnieevarest3634
@winnieevarest3634 2 года назад
SO LOVELY INSPIRING esp single mothers
@missm729
@missm729 Месяц назад
I love people who appreciate their life journey and understand what it means to lack. I hope Mengi's kids will learn from this much love Madam Rita.
@abuuswahili
@abuuswahili 2 года назад
Salama you made it wonderful again.Her life is so inspiring.But I like also the signature at the end😍
@yusuphmligiliche8353
@yusuphmligiliche8353 2 месяца назад
Heshima sana da Rita kwasababu mimi nilifanya Kazi nyingi na kampuni yako ya Benchmark. Ubarikiwe sis❤
@danielmsuya720
@danielmsuya720 Год назад
Pole sana madam Ritha, Sijui sana kuhusu wewe lakini na furahi sana kwa Maisha yako ambayo Yanamafundisho makubwa na Muhimu sana. Wewe ni Mwanamke Mvumilivu na Mnyenyekevu na usiyeweka vitu rohoni kwa chuki. Umewasaidia wengi na utaendelea kuwasaidia wengi maana huu ni wito kwako na wewe ni Baraka.
@edwinmbugua7738
@edwinmbugua7738 2 года назад
Tunaomba Salama na Mr Nice
@benny5424
@benny5424 2 года назад
What an interview salama it is so strong
@nadiashabani575
@nadiashabani575 2 месяца назад
Nakuelewa sana madam Ritha coz nimepitia hao naelewa sana
@evelinekivuyo9713
@evelinekivuyo9713 Год назад
This is the best interview I’ve ever had.Salama tunaomba tena salama we have a lot to learn from her 😊
@mosessarya2174
@mosessarya2174 2 года назад
you are a really inspirational figure
@medicalphysicsbiomedicalen1707
@medicalphysicsbiomedicalen1707 2 года назад
I love madam Rita. Nice interview
@magesalugwesa4449
@magesalugwesa4449 2 года назад
Aise salama I love what you do keep it up
@viviannjoki9989
@viviannjoki9989 2 года назад
So lovely
@josephmihayo6236
@josephmihayo6236 3 месяца назад
This was a nice interview so far. Seems Ritha was so so beautiful at her younger ages. No man could dare to walk out of her!
@BlandinaKahuru-ur5el
@BlandinaKahuru-ur5el 3 месяца назад
You have a golden heart madam Lita. God bless you❤
@joramelishamghwira2425
@joramelishamghwira2425 2 года назад
Good interview Salama, your among top interviewer
@googleus4903
@googleus4903 2 года назад
I like your outfit SALAMA It's very DOPE
@jescarobertkiswaga1580
@jescarobertkiswaga1580 Месяц назад
Nampenda sana Madam Ritta nikimuona
@mosesallanadam1955
@mosesallanadam1955 3 месяца назад
Madam Ritha you are impeccable, and thanks for sharing.
@asimwemukoyogo7325
@asimwemukoyogo7325 Год назад
What an interview.. Salama ujua sanaaa
@ellybrown5989
@ellybrown5989 3 месяца назад
Asante sana Salama, Asante Rita, Mbarikiwe sana.
@rehemarwanda6039
@rehemarwanda6039 2 года назад
Good switch Salama...I love U🥰
@NeemaSwai-sl3fh
@NeemaSwai-sl3fh 3 месяца назад
Madam Rita nina mwengi ya kukueleza. Watu wengi wananifananisha nawe na wengine wananiambia mie ni ndugu yako ila siku nikukutana nawe nitakuambia mengi.ingiwa kuna siku moja nilikuona peacock hotel na siku nyingine nilikuona southern hotel ila haikuwa raisi kuongea nawe. Ila kuna jouney unayopitia same to me
@NataliaKenny-vb6os
@NataliaKenny-vb6os 2 месяца назад
Naomba majina ako nikuangalie🎉
@bahatiapollo4892
@bahatiapollo4892 2 месяца назад
Em nikuone
@hatujuanisalum9354
@hatujuanisalum9354 3 месяца назад
Hajui kumdharau mtu .kwenye bongo star alikua hampond mtu kila mshiriki alikua anamsifia kua amefanya vizuri hata kama anajua hajashinda.mama wa ajabu sana mtu mzuri sana huyu jamani.na very very beautful woman
@aminanamoyo83
@aminanamoyo83 2 года назад
interview was 👍👌🥰👏 🙌🇨🇭🇹🇿
@glowingspirit606
@glowingspirit606 2 года назад
It was just so emotional, you might wish to pass through what Madam passed through maybe utaweza fika where she is, then slap yoself and say LEARN baby, that's for you to learn.
@kilinakoshengelo2944
@kilinakoshengelo2944 2 года назад
How come she says she has seen everything good when she has never seen my smile!?
@jocelyneinarukundo3655
@jocelyneinarukundo3655 2 года назад
🤭🤣🤣🤣
@rahmashomari1048
@rahmashomari1048 3 месяца назад
We nawe😂
@kilinakoshengelo2944
@kilinakoshengelo2944 3 месяца назад
@@rahmashomari1048 Naam
@idrissansereko6403
@idrissansereko6403 3 месяца назад
Basi hayo mahojiano mgeyafanya kwa kiingereza maana yake kiingereza kingi sana vipi we Salama mwambie Rita hatupo UK topo TZ 😊😊
@josephmihayo6236
@josephmihayo6236 3 месяца назад
Ndio hasara ya kutokusoma. Jiunge na Ras Simba umuelewe Madam Ritta.
@seifseifmohamed7118
@seifseifmohamed7118 3 месяца назад
Ilitaka tujifunze mengi kutoka kwake yeye Madam Ritta. Sasa jielimishe akili yako ivuke kwenye dari ya unapopo lala ifike japo hewani
@montanaprime
@montanaprime 2 года назад
Aisee interview nzuri sana
@wanzakleruu8648
@wanzakleruu8648 2 года назад
Salama was so emotional compered to Madam. Great talk so far by the way🥂
@freduallughano2301
@freduallughano2301 3 месяца назад
That is yoyr altitute but others we saw Ritha was more emotional than Salama but this comes when you are neutral in your mindset.
@hatujuanisalum9354
@hatujuanisalum9354 3 месяца назад
Mtu mzuri sana huyu mama na mzuri sana pia wa sura ( very beautful madam
@user-it6po1le3v
@user-it6po1le3v 5 месяцев назад
Hongera sana madam Rita kwa story yako 😢
@davisminja3742
@davisminja3742 Год назад
Wachagga tunajua ku care alooo hapo kwa MZEE WETU MENGI umemtendea haki aseee hope amejigeuza alipo
@CatherineKaria-fk7fq
@CatherineKaria-fk7fq 4 месяца назад
😂😂😂ilaaa
@minaelnathanael1846
@minaelnathanael1846 5 месяцев назад
Pole sana Ritha. Mungu akusimamie
@annahkiza6362
@annahkiza6362 2 года назад
Nawashuru sana , Salama Na Mme Rita
@annahkiza6362
@annahkiza6362 2 года назад
Nawashukuru
@neemaalbert2731
@neemaalbert2731 2 года назад
I love madame ritha
@brendachibura6040
@brendachibura6040 2 года назад
More madam Rita. Pls
@zaipazzi9490
@zaipazzi9490 2 года назад
Salama umetoa macho madam anavyo lia ujue umetonesha kidonda.🥰 Nawapenda wote
@vandexan1330
@vandexan1330 2 года назад
So lovely, Interview imekuwa short sana
@hatujuanisalum9354
@hatujuanisalum9354 3 месяца назад
Nampenda sana jinsi alivyo kisha ana rohonzuri mno hata kwenye bongo star search
@annettelyimo5239
@annettelyimo5239 3 месяца назад
You are so beautiful that's why they took advantage of you... but you are blessed
@MINISTERBAHATIMPUME-px4pf
@MINISTERBAHATIMPUME-px4pf 3 месяца назад
Nakupenda sana Dada rita una moyo kama wa mtoto, nakupenda
@jayzeem14
@jayzeem14 3 месяца назад
God allowed it so that you would be strong from it and also you would teach others. Many of us were teen mothers by default and though we suffered but God gave us a resolve in life and God has blessed us with gifts that we use to mentor others! Beauty has cost us but we God has turned what they meant for ill to be a blessings! Be grateful!
@veronikabaraka3315
@veronikabaraka3315 Год назад
Tunaomba madam aludi tena
@driquesmariques9794
@driquesmariques9794 Год назад
Lady u got some history
@angelberthakatundu9475
@angelberthakatundu9475 2 года назад
Daaah!! Madam umekula Raha zote za dunia.. Hopefully na Mimi one day yes!!😂
@user-vm5yf8cs2r
@user-vm5yf8cs2r 3 месяца назад
Inazuma saanna Dada Rita pole imepita. Now look your future Iyo Ina tokeya Kwa wengi Ina nigusa piya
@mwanamfinanga8262
@mwanamfinanga8262 2 года назад
You too amazing salama...love the way you interview
@godfreybayyo8079
@godfreybayyo8079 2 года назад
Sis❤️ ..Great of all time ..the real GOAT
@ngoshachaula172
@ngoshachaula172 2 года назад
Interview ilikua kali akn madam kazidisha kizungu jamn mpaka atujelewa
@susancharles1660
@susancharles1660 Год назад
She still beautiful 😍
@abelmirwatu544
@abelmirwatu544 2 года назад
Salama mwambie Ritha aongee kiswahili.
@joiana4663
@joiana4663 4 месяца назад
huwa nakupenda sana Ritha mpambanaji wa kweli
@fakiimohamed6163
@fakiimohamed6163 2 года назад
Nice, tuletee... K.rin
@josephlorri431
@josephlorri431 3 месяца назад
K-lyn, the gold digger... alimtegeshea mzee mimba,ndo chanzo cha mateso yote ya Dr Mengi hadi kifo..
@neemaalbert2731
@neemaalbert2731 2 года назад
Rest on peace baba Mengi
@rabanfungo2408
@rabanfungo2408 2 года назад
🔥🔥
@annahkiza6362
@annahkiza6362 2 года назад
RIP Mr Mengi💔
@juliananasari2526
@juliananasari2526 4 месяца назад
Madam Ritha nakupenda sana
@user-kh8tr8xh4v
@user-kh8tr8xh4v 3 месяца назад
Malkia wa nguvu kwangu❤❤❤❤
@SharifaMohammed-el3ug
@SharifaMohammed-el3ug 2 месяца назад
Salama umempoya huyo Dada pia. Katoa siri nimewapenda
@susannesusie3217
@susannesusie3217 2 года назад
Rest in peace Mengi
@sarahsarahgilla8491
@sarahsarahgilla8491 2 года назад
Tunaomba madam Rita aongee kiswahili zaidi maana wengi hatuelewi
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 2 года назад
Wakati wenzako tunasoma wewe unacheza kibao kata .ukome😀
@happyhousekeeper
@happyhousekeeper Год назад
@@masalakulwa7601 hahaha wewe, kibao nini, 😄😄😄
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 Год назад
@@happyhousekeeper kibao kataaaa🤣
@happyhousekeeper
@happyhousekeeper Год назад
@@masalakulwa7601 hahaha 😂😂 haki Mungu
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
@@masalakulwa7601 🤣🤣
@user-cw6jq7cv2k
@user-cw6jq7cv2k 3 месяца назад
Rita now I know you, I think I love you
@miriamngosha6856
@miriamngosha6856 2 года назад
Dah feel sorry for u lov 😪
@arnesyaurio6346
@arnesyaurio6346 2 года назад
❤❤❤❤❤❤
@kadoaugust6497
@kadoaugust6497 3 месяца назад
Maisha ya mwanadamu anayajua Mungu mwenyewe
@annamakomele339
@annamakomele339 6 месяцев назад
Yaani jaqcline mengi na maadam ritha walikuwa marafiki Sanaa Cha ajabi jaqcline akamgeuka maadam ritha Ila Mungu atamlipa
@jumamofu9573
@jumamofu9573 2 года назад
Kingereza kingi sema na ww ila pole kwa kufiwa na #MENGI kumbe ilikuwa unampenda R.I.P #R_MENGI Sema we Ritha ni mzuri ila ndo hivyo unapenda kudate na madingi bila hivyo ningekupigia misele Mana nakuelewaga Sana we ni msupa mazee
@venanciapeter8059
@venanciapeter8059 Год назад
Shame on you
@godfreyjoseph4750
@godfreyjoseph4750 Год назад
Mnaharibu kipindi kwa huu uzungu wenu
@hadijagere
@hadijagere 2 года назад
😭😭😭😭💜
@rezembuses5739
@rezembuses5739 2 года назад
Mm nashangazwa na hawa wanaozaa wakiwa teenager. Huwa wanongoza kampeni za kile wanachokita mimba za utotoni. Lakini pamoja na mafanikio yao yote zaid wanajivunia watt wao.
@rahmashomari1048
@rahmashomari1048 3 месяца назад
Yes ni must kujivunia watoto coz hawakutegemea kuwa wangefika pale ukizingatia maumivu walioyapitia
@rahmashomari1048
@rahmashomari1048 3 месяца назад
Moving on ni kitu kigumu kuwa mama katika umri mdg changamoto za kutengwa, kwa bulled with everybody , kukatisha ndoto with something didn't planned lzim tukatae mimba katika umri mdogo
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
Vichwa viwili vimekutana
@ziyandamhlana8776
@ziyandamhlana8776 2 года назад
Salma Litta ni mtoto wa kishuwa acha mchezo alisoma Uganda kwamyaka ile ilikuwa ngumu sana kwanza Owens’s inker kusoma
@magesalugwesa4449
@magesalugwesa4449 2 года назад
Salama this is my best show ever ever
@graceirungu2796
@graceirungu2796 3 месяца назад
Mbna hajalisi hata nywele za kizungu hata rang 😊😊 mjeruman wa mchongo 😊😄
@queenhamduni2220
@queenhamduni2220 3 месяца назад
Yeye ni 3rd generation kwani hujamuelewa kasema baba yake ni mjerumani na msukuma. Means baba yake alikuwa half cast wa kijerumani na kisukuma na siyo mzungu. Jifunze kusikiliza na kuelewa sio kukimbilia kuhukumu
@dayana5513story
@dayana5513story 2 года назад
Madam l didn't know your my blood
@mashipeter4819
@mashipeter4819 4 месяца назад
Mungu akutunze. Nimejifunza mengi sana. Salama uko vizuri sana. Urafiki wenu udumu milele.
Далее
Salama Na Gigy Money Ep 12 | ZILE KHADITHI Part 1
25:27
POLI зовет Газана
00:12
Просмотров 794 тыс.
Самое Романтичное Видео ❤️
00:16
Incredible magic 🤯✨
0:53
Просмотров 46 млн