Тёмный

Madam Rita Afunguka Asili Yake Na Alipozaliwa "Nina Makabila Matatu" | SALAMA NA MADAM RITA PT 1 

YahStoneTown
Подписаться 394 тыс.
Просмотров 140 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
SOMETHING SPECIAL
Ms Rita Sundi Paulsen Hans ni mtu muhimu kwangu na kwa mamia kama pengine si maelfu ya wenzangu hapa nyumbani Tanzania. Yeye ni Mama kwanza, Dada kwa wengine, Aunt poa sana kwa kina Malik na Jamal, Bosi ya Mboka kwa Salama na wenzie lakini kubwa kabisa ni MJASIRIAMALI, jambo ambalo amekua akilisimamia lile analo liamini kwa miaka zaidi ya 30 sasa. Rita au Madam Rita alianza kufanya kazi toka alipokua na miaka yake ya mwanzo kabisa ya 20.
Mtoto kutoka kwenye familia ya kitajiri maana Marehemu Mzee Paulsen hakua mnyonge. Baba Mjerumani na Mama Mwenye asili ya kisukuma, kirudi na mchanganyiko wa makabila mengine kadhaa ambayo atatuambia humu ndani. Amekulia kwenye mitihani mingi mara baada ya Baba yake kufariki wakati yeye ana miaka 12 tu. Kutoka kwenye mazoea ya maisha ya kishua mpaka kupata mimba akiwa na umri mdogo na hilo kumlazimisha yeye kuondoka nyumbani akiwa na umri mdogo ndo mi naamini lililomfanya awe CHUMA mpaka leo. Naamini vile wanavyosema kila mtu na njia zake. Kila kitu kinachotokea kwenye maisha yetu kina sababu yake. Yeye kufariki kwa Baba yake ndo kulipelekea kupita KOTE alipopita. Shida na mitihani wakati mwengine huja kwa baraka tele, BARAKA ambazo mpaka leo hii ambayo mimi naandika waraka huu kwa majivuno mengi juu yake. Kweli kila kitu hutokea kwa sababu ili kitu kengine kizuri zaidi kiweze kukufuata ulipo.
Mimi na yeye tulifahamiana kwaajili ya kazi, nadhani wengi wanaijua hiyo khadhithi, ila kama hufahamu mimi na yeye makutano yetu ya kwanza yalikua ya kunipa kazi ya ku host Kili Music Awards ila hiyo kazi ilikuja baada ya pinduapindua nyingi alizo zifanya pale EATV baada ya siku moja mimi kuisema vibaya moja ya video ambazo kampuni yake ya Benchmark ilizitengeneza. Ilikua mtihani haswa baada ya kuskia naitwa tena ofisini kwake? Haya jengine lipi tena? Kumbe round hii ilikua kwa Neema sana, ila Bahati mbaya hiyo kazi wala sikuipata maana na watu wa Kili nao walinikataa kwasababu huko nyuma pia niliwasemea tuzo zao ambazo ki ukweli zilikua za kiwango CHA CHINI MNO considering hela ambazo wanazo wao kama KAMPUNI, kwa kweli lile halikua linapaswa kunyamaziwa.
Basi, peleka mbele mwaka mmoja au miwili baada ya hiyo incident akaniita tena kwaajili ya kazi ya Bongo Star Search sasa, na hii nyengine skia, nilipoitwa sikujua kama yeye ananitaka mimi kama Judge, mawazo yangu yalidhani anataka MTANGAZAJI wa shindano hilo, kumbe yeye alikua na BETTER idea, kama wazungu wanavyosema, the rest is history.
Rita ameniona mimi nakua mbele ya macho yake, nami pia nimeona transformation ya maisha yake kama Mama na Dada. Mengi amepitia ya hadharani na kwas siri, ninayo yajua na nisiyo yajua, ila ambalo nina uhakika nalo ni JINSI AMBAVYO MIMI NAJIVUNIA YEYE, kwa mishale yote ALOIKWEPA na kuendelea KUSIMAMA IMARA, Rita Paulsen Hans ni SHUJAA NA NUSU.
Mengi ameyaongea humu, ambayo ningependa uyaskie MWENYEWE bila ya mimi kudokoa lolote, hakuna chumvi wala sukari ilozidishwa humu ili ‘picha ipendeze’, badala yake ni simulizi nyundo ambazo kama kawaida zitakufanya ujifunze mambo mengi na pia kuangalia baadhi ya vitu kwa jicho jengine.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

20 мар 2022

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 135   
@Iamcameronboyce
@Iamcameronboyce 2 года назад
They’re the Definition of Independent Women ♥️
@sistersade9039
@sistersade9039 2 года назад
Wonderful interview. Wow madam Rita what a wonderful personality you have. Salama u r an amazing interviewer. Well done
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 года назад
Icon...🔥 One among my favourite people...♥️ Thank you Ecejay!
@davidnchoji
@davidnchoji 2 года назад
My favorite show with my favorite Host...I love you Da Salama since then❤️😍
@rashidopakwa6230
@rashidopakwa6230 2 года назад
Salama you're one of the best presenters in Africa.👏👏👏. That's why I like your interviews. 🔥🔥🔥✔️🇰🇪👊
@SaidChande-yl3wq
@SaidChande-yl3wq 5 месяцев назад
A pure administrator! All the best 👍 madam
@albogastmselejr4583
@albogastmselejr4583 2 года назад
Jesca Leo Kabadilisha Nguo Kumbe Ana Kijitako Cha Bunduki 🤣🤣
@Iamcameronboyce
@Iamcameronboyce 2 года назад
Madam is a whole different person. Her personality is 🔥
@nicki1885
@nicki1885 2 года назад
She’s a strong woman ! Started from the beginning, she has a beautiful soul ! 😭♥️
@mwajabujumanne9025
@mwajabujumanne9025 2 года назад
I appreciate. Sana madam kwa unachokifanya mungu azid kukulinda
@fatmamwalim-ih4ku
@fatmamwalim-ih4ku 3 месяца назад
Ki ukwe ukweli huyo Mama nanpenda sana sana*Allah ampe umri mrefu
@yusuphmligiliche8353
@yusuphmligiliche8353 2 месяца назад
Hongera sana Salama kwa hii platform ya mahojiano. Shukran kwa haya mahojiano na da Rita. Endelea na kazi bora!
@zakiakawese3222
@zakiakawese3222 2 года назад
Nakubari sana hizi Interview 👏👏✌️
@clevermngao7565
@clevermngao7565 3 месяца назад
Wanaume Mungu anatuona!! Yaani uende kumchukua mtoto wa watu ili umuendeleze Shule kwa sababu ni mdogo na alishapewa mimba akiwa na umri mdogo! Then badala ya kumuendeleza shule unamtia mimba nyingine!! Je! Huu ni ukatili au sio ukatili? Pole sana Madam Rita kwa safari hiyo ya maisha uliyopitia!!!
@maryamtan682
@maryamtan682 3 месяца назад
Wanasema akili ku mkichwa😂😂😂😂
@roseruhuta3325
@roseruhuta3325 3 месяца назад
Mada Rita ❤
@RuthBenjamin-vk8fd
@RuthBenjamin-vk8fd 4 месяца назад
God akulinde madam Ritha umeongea nimemuelewa Sanaa Sanaa endelea kubariki vijana wetu
@doreendinamica3473
@doreendinamica3473 2 года назад
hii ni exclusive yaani ..........big up salama...!
@k.d.m83
@k.d.m83 2 года назад
Tusisahau kutuma Tip kupitia Mpesa aisee, kazi nzuri wanafanya😁
@tumainkitundu1015
@tumainkitundu1015 Год назад
Madam Ritha wewe ni mtu na nusu nakubali kazi yako. Keep it up
@mustafaameir8186
@mustafaameir8186 2 года назад
She is a strong woman !
@5starsmoviecenter714
@5starsmoviecenter714 2 года назад
We call them over thinker they have smart mind, focoused, open minded and always think positive
@nicki1885
@nicki1885 2 года назад
I love the fact she didn’t want to use the words “it was an accident” and changed it to “it wasn’t planned “🙏💯
@StephenKihula
@StephenKihula 2 месяца назад
Your story put me on point to look you in a very special manner. But all in all pole Sana kwa yote uliyopitia to where you're today.
@josephgatunzi1670
@josephgatunzi1670 2 года назад
Kazi nzuri 👊🏿
@mussakhamis2377
@mussakhamis2377 2 года назад
Good interview
@karutomdee3107
@karutomdee3107 4 месяца назад
Mada masha allah jamn nakupenda jamn sirias toka zamani sema nafasi nakosa kpzzzzzz jaman nakupenda eee nko mkoa eee
@raphaelkessy7360
@raphaelkessy7360 3 месяца назад
Ki King'eng'e kimezidi banaaaa
@huberturio3743
@huberturio3743 2 года назад
Salama mnoma
@SalmaJuma-xv9qp
@SalmaJuma-xv9qp 7 месяцев назад
Nzurii
@neemaalbert2731
@neemaalbert2731 2 года назад
Madame ritha mnyamwezi sanaaa🤪❤️
@coneephraim7756
@coneephraim7756 2 года назад
Salama...... you ar so good and fit on presenting a sessions with..... to me you ar not boaring in all of ur ukorofi questions....
@shyfettymtunda4619
@shyfettymtunda4619 3 месяца назад
Kuna mambo mengi sikuwahi kuyasikia kwenye interview yoyote aliyowahi kufanya Ritha,ila leo nimepata majibu ya maswali yote niliyokuwa nikijiuliza. Umepitia mengi, lakini hukuwahi kukata tamaa pamoja na mapito yote.You are a super women🎉
@user-lz5lb1cd8o
@user-lz5lb1cd8o 3 месяца назад
Kizungu jamani warundi hatuerewi
@florakaria3793
@florakaria3793 3 месяца назад
Madam Rita pls naomba niwe rafiki yako ! ❤nitapata mengi kwako
@halimalachpat1927
@halimalachpat1927 3 месяца назад
Kupungua kwa uzuri inategemea na hali ya maisha ya kila siku ila nampenda sana huyu dada ana huruma sana mpenda watu mchapa kazi j say big up madam🎉
@DEBORAHMASANJA-yz3go
@DEBORAHMASANJA-yz3go 3 месяца назад
Hi Madam Rita nakupenda sana
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 года назад
My favorite 😘
@mazartajmohamed1437
@mazartajmohamed1437 3 месяца назад
Iron lady very difficult to understand her, genueas and confident this type of lady there are very few in this planet.
@fatmebakar1315
@fatmebakar1315 7 месяцев назад
Yani nakipenda kipindi hichi San Kwanza mazingira yake uwandaaji wake Yani nimzuri sana
@letsgrowwithm4620
@letsgrowwithm4620 2 года назад
Thats me loneeeer🙏
@Youngchimodzi823
@Youngchimodzi823 3 месяца назад
Wanawake kweli kama maua,yanachanua na baadaye kufunga. True with time we decay,urembo wake wote mzuri sana umepungua sanaaa,daah wkt ni ukuta
@FiollaIsaya
@FiollaIsaya 2 месяца назад
Huyu madamu mara mbili siku tofauti nili msalimia shikamoo alikaa kimya nilijisikia vibaya sana afu nilikua shabiki yake sana
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
🔥🔥
@TaarabChannel
@TaarabChannel 3 месяца назад
Mupitie na kwangu wapenzi..sapoti kusapotiana❤
@joycemuhoja4729
@joycemuhoja4729 Год назад
Mwaka 2023 Nakuja Bss Natamani Sanaa
@HamadiBwakame
@HamadiBwakame 2 месяца назад
Salama twawapenda s punguzen kiizungu
@rukiachamani1101
@rukiachamani1101 2 года назад
Nami ni mmojawapo wa watu wanaotaka kukaa peke yangu muda mwingi.
@josephlorri431
@josephlorri431 3 месяца назад
Mtoto mzuri wewe, kwa nini ukae mwenyewe muda mrefu? Toa nafasi, nipo
@user-oi1qy8uj6r
@user-oi1qy8uj6r 3 месяца назад
Even me dear
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Mimi ni super loner hadi watu hawanielewi na wanahisi nataka kujiua
@carolineoyugi7771
@carolineoyugi7771 2 года назад
Mek up ya Leo mbaya sana madam
@masturaabdul1007
@masturaabdul1007 2 года назад
😃😃😃😃😃sanaaaa. Mbaya mbaya mbayayaayyaa
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Hiyi make inaitwa "nude" na ndo fashion ya wakati huu
@user-nt4mw7zm7d
@user-nt4mw7zm7d 3 месяца назад
Dada salama.. mimi binafsi naona uongozi ndani yako.. hebu pita kidogo huko alafu kuna watu watakushukuru kwa maamuzi utakayochukua
@LunodzoMwinuka
@LunodzoMwinuka 8 месяцев назад
Sauti za jamaa wanaopiga picha zinasikika. Mnaweza lifanyia kazi hilo pia.
@karimukalema4613
@karimukalema4613 2 года назад
WHERE IS JESICA ????????? WE WANT HER BACK
@shukurupaul5299
@shukurupaul5299 7 месяцев назад
Omg
@alawisaid280
@alawisaid280 29 дней назад
salama jitahidi kuwaambia wapunguze kingereza siunajua wa tz tuna hiyo shida😅
@Chapesatv
@Chapesatv 2 года назад
Huyu mama wange mpa ile nafasi ya Stive nyerere kaleta vipaji vingi sana tena wakali.
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 года назад
True my dear 👍
@catenzeki678
@catenzeki678 2 года назад
Nakubaliana na ww 100 kwa 100
@ngoshachaula172
@ngoshachaula172 2 года назад
Chapesa sikubaliani naww ni tapeli
@Chapesatv
@Chapesatv 2 года назад
@@ngoshachaula172 sawa ila uliwahi kusoma mikataba yao au kujuwa makubaliano yao maana watanzania mara nyingi kusoma mikataba tunauvivu nako sana. Kwahio sote ukweli hatuujuwi tusimuhukumu.
@vj8313
@vj8313 2 года назад
Kabisa
@faithjonathan3845
@faithjonathan3845 Год назад
Am a loner too..na ni kitu kizuri sana...unafanya hata maamuzi kwa iuyafikiria wewe kama wewe. Madam Ritha ni mtu poa sana. Nakumbuka the day I met her akanisifia mpaka nikajisikia raha sana👌😘😘
@aloyceshaban1348
@aloyceshaban1348 Год назад
Mmmmh
@cobrachristian3685
@cobrachristian3685 2 года назад
Kumbe wewe n mtu wa rwanda dada yetu kalibu nyumbani🇷🇼
@ngoshachaula172
@ngoshachaula172 2 года назад
Uoni komweee hilo
@masturaabdul1007
@masturaabdul1007 2 года назад
Pole Madam ila sitaki kuwa mnafiki alokupamba kakuharibu kama hujatambuliswa nisingekujuwa😃 Madam achana na mpambaji huyoo
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 года назад
Kabisaaa
@bellabakera
@bellabakera 2 года назад
Wa kwanza leo
@abdulraufmohammedsalum6806
@abdulraufmohammedsalum6806 2 года назад
Wa kwanz mm tulia
@emmanuelonyangoochola9228
@emmanuelonyangoochola9228 2 месяца назад
Apewe heshima yake huyu mama
@nereaigogo4442
@nereaigogo4442 2 года назад
Ila kiukweli hii ni moja ya interview ngumu sana ambayo salama amewahi kufanya Imagine anam interview boss wake na rafiki yake.
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Alishawahi kumhoji kwenye kipindi chake cha zamani yeye Salama kinaitwa MKASI. Hii anamhoji ni mara ya pili.
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Salama alishawahi kumhoji huyu bosss wake kwenye kipindi chake cha MKASI kabla ya hiki
@ebbyramadhani
@ebbyramadhani 2 года назад
jesca leo vipi?
@zarayusuf2882
@zarayusuf2882 3 месяца назад
Who is madam Rita ?
@maidamhanje5993
@maidamhanje5993 2 года назад
Tupo wengi tunapenda sana kua pekee yangu nilijua ni ugonjwa
@beatricekitara5808
@beatricekitara5808 Год назад
Iyo ni shida sio kawaida
@gracekagoma3231
@gracekagoma3231 3 месяца назад
Dada ongea kiswahili bila kuchanganya kiingereza wengine hatuelewi😢😢
@yustersimon5104
@yustersimon5104 3 месяца назад
Hata hicho kiswahili kajifunza mwaya
@asmaathmani440
@asmaathmani440 Год назад
Madam nakupenda but kuhus age umetudanganya
@vj8313
@vj8313 2 года назад
Kingereza kingi madam vp ? Kumbuka kuna ambao hawajasoma wanatizama kipindi hata hiyo english yako hawaijui so speak national language banaa, all in all uko good jasiri muonyesha njia 🔥
@rommelmauma8081
@rommelmauma8081 2 года назад
Hakuna ubaya endapo mahojiano yatakuwa kwa Kiswahili au Kiingereza; kuchanganya lugha hizo mbili kunaharibu mazingira ya maudhui ya mahojiano. Chuchumilieni kuongea Kiswahili!!
@mtilimsita6675
@mtilimsita6675 3 месяца назад
Nimependa mama
@fatmebakar1315
@fatmebakar1315 7 месяцев назад
Yani madam rita story yako kwakweli inaendana Na yangu kabisa
@itanzaniaAS
@itanzaniaAS 3 месяца назад
Mimi Nina makabila 9 yani sieleweki😂😂😂😂😂kila kits nipo tofauti
@ruu6592
@ruu6592 Год назад
I lv madam Rita but she looks very difficult ☺
@sasha-ri7tf
@sasha-ri7tf 3 месяца назад
MAJIZI GROUP 😅😅😅
@amirymdee4259
@amirymdee4259 Год назад
***Napajua Umurushaka,Nkwenda,Kaisho,Murongo Kona kumi na mbili,****
@ZainabuMteti
@ZainabuMteti 6 месяцев назад
Madam pole ulipitia
@halimalachpat1927
@halimalachpat1927 3 месяца назад
Hivi mi nauliza ni nani aliwahi kuwa mtoto?nadhanni jibu ni wote usichana,umama,na uzee?je hali si inaenda kubadilika? Mangapi yamemtokea madam?linganisha jani bichi na njano uzri wake .maisha ni safari ndefu.
@user-zo8ub3tl9g
@user-zo8ub3tl9g 3 месяца назад
Alikua anaupenda tu huo mchezo
@romanarosemedard2551
@romanarosemedard2551 3 месяца назад
Be specific Sasa kitambulisho cha NiDa umejaza hayo makabila ya baba zako 3 Siku zote tunafuata ukoo wa baba Aliyeweka mimba kwa mama yako Halafu wewe unajulikana kama hata shule umepia Huko ni kujikaa Ritha
@sumayaishengoma4543
@sumayaishengoma4543 Год назад
Hapo kwenye sura zake mbili nimeziona hiyo sura yake ya kazi unaweza usiamini kama ni the same person 😂😂
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Год назад
🤣🤣
@tausiabdalla9904
@tausiabdalla9904 9 месяцев назад
Kumbe hata kama u unahela mambo ni magumu tu😅
@fidelitekarigirwamuyangwa973
@fidelitekarigirwamuyangwa973 3 месяца назад
Kama Mimi nimezaa14 nikateseka
@mack_B.
@mack_B. 2 года назад
Hivi ukisema kua hupend mtu muongo mnafiki sjh nn na nn hiv inakuaje kwa upande wako wewe mwenyew hivyo vtu u didn't get au manake uongo kuuepuka Ni Mara chache Sana same tu unafiki jmn tusiwe waongo katka ilo🤣🤣🤣
@naturelle1097
@naturelle1097 3 месяца назад
Where is the camera interviewer is looking away..we see legs n shoes can u be serious
@prudencemushi6948
@prudencemushi6948 Год назад
The Accent is boring.... juzi tuu the accent was well booom it has changed
@neemaalbert2731
@neemaalbert2731 2 года назад
Heshma Kwa mama Samia kurudisha wajawazito shulen
@albogastmselejr4583
@albogastmselejr4583 2 года назад
Aisee Mbona Heleni Za Madame Kama Ni Mzigo 🤣🤣 Au Basi Itakuwa Kakata Nyororo Ya Mbwaaa
@catenzeki678
@catenzeki678 2 года назад
😂😂😂😂😂😂
@mwajumalubunga1534
@mwajumalubunga1534 2 года назад
🤣🤣🤣🤣🤣🙆‍♀️🙆‍♀️
@petermanala6138
@petermanala6138 3 месяца назад
😂😂😂😂😂dar sawa bwana
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Jamani watu wanapenda kuongea vibaya
@user-gk1bk7sf5g
@user-gk1bk7sf5g 3 месяца назад
Inawezekana akawa ni mhaya wapenda English.
@KhadijaMiteya-hh8xl
@KhadijaMiteya-hh8xl 3 месяца назад
Amesha kwambia msukuma na mjerumani ujasoma comment?
@tiffanyakramJr822
@tiffanyakramJr822 2 года назад
Me hivyo viti mlivyo kalia , hata sijavielewa kabisaa.. Khaa🤗 ukihojiwa na mtu anaekujua ngumu kuficha ukweli Asante Salama
@mikhitaryankombo9604
@mikhitaryankombo9604 2 года назад
Mm binafsi nakubali hiki kipindi lkn kwauchunguz wangu nimebauni wanaongea kingereza Sasa kuliko kiswahili ndio hua siku mbaya ya kipindi
@magorymara5515
@magorymara5515 3 месяца назад
Ni lugha ya pili Tanzania kama hujui moja lazima utajua moja huko ndo ukweli
@wennybarny168
@wennybarny168 3 месяца назад
Jamani hiyo ni fashion ya make inaitwa "nude" Naona watu hawajailelewa ila iko namna hiyo Wakati prince Harry anaoa mjukuu wa Queen Elizabeth, mtoto wa prince Charles (ambaye sasa ndo king wa uingereza) watu walisema bi arusi hajatumia makeup kabisa, kumbe alitumia makeup ya milioni 30 za kitanzania. Ni make ya nude ambayo rangi zake ziko kimya. Rangi hazi-shout.
@dianerditto
@dianerditto 2 года назад
Madam Ritha mimi pia sio mnafki, nikuombe tu umfukuze kazi huyo makeup artist wako aliekufanya hvo uson kwenye interview hii
@abdulraufmohammedsalum6806
@abdulraufmohammedsalum6806 2 года назад
😆😆😆😆
@masturaabdul1007
@masturaabdul1007 2 года назад
😃😃😃😃😃😯😃😃 kweli age imeenda ila makeup mbaya sanaa
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 года назад
Hahaha kweli aiseee🤣
@tuliadamson3422
@tuliadamson3422 2 года назад
🤣🤣🤣
@mwajumalubunga1534
@mwajumalubunga1534 2 года назад
🤣🤣🤣🤣✌
Далее
HOW DID SHE WIN??
00:49
Просмотров 14 млн
FARUX RAIMOV AVJIGA CHIQDI - JAVOHIR🔥
01:01
Просмотров 1,4 млн
Shilole alivyokuwa Muhudumu wa Hoteli na kumtongoza Ray
19:43
Телега - hahalivars
0:55
Просмотров 2,4 млн
Не поймаю говоришь? ;)
0:55
Просмотров 1,8 млн