Тёмный

Salama Na DEO GRATIUS SE6 EP64 | PRIVILEGED?! PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 

YahStoneTown
Подписаться 395 тыс.
Просмотров 36 тыс.
50% 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Deo Gratias, jina tu linatosha kujielezea kama wewe nawe utakua kama mimi wa kutaka kujua maana ya majina ya watu ili uweze kujua tabia zao au ujiulize wazee wake walikua wanafikiria nini wakati wanaamua kumpa jina hilo mtoto wao. Kwa Deo maana imejibeba na imejikamilisha na kwa yeye kuamua kubaki na jina lake hilo hilo mpaka kwenye stage ambako ndo sehemu yake ya kazi inabidi hilo nalo likuambie jambo kuhusu yeye na jinsi ambavyo anajichukulia na kuyachukulia mambo ambayo ameyachagua kuyafanya.
Shukrani ziende kwa Mungu ndo maana ya jina lake, shukrani ziende kwa Mungu kwa kila alifanyalo leo, shukrani ziende kwa Mungu maana baada ya wazee wake kumsomesha kwenye shule ambayo walikua wameianzisha wao na kuhakikisha kijana wao anapata elimu ambayo anastahili lakini yeye akaamua kuiacha fani ambayo aliisoma na kuamua kuwa mchekeshaji basi nadhani Shukrani ziende kwa Mungu, Shukrani ziende kwa Mungu kwa wazazi wake kuelewa, Shukrani pia ziende kwa Mungu kwasababu mwanga umeanza kuonekana kwenye lile alifanyalo sasa.
Yeye na rafiki zake ambao ni vijana wenzake wamejikusanya na kuanzisha kundi lao linaloitwa Watu Baki, ila hawakuamka tu wakaanzisha, kuna ka story hapo nyuma yake ambapo ndo panaleta maana kwenye maisha yetu na yao kama watafutaji. Deo anakumbuka audition ya kwanza ya Stand Up Comedy ambayo aliwahi kuifanya na akashinda huko Mbagala, chini ya shindano lililokua likisimamiwa na Evans Bukuku, Deo anakumbuka kushinda MILIONI nadhani kwenye shindano hilo ingawa alipofika home aligundua kuna mwana alichomoka na elfu kumi yake, yaani kuna mwana alimuangalia Deo, kisha akakiangalia kibunda alafu akasema nah, hawezi kumpa yote lol.
Courage ya kufanya mengine mengi ikiwa na pamoja na ambayo yanaendelea leo ilianzia hapo. Mengine yakabaki story!
Story ya kujikusanya na wanae enzi za Cheka Tu na baadae kuamua kundoka na kuanzisha WatuBaki ilikua mmoja inabidi awe na uthubutu na uthubutu huo uliwezekana na mpaka leo wamesimama na wana time yao kwenye DSTV ambayo inatoa burudani nzuri tu kwa watu wao na vile vile bado matamasha ya nje wanafanya wao kama wao.
Kwa wengi ikiwa pamoja na mimi tulipewa story kwamba Deo ni mtoto flani wa kishua alokua kutoka kwenye familia inayokula wali kwa kijiko na ndo maana baadhi ya mambo ilikua rahisi kwake kufanyika kwasababu ana uwezo wa kurudi nyumbani kwa Baba na Mama na akarudi na mzigo wa kutosha ambao unasaidia mambo yaende. Ila kwa mujibu wake, hiyo si habari na wala yeye hajatoka kwenye mazingira hayo ambayo wengi wanadhani ametokea.
Bado safari ndo kwanza imeanza na kwa wenzake yeye akiwa kama kiongozi anaamini kama wakitulia pamoja na kufuata maono yao basi mengi mazuri tu yatakuja, ila sasa huo uwezo wa kuweza kutulia pamoja na kutengeneza kitu kikubwa na kizuri ndo inawezakana ikawa mtihani. Si wengi wameweza ingawa wapo ambao wameanza pamoja na mpaka leo wanaunguruma pamoja. Inawezekana na yangu matumaini wao pia wataendelea kuwa WatuBaki kwa muda wote ulobaki.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪RU-vid Link bit.ly/RU-vidSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Развлечения

Опубликовано:

 

24 апр 2023

Поделиться:

Ссылка:

Скачать:

Готовим ссылку...

Добавить в:

Мой плейлист
Посмотреть позже
Комментарии : 70   
@fadhilimwakaje154
@fadhilimwakaje154 Год назад
This guy deserves more recognition than he got..keep up deo 👊
@dorisfabian4776
@dorisfabian4776 Год назад
My favorite comedian.. Deo gratius
@camillah1097
@camillah1097 Год назад
Mungu mwema kaka utafika mbl sana unatisha kwenye jua kali nakupenda sana kk Deo
@aloyceshaban1348
@aloyceshaban1348 Год назад
Duke on 🔥🔥🔥🔥
@sumayaishengoma4543
@sumayaishengoma4543 Год назад
Genious himself Deoooooooooi🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉
@skigen
@skigen Год назад
I love listening to Deo, he's a talented story teller.
@agnesmussa197
@agnesmussa197 Год назад
Salama Tunaomba Wachambuzi Wa Mchongo pia 🙏🙏🙏
@Lugonela
@Lugonela Год назад
Very smart guy
@sarahsesa8851
@sarahsesa8851 Год назад
Napenda kingereza chako very super
@chiccynaturaldamnhot877
@chiccynaturaldamnhot877 Год назад
Wow nimependa sana when he explained about Utu baki!!
@movierecapsswahili1042
@movierecapsswahili1042 Год назад
I truly love this guy
@goodlucktemu3149
@goodlucktemu3149 Год назад
Deo ni mchekeshaji bora kuliko wote apa Tz kwa anaebisha amfatilie.
@jasirimjasirimedia7940
@jasirimjasirimedia7940 Год назад
This man is genius keep it up brother
@asterialucas4680
@asterialucas4680 Год назад
I like this 👍
@johnwilfred3920
@johnwilfred3920 Год назад
Joel Arthur Nanauka
@JonasMbilinyi-py2hg
@JonasMbilinyi-py2hg Год назад
Love this guy
@KaijageNdyanabo-xx3eq
@KaijageNdyanabo-xx3eq Год назад
Huyo broo wetu kioaji kutoka ifoza mtoto wa mzee mboya Daah broo mm nàkukubali mno
@JoeMziwanda
@JoeMziwanda Год назад
msera ni genius sana huyuuu
@bigdaddy_faustinjumong4427
@bigdaddy_faustinjumong4427 Год назад
Bro Juwa kama unapendwa saaaana 🔥💪
@christinasinderema3005
@christinasinderema3005 Год назад
Hahaaa linda linda
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 Год назад
Nampendaga huyu kaaka...anawaigiziaga lafudhi watu wa ifakara utacheka ufe ..very genious aise
@heightsmays5963
@heightsmays5963 Год назад
Tunamuomba Moto Mabanga
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
🤣😂Linda Linda 🤣
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 Год назад
Anaongea deep sana kisomi..mabongolala hawawez mwelewa
@BIGBOSS-hl3bu
@BIGBOSS-hl3bu Год назад
Sauti ya huyu mwamba inafanana sana na idriss sultan😂😂
@dankirunda3368
@dankirunda3368 Год назад
Safi HomeBoi #Deo
@ashaidd2912
@ashaidd2912 Год назад
Plz Joel nanauka salama
@maryamconstantine2232
@maryamconstantine2232 Год назад
Nilivyomuona huyu kaka nikaja mwenyewe 😂😂
@derickdepota101
@derickdepota101 Год назад
Deo mtu safi saana🙌🏿
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
Joel nanauka please
@dullah5733
@dullah5733 Год назад
Salama katoka London innit that’s why there was money involved innit 😅😂innit innit 😂
@Angle-lm3sb
@Angle-lm3sb Год назад
🙏🙏
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Год назад
Juma lokole please
@official-madudu4959
@official-madudu4959 Год назад
Namsikia kyombo deo akiongea
@JoeMziwanda
@JoeMziwanda Год назад
ANAKITUUU ATAFIKA MBALII😂
@azizaedina8088
@azizaedina8088 Год назад
🥰🥰🥰🥰
@zebedayobiswalo1924
@zebedayobiswalo1924 Год назад
Diamond platnumz please
@dianerditto
@dianerditto Год назад
I love deogratius much, good interview 🥰
@rehematawalani733
@rehematawalani733 Год назад
RRINDA RRiNDA umemuacha wapi weee no unaweza na RRiNDA RRINDA
@rizikiurio1133
@rizikiurio1133 Год назад
Joel nanauka pleaseeeeee 😊
@haphsamaulid304
@haphsamaulid304 Год назад
Mtot WA mama mboya😂😂😂
@haniphadaud667
@haniphadaud667 Год назад
Wachambuzi Wa Mchongo 🏃🏃🏃
@priscamnzava2656
@priscamnzava2656 Год назад
Home boy
@ishe_ngo8926
@ishe_ngo8926 Год назад
Siku nyingine tumia lugha moja kiingereza haieleweki kiswahili haieleweki pia. Siku nyingine tumia kiswahili hutaeleweka vizuri.
@fadhilimwakaje154
@fadhilimwakaje154 Год назад
Sio kwamba wewe ndo una uelewa mdogo 🤔
@Unique653
@Unique653 Год назад
Jifunze kingereza ndugu yangu, utateseka sana
@bahatijonas2183
@bahatijonas2183 Год назад
Tuletee WACHAMBUZI WA MCHONGO Ganslay na Headmaster
@rehematawalani733
@rehematawalani733 Год назад
Kweli comedy imekukontro yaani nacheka kwa kuchekesha
@julianamaganga4803
@julianamaganga4803 Год назад
Toomuch talking but he's goodguy
@fakiikibakola1300
@fakiikibakola1300 Год назад
Swali moja majibu 100
@godfreymiho4927
@godfreymiho4927 Год назад
Huyo jamaa ni hatar
@lucydelina1749
@lucydelina1749 Год назад
Salma naomba uniite na mim jamn
@olicej7837
@olicej7837 Год назад
Siku ukiitwa uniambie na mimi nikusindikize🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂
@officialbntrasool5223
@officialbntrasool5223 Год назад
Salama uniite mim siku moja 😊
@olicej7837
@olicej7837 Год назад
Siku ukiitwa na mimi uniambie nikusindikize
@officialbntrasool5223
@officialbntrasool5223 Год назад
@@olicej7837 😂😂😂
@vonniemarry2680
@vonniemarry2680 Год назад
Hachoshi kumsikiliza
@domycossan1395
@domycossan1395 Год назад
Kwa mara ya kwanza ndo najua maana ya Mtu Baki au Watu Baki
@derickdepota101
@derickdepota101 Год назад
Deogratius mtu na nusu
@mrs2918
@mrs2918 Год назад
STIFF Ifakara moja,
@emmamatemu8225
@emmamatemu8225 Год назад
Hii kuchanganya kiswahili na Kienglish sometimes inakera
@gilmangeorge366
@gilmangeorge366 Год назад
Jifunze English bn
@paulalove1223
@paulalove1223 Год назад
​@@gilmangeorge366 😂😂😂
@macrinadallu5462
@macrinadallu5462 Год назад
​@@gilmangeorge366 😅😅
@Bongodailyhabari
@Bongodailyhabari Год назад
Mtu umezaliwa na MD na afisa af useme sio wa kishua c'mon we ni wakishua manzee period. acha kutuchora
@kokusimabayona4179
@kokusimabayona4179 Год назад
Kwakweli anatuchora,. Gari wamenunua akiwa form 2 wakati wengine wazazi wao wanastaafu bila hata gari Ila wabongo
@maggieluvuno4666
@maggieluvuno4666 Год назад
Dereva wa Bobo na Linda Linda
@bm4tv602
@bm4tv602 Год назад
Kingereza Cha mjinga huyu ni super
@salhamrishoi4943
@salhamrishoi4943 Год назад
Kasoma❤❤
@julianamaganga4803
@julianamaganga4803 Год назад
Toomuch talking but he's goodguy
Далее
CHEKA TU. Kings Edition. Deo Gratius kwenye stage.
26:59