Тёмный

Salama Na FETTY DENSA SE6 EP70 KUTOKA UBAVUNI PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 394 тыс.
Просмотров 14 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kwa ambao wanafuatilia mpira hapa nyumbani wanamjua mchezaji huyu mahiri wa Simba Queens lakini ambao wanafuatilla soka la wanawake hawa watakua wanaelewa uwezo binafsi na uhodari wake wa kucheza namba tofauti tofauti uwanjani ila ukimkuta kaikamata mbavu ya kulia aidha kwa Simba au timu ya Taifa ya Tanzania. Fatuma Issa ni mtu na nusu, hakuna mpenzi wa mpira au kocha yoyote wa mpira anaweza akamuacha kwenye benchi wakati team inatafuta matokeo au inataka kuwaonyesha walofika kuwaangalia vipaji ambavyo wanavyo kwenye kikosi chao. Kwa yoyote yule na kwa vyovyote vile, Fetty Densa, ni lazima AANZE.
Ananikumbusha sana mimi na rafiki zangu wakati tunakua, tulikua chizi michezo hasa baada ya kufika shule ya Sekondari, ilikua kama lazima kila mmoja kuwa na uwezo wa kucheza zaidi ya mchezo mmoja ili tuwe na vikosi imara inapotokea kwenda kufanya uwakilishi wa shule, mkoa au nchi. Binafsi nilikua na uwezo wa kucheza Basketball na table tennis tu ila nina marafikia kama kina Kalova na Mboni Mntambo ambao wao walikua wanacheza Basketball, Netball, Volleyball na chochote kitakajokuja mbele ambacho kinatumia mpira kucheza lol, na tena VIZURI, sio kujazia namba tu uwanjani. Naye Fetty ni kama wanangu hao kutokana na maongezi yetu. Ananiambia hata shuleni mwalimu na wanafunzi wote katika shule yao walikua wakifahamu na kujivunia yeye sana.
Akiwa anakua huko Morogoro Fetty ni ‘mtoto wa Bibi’ zaidi, yeye ndo alomlea na kumtunzia siri zake zote, na ndo alomfundisha kupika na kumkumbusha kwamba yeye ni mtoto wa kike kwahiyo alihakikisha pia mjukuu wake kwenye masuala ya kupika na usafi wake na wa nyumba pia haachi kujifunza. Bibi pia ndo alipewa ahadi ya kwamba kuna siku mjukuu atakuja kuwa mchezaji hodari kuwahi kutokea hapa nyumbani na so far, so good. Babu yake nae hakua nyuma kwenye kumsifia mjukuu wake pale anapofanya vizuri jikoni kwasababu pengine kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili ampe moyo mjukuu wake.
Fatuma anatuambia humu kwenye maongezi yetu jinsi ambavyo alihangaika mkoani Morogoro kupata team ya kucheza na jinsi ambavyo alijutuma toka siku ya kwanza kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Ukimsikiliza kwa makini utagundua kama ni mtu mwenye mawazo ya mbele kuliko hata umri wake, hiyo inamsaidia pia inapofika wakati wa kufanya maamuzi anapokua ndani na nje ya uwanja. Unaweza ukajiuliza kwa kipaji chake na ujuzi wake kwanini hachezi nje ya nchi? Kwanini amekua Simba huu msimu wake wa nne na amekua akicheza kwa kiwango cha juu sana? Densa anatupa majibu ya swali hilo ambalo nina uhakika wengi wao wamekua wakijiuliza.
Mahusioano yake na Mama yake ambaye alikua mmoja kati ya wanenguaji wazuri miaka iliyopita na ndo alimfanya pia mwanae naye atake kuwa Densa (ndo jina la Fetty Densa lilikotokea). Wana mahusiono ya aina gani? Mama alilichukuliaje suala la Binti yake kuchagua soka? Na Mzee wake nae yuko wapi? Nafasi yake kwenye team yake? Team ya Taifa je? Experience ambayo waliipata Morocco wakati Simba ilipoenda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Africa? Vipi kuhusu mpira wa miguu wa wanawake hapa nyumbani? Pesa ipo? Muelekeo je?
Haya maongezi ni moja ya maongezi bora ambayo nimeshawahi kufanya na natumai yatafungua milango kwa watoto wa kike na wazazi wao wengi kuelewa na kuipambania fursa hii ambayo Dunia nzima imeanza kuielewa.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

4 июн 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 26   
@user-qb4vx2rs7e
@user-qb4vx2rs7e 5 месяцев назад
Safi sana
@yusufsong7993
@yusufsong7993 Год назад
Safi sana nazani ndio mchezaji wa kwanza kuojiwa wa Simba Qween
@maishaforreal7798
@maishaforreal7798 Год назад
DIZASTA VINA MUPENI PLATFORM ANATALENT KUBWA SALAMA NA NI GENIUS
@musambaruku6661
@musambaruku6661 Год назад
Yaah yaah
@manalickmasha302
@manalickmasha302 Год назад
Sema intro ya hii show ni epic sana.
@abuujuhayfa4321
@abuujuhayfa4321 Год назад
Salaama na fety umetisha saana
@arownabdul9578
@arownabdul9578 Год назад
I like the interview dada salama, judge mweny roho mbaya🤗🤗 (kidding) , mimi nasugest next podcast iwe na richstar, digital person
@chamyfx9377
@chamyfx9377 Год назад
Safi sanaaa
@cadeauwatanga5686
@cadeauwatanga5686 Год назад
@salama ,tunaomba interview yakufata iwe ya @Fei toto ,nice good job
@fathiyahmuzney7367
@fathiyahmuzney7367 Год назад
Salama nakukubal sana❤
@Alkebulan-Afrika
@Alkebulan-Afrika Год назад
Salama na FRED VUNJA BEI
@niite_cousin1362
@niite_cousin1362 Год назад
My best interviews so far are: Salama na isaya yunge Salama na Togolani mavura Salama na iddris sultan Salama na daniel kijo Salama na auntie ezekiel Salama na sheikh kipozeo Waiting interview : salama na sheikh kundecha , salama na yerico nyerere …..
@Gaddafi-knight
@Gaddafi-knight Год назад
Salama naomba utuletee nyandu tozzy
@adinanhashim3630
@adinanhashim3630 10 месяцев назад
Salamaaa tuletee Shekhe mazinge
@dianerditto
@dianerditto Год назад
😂😂😂❤nimepentaaaaaa
@godfreymiho4927
@godfreymiho4927 Год назад
👍
@benancejohn1198
@benancejohn1198 Год назад
Mtoto wa Msamvu 🙌
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Год назад
Kwanini wasingekupanga na Simba king, ili tupate ushindi 💪
@elzearselestine5000
@elzearselestine5000 Год назад
Salama mlete na diamond tunataka kujifunza kutoka kwake
@deetz255
@deetz255 Год назад
😂😂
@maishaforreal7798
@maishaforreal7798 Год назад
DIZASTA VINA
@honestyerasto
@honestyerasto Год назад
Nadhani wachezaji hawatakiwi kulalamika kutokuruhusiwa kuingia uwanjani bure. Viingilio wanatakiwa kulipa na hata hivyo sio hela nyingi kwao.
@ashumohd2192
@ashumohd2192 Год назад
Sauti ya Fetty km ya zamarad
@wildanimalsdocumentary1255
@wildanimalsdocumentary1255 Год назад
Walete watu wakubwa wenye mafanikio makubwa kweny kipindi tunatak kujifunza kupitia wao especially wafanya biashar na wasanii hata kam ni wachezaj bhc wenye majina salama....🙏🏽🙏🏽🙏🏽
@doreensportswear_
@doreensportswear_ Год назад
HUYU NI FATMA DENSA WA SIMBA QUEENS
@e45mussa78
@e45mussa78 Год назад
Tunaomba interview with @millardayo
Далее